Kumiliki gari kunaficha umasikini

Kumiliki gari kunaficha umasikini

Ingawa ndiyo kwanza naanza maisha ila gari ni miongoni mwa vipaumbele vyangu pale 'mishemishe' zitapokaa vizuri. Kuna kipindi mzee wangu alikua anaumwa sana na safari za kwenda na kurudi kutoka hospital zilikuwa ni za kila siku, sio siri tulipata shida sana kwani tulikuwa tunatumia 35-40 kila siku za kukodi gari, bado na za kumlipa dereva na hali ilikua hivi kwa takribani miezi miwili. Sasa hivi 'mzee' amepata nafuu ameapa huu mwaka haumalizi lazima aweke hata 'babywalker' uani ili kupunguza karaha.
 
Mk
Gari bhana.

Wanaomiliki magari wanaaminika sana kwamba wana hela, hawana dhiki.

Mtu mwenye gari anaeleweka haraka sana na anaaminika mno kuliko wewe unayetembelea ngondi ama Toyo.

Gari ni kama shetani fulani.

Gari huficha umaskini kwa kiasi kikubwa sana.
Mkuu mm sina gari lakini naaminika na kueleweka sana tofaauti na unavyofikiria.
 
Yaani umenikumbusha jana nilikwenda kwenye Pub flani na hawanijui nikanywa hela ikakata..nikanywa tena...mwisho nikamwambia mwenye Pub nitakucheki kesho...na gari nilikuwa nimepaki mlangoni kabisa..hakunibishia
 
Ukipakiwa kwenye gari, halafu ukacheki nyuma na ukaona kuna kidumu cha mafuta kipo standby. Nakushauri ushuke, bora uchukue bodaboda au uber.

Au lasivyo kuna kusaidia kuisukuma muda wowote, [emoji18]
hahaha umenikumbusha mbali iko siku tulitoka club na gari ya mshkaji saa nane usiku mafuta yakakata...mfukoni hatuna kitu ilibidi tugeuke walinzi mpaka asubuhi
 
KUNA WALE WANAOMILIKI GARI KUNG,OLEA WATOTO WAKALI MJINI...DAAH NA WASICHANA WASIVYOPENDA TABU BASI KIULAAIIINI WANAZAMA
 
Gari ya anasa ndio chanzo cha umaskini, kabla hujanunua gari ni lazma utengeneze chanzo cha mapato ya kuliendesha, maana litahitaji elfu 10-30 kwa siku kulingana na condition yake na ukubwa wa engine.Ukiwa na chanzo kimoja cha kipato ndio utegemee kuendeshea gari hakyanani hutakaa uinjoy, ipo siku utalipaki tu unless otherwise uwe kibopa.
Nakumbuka kipindi napush range rover P38 ile gari ilikuwa 4.6 HSE inakamua 30k kwa misele ya daily tu. Kwenda BMTL/JHPIEGO na kurudi kitaani ila nissan bluebird 1.5 ltr engine ikawa inakaribia kufunga week on the same fuel amount ya 30k.
Ila lazma uwe na chanzo cha mapato nje ya mshahara ili kuinjoy ndinga.
nna jirani yangu gar inatembea tar 28 hari tar 1 au 2 inapaki [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], na tunaishi nnje ya mji huku alafu yeye kila siku lazima aende town namuoneaje huruma!! natamani kumshaur aiuze annue ki paso maana anateseka aisee usafiri wa huku ful kuunga kuunga.
 
Kwanza nikusahihishe hakuna binadamu anaemiliki gari bali gari ndilo linakumiliki

Pili hakuna masikin anaeweza kumilikiwa na gari,masikini hua anawaza kula zaid kuliko kumilikiwa na kitu... Haya endeleeni
 
Ningekuwa sijawahi miliki gari, ningekuwa na nyumba tatu Dar. Gari inakula pesa we acha. Kwa mwezi ukiweka wese la laki tatu ni sawa na pesa ya tofali mia tatu. Kwa mwaka je?
 
Back
Top Bottom