Mungu ni mwema au Mungu ni mkatili?

Mungu ni mwema au Mungu ni mkatili?

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
750
Reaction score
1,745
Kosa kubwa ambalo hawa Wazungu na Waarabu walilifanya wakati wanatunga hizi stori zao ni kumpaka rangi MUNGU aonekane ni mkatili. Fungua vitabu vyao uone
Kwenye hivyo vitabu vyao, Mungu anaangamiza mauaji ya halaiki na huyo huyo anabariki.

Kwenye hivyo vitabu, Mungu anasema yeye ndiye anayeleta maafa na uovu (Isaya 45:7).
Kwenye hivyo vitabu, Mungu anamtuma pepo mchafu kutesa watu.

Walichokosea ni kumfanya Mungu aonekane mkatili na muangamizaji, wakimpa sifa ambazo ninyi mnasema ni za Shetani, kumbe ni wao ndio wamechanganya madesa.
Badala ya kumfanya MUNGU kuwa MWEMA kwa asilimia mia moja Mungu wa nuru, amani, na upendo usio na masharti wakachanganya roho ya kikatili ndani yake ili watutawale.

Wazungu na Waarabu walitengeneza movie ya kutisha. Wamemweka Mungu upande mmoja na kumpa kazi ya kutesa na kuangamiza watu, halafu wakamweka Shetani upande mwingine kama kisingizio.

Mungu aliyeandikwa kwenye Biblia yenu na Kurani yenu, ambaye mnamtetea ni mhusika aliyetungwa na wageni akiwa na sifa za kikatili.

Walipaswa kumuacha Mungu awe MWEMA pekee, lakini kwa sababu walikuwa na ajenda za kututawala, wakamtengeneza Mungu anayefanana na ukatili wao wa kikoloni na kibeberu.

Mungu yupo na ni mwema 100% Lakini sio huyo wa kwenyekaratasi zilizotungwa na wageni kuja kutuvuruga akili zetu!..

Hebu someni hivi vifungu vyenu muone jinsi walivyomdhalilisha Mungu na kumfanya kuwa muangamizaji.

Kutoka 32:27 Mungu anawaambia watu wauane, kaka amuue ndugu yake!

1 Samweli 15:3 Mungu anaamuru mpaka watoto wachanga na wanyama wauawe!

Kurani Inasema Nitatia hofu katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo, na wapigeni katika kila ncha ya vidole."

Hivi kweli? Huyu ndiye Mungu mnayemsujudia? Huyu ni Mungu au ni jenerali wa vita wa Kiarabu au Kizungu? Hapa ndipo walipochemsha! Wangemfanya MUNGU kuwa MWEMA pekee, Mungu ambaye ni nuru tupu, asiye na chembe ya ukatili, tusingekuwa hapa tunabishana leo.

Hivi vitabu vililetwa kututawala na kutuliza amani duniani kwa kutumia hofu. Wazungu na Waarabu walijua fika kuwa ili kumfanya binadamu awe mtumwa mnyenyekevu, ni lazima umtengenezee hofu ya kitu asichokiona.
 
Ni mkatili, Adam na Eva walikula katunda tu na akawapa adhabu kali!! Anavyomruhusu shetani kuleta maafa!! Huo ni ukatili uliokubuhu.
 
Lakini pia inafikirisha.... Mungu muweza wa yote aliwapa majaribu Adam na Eva waliposhindwa akakasirika akawapa adhabu Kali Ina maana hakujua kama wangefanya kosa? basi sio muweza wa yote.🤔
 
Wafia DINI na kondoo wa bwana mnaitwa huku ukweli lazima usemwe maana uongo umetawala sana.
 
Mungu hamlazimishi yoyote kumuamini kuwa yeye ni Mwema au Mkatili.
Imani yako ndio itaamua umuone yeye ni Mwema au siyo mwema.

Kama unaona Mungu ni mwema basi usihangaike na upande mwingine ambao unaona yeye ni mkatili.
Mungu hapungukiwi na chochote pale mtu anapoamua kutomuona mwema.

Hata mawe yanaweza kumuona yeye ni Mwema!
 
Imani na akili nani anamuongoza mwenzake?
Je wewe unaongozwa na Imani na sio akili???
 
Kosa kubwa ambalo hawa Wazungu na Waarabu walilifanya wakati wanatunga hizi stori zao ni kumpaka rangi MUNGU aonekane ni mkatili. Fungua vitabu vyao uone
Kwenye hivyo vitabu vyao, Mungu anaangamiza mauaji ya halaiki na huyo huyo anabariki.

Kwenye hivyo vitabu, Mungu anasema yeye ndiye anayeleta maafa na uovu (Isaya 45:7).
Kwenye hivyo vitabu, Mungu anamtuma pepo mchafu kutesa watu.

Walichokosea ni kumfanya Mungu aonekane mkatili na muangamizaji, wakimpa sifa ambazo ninyi mnasema ni za Shetani, kumbe ni wao ndio wamechanganya madesa.
Badala ya kumfanya MUNGU kuwa MWEMA kwa asilimia mia moja Mungu wa nuru, amani, na upendo usio na masharti wakachanganya roho ya kikatili ndani yake ili watutawale.

