sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Kuna uzi nimetoka kuusoma humu nami wacha nikazie
Na ndivyo ilivyo hata kwenye ukoo wetu, wengi wamesomea Sheria, Uhandisi ama Udaktari.. Wachache sana wamesomea Accounting baada ya kushindwa kuchagua kozi hizo tatu.
Hata mimi nimesomea kimoja wapo na nikiri kwamba nilipata msaada mkubwa kwenye ushauri, guidance na kwenye ajira nilishikwa mkono a.k.a connection maana nilisomea vitu ambavyo kuna ndugu tayari wanajua michakato yake, ningesomea mambo mengine ingebidi nipambane sana kivyangu.
Yes, na mimi ndicho nilichowakazia Watoto wasomea... udaktari, sheria au Uhandisi (kuna moja anapenda mambo ya computer nampa motivation aje asomee computer engineering yenye uzito kuzidi IT na computer science).
Katika hizi kozi nimewapa ahadi kwamba iwe isiwe lazima ntasomesha nje ya nchi wacha nijibane tu,
Ikija kutokea wameshindwa kabisa basi wasomee Accounting au na hio ufamasia niliyoiona post nyingine ila watasomea vyuo vya hapa hapa kwetu.
Nje ya hapo waje kujisomesha kwa ada zao.
Hata kwa wa israel, wahindi na wanaijeria, makundi ambayo hata Marekani yana asilimia kubwa ya wasomi kwenye jamii zao (wakiongozewa na wanaijeria) nimeona nao falsafa zao ni hizo hizo DOCTOR, ENGINEERING, LAWYER.
Najua kuna watu watakuja kusema kuna wengine wamesomea insurance wana ajira wakati wengine wamesomea hizo kozi wapo mtaani, kuna darasa la saba hawajasoma vyuoni wametoboa zaidi kuzidi waliosomea kozi hizo, n.k. niwajuze tu ya kwamba hizo kozi nilizosisitiza zina zina probability rate nzuri ya kuajiriwa kwenye system, na muhimu zaidi zipo fursa za kujiajiri. waweza kupiga hybrid pia ofisini + biashara zako.
Najua pia kuna watu watakuja kusema ajira ni utumwa, hahahaha, ni kwamba aina hii ya watu mara nyingi wana wazazi au ndugu walioajiriwa serikalini huku chini chini basi wakiona mtu hawezi kununua hata kagari wanaona ajira zotee hazina kitu, Zungukeni mjionee nyie! Mshahara haujawahi kumtajirisha mtu lakini watu wanaishi maisha standard wanafaidi mema si haba, wanasomesha watoto private, wanakula vizuri, wanai nyumba kadhaa, magari yapo, n.k.,
Ni kweli kujiajiri biashara zinatengeneza matajiri ila usije kuthubutu kusema waajiriwa wote uchumi unawatesa, alafu hata hizo biashara huwa zinaongelewa kwa juu juu, huku watu wanaofeli huwa wanapata shida si mchezo, mtu anaweza kuamka alfajiri anarudi usiku kaindia elf 5 tu, hapo hujazungumzia madeni, marejesho ya mkopo, kufilisika, n.k.