Kumiliki gari kunaficha umasikini

Kumiliki gari kunaficha umasikini

Kwa mliooa gari ukiwa nalo kuna uzuri na karaha zake
Karaha zake
Mkeo akiona umempa mwanamke mwingine lift asiyemjua na tena akawa siti ya mbele ni shida
Ila yeye kumpa mwanamme lift hata usiyemjua mwanamme ukiona sio shida.

Ukute mwanamke mafuta kwenye gari kaweka yeye wewe ukatoka nako kusikojulikana ni kero
Ukinunua gari mwanamke ajue tu kuendesha kosa linakuwa lake especially kama huna mcheche na magari.

Sisi wanaume kumpa mwanamke usiyemju lift ni rahisi kuliko kumpa mwanaume mwenzio
Wanawake wao ni kinyume kumpa mwanamke mwenzake lift asiyemjua ni mwiko akome ila kumpa lift mwanaume asiyemjua ni kawaida maana anapiga hesabu likizima ana ulinzi anaweza msaidia kusukuma sio mwanamke mwenzake.

Kama ndoa yako na mkeo inayumba gari linaweza kuzidisha myumbo mwanaume ukiwa na tabia ya umalaya tayari umeshapata kivutio madem hivyo mke vile anajua tabia yako mtagombana sana.

Nilipokuwa chuo siku moja nilishangaa sana inakuwaje lecturer ana gari lake wakienda kazini na mke naye ana gari lake kila mmoja kwa wakati wake anakwenda na gari lake.Nilijiuliza sana kwanini wasitumie moja ila kua uyaone nimekua na nimeshayaona ajili ya kuondoa kero kama hizi.Kama mna uwezo kifedha ni vyema kila mmoja akawa na gari lake.

Ukimpita jirani yako bahati mbaya vioo vyako kama ni tinted ila ndani kumbe kuna watu hawaoni ni kosa majirani watasema hutoi lift unaringa.

Ukipita sehemu ukute mtu analima mchicha wake ukakanyaga maji yakaruka yakanyweshea mchicha yule mwenye mchicha atasema unafanya makusudi kwa vile una gari kumbe hajui anatakiwa akushukuru kwa kumsaidia kunywesha michicha yake.

Ukiishi sehemu ambayo mwenye gari ni wewe peke yako utapata kero nyingi watu kukuomba msaada wa dharura hata kama ni saa nane usiku ukute mtu mkewe anakwenda kujifungua.Kibaya zaidi uwe huna mafuta au gari labda lina hitlafu ukiwapa ukweli hawatakuelewa watasema unaringa.

Wengine wanaweza hata kudiriki kufunga njia usipite na gari lako.

All in all yote yanavumilika ila kwa dunia ya sasa gari ni muhimu kama una uwezo is no longer a luxury kama vile zilivyoanza kuingia simu za mkononi mwanzoni.
 
Back
Top Bottom