Kahama: Paul Makonda ataka Caroline apewe eneo la Serikali, Mkurugenzi asema kumiliki Ardhi ni jambo la kisheria sio siasa

Mr Beast

Senior Member
Nov 8, 2023
184
295
IMG-20240129-WA0036.jpg
Haraka haraka kwenye mada,

Mhe Paul Makonda, mwenezi wetu pole na hongera kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya katika kulijenga na kulitetea Taifa letu na chama chetu Cha Mapinduzi, hakika unastahili pongezi kwa hili.

Mhe Paul Makonda, Majuzi wakati ukiwa hapa Kahama kuna jambo lilinishtua na roho ikaumia sana wakati unalazimisha yule dada Caroline apewe eneo ambalo ni mali halali ya Serikali (Umma).

Mhe Paul Makonda, Nilishangaa zaidi kuona kwanini hawa watu wabaya watumie jukwaa lako kutengeneza Uongo na kutaka kuiba mali za umma zilizopo kihalali huku wakikuhusisha wewe katika nia zao hizo ovu?

Mhe Paul Makonda, yule mama Caroline aliyekuwa anakulilia kisanii pale viwanjani Mimi namfahamu na mgogoro wake pia naufahamu vizuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho ulidanganywa.

Mhe Paul Makonda, Nafahamu Mama huyu tangu alivyoshindwa kesi katika mahakama ya Wilaya ya Ardhi Kahama na baadae akakata rufaa Mahakama kuu Shinyanga mahakama zote hizi zilitamka kuwa lile ni eneo la Serikali (umma).

Mhe Paul Makonda, Kama utataka kujiridhisha zaidi mwambie akuletee uamuzi wa mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga kama alivyodai mbele ya umma kuwa ameshinda kesi.

Mhe Paul Makonda, Ukweli kuhusu madai ya Caroline unaweza pia kuwauliza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Sophia Mjema au aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Anamringi Macha ambae Sasa ndio Naibu Katibu Mkuu wa Chama chetu hawa wote wanamfahamu Caroline na eneo pia wanalifahamu watakupa ukweli wote.

Mhe Paul Makonda, najiuliza kwanini mtu atake kuchukua eneo la Umma na wewe bila kujali Wala kudadisi kwa kina unataka kumpa sapoti achukue mali ya Serikali (umma) kwani huoni kama kwa kufanya hivyo unachochea mgogoro zaidi?

Mhe Paul Makonda, Nataka nikueleze kuwa Kahama tunamkurugenzi ambae kwanza hanunuliki lakini pili ni mtu mwadilifu na anauchungu na mali za Serikali ndio maana unaona hataki janja janja hizi za watu kupora mali za umma.

Mhe Paul Makonda, Wilaya ya Kahama imepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kwa haraka na Watanzania wanalijua hili ukilinganisha na Halmashauri nyingine zote hapa Tanzania bara na hata huko Visiwani.

Mhe Paul Makonda, kama Kuna sababu tatu kubwa za Kahama kuwa hivi ilivyo Leo basi moja ni uwepo wa huyu mkurugenzi mwadilifu na ndio sababu Halmashauri zote Tanzania wanakuja kujifunza hapa Kahama " Mkurugenzi huyu ni shamba darasa kitaifa "

Mhe Paul Makonda, Mkurugenzi huyu kaitoa Kahama kwenye Halmashauri ya Wilaya hadi leo ni "Municipal council" Waswahili tunasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe ukweli ni kwamba binadamu wote tunayo madhaifu ila huyu anajitahidi sana kuyapunguza.

Mhe Paul Makonda, Najua unajua mtu anayefañya kazi vizuri wakati wote hapendwi hasa na majizi na wapigadili, Ukweli mchungu huyu jamaa sio mwizi Wala mlarushwa TAMISEMI wanajua hivyo na ndivyo ilivyo.

Mhe Paul Makonda, hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa ukusanyaji wa Mapato Tanzania kama sio Kahama tena hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa miradi ya maendeleo kwa Fedha za ndani kama sio Kahama au hebu nitajie Wilaya moja inayoitwa Mkoa wa Kikodi hapa Tanzania kama sio Kahama.

Mhe Paul Makonda, Tunapopata vijana waadilifu na Waaminifu kama hawa lazima tuwapongeze na kuwatia moyo nasio kuwakemea na kuwadhalilisha mbele ya halaiki bila kujali kazi kubwa wanayoifanyia nchi yetu.

Mwisho, Tupelekee salamu zetu kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwambie kura zake za mwaka 2025 Kahama zimetimia hata kama Uchaguzi utakuwa ni kesho mama anashinda kwa kishindo.

Ni mimi Mabula Malunde Sitta.
 
Andiko lilianza kitaalam sana na kiuweledi juu ya namna ya kutatua kero pasipo double standard. Ghafla likawa na UCHAWA wa mfuagilia DED kana kwamba ameliandika kujifuta machozi au kupata utetezi au ametuma watu a.k.a wapambe.

Likaishia na Tamko langu la sasa

"KWA HALI HII YA KUKATIKA KWA UMEME."
"Twende na mama. MITANO TENA
 
Makonda anaendesha kesi jukwaani, hasikilizi pande zote, na mara zote anaona upande wa serikali ndio umekosea.

Ni sawa na Jerry Silaa pale Mwanzaa, kaamua kumnyanganya eneo afisa ardhi ili ampe shosti wake Kamani wa UVCCM

Hata ile issue ya waziri Nicas Mahinda, yule dogo aliyekuwa anatamba sana ni mshikaji wa muda mrefu wa Jerry Silaa, kwa hiyo hatujui ushkaji wake na watu ataumiza wangapi. Na kwa nini asishauri watu waende Mahakamani kuliko kuiingiza serikali katika migogoro ili kusaidia washkaji zake.

Haifahamiki kama anafanya consultation na ofisi ya mwanasheria mkuu au wakili mkuu wa serikali kabla ya kutamka ugoro wake.
 
Huyu Mkurugenzi wa Kahama ni mwadilifu sana na kama tungekuwa na Wakurugenzi 100 tu kama hawa basi Taifa lingekuwa mbali sana
Nchi ingekuaje mbali na taifa alipendi watu waaminifu?. Hata huyo makonda ambaye kila wakati unamtamka mheshimiwa mheshimiwa yupo hpo sababu waovu mnawapenda zaidi kuliko waadilifu na waaminifu. Makonda Ni sehemu ya watu waovu katika taifa hili. Nakupa mfano mdogo Sana Mh Lukuvi alipokuwa waziri wa ardhi alikomesha kabisa huu Upumbavu wa migogoro ya ardhi wakamtoa leo migogoro imerudi kila sehemu. Alafu makonda anazurura kujifanya anatatua kitu ambazo wanakitengeneza wenyewe . Hii nchi inapenda Sana watu waovu na kuwasifia.
 
Andiko lilianza kitaalam sana na kiuweledi juu ya namna ya kutatua kero pasipo double standard. Ghafla likawa na UCHAWA wa mfuagilia DED kana kwamba ameliandika kujifuta machozi au kupata utetezi au ametuma watu a.k.a wapambe.

Likaishia na Tamko langu la sasa

"KWA HALI HII YA KUKATIKA KWA UMEME."
"Twende na mama. MITANO TENA
Hapana Makonda ameahidi kumngo'a huyu Mkurugenzi regardless yote aliyoyafanya nadhani ndio maana mwandishi kamkumbusha haya,
 
Haraka haraka kwenye mada,

Mhe Paul Makonda, mwenezi wetu pole na hongera kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya katika kulijenga Taifa na chama chetu Cha Mapinduzi, hakika unastahili pongezi kwa hili,

Mhe Paul Makonda, Majuzi wakati ukiwa hapa Kahama kuna jambo lilinishtua na roho iliniuma sana wakati unalazimisha yule dada Caroline apewe eneo ambalo ni mali ya Serikali ( Umma )

Mhe Paul Makonda, Nilishangaa sana kwanini hawa watu wabaya watumie jukwaa lako kutengeneza Uongo na kutaka kuiba mali za umma zilizopo kihalali tena wakikuhusisha mpaka wewe katika nia zao hizo ovu!!??

