Puna
JF-Expert Member
- Oct 9, 2013
- 2,789
- 4,925
Taarifa nilizozipata hivi punde ni kuwa Kuna mapambano kati ya wananchi na Polisi Kijiji Cha Mbesa kata ya Mbesa, Tarafa ya Nalasi,Wilaya ya Tunduru, jimbo la Tunduru kusini.
Polisi wanavunja milango nyumba Hadi nyumba kukamata wanaume,wengi wamekimbilia mashambani.Mwenye taarifa Zaidi atujuze.
Confirmed ‼️
Kutoka chanzo changu cha uhakika ni kuwa:-
Chanzo Cha mgogoro ni wafugaji jamii ya Wamag'ati kulisha mashamba ya watu pamoja na kuiba vyakula.
Siku kadhaa nyuma kulitokea mgogoro baina ya wakulima na wafugaji mgogoro uliopelekea kifo Cha mkulima.Wananchi walilalamika hawakupata msaada kutoka kwa kiongozi yoyote.Sasa siku ya Jana Polisi walifika kijijini hapo na Kwenda Hospital ya Mbesa Mission kutaka kuupima mwili,wananchi wakagoma wakidai kuwa Sababu ya kifo inajulikana ndipo mkutano wa Kijiji uliitishwa kujaribu kuweka sawa hapo ndipo vurugu zilipoanzia.Wamechoma moto Ofisi ya Kijiji Cha Mbesa airport na Mbesa Kijijini (Vijiji viwili ndani ya Kijiji kimoja) wamechoma Ofis ya kilimo ya kata ndipo FFU kutoka Songea wakaletwa Gari 6 jamaa wamepiga mabomu ya machozi na kuanza kukamata wanaume wote nyumba Hadi nyumba.
Polisi wamevunja Tv,viti,mageti,Sofa,sabufa,matenk ya maji,vitanda nk.Wanaume wamekimbilia Polini na vijiji vya jirani kama Mbati,Chikomo,Nalasi na Lijombo huku wengine wakikimbilia Tunduru mjini.
NB: Taarifa za muda huu ni kuwa Polisi wameanza kuwafuata wanaume wa Mbesa waliokimbilia vijiji vya jirani.Mniwie radhi kwakuwa uhandishi nao ni kozi maalumu kama Kuna mahali sijaeleweka.