Wazungu na Waarabu walitengeneza movie ya kutisha. Wamemweka Mungu upande mmoja na kumpa kazi ya kutesa na kuangamiza watu, halafu wakamweka Shetani upande mwingine kama kisingizio.

Mungu aliyeandikwa kwenye Biblia yenu na Kurani yenu, ambaye mnamtetea ni mhusika aliyetungwa na wageni akiwa na sifa za kikatili.

Walipaswa kumuacha Mungu awe MWEMA pekee, lakini kwa sababu walikuwa na ajenda za kututawala, wakamtengeneza Mungu anayefanana na ukatili wao wa kikoloni na kibeberu.

Mungu yupo na ni mwema 100% Lakini sio huyo wa kwenyekaratasi zilizotungwa na wageni kuja kutuvuruga akili zetu!..

Hebu someni hivi vifungu vyenu muone jinsi walivyomdhalilisha Mungu na kumfanya kuwa muangamizaji.

Kutoka 32:27 Mungu anawaambia watu wauane, kaka amuue ndugu yake!

1 Samweli 15:3 Mungu anaamuru mpaka watoto wachanga na wanyama wauawe!

Kurani Inasema Nitatia hofu katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo, na wapigeni katika kila ncha ya vidole."

Hivi kweli? Huyu ndiye Mungu mnayemsujudia? Huyu ni Mungu au ni jenerali wa vita wa Kiarabu au Kizungu? Hapa ndipo walipochemsha! Wangemfanya MUNGU kuwa MWEMA pekee, Mungu ambaye ni nuru tupu, asiye na chembe ya ukatili, tusingekuwa hapa tunabishana leo.

Hivi vitabu vililetwa kututawala na kutuliza amani duniani kwa kutumia hofu. Wazungu na Waarabu walijua fika kuwa ili kumfanya binadamu awe mtumwa mnyenyekevu, ni lazima umtengenezee hofu ya kitu asichokiona.

Hoja zako ni hisia, si ushahidi.
Kusema Biblia na Qurani "zilitungwa na Wazungu na Waarabu" ni kudai jambo kubwa bila kuthibitisha.

Biblia iliandikwa karne nyingi kabla ya ukoloni wa Ulaya, na Qurani iliteremshwa katika mazingira ya kihistoria yanayojulikana.

Ukikataa vitabu hivyo, leta ushahidi wa kihistoria, si nadharia za njama. Maoni binafsi hayawezi kufuta historia.
 
Lete ushahidi wewe viliteremshwa na nani na kutoka wapi usiseme Karne nyingi be specific MUNGU HANA DINI WALA KITABU
 
Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kwamba Biblia iliandikwa na waandishi mbalimbali wa Kiyahudi na Kikristo katika vipindi tofauti, huku Qurani ikihifadhiwa kama ufunuo alioupokea Muhammad.

Ukisema havikutoka kwa Mungu, hilo ni dai lako. Sasa wewe uthibitishe nani alivitunga na ushahidi wako ni upi. ??

Kusema "Mungu hana dini wala kitabu" ni maoni, si ushahidi wa kihistoria.
 
Ivi unajua kwamba kuruan ni biblia iliyoandikwa kwa lugha ya kiarabu tofauti ni ndogo sana lakini pia unajua kwamba chimbuko la uislam ni Roma kanisa katoliki?
 
Hayo siyo madai yanayoungwa mkono na historia.

Qurani si tafsiri ya Biblia kwa Kiarabu, na Uislamu haukutokana na Kanisa Katoliki wala Roma.

Kama una ushahidi wa kihistoria kutoka vyanzo vinavyotambulika, uwasilishe.

Madai makubwa yanahitaji ushahidi mkubwa, si kauli tu.
 
Wewe kumbe unafuata historia aliyoandika mzungu ivi unadhani kuitawala Dunia ni Kitu rahisi eeh mzungu amechakachua kila Kitu na kupitia DINI ndio amefanikiwa sana unaweza kuniambia kwanini china na Japan hakuna DINI? Kwahiyo kule Mungu hausiki?

we
 
Kila wakati sema Mungu ni mwema uepukane na dhahama za walimwengu

Onesha point nzitonzito ushughulikiwe au ujifanye mjinga ubembee.... Jiongeze mtu wangu
 
Wewe kumbe unafuata historia aliyoandika mzungu ivi unadhani kuitawala Dunia ni Kitu rahisi eeh mzungu amechakachua kila Kitu na kupitia DINI ndio amefanikiwa sana unaweza kuniambia kwanini china na Japan hakuna DINI? Kwahiyo kule Mungu hausiki?

we

Kama unakataa kila historia kwa sababu imeandikwa na "Mzungu", basi hicho unachokijua kuhusu China na Japan unakitoa wapi?

Pia ni kutoka historia.

Halafu kusema China na Japan "hazina dini" kunaonyesha hujui historia, zote zina dini na falsafa kama vile Ubudha, Ushinto, Utao na Ukonfyushasi.

Hoja ijengwe kwa ushahidi, si nadharia za njama.
 
Upo sahihi hizo ni DINI zao za asili Yao sio za mzungu wala muarabu wewe umeacha asili yako unafuata DINI za wazungu na waarabu.
 
Back
Top Bottom