Kumtetea Mungu ni kazi sana!

Kumtetea Mungu ni kazi sana!

Unapomuitaji anapatikanika

Katika Biblia (Mathayo 6:8) Yesu anasema Baba anajua mahitaji yako kabla hujamwomba. Katika Uislamu, Mwenyezi Mungu anajua yote.

Yatupasa kumuomba na kumlilia shida zetu kama baba yako mzazi anaekulea
Sasa kama anajua na hafanyi, shida inakuwa nini? Si wanasema ana upendo wote?
 
Mungu sio mwanadamu
Mungu ana viungo vyote vya mwanadamu kama vile:
Kichwa
Macho
Masikio
Mdomo/Kinywa
Ulimi
Miguu
Mikono
Vidole
Roho
Moyo
Akili
Pia ana sifa zote za mwanadamu kama:
Mawazo
Hasira
Wivu
Anajuta
Anafurahi
Anapumzika
Anatembea
Hajui baadhi ya vitu
Anakula njama
Ana mipango
Ana kinyongo
Anachoka

Kwahiyo, Mungu = mwanadamu.
Kiuhalisia mwanadamu ndio alumuumba Mungu, sio Mungu alimuumba mwanadamu.
 
Mkuu umewaza nini mpaka ukataka kumtetea Mungu? Unataka kumtetea kwa lipi wakati vyote alivifanya yeye?

Mungu hatetewi na kama atataka bhasi atajitetea mwenyewe kwa uwezo wake mwenyewe.

Yaliyotokea Nepal ni ujinga wa mwanadamu tuu, Mungu asihusishwe kabisa.

Huoni kwamba zile nyumba zilijengwa kwenye mkondo wa maji? Ujinga ni kuamini kwamba maji yakipungua kwa miaka hamsini au mia mbili bhasi hapo pameshakua nchi kavu.

Ukitaka Mungu afanye nini pale?

Kuhusu hao wanaosema sijui Mungu amekasirika hata hawaelewi wanachozungumza. Ukisoma biblia kitabu Cha Mwanzo kuna mahali Mungu anasema "Nimempenda Yakobo na nimemchukia Esau" Je! Esau alimkosea Mungu Nini?

Ukiendelea kusoma utaona Yakobo alizulumiwa na mjomba wake mara 7 Je! Mungu alishindwa kumtetea na dhulma ya mjomba wake?

Mbele utaona Esau nae alikuja kuwa na Mali nyingi tuu, Sasa Je? Mungu alimchukia Esau kwa kutokumfanya kuwa sehemu ya Taifa la Israel?

Mkuu naomba tuache kumshirikisha Mungu katika ujinga wetu wanadamu. Mungu atabaki kuwa Mungu na mapenzi yake ndio yatatimia.
 
Wenyewe wanaelewana sababu wanaamini katika lugha moja, wewe huijui lugha ya imani yao ndo maana unaona ni kazi sana. Ukielewa lugha ya imani yao si kazi.
 
Kwanza ,hakuna uhusiano na adhabu ya kuharibu na kifo, vifo vinatokea kila siku ..Unachotakiwa kujua ni kwamba kuna sababu elfu moja ya binadamu kufa ,na kifo kipo ...Ukitaka kujua Mungu yupo au hayupo ,basi hao hawakutaka kufa ila kuna kitu kimefanya hivyo ,wameishi hapo miaka na miaka ilikuwa ni sehemu salama kwao ,ila bado ni dhaifu wamekufa wakiwa na ndoto zao wala hakuna aliyepanga yatokee ili ni Mungu Mkuu.


Binadamu ni dhaifu kiasi hajui kesho yake ,anawezaje kukataa uwepo wa Mungu?
Kifo sio adhabu
 
Siamini hivyo.
Suala si wewe unaamini nini.

Kama hayupo, atakuwa hayupo tu bila kujali unaamini hivyo au huamini hivyo.

Kwa hiyo, unavhoamini wewe si muhimu, muhinu ni ukweli.

Ukweli ni ukweli tu, hata kama huuamini.

Na mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo, unaamini tu.

Thibitisha Mungu yupo, usiseme tu unaamini.
 
Back
Top Bottom