Mayai ya Kuku wa Kienyeji yanauzwaje?

MaT2B

JF-Expert Member
Jul 12, 2019
400
1,003
Mwezi uliopita nilinunua Mayai thelethini ya kuku wa kienyeji.

Kwa ajili ya kula.

Nimetumia mayai kama 10. Halafu ukapita muda kama wiki. Bila kula mayai.

Juzi nikachukua kuchemsha, naona ni kama yameharibika. Yanakuwa yana maji, halafu ile layer nyeupe inakuwa ngumu kweli.

Ukikangaa ndio sio kabisa.

Nimemuuliza muuzaji kasema inatakiwa niyatunze kwenye fridge, eti joto linaharibu mayai.

Lakini nakumbuka nyumbani tulikuwa tunatunza kwenye kabati tuu, na sikuwahi yakiharibika.

Msaada, mayai yanakaa muda gani hadi kuaribika na njia gani ya kutunza.

Mayai yangu 18 ni hasara sana.

Angalizo: mayai ni ya kuku wa kienyeji.
 
Hili joto lililokuwa hapa Dar mkuu, usipojua namna ya kuyatunza kwenye ubaridi kiini kinayeyuka ndani ya siku tatu tu.
 
Back
Top Bottom