Mhe Paul Makonda, yule mama Caroline aliyekuwa anakulilia pale viwanjani Mimi namfahamu na mgogoro wake kuanzia mwanzo mpaka mwisho naufahamu pia,

Mhe Paul Makonda, Mama huyu tangu alivyoshindwa kesi katika mahakama ya Wilaya ya Ardhi Kahama na baadae akakata rufaa Mahakama kuu Shinyanga mahakama zote hizi zilitamka kuwa lile ni eneo la Serikali ( umma) kama utataka kujiridhisha mwambie akuletee uamuzi wa mahàkama kuu kama alivyodai ameshinda kesi,

Mhe Paul Makonda, Ukweli kuhusu madai ya Caroline unaweza pia kuwauliza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Sophia Mjema au aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Anamringi Macha ambae Sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama chetu hawa wote wanamfahamu Caroline na eneo pia wanalifahamu watakupa ukweli wote,

Mhe Paul Makonda, kwanini mtu atake kuchukua eneo la Umma na wewe bila kujali Wala kudadisi kwa kina unataka kumpa sapoti achukue mali ya Serikali( umma)?

Mhe Paul Makonda, Nataka nikueleze kuwa Kahama tunamkurugenzi ambae kwanza hanunuliki lakini pili ni mtu mwadilifu na anauchungu na mali za Serikali ndio maana unaona hataki janja janja hizi za watu kupora mali za umma,

Mhe Paul Makonda, Wilaya ya Kahama imepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kwa haraka na Watanzania wanalijua hili ukilinganisha na Halmashauri nyingine zote hapa Tanzania bara na hata Visiwani,

Mhe Paul Makonda, kama Kuna sababu moja kubwa ya Kahama kuwa hivi ilivyo Leo basi ni uwepo wa huyu mkurugenzi na ndio sababu Halmashauri zote Tanzania wanakuja kujifunza hapa Kahama ( Mkurugenzi huyu ni shamba darasa kitaifa )

Mhe Paul Makonda, Mkurugenzi huyu kaitoa Kahama kwenye Halmashauri ya Wilaya hadi leo ni "Municipal council" Waswahili tunasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe,

Mhe Paul Makonda, Najua unajua mtu anayefañya kazi vizuri wakati wote hapendwi hasa na majizi na wapigadili, Ukweli mchungu huyu jamaa sio mwizi Wala mlarushwa TAMISEMI wanajua hivyo na ndivyo ilivyo.

Mhe Paul Makonda, hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa ukusanyaji wa Mapato Tanzania kama sio Kahama tena hebu nitajie Halmashauri moja inayoongoza kwa miradi ya maendeleo kwa Fedha za ndani kama sio Kahama au hebu nitajie Wilaya moja inayoitwa Mkoa wa Kikodi hapa Tanzania kama sio Kahama,

Mhe Paul Makonda, Tunapopata vijana waadilifu na Waaminifu kama hawa lazima tuwapongeze na kuwatia moyo nasio kuwakemea na kuwadhalilisha mbele ya halaiki bila kujali kazi kubwa wanayoifanyia nchi yetu.

Mwisho, Tupelekee salamu zetu kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwambie kura zake za mwaka 2025 Kahama zimetimia hata kama Uchaguzi utakuwa ni kesho mama anashinda kwa kishindo.



Ni Mimi Mabula Malunde Sitta.
Mkurugenzi simama hivyo hivyo hata kama utabaki peke yako Mungu atakutetea
 
Back
Top Bottom