Wakuu nimetafakari sana nimegundua kumiliki gari ukiwa TZ sio jambo dogo tofauti na nchi jirani. Gari linachukua pesa zako nyingi sana kwa mara moja. Kwa mfano ukiagiza gari ulilolipia labda Tsh 10m itakulazimu uandae kiasi kama hicho ndani ya siku 45 ulipie kodi na gharama zingine za kuingiza gari nchini. Ni jambo zito. Nchi kama Zambia hilo gari la 10m unaweza lipia kiasi kisichozidi Tsh 4m kodi na gharama zingine zote ndo maana majamaa wananunua sana magari. Gari kama Passo wao hulipia Tsh 1.8m hadi 2.6m
Kimsingi ukiwa Tanzania bora ujiunge na kundi la baba wenye nyumba kisha gari ifuatie baadae. Nyumba ya kawaida ukiwa na 2m inafanya kazi kubwa. Vinginevyo unaweza kujiumiza sana kugharamia gari kwa mtu ambaye ndo umeanza biashara au ajira.
Huu uzi uzingatiwe sana na vijana wadogo.