Kuna martial art bora kuliko Judo?

Kuna martial art bora kuliko Judo?

Kick Boxing inatajwa kuwa hatari mkuu, pia kuna systema ya Russia na kuna Krav Maaga ya Israel nayo ni balaa sana, withing seconds ni mashambia mfululizo yanafanyika. Bila kusahau Muay Thai ya Asia huko.
 
Martial art maana yake ni sanaa ya mapigano.

Michezo yote ya mapigano inaingia humo kuanzia karate, kung fu , wushu, boxing, capoeira , jeet kun do , judo, taekwondo nk
Sanaa ya Mapigano?!?! Hapana.
Sanaa ya kujilinda/Kujihami kwa mikono mitupu bila silaha..unaugeuza mwili unakuwa silaha yako.
Karate...ilianza baada ya watawaliwa kukatazwa kumiliki silaha na watawala..vile vile Capoeira kule kwenye mashamba ya Brazil na visiwa vyake.
 
Nimeona wacheza Judo wakiwadhibiti watu wa martial arts zingine bila hata kustrike
Inategemea sasa kwa mfano Brazilian Jiu-Jitsu na Jiu-Jitsu halisi ya Japan wanaweza cheza vizuri sana na mtu wa judo au Russian Sambo kwasababu hizo zinajumuisha sana takedowns na ground fighting hata mtu wa MMA.

Ila unapokuja kwenye swala la full contact martial arts kuna michezo kama Muay Boran achana na hii mpya Muay Thai ambayo ni ya kisasa kabisa kuna Muay Boran ambayo inatokea pande tofauti ikijulikana kama Muay Chaiya, Muay lopburi, Muay Korat, Muay Thasao hiyo mara nyingi huweza kulinganishwa na karate hasa kyokushin karate ya Mwanzilishi Matsutatsu Oyama.

Hapo bado hatujazungumzia martial arts za china (Kung Fu, wushu, jeet ku do n.k), Philippines (Eskrima), Korea (Tae kwon do), Brazil (Capoiera), Guatemala (tem'v ka), France (French Savate), Western Boxing n.k

Katika Martial arts kimsingi hakuna saana ipi bora ila zipo deadly japo kimsingi hutegemeana sana na wapiganaji wanaokutana yupi ni bora katika sanaa yake kuimudu sanaa nyingine.

Ndiyo maana hata military martial arts zinachanganywa baadhi ya sanaa ili upate kitu kimoja ambacho ni kipana kwasababu hawa watu hawafundishwi mashindano bali ni kuua na mara nyingi wanatumia hizi arts zimekamilika kila angle..
(Boxing, krav maga, karate, judo, Jiu-Jitsu)
 
Kick Boxing inatajwa kuwa hatari mkuu, pia kuna systema ya Russia na kuna Krav Maaga ya Israel nayo ni balaa sana, withing seconds ni mashambia mfululizo yanafanyika. Bila kusahau Muay Thai ya Asia huko.
Systema na krav maga ilikuwa introduced kwa ajili ya matumizi ya majeshi na wana usalama wa nchi za Israel na Russia ila baadae ndiyo zimekuja kuzagaa mitaaani.
Hizo kumbuka hazina mashindano wala rank za mikanda.
Muay Thai ni sanaa ya kisasa ambayo ilitokana na Muay Boran ambayo pia ilitumika katika majukumu ya kijeshi ili kukabiliana na wakoloni wakati Thailand ikitafuta uhuru wao hii nayo ilikuwa ni hatari na ngumu kujifunza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom