Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,161
- 1,493
Dunia kwa ujumla inapitia changamoto ya matarajio ya kuporomoka kwa uchumi, kwa kuwa Tanzania ni sehemu ya Dunia pia inapitia changamoto ya mfumuko wa bei( kwa Afrika Mashariki Tanzania ni nchi ambayo imedhibiti mfumuko wa bei kuliko nchi nyingine)
Ni muhimu Watanzania kujua Serikali hii ya awamu ya sita imefanya kila jitihada kuhakikisha kuwa
1.Huduma za Afya zinaboreshwa kwa kuhakikisha Kila mkoa na Wilaya kuna Hospital zenye Wataalam wa kutosha na vifaa vya kutosha. Kila kata kuna vituo vya Afya ambavyo vina Watalaam , vifaa na dawa za kutosha. Aidha kila kila kijiji kwa sasa kuna Zahanati yenye Wataalam wa Afya wa kutoa huduma kwa Watanzania.
2. Elimu.. Serikali ya awamu ya sita imejenga kila mkoa Shule Maalum ya masomo ya Sayansi kwa ajili ya watoto wa kike. Kwa sasa hakuna kata isiyokuwa na shule y Sekondari. Asilimia 95 ya Watoto wanaomaliza darasa la saba wanaendelea na Elimu ya Sekondari. Kwa sasa Wanafunzi wote wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati, awamu hii yamejengwa madarasa ya kutosha kwa kila shule iliyopo Tanzania. Kama kuna Mwnafunzi anakaa chini basi Mkurugenzi wa eneo hilo anafaa kujitathimini.
3. Umeme, yawezekana hii ndio ikawa historia ya Tatizo la umeme Tanzania. JNHPP na miradi mingine ya nishati ya upepo, jua inayoazishwa inaiweka Tanzania kuwa ni moja ya nchi itakyokuwa na nishati ya ziada mpaka kuweza kuuzia nchi nyingine za Afrika Mashariki.
4. Barabara, kwa sasa unatoka Dar Es Salaam mpaka Kigoma, Katavi, Rukwa, Mtwara barbara zote zimeunganishwa kwa mtandao wa lami. Barabara zote zinafikika kipindi chote cha miezi 12.
5.Ugatuzi wa madaraka, ni awamu hii ambayo Watanzania wameshika hatamu ya uongozi, Madaraka yako kwa Wananchi. Watanzania wanaelewa na kusimamia miradi inayoazishwa.
6. Awamu hii ndio imetenda haki kwa Watumishi wa Umma, Watumishi wa Umma ambao miaka mingi walistahili kupanda madaraja na hawakupandishwa sasa wamepandishwa mseleleko. Watumishi wote wamelipwa madai yao yote waliyokuwa wanadai kwa miaka mingi.
Hakuna Taifa lisilo na changamoto, Tuendelee kuiombea Tanzania.
Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania
Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan