Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Hahh na wewe umechoka kufikiria kuhusu chanzo cha ulimwengu kaka?,.. usichoke mwisho wa kufikiria ni either ubongo upate hitilafu au kifo.

Ni kweli mkuu wachache wanaoweza waendelee na harakati, mimi binafsi najoweka pembeni mkuu, naona ni ngumu sana kufahamu bila shaka mwanzo ulikua vipi.

Na kwenye tafiti mimi ni muumini mkubwa sana ws tafiti ila kwenye hili la mwanzo nini , nakupa mfano wa huyu mwamba kupitia hii youtube shorts video

Simple summary yake nimekubaliana nayo

View: https://youtube.com/shorts/bHFjtQHLi5U?si=4pB5-B7xQMsdvAGK
 
Kaka upo sahihi,.. Ila ukweli ni kwamba Binadamu tumepewa sehem ndogo kwenye elimu na kama elimu juu ya chanzo cha ulimwengu (Jinsi ilivyoumbwa) ingekua ndani ya uwezo wetu kufahamu basi mpaka leo naamini kwa jinsi binadamu tulivyopewa uwezo wa kudadisi na kutafuta majibu ya maswali basi huenda mpaka leo tungekua tumepata jibu la swali hilo ambalo naamini kila binadamu aliyezaliwa akiwa na utimamu wa akili anajiuliza,.... so kimsingi mimi nadhani kuna baadhi ya elimu Mwenyezi Mungu aliamua zibaki kwake tu kwa mfano hakutaka kutupa uwezo wa kujua kwamba kwa nini Yeye ana uwezo wa kuwepo pasipo kutegemea uwepo wa kitu kingine chochote (Ilhali Binadamu sisi kutokana na kiwango cha ufahamu wetu ni kwamba ili kitu chochote kiwepo kinahitaji kufanywa au kutengenezwa uwepo wake).

Ndiyo maana hata Qur'an inasema kwamba Binadamu tumepewa sehemu ndogo kwenye ujuzi " وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا......" hivyo kuna vitu kuvijua ni ngumu sana maana inaonekana vipo nje ya uwezo wetu na kadri tunavyojiuliza maswali tunaibua maswali mengine yasiyo na mwisho,.. na ndiyo maana inapaswa tuamini na tukubali (surrender) kwamba baadhi ya vitu vipo nje ya uwezo wetu wa kufikiri...,
 
Ni kweli mkuu wachache wanaoweza waendelee na harakati, mimi binafsi najoweka pembeni mkuu, naona ni ngumu sana kufahamu bila shaka mwanzo ulikua vipi.

Na kwenye tafiti mimi ni muumini mkubwa sana ws tafiti ila kwenye hili la mwanzo nini , nakupa mfano wa huyu mwamba kupitia hii youtube shorts video

Simple summary yake nimekubaliana nayo

View: https://youtube.com/shorts/bHFjtQHLi5U?si=4pB5-B7xQMsdvAGK

Yap jamaa yupo sahihi Sayansi haielezei kila kitu kwenye universe na wala kupitia Sayansi bado hakuna majibu 100% ya Mwanzo ulikuaje na ndiyo maana kwenye Sayansi nadharia zinatumika zaidi kwasababu still mpaka sasa umbali kati yetu na ukweli juu ya jinsi mwanzo ulivyokua hauwezi kupimika......
 
naam mkuu
 
Mimi nina mtizamo tofauti kidogo, Tunaposema kuwa nishati haikuumbwa SI KWELI TUNAKOSEA, Chakula ni kichocheo cha nishati, kuni zinachochea moto ili tupate nishati ILIYOKO NDANI YAKE.
Kwa ufupi mmea una nishati, mwanadamu ana nishati na Mungu ni nishati.
Ukiwa kama nishati unatetema, unatetema katika viwango tofautitofauti mfano 3D,4D na 5D Kutegemeana na mwili wako umepata kichocheo cha uwezo gani mfano: huzuni,furaha,hofu, Mapenzi, uhalisi n.k katika hizi nishati inayokupa mtetemo wa juu zaidi ni uhalisia(Authenticity) ukiwa katika uhalisia wako unakuwa na mtetemo wa hali ya juu sana.

Mkuu mimi naona umechanganya Vyanzo vya Nishati na Nishati yenyewe!
Kuni, Chakula haviumbi nishati bali vinahifadhi nishati ambayo hubadilishwa kutoka njia Moja kwenda nyingine.

Na pia kusema Mungu ni nishati naona kama unachanganya mambo.
Nishati katika fizikia inaelezeka Kwa vigezo vinavyopimika.
Lakini Mungu ni mambo ya kiroho, huwezi kumpima Kwa vigezo vinavyotumika kwenye fizikia.
 
Matter can neither be craeted or destroyed.
 
Hizo tafiti, dadisi na majaribio mbalimbali mpaka leo bado hazijatoa jibu kuhusu chanzo cha ulimwengu,.. na ndiyo maana hata ukijaribu kufikiria mwenyewe akili yako haijui wapi unatoka na wapi unaelekea,.. tumejikuta tupo katikati ya safari mwanzo ni mbali na mwisho pia ni mbali,..
Ndio hakuna jibu mpaka sasa.

Pia dini hazina jibu kuhusu chanzo cha ulimwengu.

Mungu si chanzo cha ulimwengu.
 
Huu mjadala nitahitaji ukae hivi mapema kabisa ili niweze kueleweka kabla sijagusia kitu chochote!.

Maswali mengi tunayojiuliza na hatujapata majibu mpaka sasa juu ya chanzo cha ulimwengu na chanzo chetu!, ni kwasababu kuna kitu ama vitu hatujavijua bado!.
Sina hakika sana kama tutakuja kuvijua ama tusivijue hivyo mijadala ya mabishano juu ya imani za Uungu itaendelea kuwa pambe siku hata siku mpaka pale kanuni kadhaa zitakapokuja kugundulika!.

Nimeamua nianze na hitimisho ili nieleweke kwa wepesi sana!.

Nikianza na nadharia ya uumbaji inakosa majibu maana haionyeshi nani ni wamwisho ambae ameanza kuumba kila kitu!, kwani kanuni hii itamtaka nae alieumba kuumbwa! so haileti tamati ila tu italeta tamati kama kutakuwa na muingiliano wa kanuni yoyote tusiyoifahamu ambayo itakuwa na majibu!.

Mtazamo wa Uungu kwangu mimi binafsi unazidi kudidimia siku baada ya siku haswa nikiangazia mambo kadhaa ambayo yanaleta mkanganyiko aidha juu ya uwepo wake ama nadharia hii inabaki kwenye ombwe lilelile lisiloleta majibu stahiki!.

Nikitazama kati ya hivi vitu vitatu ndio naona ombwe kubwa zaidi na naona imeshinda akili yetu kwasasa (sijui kwa baadae), vitu hivyo ni muda, space (nafasi), nguvu(energy) na akili!.

Ukianza kuzungumzia mwanzo wa ulimwengu ni ngumu sana kuvitenganisha hivyo vitu maana kila kitu kinamuhitaji mwenzake naweza kusema kama ni sarafu basi hiyo ni sarafu yenye pande zote hizo!!!.
Inaonyesha kabisa mpangilio hapa ulimwenguni umekaa ki intelligent yani kunalazimika kuwe na akili ili vitu vienende kama vilivyo!, hapohapo nguvu inaingia kwani akili bila nguvu haiwezi kufanya kazi na nguvu bila akili haiwezi kuenenda ama kukaa kwenye mpangilio na hivi vyote haviwezi kupata muda wakufanya hivyo kama hakuna nafasi(space).

Mpaka hapo inakuwa ni ngumu sana kujua nini kilianza na kilianzaje na hata kama vilianza kwa pamoja basi vilianzaje anzaje sehemu isiyokuwa sehemu na vilitokea wapi sehemu ambapo hakuna sehemu!.
Ama naweza kuiweka hivi "Ni kivipi kitu kitokee sehemu ambapo hakuna sehemu na kwanini..?"

Moja kati ya kitu nilichokuja kugundua kwenye ufahamu wetu ni kuwa "Binadamu mara nyingi huwa tunawaza kile tunachokijua na ndio mara nyingi tunatolea bunifu zetu kwenye hivyohivyo vitu tunavyovijua!, Hivyo kutokana na ugumu huo ndio maana bado tupo kwenye ombwe lakushindwa kuelewa nini chanzo cha ulimwengu!.

Kwasababu gani..?
kwasababu hii hatujui hata kama tunauliza swali sahihi ama sio sahihi (chanzo cha ulimwengu ni nini..?) kwa tafsiri yetu inaweza ikawa ni sahihi maana kwa mazingira tuliyopo yametupelekea kuwaza kuwa kila kitu kuwa na chanzo lakini usikute kwenye kanuni za ulimwengu si lazima kila kitu kiwe na chanzo!, na sasa je kama hakina chanzo basi kina nini..? sasa hili ndio ombwe lenyewe ambalo hatulijui tunabaki tunagaagaa kama kidudu kilichopotea tundu lake!.

Najua ni ngumu kuwaza kitu kisichokuwa na chanzo ama kanuni ambayo haileti chanzo!, kama nilivyoandika hapo juu kuwa akili zetu mara nyingi haziwazi vitu tusivyovijua yani ni ngumu sana kuwaza kitu ambacho huna past nacho!. hata nikikuambia uwaze kuhusu kiumbe hai mpya mwenye kanuni nje na hizi tunazofahamu utajikuta unawaza kiumbe mwenye macho, pua, mdomo n.k yani bado yale mazingira yatakuandama maana ndicho unachokijua!.

Sasa tunafikaje huko tusipopajua..?
Sioni njia nyengine isipokuwa njia ni moja tu "tafiti!". ulimwengu ni kama kitabu ukiamua ukifunue na ukiamua ukifunike!, ila akili ya binadamu huwa haina chakufunika huwa inafunua basi kufunua kitabu huwa ni asili yetu shida ipo kwenye kusoma na kuelewa tu!.

Najua kwa miaka nenda rudi vitu vingi vimegundulika vimezua mijadala na kuibua fikra nyingi na mpya!, na vilevile vimezua imani ila bado havijaleta majibu makuu ya yale tunayoyataka kuyafahamu!, bado kiu hakijakatwa hakuna Mungu ama nadharia yoyote ya Uungu iliyoleta majibu yakujitosheleza juu ya kinagaubaga wa nini chanzo cha ulimwengu...?

Hivyo basi mpaka hapo sitakuwa nachakuongeza ama kupunguza!, ombwe hili ni lilelile isipokuwa nimeona majibu sehemu ambapo hakuna jibu maana penye majibu hapana majibu nafikiri ni wakati wakutazama nje ya box, ahsanteni.
Chanzo halisi cha uumbaji (Muumba) yupo na ili upate uelewa zaidi ni kwa hana mwanzo wala mwisho yupo umilele na sio kama ulivyokaririshwa na philisophy kwamba lazima kuwe na mwanzo na mwisho ila Mungu,miungu ndio wana mwanzo na mwisho.

The real source sasa anishi ndani ya uumbaji wote ndo mana kumekuwa na awakening kubwa sana wakati huu tofauti na majira zilizopita.
 
Chanzo Cha ulimwengu ni kitendawili sana.Ukifikiria kuwa ukubwa wa Dunia hii na vitu vyake vilivyomo,aliyekuwa anaiumba yeye alisimama vip?.Bado na sayari zingine kama Jupiter mars ,mercury,Venus n.k.
 
Thecoder njoo kwenye huu uzi kaka
Andiko kubwa sana hilo mkuu😅😅 na kwakifupi kwa hizi akili zetu za past hatuwezi solve hiyo puzzle.

Akili yetu inaamini kwenye references zaidi so hii inafanya wasomi wengi washindwe kujifunza vitu vipya, kwamfano tafiti nyingi huwa zimekaa zaidi kwenye kurelate na past kisha kutoa conclusion so inapotokea kitu kipya hakuna ambae atakitolea conclusion badala yake wataendelea kukifuatilia huku wakiwa wanaendelea kurelate na tabia ya kitu au vitu fulani fulani ambavyo vilikuwepo hapo past.

Kwahiyo hata procedure ambazo hufanyika kwenye uchunguzi wa vitu vingi ni history ambayo ilikua proved kwa asilimia fulani katika kutoa matokeo chanya ya jambo hilo, so jambo likiwa ni jipya na halina historia yoyote ya kuwahi kuwepo duniani hakuna akili ya kawaida ya mtu yeyote duniani itakayoweza kulitolea ufumbuzi.

Kwahiyo ujanja wetu wote inategemea kale na pasipo na kale hakuna chochote ambacho kinaweza kufanyika na mwanadamu.

Kale hutumika ili kuitabiri future but universe ikibadili tabia zake kidogo watu wote duniani wataanza kulalamika... Chukulia mfano wakulima walivyokariri majira ya Kila mwaka, so wanaenda shamba kwa kufuata ratiba zile zile ila ikitokea universe ikabadilika kidogo au ikakataa kutabirika kwa angalau miaka mitano tu, wote mtakufa njaa😂😂😂.

