Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

MIPAKA YA MAARIFA YA BINADAMU: KATI YA KINACHOGUNDULIKA NA KISICHOGUNDULIKA

Binadamu ameendelea kufanya ugunduzi mkubwa kuhusu ulimwengu anaouishi. Kupitia sayansi, teknolojia, falsafa na dini, tumeweza kuelewa kwa sehemu baadhi ya siri za asili, maisha, na mazingira yanayotuzunguka. Hata hivyo, pamoja na maendeleo hayo, bado kuna maswali ambayo yanabaki bila majibu ya moja kwa moja – maswali yanayogusa mipaka ya uwezo wetu wa kufikiri na kugundua.

Kwa mtazamo wangu, kuna pande mbili za uhalisia: upande wa kwanza ni ule ambao uko ndani ya uwezo wa binadamu – eneo ambalo linaweza kufikiwa na akili, utafiti, na teknolojia. Hapa ndipo tunajifunza kuhusu sayari, molekuli, historia ya maisha, na kanuni za fizikia. Ni upande wa kugundua, kuuliza na kujibu.

Lakini pia kuna upande wa pili, ambao uko nje ya uwezo wa binadamu. Huu ni ule upande ambao hata tukijitahidi kwa kiwango gani, hatuwezi kuufikia. Ni katika upande huu tunakutana na maswali kama:
  • Mungu ni nani na alitokea wapi?
  • Je, kuna mwisho wa anga au wakati?
  • Ulimwengu ulianza lini, na nini kilikuwepo kabla yake?
  • Je, kuna viumbe au nguvu zisizoonekana ambazo zinaweza kushawishi au kuelekeza maisha yetu bila sisi kufahamu?

Maswali haya hayajibiwi kwa miongozo ya maabara wala vitabu vya hisabati – bali kwa tafakuri, imani, na falsafa. Wapo wanaoamini kuwa kuna uwepo mkubwa, nguvu au viumbe walioko nje ya ulimwengu wetu wa kawaida, ambao wanaweza kuwa na uwezo wa kuona, kuelewa au hata kuathiri binadamu – bila sisi kufahamu.

Hili linatufikisha kwenye ukweli mmoja muhimu: maarifa ya binadamu yana mipaka. Tunaweza kugundua mengi, lakini si yote. Kwa hivyo, tunapaswa kuendeleza udadisi, lakini pia tuwe na unyenyekevu wa kukubali kuwa si kila kitu kinaweza kueleweka na akili ya kibinadamu.

Kwa kumalizia, dunia na uhalisia unaotuzunguka ni mkubwa sana. Kuna mambo ambayo tunaweza kuyafahamu kwa juhudi, lakini kuna mambo ambayo yataendelea kubaki kuwa siri. Na katika safari hiyo ya kutafuta maarifa, maswali ndiyo taa yetu – hata pale majibu yanapokosekana.
 
Kaka upo sahihi,.. Ila ukweli ni kwamba Binadamu tumepewa sehem ndogo kwenye elimu na kama elimu juu ya chanzo cha ulimwengu (Jinsi ilivyoumbwa) ingekua ndani ya uwezo wetu kufahamu basi mpaka leo naamini kwa jinsi binadamu tulivyopewa uwezo wa kudadisi na kutafuta majibu ya maswali basi huenda mpaka leo tungekua tumepata jibu la swali hilo ambalo naamini kila binadamu aliyezaliwa akiwa na utimamu wa akili anajiuliza,.... so kimsingi mimi nadhani kuna baadhi ya elimu Mwenyezi Mungu aliamua zibaki kwake tu kwa mfano hakutaka kutupa uwezo wa kujua kwamba kwa nini Yeye ana uwezo wa kuwepo pasipo kutegemea uwepo wa kitu kingine chochote (Ilhali Binadamu sisi kutokana na kiwango cha ufahamu wetu ni kwamba ili kitu chochote kiwepo kinahitaji kufanywa au kutengenezwa uwepo wake).

Ndiyo maana hata Qur'an inasema kwamba Binadamu tumepewa sehemu ndogo kwenye ujuzi " وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا......" hivyo kuna vitu kuvijua ni ngumu sana maana inaonekana vipo nje ya uwezo wetu na kadri tunavyojiuliza maswali tunaibua maswali mengine yasiyo na mwisho,.. na ndiyo maana inapaswa tuamini na tukubali (surrender) kwamba baadhi ya vitu vipo nje ya uwezo wetu wa kufikiri...,
Tatizo mtu asiyejua nyuma ya ukuta kuna nini anataka kujua ulimwengu ulianzaje na kujua elimu ambayo ni kubwa sana wala kichwa chake hakiwezi kuhimili kuelewa chochote.
 
Huenda usiite Mungu ukaita unavyotaka wewe lakini haiondoi hoja kwamba ujuzi mkubwa sana unahitajika ili kuunda Mifumo mbalimbali tuliyoikuta kwenye ulimwengu,......

Kwa mtazamo wako, Utaita vipi yule/kile kilicho nguvu ya kiakili (the genius mind/force) nyuma ya mpangilio na utaratibu ulioundwa kitaalamu unaoonekana katika huu ulimwengu? Kwa sababu kwa namna ulivyo, ulimwengu hauonekani kuwa umetokea kiholela bila ujuzi mkubwa kutumika......

Kwa mfano inaonyesha akili kubwa sana inahitajika ili kuunda mifumo mbalimbali ya viumbe hai kuanzia upumuaji, mwendo, kuzaliana na kadhalika, mifano haihesabiki,.........
Kama ulimwengu lazima uwe umeundwa na "ujuzi fulani" Hata huo ujuzi uliounda ulimwengu hauwezi kuwepo tu from nothing.

Ujuzi huo na wenyewe utahitaji kuundwa na ujuzi mwingine. Hivyo kutakuwa na msururu mrefu wa "ujuzi" mwingi usio na mwisho.
 
Hapa hujakataa kwamba ujuzi/utaalamu unahitajika ili kufanya mifumo ya universe iweze ku operate hivi tulivyoikuta,... si ndio?

Twende taratibu.
 
Ndio hakuna jibu mpaka sasa.

Pia dini hazina jibu kuhusu chanzo cha ulimwengu.

Mungu si chanzo cha ulimwengu.
Mkuu hii kauli yako ya mwisho inawalakini!, na ukisema Mungu si chanzo cha ulimwengu maana yake wewe umeshahikikisha ulimwengu mzima na umethibitisha kuwa yeye si chanzo cha ulimwengu!.. sidhani kama unahakika na usemi wako alasivyo uwe na maana nyengine!.
Ukweli ni huu mpaka sasa binadamu hatujui kuhusu chanzo cha ulimwengu hatujui kama ni Mungu ama si mungu hatujui chanzo chochote juu ya hili swala!.
 
Chanzo halisi cha uumbaji (Muumba) yupo na ili upate uelewa zaidi ni kwa hana mwanzo wala mwisho yupo umilele na sio kama ulivyokaririshwa na philisophy kwamba lazima kuwe na mwanzo na mwisho ila Mungu,miungu ndio wana mwanzo na mwisho.

The real source sasa anishi ndani ya uumbaji wote ndo mana kumekuwa na awakening kubwa sana wakati huu tofauti na majira zilizopita.
Nipe uthibitisho ndugu kuanzia kukaririshwa kwangu na wanafalsafa, pili nipe uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu muumba asie na mwanzo wala mwisho!, Tatu itakuwa vyema sana kunielimisha juu ya nadharia ya kitu kutokuwa na mwanzo na mwisho!.
 
Hii ni kweli kwasababu ni kitu kipo wazi kuanzia hapa na kuendelea sisi ndio tunatengeneza huu ulimwengu but sisi tulitengenezwa na nani na tumetokea wapi? Kwasababu ukisema tumetokea bila chanzo probability ya vyanzo vingi vya aina hii kutokea bila chanzo ingekua kubwa na ukisema kuna chanzo ambacho tumetokea lazima na hiko chanzo kiwe na chanzo so hii inakua ni infinity loop.

Labda tukubali kwamba universe huwa inajianzisha upya Kila baada ya muda fulani kwamba inafuta kizazi hiki na kuanzisha kizazi kingine kwa namna yake yenyewe.😅😅😅.

Kwasababu history inaonesha kwamba kuna uwezekano mkubwa ustaarabu wa kale ulikua more advanced kuliko huu ambao sisi tupo.

So labda Dunia kuna level fulani ya ustaarabu viumbe wakifikia ni labda wanajipoteza wao wenyewe kwa shinikizo la universe kisha viumbe vipya vinaanzishwa na kuanza tena moja.😂😂.

Au inawezekana hii sio universe pekee ambayo ipo ila labda kuna universe nyingine ambayo iko na viumbe walio more powerful than us and labda kinamna fulani wao ndio walianzisha huu ustaarabu kisha wakarudi kwenye universe yao then wanaendelea kutucontrol (something like hizo story za Aliens and blah blah kama hizo).

But vyovyote vile itakavyokua ila Mimi naamini kuna namna universe inatamani sisi tubehave ila kutokana na kelele za dunia tunashindwa that's why kuna nyakati unaweza kupata picha ya mbele ya maisha yako ukiwa umelala (wakati ambao ubongo unakua haukabiliani na kelele yoyote).
Nafikiri kuna kanuni hatujazijua bado zinavyofanya kazi na ndio maana inakuwa ngumu kujua chanzo chetu, lengo na dhima yote ya ulimwengu!.

Muda mwengine huwa nahisi bado hata lugha ya ulimwengu hatujaielewa so tunatafsiri vitu kutokana na matakwa yetu, hisia zetu na weledi wetu!.
lugha mama ya ulimwengu huenda ikawa na majibu ila hatujui kuitafsiri!.
 
(not debating, just leaving this here)

Fuata Historia utaujua mwanzo wa ulimwengu. Clear written history is available, the Lord made sure its written!

Vitabu vya Injili (Gospels) zinarekodi mababu wa YESU hadi binadamu wa kwanza.

Agano la kale ina rekodi hiyo hiyo ya kizazi cha YESU.

YESU
kaitwa mwanga wa ulimwemgu for a reason. Unatapatapa kwanini, the light is there, very clear.

Biblia ni kitabu cha historia.
 
Nafikiri kuna kanuni hatujazijua bado zinavyofanya kazi na ndio maana inakuwa ngumu kujua chanzo chetu, lengo na dhima yote ya ulimwengu!.

Muda mwengine huwa nahisi bado hata lugha ya ulimwengu hatujaielewa so tunatafsiri vitu kutokana na matakwa yetu, hisia zetu na weledi wetu!.
lugha mama ya ulimwengu huenda ikawa na majibu ila hatujui kuitafsiri!.
Wanasema lugha ya ulimwengu ni frequencey
 
Leo ni mwaka 2025.

Mwaka 2025 baada ya kuumbwa kwa ulimwengu?

Hapana.

Mwaka 2025 baada ya kuzaliwa kwa Bwana YESU..

Hujiulizi
?
 
Nafikiri kuna kanuni hatujazijua bado zinavyofanya kazi na ndio maana inakuwa ngumu kujua chanzo chetu, lengo na dhima yote ya ulimwengu!.

Muda mwengine huwa nahisi bado hata lugha ya ulimwengu hatujaielewa so tunatafsiri vitu kutokana na matakwa yetu, hisia zetu na weledi wetu!.
lugha mama ya ulimwengu huenda ikawa na majibu ila hatujui kuitafsiri!.
Uko sahihi, kuna vitu vingi sana hatuvijui ila tumeridhika kwakua dunia haifanyi mabadiliko yake kwa haraka that's why ni almost constant.

But usikute kuna commands nyingi ambazo pengine tungezijua tungeiendesha Dunia kwa namna tunavyotaka sisi ila kwakua hatuzijui basi tumeishia kuendeshwa na yenyewe.

All in all huwa napenda unavyowaza nje ya box, hii inaonesha ni kwa jinsi gani huko mbele mawazo ya namna hii yanaweza kugongana baina ya mtu na mtu kitu kitakachopelekea watu wengi waweze kubadili mitazamo na pengine hapo ndio mwanzo wa maarifa mapya utakapoibuka.
 
kutokana na kujirudia au kuwepo kwa alama zinazojirudia, mfano vitu vingi huwa mfumo wa namba za fibonacci na golden ratio 1,2,3,5,8,13
Hivi vyote ni vitu ambavyo tumevikuta duniani what if hii pia ni sehemu ya mpango wa ulimwengu kutupumbaza...

Kwasababu hizo 1,2,3,5,8,13 zinaweza zisiwe moja, mbili, tatu, tano, nane, kumi na tatu kama tunavyoamini😅😅
 
Huu mjadala nitahitaji ukae hivi mapema kabisa ili niweze kueleweka kabla sijagusia kitu chochote!.

Maswali mengi tunayojiuliza na hatujapata majibu mpaka sasa juu ya chanzo cha ulimwengu na chanzo chetu!, ni kwasababu kuna kitu ama vitu hatujavijua bado!.
Sina hakika sana kama tutakuja kuvijua ama tusivijue hivyo mijadala ya mabishano juu ya imani za Uungu itaendelea kuwa pambe siku hata siku mpaka pale kanuni kadhaa zitakapokuja kugundulika!.

Nimeamua nianze na hitimisho ili nieleweke kwa wepesi sana!.

Nikianza na nadharia ya uumbaji inakosa majibu maana haionyeshi nani ni wamwisho ambae ameanza kuumba kila kitu!, kwani kanuni hii itamtaka nae alieumba kuumbwa! so haileti tamati ila tu italeta tamati kama kutakuwa na muingiliano wa kanuni yoyote tusiyoifahamu ambayo itakuwa na majibu!.

Mtazamo wa Uungu kwangu mimi binafsi unazidi kudidimia siku baada ya siku haswa nikiangazia mambo kadhaa ambayo yanaleta mkanganyiko aidha juu ya uwepo wake ama nadharia hii inabaki kwenye ombwe lilelile lisiloleta majibu stahiki!.

Nikitazama kati ya hivi vitu vitatu ndio naona ombwe kubwa zaidi na naona imeshinda akili yetu kwasasa (sijui kwa baadae), vitu hivyo ni muda, space (nafasi), nguvu(energy) na akili!.

Ukianza kuzungumzia mwanzo wa ulimwengu ni ngumu sana kuvitenganisha hivyo vitu maana kila kitu kinamuhitaji mwenzake naweza kusema kama ni sarafu basi hiyo ni sarafu yenye pande zote hizo!!!.
Inaonyesha kabisa mpangilio hapa ulimwenguni umekaa ki intelligent yani kunalazimika kuwe na akili ili vitu vienende kama vilivyo!, hapohapo nguvu inaingia kwani akili bila nguvu haiwezi kufanya kazi na nguvu bila akili haiwezi kuenenda ama kukaa kwenye mpangilio na hivi vyote haviwezi kupata muda wakufanya hivyo kama hakuna nafasi(space).

