Kuna mtu amewahi kupata kazi ya maana kwa kutumia waganga wa jadi?

Kuna siku nliambiwa nina nuksi sana na ndio maana kila mtu anakupakazia ww ofisini. Hivyo nikaenda kwa Tawile. Baada ya kueleza kwa kina na ulinganifu tawile kwa umakini akaniambia "Pole sana mwanangu,hii dunia ina mambo mengi sana na nyie vijana mnapuuziaga. Ww umetupiwa jini wa chuki na mkata nyota hivyo itabidi ulete Kuku jogoo mwekundu na hela elf 30 kwa ajiri ya kutengeneza dawa" mwanaume niliondoka huku nikijisemea sasa wabaya wangu wataisoma namba.
Siku ya siku kwa kweli kuku mwekundu pure mlishindwa kumpata na nikaona bora nirejee tena kwa tawile ili nimwambie ili nimlete mwenye rangi nyekundu ila sickle zake ni nyeusi. Nilipofika nikakuta kuna wamama wawili na mabinti watatu wapo nje na ndani kuna mtu anahudumiwa. Palikuwa na tambara jeupe lenye maandishi mekundu na lilitutenganisha cc na mganga. Walichokuwa wanaongea niliweza kusikia na maelezo yaleyale niliyopewa mm yaani jini na alete kuku mwekundu na elf 30.
Katika ile foleni hadi mtu wa nne maelezo na maelekezo yaleyale. Hahaha nikajifanya kama naenda nje kuongea na simu ila nilipotoka nje nikarudi jumla home.
Ni usanii tu na siri hii naitoa hapa na sikuwahi kumwambia hata tetea wangu.
Sijawahi kuamini waganga tokea hapo na hawa kuku hawa watatushitakia kwa Mungu maana ndio wanaongoza kupelekwa kwa mganga.
NB: kuku akipelekwa kwa mganga hafugwi.
Inawezekana ndio hitaji lake la kwanza hilo.
 
Story hii nimeshuhudia live.

Wakati nipo dogo ndio nmemaliza 4m4..kulikua na bro wangu alipataga majanga sana..kwanza alikua dereva wa daladala..alipataga majanga kwa ajali kubwa..kisha kuja kuugua ugonjwa ambao hospitali zote alizoenda vipimo vyote hakuonekana na ugonjwa..ila aka elekezwa kwa mtaalam mmoja huko shinyanga vijijini.

Huyo mtaalamu alifanya macjekeche yake..jama alikuja kupona akarudi kwenye reli na kuendelea na mapambano ya maisha.

Ingawa jamaa alikua na familia kipindi narudi kitaani nikamkuta kachoka sana na life hana mbele wala nyumba..life la kuungaunga..anaomba kazi hapati mind you jamaa alikua dereva na leseni ipo...ila kila akiomba kazi hapati akipata ni dei waka.

Sikumoja akaniita nimwandikie barua ya kuomba kazi..kahama viwandani huko...nikamwandikia kisha akaniamba dogo kesho jiandae unisindikize mahali..

Basi kesho yake asbh na mapema nikamsindikiza mpka vijijini ndani ndani huko..kufika pale kaniambia dogo maisha ni kujipanga tunasali pia tuna pambana na upande wa pili.

Basi akafanyiwa mafekeche na mtaalamu wake..mida ya jioni tukaondoka kurudi home..kesho yake akachukua barua akatuma.

Hakukaa wiki..bhna akapata ile kazi.

Jamaa alipiga kazi..kajenga nw maisha safi tu.

Huo ndio ushuhuda wangu wa haraka haraka..ni mengi tu niliyoona.

Walokole na wafia dini za kuletewa watapinga..brainwashed creatures hawa..hawajua kua babu zetu walikua na uwezo wa kuzui au kuomba mvua ikanyesha..kama wanabisha waende kushuhudia miujiza ya kina mwanamalundi...

Dini asili zipo na zinafanya kazi kubwa.

