Kumiliki gari kunaficha umasikini

Kumiliki gari kunaficha umasikini

Ukiwa na gari hadi vizee vya mtaani vinakuheshimu...
Hata mtu mzima aliekuzidi umri atakuita "baba" au "mama". Ila kama mfuko ni wakulenga kwa manati, kidumu cha lita 5 kwenye buti hakikosekani.

Muda wowote kuna kukimbilia mafuta kituoni.
 
Hahaha,.kuna mshikaji siku moja nilipanda gari yake...kumbe futa la kuungaunga kufika kilima nyege si likazimika bana....kuangalia kwenye buti kasahau kidumu....dah nilicheka ile siku maana nikifikiria kusukuma gari shida...akabaki anahangaika nalo..kama bahati kuna mtu alipita akampa msaada
Ukipakiwa kwenye gari, halafu ukacheki nyuma na ukaona kuna kidumu cha mafuta kipo standby. Nakushauri ushuke, bora uchukue bodaboda au uber.

Au lasivyo kuna kusaidia kuisukuma muda wowote, [emoji18]
 
Kabala ya kuwa na familia sikuona kama gari ni kitu muhimu ! Baada ya kuoa na pilika za kulea, taabu nilizopitia , vile wife mjamzito kwenye daladala za mbagala. ......aiseee nilikua nalia kiume machozi ndani kwa ndani ! Mtoto mchanga na mama yake hayuko stable anaumwa. ... Kukimbilia kugombea dala dala .... Aiseeee ......aiseeeeee.....
Nilivyopata mwanya tu vuta ndinga wanangu na wife wakomboke . ...... Gari imenipa amani sana na ari ya kupambania vingine
 
Back
Top Bottom