Kuna athari gani kutumia mayai/ nyama ya kuku wa kisasa?

Amazon_kukufarm26

New Member
Jul 14, 2021
1
45
KUNA ATHARI GANI KUTUMIA MAYAI/NYAMA YA KUKU WA KISASA?
.
Kumekuwa na imani kwamba nyama au mayai ya Kuku wa Kisasa vina madhara mwilini. Madhara ambayo yamekuwa yakitajwa sana ni pamoja na kunenepa kupita kiasi, kupungua kwa nguvu za kiume, n.k.

Imani hii imekuwa ikihusishwa na dhana kwamba, Kuku wa Kisasa wanatumia madawa mengi. Hebu leo tuone hili limekaaje;

UKWELI ni kwamba Kuku hutumia madawa na chanjo kama ilivyo kwa binadamu pindi anapoumwa. Dawa na chanjo hizo huwa zimeandikwa maelezo mengi juu ya matumizi, matibabu, na muda wa kutumia bidhaa itokanayo na Kuku mara tu baada ya tiba au chanjo (Withdrawal period).

Wengi wetu huwa hatuzingatii hili na tunapoenda kinyume na maelekezo ya 'Withdrawal period', ukila mayai au nyama huweza kusababisha madhara ambayo huonekana baadae, LAKINI tukizingatia hili, mayai na nyama ya Kuku wa Kisasa havina madhara kwa watumiaji, ni kama bidhaa nyingne tu itokanayo na Kuku wa kienyeji.

Je, wewe kama mfugaji, hasa wa Kuku wa mayai unaweza kuzingatia 'Withdrawal period' ya siku 5? Fikiria unazalisha pengine trey 30 kwa siku. Kwa siku 5 ni trey 150 na pengine bei ni 8000@. Upo radhi kupoteza 1,200,000 kwa siku 5 kwa ajili ya kulinda afya ya wengine hapo baadaye?

Najua inaweza kuwa ngumu kwa wengi wetu, lakini ni vyema tukazingatia taratibu za kiafya katika mashamba yetu ya mifugo, ili kulinda afya za watumiaji wa mazao yatokanayo na mifugo yetu.

Asante.
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,602
2,000

Athari yake ni kuwa,
Kwanza hao kuku ni laboratory products ambao wamegeuzwa mifumo yao halisi ya ukuaji na kufupishwa, hivyo basi wanategemea madawa zaidi ili waweze kukua kwa haraka,
*madhara yake ni kuwa madawa haya hubaki mwilini mwa hao kuku hasa kwenye uroto wa mifupa na hivyo mlaji akiwatumia yale madawa yatafanya kazi ile ile ya kuufanya mwili wa mlaji kunenepa haraka hivyo kusababisha obesity and overweight problems,
*pia madawa ya kukuzia hawa kuku yanaweza kuwa chanzo kikubwa cha kufupisha maidha ya mlaji hasa anapotumia kwa kiwango cha juu.
* hupunguza na kuondoa asilia ya mtu/binadam, ikumbukwe kuwa kwa asilimia kubwa miili yetu hutegemeana vyakula asilia ili kuuweka mwili kuwa shupavu wenye kinga thabiti (body genuineness) hivyo matumizi ya kupindukia ya nyama bandia (artificial/lab flesh) huuweka mwili wa mtumiaji kuwa "bandia" na usiostahimili mazingira ya kawaida ikiwemo vimelea vya magonjwa na uimara wa mifupa ya mlaji (hasa kwa walioanza wakiwa watoto wadogo)

NB. TUJITAHIDI KULA VYAKULA ASILIA ANGALAU KWA KIWANGO CHA KUTOSHA ILI KUEPUKANA NA MATATIZO LUKUKI IKIWEMO NGUVU ZA KIUME(FOR MEN)
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,602
2,000

HAYA NDIO MADHARA NANE YA KULA KUKU WA KISASA.​

resize.png

kutokana na uhitaji mkubwa sana wa kuku hasa mijini ambapo kuna watu wengi sana, kuku wa kienyeji wameshindwa kabisa kutosheleza hitaji la watu hao.
teknolojia mpya ambayo iko wazi kwa watu wote imekuja na kuku wa kisasa ambao hukua ndani ya muda mfupi sana kuliko kuku wa kawaida yaani kuku wa kienyeji.

kumekua kuna elimu zikitolewa kwamba nyama nyeupe yaani kuku, samaki na ndege ni salama sana kuliko nyama nyekundu kama ngombe, mbuzi na nguruwe...ni kweli kabisa kama ukiwala wanyama hawa wakiwa kwenye asilia yao lakini ulaji wa kuku wa kisasa una madhara makubwa zaidi kuliko kula ngombe na mbuzi ambao wana nyama nyekundu.
kulingana na watu wengi kula sana kuku hawa hasa mahotelini, kwenye vyakula vya haraka kama KFC na kadhalika basi leo ntawaletea madhara ya kuku hawa kama ifuatavyo.

saratani au kansa mbalimbali; kuku za kisasa zina kemikali nyingi sana mfano kemikali phip ambazo huweza kusababisha mtu kupata kansa mbalimbali ikiwemo tezi dume na kansa ya matiti, kansa hizi zikigunduliwa mapema unaweza kupona lakini zikichelewa kugunduliwa zinakuua.