#MaendeleoHayanaChama
Sawa ngosha
 
inategemeana na imani Yako mkuu ngoja niongee from my experience Kun mwaka wakati nip college nilshawah umwa sana hadi nikastop kusoma kabsa Kila hospital nayozunguka wanakwambia wew unauvimbe Kwa tumboni zunguka muhimbili kweupe zunguka aghakhan kweupe zunguka TMJ kweupe Kuna hospital moja ya wahindi nikaenda pale fire wakanifanyia full check majibu waliyonipa wakanambia ugonjwa wako unaelekea kuwahi kama cancer apo ndio nivyo give up nikamini huu mwaka navuta aseee mm mwenyewe nilkubali narejea Kwa sir God assume nilkua na kilo kama 64 nilidrop hadi 40 ivi ila Kun mshikaji wangu nilisoma naye advance mbeya aliyawh kuja nicheki hom akanikuta nimechoka afu nimegiveup kabsa yy alikuwa mtu wa njombe akanambia mwanangu ngoja tujarbu na miti shamba mm Kun mzee nitakupeleka ukajarbu yupo njombe labda unaweza Pona mm nikakubari mwamba tukatoka hom had njombe aseee fik Kwa huyo mzee picha linaanza tumefka tumekuta Kuna foleni ila mzee Yuko fasta ikafka zamu yangu mzee akafanya mamb yak anajua mwenyewe akanambia dogo ungechelewa kidogo tu ungekua Bai Bai akanambia ila upo kwangu utapona na itakuchukua mda kidogo unahitaji uwe mvumilvu na mwenye imani afu sjahitaji hela Yako kwanza nakutiba afu utanilipa badae ukikaa vizur siku ya kwanza tu alinipa dawa Kam tatu alinipa dawa kwaajili ya kuback kumbukumbu kichwani manaa niliumwa sana hadi nikawa nasahau ovyo dawa yenyewe ni alovera Poli mbili alinipa dawa ya kukata chakula nilkua Nikilala chakula kinapanda hadi mdomoni kinatoka hadi puani afu akanipa na dawa ya kusafisha tumbo aseee nilitapika hadi nilkua nagalala chini noma sana ishu kubwa ilikua kutibu donda lilopo ndani ya tumbo aseee mzee nilipgwa miti shamba had.nikapona kabsa japo ilinichukua kama two years ivi kukaaaa sawa kitu kilichikuwa kinanishangaza dawa nyingi nilzo kuwa napewa ilikua nachuma mwenyewe tena Kwa mdomo au mguu wa kulia au alikuwa anatumwa mtoto mdogo ndio ananichumia asee hakuna ndugu yangu Wala nani ni mim au mtoto mdogo na dawa nyingi unachuma Kwa mdomo
asa nikija kweny hao wanaotafuta Kaz ndio walikua weng balaaa na biashara usiseme wenye mikesi usiseme wengine wanampigia simu kabsa mzee njoo Moshi njoo kariakoo njoo Tanga njoo Moro Yani hatuli sehemu moja in short mm nilipona kabsa hadi nimekua kibonge nafanya mazoezi ya kupunguza uzito tu nimekua tukunyema nakumbka badaae wakat nimepona alinipa dawa ya nguvu za kiume roho hiyo dawa ilikua niktumia. ilikua inanguvu sana asee kama huna demu unaweza baka had niliacha kutumia asee pia aliwah nipa kitu moja inaitwa dawa ya bahati akanambia hii utakuwa unanuia kitu unachotoka mm nikanuiza nataka mademu ebwana siwez rudia tena ule ujinga mm nilzan utani mademm walikua wananisamisha wenyewe kaka naomba namba yak mara wengine kaka umeoa mara wengine naomba uwe rafki angu asee kitu Cha ajabu Kuna kadem kaliwah nifwata nyuma nyuma toka kariakoo hadi hom bila mm mwenyewe kujua asee nilishangaa kitu kingne yan Ile dawa nilkua nikiweka chini ya sakafu nakuta sisimizi wamajea hatari yan hujui hata walikotokea ikabidi nipigie simu Kwa mzee kumueleza Hali ilivyo akanambia bad kidogo tu utasumbuliwa na majini manaa hiyo dawa mda unavyozidi kwenda inazidi kuwa na nguvu itengue ipungue nguvu kabsa ukitoka kushiriki kabla hujaoga ishike kweli kabsa niliyofanya ivyo nikaona usumbufu sipati asee hapa Dunia dawa zipo tuache utani stori yangu ndefu sana siwez maliza Leo Wala kesho
Duuh
 