Mpaka hapo inakuwa ni ngumu sana kujua nini kilianza na kilianzaje na hata kama vilianza kwa pamoja basi vilianzaje anzaje sehemu isiyokuwa sehemu na vilitokea wapi sehemu ambapo hakuna sehemu!.
Ama naweza kuiweka hivi "Ni kivipi kitu kitokee sehemu ambapo hakuna sehemu na kwanini..?"

Moja kati ya kitu nilichokuja kugundua kwenye ufahamu wetu ni kuwa "Binadamu mara nyingi huwa tunawaza kile tunachokijua na ndio mara nyingi tunatolea bunifu zetu kwenye hivyohivyo vitu tunavyovijua!, Hivyo kutokana na ugumu huo ndio maana bado tupo kwenye ombwe lakushindwa kuelewa nini chanzo cha ulimwengu!.

Kwasababu gani..?
kwasababu hii hatujui hata kama tunauliza swali sahihi ama sio sahihi (chanzo cha ulimwengu ni nini..?) kwa tafsiri yetu inaweza ikawa ni sahihi maana kwa mazingira tuliyopo yametupelekea kuwaza kuwa kila kitu kuwa na chanzo lakini usikute kwenye kanuni za ulimwengu si lazima kila kitu kiwe na chanzo!, na sasa je kama hakina chanzo basi kina nini..? sasa hili ndio ombwe lenyewe ambalo hatulijui tunabaki tunagaagaa kama kidudu kilichopotea tundu lake!.

Najua ni ngumu kuwaza kitu kisichokuwa na chanzo ama kanuni ambayo haileti chanzo!, kama nilivyoandika hapo juu kuwa akili zetu mara nyingi haziwazi vitu tusivyovijua yani ni ngumu sana kuwaza kitu ambacho huna past nacho!. hata nikikuambia uwaze kuhusu kiumbe hai mpya mwenye kanuni nje na hizi tunazofahamu utajikuta unawaza kiumbe mwenye macho, pua, mdomo n.k yani bado yale mazingira yatakuandama maana ndicho unachokijua!.

Sasa tunafikaje huko tusipopajua..?
Sioni njia nyengine isipokuwa njia ni moja tu "tafiti!". ulimwengu ni kama kitabu ukiamua ukifunue na ukiamua ukifunike!, ila akili ya binadamu huwa haina chakufunika huwa inafunua basi kufunua kitabu huwa ni asili yetu shida ipo kwenye kusoma na kuelewa tu!.

Najua kwa miaka nenda rudi vitu vingi vimegundulika vimezua mijadala na kuibua fikra nyingi na mpya!, na vilevile vimezua imani ila bado havijaleta majibu makuu ya yale tunayoyataka kuyafahamu!, bado kiu hakijakatwa hakuna Mungu ama nadharia yoyote ya Uungu iliyoleta majibu yakujitosheleza juu ya kinagaubaga wa nini chanzo cha ulimwengu...?

Hivyo basi mpaka hapo sitakuwa nachakuongeza ama kupunguza!, ombwe hili ni lilelile isipokuwa nimeona majibu sehemu ambapo hakuna jibu maana penye majibu hapana majibu nafikiri ni wakati wakutazama nje ya box, ahsanteni.
Nadhani siku binadamu akigundua sayansi ya kifo mambo mengi yatakuwa wazi. Imagine akili kubwa zilizogundua bila rejea zisingekufa, leo zingekuja na theory gani na hii tech iliyopo. Japo bado wanazaliwa wanasayansi mahiri ila kupoteza akili kubwa zisizohitaji rejea kugundua na kurithisha akili ndogo zinazohitaji rejea ili zikariri na kuendeleza kazi za akili kubwa ndo kunachelewesha mambo.
 
Uko sahihi, kuna vitu vingi sana hatuvijui ila tumeridhika kwakua dunia haifanyi mabadiliko yake kwa haraka that's why ni almost constant.

But usikute kuna commands nyingi ambazo pengine tungezijua tungeiendesha Dunia kwa namna tunavyotaka sisi ila kwakua hatuzijui basi tumeishia kuendeshwa na yenyewe.

