Ufisadi shule ya Arusha primary school

bugzbunny

JF-Expert Member
Mar 9, 2013
838
748
Shule ya Arusha primary ni moja kati ya shule kongwe sana nchini Tanzania zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza. Ilianza rasmi mwaka 1932.

Shule hii ambayo kwa sasa ipo chini ya Jiji , miezi ya karibuni imekuwa na mabadiliko mazuri ya kitaaluma, na kiutendaji, chini ya mwalimu mkuu Ridhiwan. Watoto wamekuwa wakifundishwa vizuri, ufaulu umeongezeka na chakula shuleni kizuri na ada nafuu kwa watunwa chini wenye kutaka elimu bora kwa watoto wao. Pia, rushwa imepungua, maana kulikuwa na watoto wanasoma bure pale!! Hasa wa watumishi wa serikali. Ada watu wanakunja mfukoni.

Sasa mazuri yote yanaelekea kuharibika na yote ni sababu ya local government, Yani jiji, madiwani na mkurugenzi wake.

Mfano, ada ya kutwa , pamoja na chakula ilikuwa 570000 kwa mwaka.(Hivi ni shule ya umma kumbuka). Sasa hivi, ada ni 500000 na chakula ni 350000 Yani kimsingi kuna 350000 imeongezeka! Ajabu!

Kwanini nasema ni ajabu? Shule hii inapokea ruzuku kutoka serikalini takribani milioni 60 hadi 70, makusanyo ya ada tu ni billion 1 na kitu! Alafu nusu eti ya hii pesa ni ya halmashauri kwa ajili ya maendeleo ya elimu jiji! Yani kwa kupitia ada za watoto wa watu!

Bado kuna miradi mfano ukumbi wa harusi na mikutano, kituo cha wanafunzi wa CPA! Michango pia ipo! nk. Hizi zote zinatosha sana kulisha watoto na ata kupunguza ada! Walimu wanajilipa posho milioni 125 na zaidi! Kweli? Na bado kuna baadhi ya watoto wanafika darasa la 7 bila kujua kusoma sawasawa!

Wito wangu, serikali kama ipo kweli na wananchi wa hali ya chini, ifanye uchunguzi mkubwa sana na vyombo vya dola kama TAKUKURU na vingine vihusishwe. Special Audit ifanyike!
 
Mpelekee mwanao shule za Bure hawalipi hata kumi huku Gugambwike Primary School
 
Back
Top Bottom