Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Wakuu naomba kuuliza hivi humu jamiiforum kuna kijana yeyote ambaye yupo chini ya miaka 30 ambae anamiliki gari na nyumba.Yani ambae ametafuta kwa jasho lake bila kupewa au kurithi.

Nimeuliza hivi kwa sababu mimi nina miaka 25 na ndoto zangu ni kumiliki gari na nyumba kabla Sijaoa.Lakini kila siku zinavyo sogea naona ndoto inakua ngumu kutimia.

Nikipita barabarani au kwenye kumbi za starehe naona vijana wadogo wamepaki magari yao, basi roho yangu inaumia sana.

Hivi inawezekana kweli au ni ndoto za mchana hizi ninazo ota.
Ungeuliza 2010..ningekujibu ndio tena mbili +na never giveup
 
5bd7d01739a3b7a83dcc8c3583057fdb.jpg
 
mimi isingekuwa my extended family na shida nyingi hizi, basi hadi kufikia umri huo ningekuwa na gari na nyumba and more Nashukuru Mungu niliwahi kusoma na kupata kazi nzuri katika umri mdogo, nilimaliza my master degree at the age of 24. Nikapata kazi ya kunilipa mshahara mzuri sana at the age of 25, now nina miaka 27. Namshukuru Mungu napata mshahara si haba, nikijibana naweza nunua gari, nikajenga nyumba na nyongeza kabla ya kufikia 30. Lakini doo, mshahara ukitoka tuu unapukutika hatare, Umtumie bi mdashi home, shangazi sijui mjomba nini na nini basi najukuta naendelea kuwa maskini tuu bila kupenda. saivi ndo nipo nawajengea wazazi nyumba, nimalizanane nao ndo nianze kujijenga mimi.
Sikufundishi unyimi, nakwambia nilichofundishwa na mwalimu wangu Prof. Wakuru Magigi, kwa sasa yupo wizara ya kilimo.
Prof alinifundisha hivi; ni bora uwe mnyimi sasa ili uje kuwanufaisha wajao. Kwa story yako ni wazi kuwa kama utaendelea kugawa mshahara wako basi wewe mwenyewe utabaki maskini kwa kutegemea salary na hata hao unaowagawia watabaki maskini, LABDA uwe unawapa mitaji na si pesa ya kujikimu.

Suluhisho; wanyime huku ukijibana kuweka vitega uchumi vyako ambavyo vitakuongezea kipato, ambapo utakuwa na uwezo mzuri wa kusaidia watoto wao vizuri.
 
Mkuu

Wambie wakwambie Vizuri.... Huyo wa World Vision...... Kuna kipindi walipiga sana World Vision-- Hapa lazima alimuibia Mwajiri ndio maana akaacha.

Aisee siri ya Biashara ya Kariakoo nenda usipoambia jioni tukaibe duka fulani au tukamtekee Gogolamboto utaniambia.

Mjeshi alikwenda Sudani au Alipelekwa Somalia..... Man let us be realistic bila kutoa Kafara au kujitoa kafara wewe Mwenyewe asahau... Sijui Umenielewa juu ya Kujitoa Kafara?
Bahati mbaya yoote uliyoongea ni batili.
Wa world vision aliajiriwa, akatengeneza good connection, akaandika mradi ambao ulikuwa funded hivyo yeye akawa ndo Project Manager mshahara juu na posho za safari, malazi, communication.
Kilichofuata ni matumizi mazuri ya pesa, akaanzisha biashara nyingine kwa sababu ni Manager akawa na muda wa kufanya biashara pembeni, biashara ikapanuka, mpaka akaamua kuresign. Hapo umenielewa.

Wa kariakoo acha kwanza nicheke[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] inaonyesha wewe unaona kila aliyefanikiwa basi kapitia wizi, utapeli, rushwa, kurithi, kukata mikono ya albino nk. Ila mi nakwambia kufanikiwa kunategemea na aina ya marafiki zako. Kama 80% ya marafiki zako ni wasifia bia, wewe utaepukaje kuwa mlevi??

Mjeshi hajawahi kupelekwa sudan wala kokote nje ya nchi. Zaidi kujiongeza tu kununua mashamba, bodaboda kadhaa, kununua bidhaa dar na kuituma mikoani.

Again mafanikio ni matumizi mazuri ya pesa hata mshahara ni mwanzo mzuri.
 
Tafuta mtaji ingia kwenye biashara na kilimo nguvu yako yote elekeza huko, utavipata vyote hivyo
 
Inawezekana. Ishu ni kujtambua na kuwa na bidii kwa kla oppotunity ilyoko mbele yako. Ukifuatilia wengne na kuanza kuumia moyo negatively, utatoka kwenye reli na kutumbukia shimoni.
 
