Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,124
Ndugu zangu watanzania tuwe makini na wanasiasa hasa kipindi cha uchaguzi. Tuliona namna wanasiasa wa kanda ya ziwa walivyopambana kushangilia uvuvi haramu wakidai ziwa ni mali yao na wapo tayari libaiki kama swimming pool . Kauli hizi walizitoa wakitaka watu wavue bila kudhibitiwa na wamefanikiwa. Lake Tanganyika, Nyasa na Victoria hakuna tena udhibiti madhubuti. Hapa kuna watu walilipwa na wameendelea kulipwa kujifanya wanawalinda wananchi kumbe wanalinda malengo yao ya kuuza nyavu, kunufaika na mazao yaziwani nk
Baada ya wanasiasa kufanikiwa huko sasa wamehamia kwenye vita dhidi ya tembo na wanyapori. Kampeni kubwa inayoendelea ni kusema wanyama siyo bora kuliko wanadamu. Hao wanaosema haya wamesoma na wana akili timamu kabisa lakini wananufaika na uhalifu wanakupigia kelele. Tumemsikia kiongozi mmoja wa ACT huko Kusini akizungumza na wananchi, tumesikia bungeni, tumesikia Serengeti na maeneo mengine.
Hawa wote wanatafuta namna yakubariki mauaji ya wanyamapori. Niwaombe wananchi tusidanganywe na wasaka madaraka tuangalie kwa jicho pana hoja zao. Tusipojipanga vyema wao na familia zao watauza hizi rasilimali na watakwenda kujenga au kununua makazi Ulaya. Tuwapige vita wanashangilia uvuvi haramu na wanaoshangilia mauaji ya wanyamapori. Watoto wetu watahitaji samaki huko tuendako kuliko tunavyohitaji sana. Watoto wetu watahitaji kutembelea mbuga za wanyama na kuona big 5 zaidi yetu. Huu ni urithi wetu tusiuze