All in all huwa napenda unavyowaza nje ya box, hii inaonesha ni kwa jinsi gani huko mbele mawazo ya namna hii yanaweza kugongana baina ya mtu na mtu kitu kitakachopelekea watu wengi waweze kubadili mitazamo na pengine hapo ndio mwanzo wa maarifa mapya utakapoibuka.
Watu hudharau vitu vidogo nakuona havina majibu lakini ukija ukakaa chini ukafikiria unaweza kushangaa sana!, moja kati ya kitu ambacho tumekizoea na tuankichukulia easy lakini kwangu mimi naonaga kama ni kitu cha ajabu ni "space!" nashangaa jinsi ilivyo inavyoweza kupitisha mawimbi ya kila namna halafu kitu kinachoniwazisha zaidi ni ukitoa space unabaki na nini..?😅
Hichi kitu huwa kinanifanya muda mwengine niwaze huenda tunauliza maswali ambayo si sahihi!.. lakini bado hatujui kama ni sahihi ama si sahihi na ndio maana nikahitimisha kuwa lazima tujikite kwenye tafiti binadamu hatuna asili ya kukaa nakutulia tu lazima tujue kwenye hichi chungu kuna nini...???

Ni watu wachache tu hawajabadili mitazamo wanaweza kuona unahoji mambo yakipuuzi!, lakini hakuja ujuzi unakuja bila kuhoji na tafiti!. Maisha/uhai ni sanaa na ni sayansi pia itategemea utajivika vazi lipi kati ya hayo!.

By the way mfano nawashangaa sana watu wanaoshangaa namna gravity inavyofanya kazi kwenye dunia yetu nakuona ni kama longolongo nakuanza kusema dunia ni flat..!!! ila hivyo viumbe sikuhizi sitaki kubishana navyo ila wanatakiwa wajifunze kuhusu space ilivyo inavyo behave n.k basi hawatakuja kuona tabu kuelewa kuwa dunia ni duara!.
 
Nadhani siku binadamu akigundua sayansi ya kifo mambo mengi yatakuwa wazi. Imagine akili kubwa zilizogundua bila rejea zisingekufa, leo zingekuja na theory gani na hii tech iliyopo. Japo bado wanazaliwa wanasayansi mahiri ila kupoteza akili kubwa zisizohitaji rejea kugundua na kurithisha akili ndogo zinazohitaji rejea ili zikariri na kuendeleza kazi za akili kubwa ndo kunachelewesha mambo.
shida sio hiyo mkuu shida ni life style!, wapo watu manguli sana wakuwaza kushinda hata hao unaowaona ma genius!, isipokuwa watu hawapo focus na vitu kama hivyo, hivyo wanajikuta wachache wanaoweza kuwaza vitu kama hivyo na kufocus wanafaulu!.
jifikirie mtu anazaliwa system anayokitana nayo ni kuabudu nakuaminishwa maswala ya Mungu wa kwenye vitabu na hapohapo bado anakutana na aina ya maisha ambayo yanamtaka aishi kwa kutafuta fedha nakuwaza mambo yakwawaida tu ya kila siku!.

Angalia hata vyakula tunavyokula ni junk food kila siku kwasababu ya biashara na ndoto za watu zakujipatia fedha!, wala si kula chakula huku ukimakinika nini unatakiwa ule kuongeza nini chenye manufaa kwenye mwili wako!.
Kama ni safari basi bado ni ndefu mno!, kuna vitu unatakiwa uvitoe kichwani mwa watu na hapo utakutana na vita kubwa mno yani binadamu mpaka aje kufikia ustaarabu wa angalau asilimia 50 basi kazi ni kubwa mno!..😅
we mpaka leo watu wanaishi kwa kumpigania Mungu yani kiumbe kilichoumba ulimwengu na kina kila aina ya uwezo nguvu n.k ati kikitukanwa we unakipigania...!! halafu wewe ukivamiwa tu hata na kibaka hakikupiganii unakabwa na unatoa vitu bila tabu!.. sasa hii akili uje uibadili ifikie uelewa na ustaarabu wa walau asilimia 50 basi utakuwa umepiga hatua kubwa mno!. kifupi safari bado ni ndefu maana wanao wa brain wash watu hawataki kuwaachia maana wanapata faida na hao waliokuwa brain washed hawataki kuwaza nje ya box watoke humo!.
 