lehemu au cholestrol; kuku wa kisasa wana lehemu nyingi sana, hii ni kemikali ambayo ni moja ya vyanzo vikuu vya kuziba mishipa ya damu hasa ya moyo na kuleta magonjwa ya moyo.
tafiti zinaonyesha kuku hawa wana lehemu au cholestrol nyingi kuliko nyama za ngombe au mbuzi na mayai yao yana lehemu mara tatu zaidi ya nyama ya ngombe na mbuzi.

kuongezeka uzito; kuku wa kisasa wameonyesha kuongeza watu uzito zaidi kuliko kuku wa kienyeji kwani kuku hawa wanakua na nyama nyingi sana ambazo huwafanya watu wazile kwa uroho, hii huweza kusababisha magonjwa ya moyo, kisukari na kiharusi.kumbuka kuku hawa hawafanyi mazoezi yeyote tufauti na kuku wa kienyeji ambao hutembea sana.

huongeza sumu mwilini; kuku hawa kama nilivyosema mwanzo hukuzwa kwa kemikali nyingi sana ambazo huwakuza mara tatu zaidi haraka kuliko kuku wa kawaida, sumu hizo ni chanzo ya magonjwa kama kansa, kusahau sana uzeeni kitaalamu kama alzhaimer disease, magonjwa ya mishipa ya fahamu na kadhalika.
magonjwa haya hushambulia sana wazee hasa nchi zilizoendelea kama marekani, ujerumani, uingereza na kadhalika sababu ya mfumo wao wa kula hauna vitu asilia kabisa.

huongeza usugu wa dawa za binadamu; kuku hawa hupewa vyakula vyenye dawa za antibayotiki ambazo huwasaidia wasiugue na kufa hata kwenye mazingira magumu, sasa dawa hizi huliwa na binadamu na kumfanya azizoee sasa ikitokea anapata ugonjwa dawa nyingi atakazokula zitakataa kumtibu sababu mwili wake umeshazoea dawa.

mafua ya ndege; mafua haya yameua watu wengi sana nchi zilizoendelea na kuwaacha wengi wagonjwa kitandani, avian flu ni moja ya magonjwa tishio ambayo husababisha viungo mbalimbali mwilini kushindwa kufanya kazi.

kukua haraka kwa watoto; daktari mmoja wa mifugo kwenye chuo kikuu cha zambia ambaye amehusika sana na tafiti za kuku hawa anasema kwamba kuku hawa wanawekewa homoni za ukuaji kitaalamu kama growth hormone ili wakue haraka na madhara yake huathiri sana watoto ambao wanakua na kujikuta wanakua na kubalehe kabla ya wakati.

kuishiwa nguvu za kiume: sababu maini ya kuku ndio yanahifadhi sumu zote za mwili wa kiumbe chochote, tafiti zinaonyesha ulaji wa maini wa kuku wa kisasa kunaweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume.
chanzo. HAYA NDIO MADHARA NANE YA KULA KUKU WA KISASA.
 
Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
11,572
2,000
Utafiti usio rasmi ni kwamba kuku wa kisasa pamoja na mayai yake yanamfanya mtu kuwa na ngozi mwororo, makalio makubwa, kunenepeana bila hisabati, uvivu, kuwa mlainilaini kama mtoto na kumfanya mtu awaze kikukukuku... Yani mtu hawezi kukaa masaa mawili bila kuonja kitu
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,602
2,000
mayai.jpg

Mayai ya kuku wa kisasa yadaiwa kuwa hatari​

Summary

Akizungumza leo wakati alipozindua bodi mpya ya ushauri ya wizara kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Mwalimu amesema amehakikishiwa na wataalamu hao kuwa dawa zinazotumika kwenye mayai na kuku hao zinabaki ambapo si salama kwa afya ya binadamu.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mayai ya kuku wa kisasa yanayotengenezwa nchini yamedaiwa kuwa na mabaki ya dawa ambazo ni hatari kwa afya ya binadamu.
Akizungumza leo wakati alipozindua bodi mpya ya ushauri ya wizara kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Mwalimu amesema amehakikishiwa na wataalamu hao kuwa dawa zinazotumika kwenye mayai na kuku hao zinabaki ambapo si salama kwa afya ya binadamu.
Mwalimu amesema kutokana na dawa hizo kubaki kwenye mayai na kuku hao ameitaka TFDA kufanya utafiti ili kujua kiwango kipi cha dawa zilizopo ili Serikali iweze kuchukua hatua za haraka.
“Hivyo tuwaachie TFDA waendelee na utafiti wao na wanapobaini ni kiasi gani cha dawa zilizomo kwenye mayai na kuku hao watuambie haraka dawa zipi hazitakiwi na zipi zinatakiwa ili kulinda soko la ndani,”amesema.
Pia amewatahadhalisha wataalamu wa TFDA wasihofie kutoa majibu haraka kwa kufikiri kuwa watakwamisha soko la ndani hivyo wanatakiwa wawe wa kweli ili tatizo lililopo liweze kupunguzwa. chanzo. Mayai ya kuku wa kisasa yadaiwa kuwa hatari
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom