Amazon_kukufarm26
New Member
- Jul 14, 2021
- 1
- 2
KUNA ATHARI GANI KUTUMIA MAYAI/NYAMA YA KUKU WA KISASA?
.
Kumekuwa na imani kwamba nyama au mayai ya Kuku wa Kisasa vina madhara mwilini. Madhara ambayo yamekuwa yakitajwa sana ni pamoja na kunenepa kupita kiasi, kupungua kwa nguvu za kiume, n.k.
Imani hii imekuwa ikihusishwa na dhana kwamba, Kuku wa Kisasa wanatumia madawa mengi. Hebu leo tuone hili limekaaje;
UKWELI ni kwamba Kuku hutumia madawa na chanjo kama ilivyo kwa binadamu pindi anapoumwa. Dawa na chanjo hizo huwa zimeandikwa maelezo mengi juu ya matumizi, matibabu, na muda wa kutumia bidhaa itokanayo na Kuku mara tu baada ya tiba au chanjo (Withdrawal period).
Wengi wetu huwa hatuzingatii hili na tunapoenda kinyume na maelekezo ya 'Withdrawal period', ukila mayai au nyama huweza kusababisha madhara ambayo huonekana baadae, LAKINI tukizingatia hili, mayai na nyama ya Kuku wa Kisasa havina madhara kwa watumiaji, ni kama bidhaa nyingne tu itokanayo na Kuku wa kienyeji.
Je, wewe kama mfugaji, hasa wa Kuku wa mayai unaweza kuzingatia 'Withdrawal period' ya siku 5? Fikiria unazalisha pengine trey 30 kwa siku. Kwa siku 5 ni trey 150 na pengine bei ni 8000@. Upo radhi kupoteza 1,200,000 kwa siku 5 kwa ajili ya kulinda afya ya wengine hapo baadaye?
Najua inaweza kuwa ngumu kwa wengi wetu, lakini ni vyema tukazingatia taratibu za kiafya katika mashamba yetu ya mifugo, ili kulinda afya za watumiaji wa mazao yatokanayo na mifugo yetu.
Asante.