Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Sio lazima utoboe kwa hela za wazazi. Nina mifano kama 3 real. Kuna rafiki yangu under 30 kaacha kazi mwaka jana pale World vision anamiliki mark x kali na nyumba. Hajarithi chochote. Mwingine alivyomaliza chuo kapiga ymachinga kariakoo kisha kashirikiana na wenzie kupanga chumba kariakoo, sasa hivi anapiga biashara china, india, tz. Kama unajua kodi ya chymba pale kariakoo utaelewa, Hajarithi kokote.
Mwingine ni ndugu yangu kabisaa, mwanajeshi sasa hivi anamalizia mjengo kigamboni, napiga nae story anasema mwezi wa saba ananunua gari. Naye hajarithi chochote na ni under 26.
Kiukweli sometime miaka tunayotumia kwenye elimu zetu hizi za calculus, zinatucheleweshea maendeleo kutufanya watafuta kazi
yaani kweli jombaaa
 
miaka 23 nyumba 6 magari 5 ila za urithi,.....
 
Kama ulishindwa enzi ya mkwere kwa age hiyo kwa Magu sahau plus ten years Magu akiondoka ndio utamiliki
Mkuu kama umeongea ukweli sana. Maana enzi za JK dili ziliwafanya watu waonekane tajiri sana, hasa vijana wadogo.
 
Ndio tatizo la misukule ya ccm hata kuangalia kwenye website za soko la mitaji hamtaki mnachoweza ni kusaini tuu
Hii tu 2017 mpaka kufika 2019, matusi yatakuzi tu na kadri umri wako unavyozidi ndivyo matusi yatachorwa katika paji la uso wako kwa strss.
Ngoja mkunjwe na Dr. JPM mlizoea kudanganya wachache kwa kelele sasa watanzania wengi wanaona kwa macho kazi zifanywazo na CCM na hivyo wanajua ukweli.
Hapa kazi tu!
Wakuu naomba kuuliza hivi humu jamiiforum kuna kijana yeyote ambaye yupo chini ya miaka 30 ambae anamiliki gari na nyumba.Yani ambae ametafuta kwa jasho lake bila kupewa au kurithi.

Nimeuliza hivi kwa sababu mimi nina miaka 25 na ndoto zangu ni kumiliki gari na nyumba kabla Sijaoa.Lakini kila siku zinavyo sogea naona ndoto inakua ngumu kutimia.

Nikipita barabarani au kwenye kumbi za starehe naona vijana wadogo wamepaki magari yao, basi roho yangu inaumia sana.

Hivi inawezekana kweli au ni ndoto za mchana hizi ninazo ota.
 
25 ni kikongwe sana kwenye achievements ulizozitaja, unatakiwa uwe umeshamiliki bank yenye matawi sio ya nchi hii
REDEEMER [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] we mkuu ni muongo
 
Wakuu naomba kuuliza hivi humu jamiiforum kuna kijana yeyote ambaye yupo chini ya miaka 30 ambae anamiliki gari na nyumba.Yani ambae ametafuta kwa jasho lake bila kupewa au kurithi.

Nimeuliza hivi kwa sababu mimi nina miaka 25 na ndoto zangu ni kumiliki gari na nyumba kabla Sijaoa.Lakini kila siku zinavyo sogea naona ndoto inakua ngumu kutimia.

Nikipita barabarani au kwenye kumbi za starehe naona vijana wadogo wamepaki magari yao, basi roho yangu inaumia sana.

Hivi inawezekana kweli au ni ndoto za mchana hizi ninazo ota.
Webb;
Naona una ndoto nzuri, cha kufanya ni wewe mwenyewe kuwa na kipaombele ktk mipango, nia na malengo yako.
Wapo vijana wengi tena wa kawaida kabisa ktk umri huu even below wanafanya mambo makubwa cha kukumbuka hapa ni kuchapa kazi bila kujali ulivyo, achana na story za vijiweni au tamaa ya vitu usivyoweza kufanya!
 
Nilivyoanza ujasiriamali miaka kadhaa nyuma wakati bado nikiwa mdogo sana, vitu ambavyo vilinimotivate vilikuwa ni Gari kali, kuishi Mbezi Beach, kuvaa nguo kali kali, kupiga misele na Celebrities, kua na mademu wakali... nilivyopata hivyo vyote nikaja kugundua ni utoto tu, jambo ambalo nimelipa kipaumbele ni kujipa na kujipa tena knowledge, nilikuja kugundua kua na knowledge kamwe hautafilisika, nilikuja kugundua network ni jambo la msingi sana sana ili uwe sustainable milele, zaidi ya yote the most powerful thing ni kuwainua wale ambao bado wapo chini...

Boss, wekeza kwenye knowledge, jipe elimu afu jipe tena. Nina 23 yrs, nasukuma luxury car, nasafiri popote duniani bila kuhofia kufilisika, sijajenga bado, lkn siku nikijenga basi nina uhakika itakua ni hekalu fulani... hakuna mtu amewahi kufilisika knowledge!!

Na ukipata usipigie watu kelele... stay humble, usidharau watu, usiite watu kwa miruzi... just remain cool and be cool
Haha mkuu unasukuma lAmborghini nini
 
Kama Upo ndani ya Rat Race hutakuja kumiliki hivyo vitu ndani ya 30. Ila kwa wafanyabiashara ni kwaida. Under. Rat race wengi hujenga wanapofikisha 50s pale wabapopokea za kiinua mgongo.
 
Inawezekana mbona mi 29 nina gari nimenunua 2.5M ila linatembea sana gereji kuliko barabarani na nina chumba na sebule mambo yanawezekana bhn ni uamuz tu
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Nyumba na Gari sio kipimo cha maendeleo...!! Katika uchumi Nyumba na Gari ni liabilities na sio Assets...!! Ukiongelea mafanikio ya kiuchumi ya mtu binafsi ni lzma awe na Assets kama miradi mbalimbali inayokuingizia pesa na sio kutoa pesa mfukoni..!! Unaweza ukawa na nyumba na gari alafu still bado ukawa kapuku...!!

Ukirudi kwenye swali lako....
Inawezekana kupata assets nyingi ukiwa under 25...!! Ila *kama* hukupitia system ya shule( esp. kusoma chuo kikuu ) Wapo waliopitia chuo kikuu wakafanikiwa lkn si wengi kama ambao wana hustle kitaa...!!
 
Njoo 'machimboni' ujionee unaweza kujutia ni kwanini nilienda chuo kusoma mavitu magumu kinoma wakati short cut ya maisha ipo huku! Yaani miaka 22 wewe tayari ni 'fogo' unaye itwa 'mzee' 'mkurugenzi'
Hua nawish kufanya biashara ya madin but sjajua wapi pa kuanzia.Machimbo gan mkuu
 
Wengine wanaandika wanavyo wakati wamenunuliwa na baba/mama zao au kurithishwa.useme unacho kama tu ume-hustle mwenyewe

Does it make a difference.. kwani ukipewa si unakuwa nacho, unadhan ni mchezo kumaintain ?
 
Back
Top Bottom