Watu hudharau vitu vidogo nakuona havina majibu lakini ukija ukakaa chini ukafikiria unaweza kushangaa sana!, moja kati ya kitu ambacho tumekizoea na tuankichukulia easy lakini kwangu mimi naonaga kama ni kitu cha ajabu ni "space!" nashangaa jinsi ilivyo inavyoweza kupitisha mawimbi ya kila namna halafu kitu kinachoniwazisha zaidi ni ukitoa space unabaki na nini..?😅
Hichi kitu huwa kinanifanya muda mwengine niwaze huenda tunauliza maswali ambayo si sahihi!.. lakini bado hatujui kama ni sahihi ama si sahihi na ndio maana nikahitimisha kuwa lazima tujikite kwenye tafiti binadamu hatuna asili ya kukaa nakutulia tu lazima tujue kwenye hichi chungu kuna nini...???

Ni watu wachache tu hawajabadili mitazamo wanaweza kuona unahoji mambo yakipuuzi!, lakini hakuja ujuzi unakuja bila kuhoji na tafiti!. Maisha/uhai ni sanaa na ni sayansi pia itategemea utajivika vazi lipi kati ya hayo!.

By the way mfano nawashangaa sana watu wanaoshangaa namna gravity inavyofanya kazi kwenye dunia yetu nakuona ni kama longolongo nakuanza kusema dunia ni flat..!!! ila hivyo viumbe sikuhizi sitaki kubishana navyo ila wanatakiwa wajifunze kuhusu space ilivyo inavyo behave n.k basi hawatakuja kuona tabu kuelewa kuwa dunia ni duara!.
Ndio hivyo mkuu, Dunia iko na mambo mengi ya kustaajabisha...

Shida ya tafiti pia zinategemea ulimwengu utoe majibu na ikitokea umegoma kutoa majibu basi hiyo tafiti haitakua na ukomo na mwishowe itaishia njiani.

Kwasababu ukiangalia tafiti nyingi ambazo zimeleta majibu ni zile ambazo Zina mfanano na kale au zile ambazo ziko na tabia fulani za kujirudia rudia katika mpangilio fulani ambao unaeleweka kinyume na hapo huwa ni ngumu kupata majibu na hapa ndio huwa Mimi nasema ulimwengu umegoma kutoa majibu.

Kwahiyo ukitulia vizuri unaweza kusema ulimwengu umejiwekea mipaka yake ambayo hairuhusu mtu yeyote kuifikia na zile sehemu ambazo tunaweza kuzifikia ni kwakua ulimwengu wenyewe uliamua hivyo.

Ndio maana hata hizi revolutions zinazotoa huwa hazitokei tu bali zinatokea kwa nyakati, now tupo kwenye hii zama ya AI ambazo hizi kimsingi ni product ya programming languages ambazo ukirudi nyuma kufuatilia namna hizi language zilitokea unaweza kujikuta unapata infinity loop nyingine.

Kuna kitu hakipo sawa...
 
The Bible says in the beginning there Lord created the heavens and the earth.

Science says the Universe had a beginning.

Endeleeni kutapatapa.

PS: Science is a tool to discover the Lord's creation. Beware "science" has turned into politics.

For us laymen its not what "science" says anymore its "who" said it. You'll be surprised how much deception is spread to the masses as scientic facts.

Back
Top Bottom