Listen, kitendo cha kushindwa kuvuta na kutoa hewa wote tunaamini kwamba ni kifo kwakua historia tuliyoikuta imetuamunisha hivyo, na haujawahi kuwa na historia ya tofauti na hapo lakini what if hii historia iko wrong na haikufanyiwa utafiti wowote?...

Unajua wanyama wakali na ambao sio wakali kwa experience ya past ambayo kuna watu wameipata kwa maumivu makali na wakaamua kurithisha historia hiyo kizazi na kizazi.

Mtoto anavyokua huwa anajaribu kila kitu kwakua Hana experience na chochote na hapo watu wanasema bado Hana akili ndio maana anafanya hivyo, lakini kadri anavyokua anapata uzoefu kwa kujifunza kwa maumivu au kuhadithiwa na wale waliomtangulia nae ndio anatofautisha kipi ni kipi... So everything in your brain ni history and once ukaja na kitu kipya kabisa ambacho hakijawahi kuwepo duniani na ukashindwa kuprove basi wasomi wote watakuona wewe ni mwehu, so hakuna namna mnaweza kuyajua mambo hayo kwa akili hizi za past.

Na the bad thing ni kwamba ili universe ikucontrol vizuri ikakuwekea mipaka miwili sayansi na dini.

Sayansi inataka uamini kitu kwa kuthibitisha na kale while dini inakutaka ubaki kwenye upast wako na wala usianze kuacha ubongo wako uelee kwenye hoja nzito za future😅😅😅 mnajikuta mpo mpo tu na ulimwengu unaendelea kuwaamulia Kila kitu mnachotakiwa kufanya na hata mnavyotakiwa kuishi over and over again.
 
Kuna Theory ambayo huwa nahisi itakuwa ni kweli, inatokana na kardshaev scale ya civilization inavyo kuwa advance , na michio kaku kwenye quantum comuputer,

Inasema kwamba huenda ulimwengu sisi wenyewe ndio tumeutengeneza/tutautengeneza, kila jamii inavyozidi kuwa advance kwenye technologia ndio tunakuwa na uwezo wa kufanya vitu vikubwa kama kutengeneza portals kupata vifaa vya kwenda kasi, na ukiongezea na time jinsi livyo huenda tukawa tumetengeneza/tutatengeneza ulimwengu sisi wenyewe kwa msaada wa quantum computer
 
Mkuu mimi naona umechanganya Vyanzo vya Nishati na Nishati yenyewe!
Kuni, Chakula haviumbi nishati bali vinahifadhi nishati ambayo hubadilishwa kutoka njia Moja kwenda nyingine.

Na pia kusema Mungu ni nishati naona kama unachanganya mambo.
Nishati katika fizikia inaelezeka Kwa vigezo vinavyopimika.
Lakini Mungu ni mambo ya kiroho, huwezi kumpima Kwa vigezo vinavyotumika kwenye fizikia.
Kuchochea sio kuumba,
Energy is the fundamental physical property that can be transferred to a physical system to do work, and it exists in various forms, such as potential (stored) and kinetic (motion). A core principle is the law of conservation of energy, which states that energy cannot be created or destroyed but can change from one form to another. Examples of energy include heat, light, chemical, electrical, and nuclear energy, and it powers everything from living organisms to machines and natural processes.

Key Concepts
  • Definition: Energy is the capacity to do work.

  • Conservation: Energy is a conserved quantity; it is transformed, not lost or gained.

    • Forms of Energy:
        • Potential Energy: Stored energy, such as chemical, gravitational, and nuclear energy.
        • Kinetic Energy: Energy in motion, including thermal, light, sound, and electrical energy.
Where Energy Is Found
    • Living Organisms: Energy from food fuels growth, reproduction, and life processes.
    • Machines and Technology: Energy powers devices, lights homes, and drives industrial processes.
    • Natural World: Plants use solar energy, which is then passed through the food chain to animals.
 
Kuna Theory ambayo huwa nahisi itakuwa ni kweli, inatokana na kardshaev scale ya civilization inavyo kuwa advance na michio kaku kwenye quantum comuputer,
Inasema kwamba huenda ulimwengu sisi wenyewe ndio tumeutengeneza/tutautengeneza, kila jamii inavyozidi kuwa advance kwenye technologia ndio tunakuwa na uwezo wa kufanya vitu vikubwa kama kutengeneza portals kupata vifaa vya kwenda kasi, na ukiongezea na time jinsi livyo huenda tukawa tumetengeneza/tutatengeneza ulimwengu sisi wenyewe kwa msaada wa quantum computer
Hii ni kweli kwasababu ni kitu kipo wazi kuanzia hapa na kuendelea sisi ndio tunatengeneza huu ulimwengu but sisi tulitengenezwa na nani na tumetokea wapi? Kwasababu ukisema tumetokea bila chanzo probability ya vyanzo vingi vya aina hii kutokea bila chanzo ingekua kubwa na ukisema kuna chanzo ambacho tumetokea lazima na hiko chanzo kiwe na chanzo so hii inakua ni infinity loop.

