Wafugaji wa kuku wa nyama tupeane mbinu kuhusu chakula

Malingumu

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
616
429
Habarini wafugaji wenzangu. Nina imani mifugo yenu inaendelea vema.

Mimi ni mfugaji mdogo na si wa siku nyingi sana, kwa kipindi nilichofuga mpaka sasa nimeweka malengo makubwa ya kufika mbali kwa hawa kuku wa nyama.

So far uwezo wangu kwa sasa ni kuku 500 wa nyama(broiler), naona nimekua maana nilianza na chini ya 400.

Changamoto niliyoiona ni kwenye bei ya soko ukilinganisha na Gharama za chakula. Kwa sasa nafuga kuku wa nyama, japo nilianza na kuku wa mayai hapo nyuma. Kwa kuku wa mayai nilikuwa natengeneza chakula mwenyewe na angalau nilikuwa naona faida kidogo.

Nimewaza kufanya hivyo pia kwa kuku hawa wa nyama KWAMBA NIWE NATENGENEZA CHAKULA MWENYEWE.

Nimewaza hilo maana naona kulisha kuanzia STARTER mpaka FINISHER kwa kununua hichi cha mudukani inakamua kidogo.

Naomba tushee kama kuna mwenye uzoefu wa kutengengeneza chakula kwa ngazi ya GROWER na FINISHER.

ASANTENI.
 
Nami natamani kusikia zaidi.

Najipanga kuanza huu ufugaji na nimekamilisha Banda.

Nawaza kwa kupata mbegu nzuri.
 
Back
Top Bottom