Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 21,748
- 46,674
Hichi ulichoongea nacho kina ukweli.shida sio hiyo mkuu shida ni life style!, wapo watu manguli sana wakuwaza kushinda hata hao unaowaona ma genius!, isipokuwa watu hawapo focus na vitu kama hivyo, hivyo wanajikuta wachache wanaoweza kuwaza vitu kama hivyo na kufocus wanafaulu!.
jifikirie mtu anazaliwa system anayokitana nayo ni kuabudu nakuaminishwa maswala ya Mungu wa kwenye vitabu na hapohapo bado anakutana na aina ya maisha ambayo yanamtaka aishi kwa kutafuta fedha nakuwaza mambo yakwawaida tu ya kila siku!.
Angalia hata vyakula tunavyokula ni junk food kila siku kwasababu ya biashara na ndoto za watu zakujipatia fedha!, wala si kula chakula huku ukimakinika nini unatakiwa ule kuongeza nini chenye manufaa kwenye mwili wako!.
Kama ni safari basi bado ni ndefu mno!, kuna vitu unatakiwa uvitoe kichwani mwa watu na hapo utakutana na vita kubwa mno yani binadamu mpaka aje kufikia ustaarabu wa angalau asilimia 50 basi kazi ni kubwa mno!..😅
we mpaka leo watu wanaishi kwa kumpigania Mungu yani kiumbe kilichoumba ulimwengu na kina kila aina ya uwezo nguvu n.k ati kikitukanwa we unakipigania...!! halafu wewe ukivamiwa tu hata na kibaka hakikupiganii unakabwa na unatoa vitu bila tabu!.. sasa hii akili uje uibadili ifikie uelewa na ustaarabu wa walau asilimia 50 basi utakuwa umepiga hatua kubwa mno!. kifupi safari bado ni ndefu maana wanao wa brain wash watu hawataki kuwaachia maana wanapata faida na hao waliokuwa brain washed hawataki kuwaza nje ya box watoke humo!.
Binafsi huwa nikiangalia dunia na mifumo yake huwa nashindwa kuelewa kwanini binadamu tuna akili kuliko wanyama ila hazitusaidii kuwa tofauti na wanyama linapokuja suala la mfumo wa kutuwezesha kufahamu maisha ni nini.
Tumejiwekea mipaka na matabaka ya kufikiri kwa jina la uchumi, tukajibana kimaeneo na kuyapa majina kuwa hii ni nchi na tukabuni mtindo wa kuishi tukauita siasa na kutengenezea mifumo ya ulinzi dhidi ya binadamu.