Labda tukubali kwamba universe huwa inajianzisha upya Kila baada ya muda fulani kwamba inafuta kizazi hiki na kuanzisha kizazi kingine kwa namna yake yenyewe.😅😅😅.

Kwasababu history inaonesha kwamba kuna uwezekano mkubwa ustaarabu wa kale ulikua more advanced kuliko huu ambao sisi tupo.

So labda Dunia kuna level fulani ya ustaarabu viumbe wakifikia ni labda wanajipoteza wao wenyewe kwa shinikizo la universe kisha viumbe vipya vinaanzishwa na kuanza tena moja.😂😂.

Au inawezekana hii sio universe pekee ambayo ipo ila labda kuna universe nyingine ambayo iko na viumbe walio more powerful than us and labda kinamna fulani wao ndio walianzisha huu ustaarabu kisha wakarudi kwenye universe yao then wanaendelea kutucontrol (something like hizo story za Aliens and blah blah kama hizo).

But vyovyote vile itakavyokua ila Mimi naamini kuna namna universe inatamani sisi tubehave ila kutokana na kelele za dunia tunashindwa that's why kuna nyakati unaweza kupata picha ya mbele ya maisha yako ukiwa umelala (wakati ambao ubongo unakua haukabiliani na kelele yoyote).
 
Ndio hakuna jibu mpaka sasa.

Pia dini hazina jibu kuhusu chanzo cha ulimwengu.

Mungu si chanzo cha ulimwengu.
Huenda usiite Mungu ukaita unavyotaka wewe lakini haiondoi hoja kwamba ujuzi mkubwa sana unahitajika ili kuunda Mifumo mbalimbali tuliyoikuta kwenye ulimwengu,......

Kwa mtazamo wako, Utaita vipi yule/kile kilicho nguvu ya kiakili (the genius mind/force) nyuma ya mpangilio na utaratibu ulioundwa kitaalamu unaoonekana katika huu ulimwengu? Kwa sababu kwa namna ulivyo, ulimwengu hauonekani kuwa umetokea kiholela bila ujuzi mkubwa kutumika......

Kwa mfano inaonyesha akili kubwa sana inahitajika ili kuunda mifumo mbalimbali ya viumbe hai kuanzia upumuaji, mwendo, kuzaliana na kadhalika, mifano haihesabiki,.........
 
Kuna Theory ambayo huwa nahisi itakuwa ni kweli, inatokana na kardshaev scale ya civilization inavyo kuwa advance, na michio kaku kwenye quantum comuputer,

Inasema kwamba huenda ulimwengu sisi wenyewe ndio tumeutengeneza/tutautengeneza, kila jamii inavyozidi kuwa advance kwenye technologia ndio tunakuwa na uwezo wa kufanya vitu vikubwa kama kutengeneza portals kupata vifaa vya kwenda kasi, na ukiongezea na time jinsi livyo huenda tukawa tumetengeneza/tutatengeneza ulimwengu sisi wenyewe kwa msaada wa quantum computer
Hiyo theory haikaribiani kabisa na ukweli,... huwezi ukasema sisi wenyewe ndiyo tumeutengeneza ulimwengu wakati hatujui hata ulimwengu umetokea wapi,.. yaani hatuujui ulimwengu kiundani na uhalisia wake how come tuseme sisi tumeutengeneza?,. na kabla ya kuutengeneza tulikua tunaishi wapi, tulisimamia wapi kuutengeneza ulimwengu....
 
Inakuwa kama timeloop, cause inakuja baada ya effect, kutokana na kuwa advance tuna unlimited free energy, tuna quantum computer, tuna kuwa na god like characteristics hivyo tunagundu namna ya kutengeneza universe ila ili kutengeneza universe unahitaji energy equivalent na ya whole universe hivyo tunatumia hyo energy ku tengeneza universe ila kwenye mchakato tuna destroy universe pia tuna create universe.
Ni crazy idea ila kwenye quantum mechanics inawezekana
 
Back
Top Bottom