Wapo tena wengi cha msingi pambsna b4 45 uwe navyo.........
Very realistic age kwa mtu aliyetoka family ya kawaida na ambaye baada tu ya kupata kibarua tayari ana wajibu wa kusaidia ndugu zake na tena his success ni sababu ya hassle zake mwenyewe....no godfather, nothing.
 
ACHANA NA HUO UJINGA MDOGO WANGU, WEWE TAFTA CASH IN FLOW BAASI. MAMBO YA NYUMBA NA GARI YATAKUJA UKIWA NA VITEGA UCHUMI KIBAAO HAPO HUTAWAZA GARA ZA KAWAIDA UTAWAZA MAGARI YA MAANA NA MIJENGO YA MAANA CHA MUHIMU TAFTA CASH KAKA
 
Kijana huo umri kwa wasomi ....wengi wanakuwa wapo vyuoni....ama ndio kwaaaanza wanakamata ajira zao za kwanza mara baada ya kutoka vyuo...hivyo sio rahisi kumiliki mali hizo....ila kwa wafanyabiashara vijana ambao wengi wao ambao hawakupita kwenye elimu zetu hizi.....form four six ...chuo.....kwa umri huo tayari walikuwa na uwezo wa kumiliki nyumba na gari....pia vile vile vijana ...waliowahi kukaa kwenye vitengo ....TRA kama tax assessors bandarini.....kwenye mabenk vijana wale wa faulo flani hv.....nk..vijana wa umri huo ....wakati wa JK tayari walikuwa na uwezo wa kumiliki hayo mambo....ila sio kwa zama hizi.
 
duh nina 30 ndo najenga now sina gari mmh tunatofautiana sana naomba Mungu nipate gari kabla ya 35
 
inawezekana ila bila kushikwa mkono na ndugu baba mama dada kaka....rafiki, wakiumeb ao wakike. haiwezekani kabisa
 
Bahati mbaya yoote uliyoongea ni batili.
Mkuu, Worldvision ipi aisee, nilikiwa worldvision, Miradi ya Worldvision Tanzania ni wasimamizi tu, Wazungu wanafanya survey na ku-fund miradi Na hakuna mtu aliwahi kupata promotion ya namna hiyo Eti kwa kutengeneza wazo la mradi then akawa project manager huo ni uongo mtupu, muulize vizuri akwambie ukweli, Pia Kwa world vision yaan jamaa wanabana sana Uwe Cluster ama uwe Head office, ni ngumu kufanya Business ya pembeni na kuwa na usimamizi mzuri. Afu design kama huyo jamaa unayemsema nimeshamfahamu kwa nilivyopitia comment zako humu, nikwambie tuu sio ukweli akwambie alichofanya. Kwa wanajeshi na huyo jamaa wako wa kariakoo sijui kwakweli, ila kwa worldvision mmhhh acha kamba bro.
 
Kwa sasa nina 29 naelekea 30 na sina hivyo ingawa nilikuwa na gari nikauza. Lakini kila nikifikiria mistakes ambazo vijana wengi tunafanya kwa ajili ya show off naamini kama tukiwa serious tuna weza kuwa na zaidi ya hivyo kabla ya 30.
 
Mkuu, Worldvision ipi aisee, nilikiwa worldvision, Miradi ya Worldvision Tanzania ni wasimamizi tu, Wazungu wanafanya survey na ku-fund miradi Na hakuna mtu aliwahi kupata promotion ya namna hiyo Eti kwa kutengeneza wazo la mradi then akawa project manager huo ni uongo mtupu, muulize vizuri akwambie ukweli, Pia Kwa world vision yaan jamaa wanabana sana Uwe Cluster ama uwe Head office, ni ngumu kufanya Business ya pembeni na kuwa na usimamizi mzuri. Afu design kama huyo jamaa unayemsema nimeshamfahamu kwa nilivyopitia comment zako humu, nikwambie tuu sio ukweli akwambie alichofanya. Kwa wanajeshi na huyo jamaa wako wa kariakoo sijui kwakweli, ila kwa worldvision mmhhh acha kamba bro.
Hahahaaaa, haya bwana ingawa unasema ulikuwa hukohyko ila nakwambia huyo jamaa aliandika proposal na ikawa funded akiwa ni mwajiriwa wa worldvision. Alifanyaje; tuishie hapo.
Na kwamba wanabana sana, huyo jamaa alikuwa ndo msimamizi wa project, so kuandika nipo field siku tano na kutumia siku tatu, nyingine kwenye biashara ni kawaida.
Sehemu nyingi kwenye private sector (labda muuza duka) wanajali sana umefanya nini, si uwepo wako.
 
Back
Top Bottom