Kumkamata Aliyepiga picha watoto wakiwa chini ni kumuonea, zipo shule nyingi watoto wanakaa chini

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Kufuatia sakata la picha liyopigwa ikionesha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sinde wakiwa wamekaa wakisoma chini bila madawati na Serikali ikionekana kung'aka kwa kumuweka ndani anayesemekana kupiga picha hiyo ni sawa na mbuni kujifunika kichwa huku mwili ukiwa nje na akidhani kajificha. Soma Mbeya: Mwalimu aliyesambaza picha za Wanafunzi wamekaa chini, aingia matatani

foyxyjpxsaa5dru-jpg.2510070

Kwa Tanzania hii siyo Sinde pekee ambayo watoto wanasoma wakiwa chini bila madawati hivyo hata serikali ikijaribu kumtoa kafara huyo mpiga picha na raia mwema ili iweze kuficha aibu yake ni sawa na bure kwa kuwa ukweli ni kuwa hali hiyo ipo kwa shule nyingi nchini japo makujwaani mnajinadi kuwa mmeboresha mazingira ya elimu ila ukweli ni kuwa watoto wanasoma katika mazingira magumu sana.

Turudi Sinde, imeonekana baada ya Viongozi kufika hapo shuleni madawati yalikuwepo darasani hivyo kuonekana huyo mpiga picha anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo alizusha ili kuleta taharuki.

Najiuiliza nani anadanganya kati ya Mwalimu na Serikali?
  • Je, Mwalimu alitoa madawati na kuwaamuru wanafunzi wakae chini ili apige picha asambaze uongo?
  • Je, baada ya Serikali kuona taarifa imefika kwa wananchi wakaweka madawati ili waweze kukanusha taarifa ya awali ionekane alizusha na aadhibiwe ili kuwatia hofu wengine wasifichue maovu?
Baada ya sinema hii nini kitajiri, iwapo Serikali itafanikiwa katika hili basi ni wazi watu wataingia ganzi kufichua madhaifu au uovu wowote hata unaoonekana kwa macho na kufanya jamii ibaki katika giza na maumivu ya kuishi na uduni kwa kuwa ukisema inabadilishwa na unakuwa mhalifu na kushikwa na polisi.

Iwapo Mpiga picha au picha ikaweza kuthibitisha kuwa ni kweli walikuwa wanakaa chini kwa kukosa madawati basi ni wazi Serikali itapata aibu na itakuwa imejishushia zaidi heshima na kufanya hata ikiwa wanakanusha kitu hata kama ni kweli kilizushwa jamii ione wanadanganya kama ambavyo imekuwa hapo zamani.

Leo tukisema kila shule ilete takwimu za watoto wanaokaa chini au picha nchini hapa Serikali itaweka ndani nchi nzima kwa kuwa ni nyingi na si Sinde pekee, au kwakuwa anatoka Spika wa bunge ndio maana Serikali imeona haifai taarifa hii itoke kwa umma? Shule nyingi hazina madawati japo tumejaza misitu na tunajimwambafai kuupiga mwingi katika elimu.

Badala ya Serikali kuhangaika na watoa taarifa kuwakamata iboreshe shule zote kwa kuhakikisha zina miundombinu inayotakiwa kuanzia madawati, vyoo, madarasa na vifaa vya kufundishia kwa kuwa naamini uwezo huo upo ila havifanyiki kwa kuwa hakuna anayeona maumivu ya mtoto wa kitanzania kukaa chini kwa kuwa watoto wa wenye mamlaka hawasomi shule za Serikali.

Pia soma:
 
Kama ni kweli Watoto wetu wanakaa sakafuni halafu fedha zetu zinapigwa kila uchwao wanafikiri Watanzania ni Mazuzu.
 
Hii shule au niite hilo darasa huwa halina madawati, hata nikitazama sura za hao wanafunzi hapo darasani, na namna wengine walivyojiongeza kuandikia juu ya goti napata uthibitisho wa mawazo yangu.
 
1977 nilitumia darasa kama hilo!
 
Aisee hivi kwanini wamekanusha kwa kutumia nguvu vile kuficha.
 
Halafu hivi watu walipe kodi halali na kamili?

Serikali kuingiza siasa kwenye kila jambo kunawavunja sana moyo wa kulipa wananchi mwenyewe nikiwepo maana hatuoni hela zinakoenda zaidi kusikia kila uchwao hapa wamepiga kule wamepiga na kule wanajiandaa kupiga.
 
Kufuatia sakata la picha liyopigwa ikionesha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sinde wakiwa wamekaa wakisoma chini bila madawati na Serikali ikionekana kung'aka kwa kumuweka ndani anayesemekana kupiga picha hiyo ni sawa na mbuni kujifunika kichwa huku mwili ukiwa nje na akidhani kajificha. Soma Mbeya: Mwalimu aliyesambaza picha za Wanafunzi wamekaa chini, aingia matatani

foyxyjpxsaa5dru-jpg.2510070

Kwa Tanzania hii siyo Sinde pekee ambayo watoto wanasoma wakiwa chini bila madawati hivyo hata serikali ikijaribu kumtoa kafara huyo mpiga picha na raia mwema ili iweze kuficha aibu yake ni sawa na bure kwa kuwa ukweli ni kuwa hali hiyo ipo kwa shule nyingi nchini japo makujwaani mnajinadi kuwa mmeboresha mazingira ya elimu ila ukweli ni kuwa watoto wanasoma katika mazingira magumu sana.

Turudi Sinde, imeonekana baada ya Viongozi kufika hapo shuleni madawati yalikuwepo darasani hivyo kuonekana huyo mpiga picha anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo alizusha ili kuleta taharuki.

Najiuiliza nani anadanganya kati ya Mwalimu na Serikali?
  • Je, Mwalimu alitoa madawati na kuwaamuru wanafunzi wakae chini ili apige picha asambaze uongo?
  • Je, baada ya Serikali kuona taarifa imefika kwa wananchi wakaweka madawati ili waweze kukanusha taarifa ya awali ionekane alizusha na aadhibiwe ili kuwatia hofu wengine wasifichue maovu?
Baada ya sinema hii nini kitajiri, iwapo Serikali itafanikiwa katika hili basi ni wazi watu wataingia ganzi kufichua madhaifu au uovu wowote hata unaoonekana kwa macho na kufanya jamii ibaki katika giza na maumivu ya kuishi na uduni kwa kuwa ukisema inabadilishwa na unakuwa mhalifu na kushikwa na polisi.

Iwapo Mpiga picha au picha ikaweza kuthibitisha kuwa ni kweli walikuwa wanakaa chini kwa kukosa madawati basi ni wazi Serikali itapata aibu na itakuwa imejishushia zaidi heshima na kufanya hata ikiwa wanakanusha kitu hata kama ni kweli kilizushwa jamii ione wanadanganya kama ambavyo imekuwa hapo zamani.

Leo tukisema kila shule ilete takwimu za watoto wanaokaa chini au picha nchini hapa Serikali itaweka ndani nchi nzima kwa kuwa ni nyingi na si Sinde pekee, au kwakuwa anatoka Spika wa bunge ndio maana Serikali imeona haifai taarifa hii itoke kwa umma? Shule nyingi hazina madawati japo tumejaza misitu na tunajimwambafai kuupiga mwingi katika elimu.

Badala ya Serikali kuhangaika na watoa taarifa kuwakamata iboreshe shule zote kwa kuhakikisha zina miundombinu inayotakiwa kuanzia madawati, vyoo, madarasa na vifaa vya kufundishia kwa kuwa naamini uwezo huo upo ila havifanyiki kwa kuwa hakuna anayeona maumivu ya mtoto wa kitanzania kukaa chini kwa kuwa watoto wa wenye mamlaka hawasomi shule za Serikali.

Pia soma:
Tuliambiwa nchi imeingia kwenye uchumi wa kati na ni Dona country imekuwaje tena tumerudi nyuma hebu tusaidiane tueleweshane tatizo nini??
 
Back
Top Bottom