Majibu ya Sayansi kwa swali maarufu la Atheists. Kwanini hakuna uwezekano kwamba ulimwengu ulikwepogi tu milele. Vita kali dhidi ya Atheists Ep4

Majibu ya Sayansi kwa swali maarufu la Atheists. Kwanini hakuna uwezekano kwamba ulimwengu ulikwepogi tu milele. Vita kali dhidi ya Atheists Ep4

Prof Phraoh AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
1,268
Reaction score
2,310
‎Atheists wengi wanaposikia hoja ya Mungu kama Muumba wa ulimwengu wanajibu haraka kwamba "Ulimwengu ulikuwepo milele hauhitaji muumba."

‎Jibu hilo linaonekana rahisi. Linaonekana la akili. Linaonekana kama njia nzuri ya kukimbia swali zito.
‎Lakini ni sayansi sio mimi P h a r a o h sayansi yenyewe inakataa jibu hilo kwa nguvu kubwa.

‎ni sheria ya sayansi kua nishati haiwezi kuundwa wala kuharibiwa inabadilika tu kutoka hali moja kwenda nyingine.

‎Hii inamaanisha nini?

‎Nishati yote iliyopo sasa ilikuwepo tangu mwanzo. inachofanya ni ku badilika tu.

‎Swali linakuja moja kwa moja
‎Nishati hiyo yote ilianza wapi?
‎Kama ulimwengu ni wa milele nishati hiyo ilikuwepo milele. Lakini sheria ya pili inakuja na kulipiga jibu hilo chini kabisa na kuivunja vunja hoja ya atheist kwa ushahidi wa kisayansi

‎Sheria hiyo ya pili inasema ulimwengu unaelekea entropy disorder inayoongezeka siku zote kwenda mbele tu. Kila mchakato wa asili unapoteza nishati inayoweza kutumika.


‎Maana yake kwa lugha rahisi:
‎Kila kitu kinachofanya kazi jua, nyota, nishati yoyote polepole polepole inaisha. Inakwenda. Haiwezi kurudishwa
‎ ( hata jua letu siku moja litaisha )

‎Fikiria mshumaa unaowaka. Unaungua unapotea hauwezi kurudi kuwa mshumaa tena.

‎Vivyo hivyo nyota zinaungua na kutoweka. Nishati inapotea polepole. Ulimwengu unakwenda kuelekea heat death hali ya giza kamili ambapo hakuna nishati, hakuna mwendo, hakuna kitu.

‎Kama ulimwengu ungekuwa wa milele kwa wakati uliopita ungekuwa tayari umefika heat death.
‎Giza kamili. Hakuna nyota. Hakuna nishati. Hakuna chochote.

‎Lakini tuko hapa. Jua linawaka. Nyota zinaungua. Nishati ipo.
‎Hii inamaana moja tu mchakato huu haukuanza milele iliyopita. Ulianza mahali fulani.

‎Mwaka 1927 mwanasayansi Georges Lemaître aligundua kwamba ulimwengu unaendelea kupanuka.
‎Kama unapanuka sasa maana yake awali ulikuwa mdogo. Mdogo zaidi. Mdogo zaidi hadi mahali fulani palipokuwa na mwanzo.
‎Mwaka 1964 Arno Penzias na Robert Wilson wakigundua cosmic microwave background radiation mwangwi wa mlipuko wa mwanzo Big Bang.
‎Ushahidi haukuwa wa dini ulikuwa wa kisayansi kabisa. na walishinda Nobel prize

‎Stephen Hawking atheist na mwanasayansi mkubwa alikubali kwa kusema

"Almost everyone now believes that the universe, and time itself, had a beginning at the Big Bang."

‎Kama vitu vinaweza kuanza kuwepo bila chanzo basi kwa nini vitu vyote visianze kuwepo bila chanzo kila wakati bila mpangilio wowote?
‎Kwa nini tembo wasianze kutokea jikoni kwako sasa hivi bila chanzo?
‎Kama jibu lako ni haiwezekani umekubali vitu haviwezi kuanza from no where

‎Wengine husema basi na Mungu Lazima awe na chanzo hilo swali la ''Mungu alitoka wapi'' lina imagine kwamba Mungu ni kitu cha ndani ya ulimwengu kinachohitaji chanzo kama vitu vingine.
‎Lakini Mungu kwa definition ni Necessary Being kitu ambacho kipo kwa asili yake yenyewe kisichohitaji chanzo kingine.

‎Swali la kweli sio "Mungu alitoka wapi" bali "kwa nini Necessary Being lazima iwe Akili badala ya ulimwengu wa kimaada?"
‎Na jibu ni hili ulimwengu wa kimaada unaonyesha mwanzo Akili Kubwa hainyeshi mwanzo wowote.

‎Arno Penzias aliyegundua mwangwi wa Big Bang ambayo Big bang atheist wengi huitumiankama reference yao bila kujua inawakaba wenyewe

‎Aliyegundua alisema hivi:

"The best data we have are exactly what I would have predicted had I nothing to go on but the five books of Moses"

‎( alisema hana jibu zaidi ya hapo labda atumie Vitabu vitano vya musa (torati) )
 
Labda tu kwa kukusaidia,
Ingia google halafu search "Motivated Reasoning", soma concept yote uielewe vizuri na pia jifunze njia za kucope hiyo situation.

Ukiijua hiyo itakusaidia sana kuziangalia hoja za wachangiaji kwa undani zaidi, na hapo utakuwa umequalify kuingia kwenye mijadala mizito kama hii unayopenda kuianzisha.
 
Labda tu kwa kukusaidia,
Ingia google halafu search "Motivated Reasoning", soma concept yote uielewe vizuri na pia jifunze njia za kucope hiyo situation.

Ukiijua hiyo itakusaidia sana kuziangalia hoja za wachangiaji kwa undani zaidi, na hapo utakuwa umequalify kuingia kwenye mijadala migumu kama hii unayopenda kuianzisha anzisha.
Mijadala hii ipo kimkakati Zaidi
 
Kama Mungu angekuwepo kama mnavyosema. Basi kusingekua na vifo na hata kama vifo vingekuwepo, basi vingekua vya aina moja kama ilivyo kwa sababu za uhai kwa wanyama.

Issue ipo hivi, huenda hivi tunavyoviona ni tone la maji baharini kulinganisha na vilivyopo ambavyo vipo nje ya upeo wa macho yetu. Hebu jiulize. Je, mwisho wa ukomo wako wa kuona ndo ukubwa ulimwengu? Kama sio, je huko kunakoendelea kuna vitu gani vingine?

Umeshawahi kufanya jitihada za kutaka kujua zaidi vilivyo nje ya uwezo wa uono?

Kama hujawahi, basi usiwe na jibu la uhakika kuwa Mungu ndiye muumba
 
Ulimwengu ulianzishwa na Mungu na mwisho wake upo...namaanisha; Ulimwengu sio wa milele?
Quran imeshatueleza kuwa kuna siku Jua litatokea magharibu na baada ya hapo kutatokea kishindo kikubwa sana ambapo dunia itasagika sagika na hapo ndio utakuwa mwisho wa dunia
Kwa waliosoma Physics, wanajua kuwa Jua (Sun), ndio lina shikilia hii solar system; sasa kwa sababu linatoa nguvu inamaan inapungua...hivyo itafika wakati nguvu linayo itoa haitaweza kushika sola system na ndio hapo sayari na nyota kila kimoja kitaenda kivyake vyake na Kugongana baadhi ya sayari na kusagika sagika....
HATA KWA AKILI YA KAWAIDA, HAIWEZEKANI UMUUE MTU AU UMTESE KWA SABABU YA NAFASI AU UWEZO WAKO HALAFU IISHE HIVI HIVI.....LAZIMA KUNA MAHALA ATAPATIWA HAKI YAKE NA NDIO SIKU ZA MALIPO (DAY OF JUDGEMENT)....KAMA UNA AKILI OGOPA SANA HIYO SIKU....ni siku ngumu kuliko ugumu wowote ulio ushuhudia hapa duniani....
 
Back
Top Bottom