Hakuna kitu kama hicho kazi una apply kupitia portal au email je utaroga mfumo wa computer?
Tatizo vijana wenzetu wamevurugwa na maisha na wanazidi kuji vuruga zaidi. Haya mambo ni imani maana kuna watu wamezaliwa katika familia au koo zenye kuendekeza ushirikina so wanafikiria kila jambo ni ndumba tu. Imagine, sampuli ya watu hawa wanakua wasindikizaji tu maana hata wakibahatika wanakua mizigo hawana ile feeling ya kuhustle in reality. All in all, Vijana wenzangu endeleeni na ndumba na kuroga ili mfanikiwe na endeleeni kuwaangalia wanaume wanaotoka jasho na kuumiza kichwa wakiwa wanapambania fursa.
 
Achana na waganga matapeli wa dar hao.

Njoo huku kwetu morogoro nikupeleke kwa wataalamu huko ifakara ndani ndani.

Vijana msione watu ni mawaziri mkadhani ni bahati, ile ni kazi ya ndumba
Ifakara sehemu gani kuna mganga zaidi ya kukaa matapeli tu.
Mganga mwenyewe hana kazi ndio akupe wewe kazi.
Wajinga ndio waliwao.
 
Achana na hizi kazi za kwenye vijikampuni uchwara vya wachina au wahindi.

Nauliza kuna mtu amewahi kupata kazi ya maana either serikalini au kwenye makampuni ya kimagharibi na NGO kwa nguvu za witch doctors a.k.a waganga wa jadi?

Kama yupo ebu aje hapa atoe ushuhuda wake ili na sisi tukajaribu bahati zetu huko.

Asante
Itakuwa ngumu sana kuhusishanisha kupata kazi na huo u-witchdoctor. Inabidi ukawaulize na waliokuwa kwenye interview panel kuwa walijisikiaje alipoingia candidate huyo mwanzo mpaka mwisho.
 
Mkuu.umenikumbusha kuna kipindi bro wangu alikua na kesi ya roberry..tukaenda huko morogoro kwa mtaalamu..at the beginning bro alikua kapigwa 30 yrs..surprisingly bro akachomoka kwenye rufaa kama babu alivyotuahidi.
Kaka yako ni jambazi na mnamuacha uraiani
 
Mganga anaweza kukupa dawa, na certificate yako ukamuendesha mwenye degree kama gari. Wapo wengi makazini wanaotamba kwa ajili ya waganga. Ila maana mafanikio ni siri, wametulia na wanapasua Sala kama kawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka mwaka 2010 kuna jamaa yangu alipataga kazi alipewa dawa na mganga mimi nilikataa sababu ya imani yangu.
Leo hii mimi nipo kitaa nilipataga kazi ikayeyuka na nikapoteza kila kitu. Jamaa yangu ni finance and administration director wa NGO kubwa tu hapa bongo na amefungua pub inakimbiza sana mjini kwa kifupi jamaa ana kila kitu anachotakiwa kuwa nacho kijana aliyefanikiwa. Sijawai kumuuliza tangu wakati ule kama alitumia tena ndumba nyingine ila na mimi nafikiria kwenda kwa mtaalam anisaidie hali yangu ya maisha imekuwa mbaya kazi zimefungwa.
 
Nakumbuka mwaka 2010 kuna jamaa yangu alipataga kazi alipewa dawa na mganga mimi nilikataa sababu ya imani yangu.
Leo hii mimi nipo kitaa nilipataga kazi ikayeyuka na nikapoteza kila kitu. Jamaa yangu ni finance and administration director wa NGO kubwa tu hapa bongo na amefungua pub inakimbiza sana mjini kwa kifupi jamaa ana kila kitu anachotakiwa kuwa nacho kijana aliyefanikiwa. Sijawai kumuuliza tangu wakati ule kama alitumia tena ndumba nyingine ila na mimi nafikiria kwenda kwa mtaalam anisaidie hali yangu ya maisha imekuwa mbaya kazi zimefungwa.
hahahahahhaahaahaha
 
Back
Top Bottom