Kuna nini Hospitali ya Kairuki?

Kuna nini Hospitali ya Kairuki?


Sidhani kama kuna sehemu/hospitali walio wakamilifu. Kitu cha msingi ni kutenda kazi kwa kadiri ya uwezo wetu na kuzingatia misingi ya maadili.

Kufanikiwa kwa upasuaji kunategemea mambo mengi ikiwemo ustadi wa daktari, kiwango cha ugonjwa, afya ya mgonjwa kwa ujumla, nk.

Hivyo, wakati tunalaumu upande mmoja tufanye tathmini ya upande wa pili kabla ya kurukia kwenye hitimisho.
 
Naomba nikupinge mkuu, mama mjamzito anapopata kifafa cha mimba njia ya kubwa ya kumfanya asipoteze uhai ni mtt kuzaliwa. So mama akiwa kwenye iyo hali lzm afanyiwe operation sababu anakua hawezi kupush...nikiwa kama mhanga wa kifafa cha mimba waliwai kunifanyia operation nikawa salama mimi na mtoto

Mgonjwa wangu mtoto alishafia tumboni, lakini wao wakanificha na kuforce operation nikakataa, nikamhamishia muhimbili ambako walikataa kumfanyia operation kwa kigezo cha kumtia mama ubovu wakati mtoto keshafariki, alipewa dawa za uchungu na akajifungua kawaida na akapona wenzangu waliokubali operation walipoteza wapendwa wao
 
Jambo usililijua ni sawa na usiku wa giza but kuna siri kubwa sana ndani yake.
ILI KUJIFUNZA NI LAZIMA UFUNGUE NA ILI UFUNGUE NI LAZIMA UJIFUNZE
Kwa walio nielewa hongera na kwa wasio nielewa poleni.
Karibuni tusome kairuki kwa vitendo
 
kuna ukweli hapa ingawaje unapingwa kwa nguvu nyingi. MTU hawezi tu kurupuka akaandika lazima yamemfika. Njia pekee ya kumpinga mleta mada ni kufanya mabadiliko
 
Kimsingi mimi kilichonitisha na kuniacha na maswali mengi kwanza ilikuwa ni gharama ambayo ni 1.5m per operation pili ni ule ushawishi na usumbufu niliopata toka kwa yule doctor, akinipa pressure isiyoisha nitoe uamuzi wa mgonjwa kupasuliwa..! Udadisi wangu ukaniongoza kujua kitu kibaya kabisa kwamba operations za pale ni chanzo kikuu cha mapato kwa madokta manesi na wahudumu wao na vilevile ni sehemu ya practical kwa wanafunzi wao
Operation moja doctor anaondoka na kati ya laki 3-5 na kwakuwa wengi ni partime hivyo hufanya namna za kuforce operations ili watunishe mifuko yao, maadili ya kazi yamewekwa kwenye kaburi la sahau
 
Majuzi nlikua hosp ya tmj kukawa na taarifa za msiba wa dakt bingwa mmojawapo hapo tmj ambae alienda mufanyiwa operation kwa dkt kairuki.wanasema alienda mzima kabsa tena anadrive mwenyewe akiwa na familiya yake...baada ya operation the next day alifariki dunia.hii nimeikuta juzi tu nlikua hapo tmj hospitali
 
Mgonjwa wangu mtoto alishafia tumboni, lakini wao wakanificha na kuforce operation nikakataa, nikamhamishia muhimbili ambako walikataa kumfanyia operation kwa kigezo cha kumtia mama ubovu wakati mtoto keshafariki, alipewa dawa za uchungu na akajifungua kawaida na akapona wenzangu waliokubali operation walipoteza wapendwa wao

Mtoto akishafia tumboni njia bora ni vaginal delivery ila kama mtoto ni mkubwa au amekaa vibaya operation inaweza fanyika pia
 
Jamani nimempeleka mke wangu pale, anasubiri upasuaji, mbona mnataka kuniua abaki mgonjwa
 
Mtoto akishafia tumboni njia bora ni vaginal delivery ila kama mtoto ni mkubwa au amekaa vibaya operation inaweza fanyika pia

Kesi yangu ilikuwa tofauti kidogo, yule daktari alikuwa kaniaminisha kuwa mtoto yuko hai kwahiyo nisihofu wakati kiuhalisia alikuwa keshafariki, alituomba tununue na nguo kabisa na tulifanya hivyo kweli
 
Nilishawahu kulalamika hapa kuhusu kitengo cha meno na dr. yule wakichaga.....watu wakapuuzia sasa leo inakuja hii kali zaidi..
 
Kwenye operation vingi vinachangia pengine maandalizi si mazuri au operation yenyewe haifanyiki kwa uangalivu room haiko sterile vyakutosha na huduma anayopewa mgonjwa baada ya opp vinachangia sana kufa kwa mgonjwa au kupata maambukizi mengine
 
Hii nillipata toka kwa jamaa yangu aliyekuwa akifundisha pale chuoni; wanafunzi wakifeli sana somo lako unawekwa chini na uongozi wa chuo ili mambo yaende sawa na wanafunzi wafaulu. Nikajiuliza, sasa kama wanafunzi wa udaktari wanafanyiwa mishe ili wafaulu mitihani yao, kutakuwa na usalama kweli kwa wagonjwa watakaokuwa wanawatibu pindi watakapokuwa madaktari?
Nadhani mchanganyiko huu wa biashara (kwa asilimia kubwa) na huduma (kwa asilimia ndogo) si mzuri katika sekta ya afya nchini.
 
Hii nillipata toka kwa jamaa yangu aliyekuwa akifundisha pale chuoni; wanafunzi wakifeli sana somo lako unawekwa chini na uongozi wa chuo ili mambo yaende sawa na wanafunzi wafaulu. Nikajiuliza, sasa kama wanafunzi wa udaktari wanafanyiwa mishe ili wafaulu mitihani yao, kutakuwa na usalama kweli kwa wagonjwa watakaokuwa wanawatibu pindi watakapokuwa madaktari?
Nadhani mchanganyiko huu wa biashara (kwa asilimia kubwa) na huduma (kwa asilimia ndogo) si mzuri katika sekta ya afya nchini.

Ethics za taaluma zinakiukwa waziwazi kwenye kila sekta lakini hakuna anayejali wala kuchukua hatua, lakini hili la afya na uhai wa watu ifike mahali sasa huduma zitenganishwe na biashara
Sera ya taifa ya afya iweke clear demarcation kati ya biashara na huduma ili kuweza ili uwepo uwajibikaji wa wazi linapotokea tatizo
 
KAIRUKI NI MAJANGA. wengi watasema hapa lakini ni ukweli. alipasuliwa mama mmoja sababu y uvimbe kwenye jino. hakurudi yule mama. maana kwanza sijui walimfanyaje hadi tukatamani asingeenda kulingoa jino.

juzi hapo kuna rafiki yangu alilazwa hapo mtoto alikua na malaria. ile anatoka doc akakagua dawa akagundua nesi alikua anampa mtoto dawa dozi kubwa zaidi ikabidi wamlaze tena kuflash ile dozi ilozidi, tunamshukuru mungu anaendelea vema.

haha uuwi juzi tu rafiki yangu mwengine alienda hapo akaambiwa lazima apasuliwe as mtto ameongezeka. akataka kuondoka lakini doc akamhakikishia it will be safe. akalazwa asubuhi kaamshwa saa kumi awekwe tayari. kawekwa mpira wa mkojo na drip lakini hadi saa nane mchana doc hajaja wala hapokei simu. baadae wakaingizwa kufanyiwa upasuaji lakini na doc mwingine. hapo wametembea na catheter na drip from wodini to theater hahaha na kale kampira kanavouma sasa.

hata yule doc wake aje kumchungulia neeehi. hadi kaondoka. siku anarudi kimakosa wa reception wakampeleka kwa jeneral. huko akarudishwa balaa sasa alipofika kwa gyno. alisemwa vibaya hadi akakoma. kwaza doc akaanza kumuliza kwanini kaenda kwa general. INA maana huwajui magyno wa hapa hadi unakwenda huko. we si unajijua ni op. akamwambia mi sikufahamu maana meambiwa doc wangu hayupo so reception ndo wamekosea, Haya sema shida yako. akajieleza doc akamwambi unalalamika kwani hujui op ndo kilema chako cha maisha. panda hapo tuone, weee akambandua bandej vibaya kidonda kikaachia akamwambia kiko ok ondoka. yule dada aliponea aghakhan.

so kwa kiburi chao hao watu wa kairuki na hosp nyingine pia wagonjwa wengi wanakufa hovyo. gyno mzuri ni clementina lakini nae kutwa kucha yuko mara mikutanoni mara kasafiri ili mradi hayupo mara nyingi.

kuna uzembe mwingi hasa ukute unahudumiwa na wanafunzi wanakufanya we shamba darasa. kifo hupangwa na Mungu lakini wale wanakuletea kabisa .
 
Mleta mada hii umenikumbusha mbali nimepata uchungu sana nilipoteza mke wangu Monica mwaka juzi na alikuwa staff mwenzao hospital hiyo haifai jamani. mwenye kupinga cku apeleke ndg yake kwenye upasuaj km atarudi.
 
Back
Top Bottom