mchecheto
JF-Expert Member
- Oct 30, 2014
- 1,532
- 1,479
Kwa wanandoa.
it doesnt matter kwa wanani...we mwenyewe hapo hujaolewa ika unaonjaga
Kwa wanandoa.
Jana jioni nilikuwa mahali having dinner with a friend, sasa kuna vijana kama wa4 walikuwa meza ya jirani wanakula na kunywa, baada ya muda jamaa mmoja kati ya wale wa4 akaanza kulia hadi ikabidi mwenzao mmoja aondoke nae akampakia kwenye gari haoo wakaondoka.
Sasa ndio tukawa interested kujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea mpaka mtoto wa kiume atoe chozi namna ile, ikabidi tujongee tupate kuuliza maana tulihisi ni msiba.
Ndio tukapewa story;
Jamaa alikuwa na mchumba wake ambae wamedumu kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja na miezi4 na walitaraji mwezi wa6 mwaka huu wafunge ndoa. Na katika mahusiano yao walikubaliana hakuna kugegedana hadi watakapofunga ndoa.
Awali walikubaliana kuanza mipango ya kutambulishana mwezi wa11, na kijana alimpeleka binti kwao, ikawa imebaki kijana kwenda kwa akina binti na walikubaliana waende mwezi wa12, ila baadae binti akahairisha na kumueleza kijana kuwa isingekuwa muda mzuri kwani kwao kuna matatizo ya kifamilia.
Kumbe binti kule alikokua alianzisha mahusiano na kijana mwingine na mapenzi yalikuwa motomoto kabisa na walikuwa wakila tunda kama kawaida, baadae binti akanasa ujauzito na ndio kisa cha kumwambia kijana asubiri kwanza kwenda kujitambulisha.
Baada ya kunasa ujauzito wakakubaliana wahalalishe mahusiano yao kwa kutambulishana na waanze michakato ya kufunga ndoa na mwanaume alompa ujauzito. Mipango ilianza vyema kabisa na wakapanga kufunga ndoa mwezi wa4 mwaka huu.
Binti alishindwa namna ya kumueleza kijana ikabidi aanze visa tu, kwanza akamwambia kijana ameamua kurudi kuishi nyumbani kwao kwa muda maana mambo hayaendi vizuri hivyo hawakuonana tangu disemba, akimuuliza kuhusu mipango ya kutambulishwa ukweni anamjibu asubiri.
Sasa kati ya hao friends wake aliokuwa nao jana alipata habari bibie anaolewa na mipango iko hatua za mwisho kabisa. Jana ndio katika maongezi ndio anamwambia rafiki yake kuwa "yaani wewe na J kwa jinsi mlivyokuwa mnapendana nilijua mngeoana kabisa, kwani nini kilitokea mkaachana?" Jamaa akamjibu, "J bado tunapendana na hatujaachana na mwaka huu lazima tufunge ndoa Mungu akijaalia".
Rafiki mtu akahisi jamaa anatania.
To cut the story short, jamaa akaelezwa kila kitu na ili kuthibitisha akampigia rafiki wa J simu na akamthibitishia kuwa J anaolewa, ndio jamaa kupatwa na mshtuko na kuanza kulia.
all men ambao hawana experience na wanawake na hawajui vizur ugubegube wa wanawake, naturally they're good in their hearts sema wengi wao wanakutana na wrong women who take advantage of them kui
Hebu nipe maujanja.
Haha, that food was so good asee!
Jamani huyu kaka kanitia huruma, most men wangekuwa hivi dunia ingekuwa paradise ndogo.
Inatia sana faraja kujua kuna men wa hivi.
Kuna wanaoonha na wanatendwa na wanalia vile vile, kwahiyo kuonja hakukufanyi uwe safe.Sio uchochezi, ni msaada kwa vijana. Wengi wamekuwa wakilialia ovyo, hata humu jf.
Vijana wanajiua, wanaamua kuwa walevi kisa kutendwa.
Wakiwa na utaratibu wa kuonja mapema angalau haya majanga yatapungua kwa kiasi fulani.
Teh teh teeeeh!! As if nyie hatugeukagi na kutuachia maumivu!! Ujue rate ya wanawake wanaotendwa ni kubwa kuliko wanaume wanaotendwa!Wengine wanahangaika kutafuta dawa za kuongeza mitalimbo, hata tungekuwa na mitalimbo ya chuma hawa viumbe hawachelewi kubadilika. Hawaridhikagi hata kidogo.
Wenzio huwa na malengo zaidivya kugegedana, katika case hii utaona kuwa malengo yake na yako ni tofauti kabisaaaa. Sio wote wamekengeuka.Ndio maana nikipata kademu kapya nafanya maujanja nimgegede mapema zaidi ya mara tatu ili tukiachana isiniume sana.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]I think we must prioritize intentions to create legal relationships katika mapenzi ya sasa maana kuumizana kumezidi. Tukienda kisheria itasaidia sana maana atakaevunja mkataba wa uhusiano wetu itabidi alipe damages. Sio jitu unalisomesha toka O'level mpaka degree halaf mwishoni linakuja kuropoka kirahisi tu.."we sio type yangu!" ilihali umewekeza muda wako mwingi na mamilioni ya fedha kwake.
Inabidi hio kauli yake iambatane na indemnity charges tusileteane upuuzi!!!
Unajua ile ukipenda na kutrust too much, ukiambiwa jambo unaamini tu, kumbe mambo yashaharibikaDuh! inahitaji moyo kuangusha mchozi kwa penzi. Hii njemba ilitakiwa istuke mapema ilipoona mambo ndivyo sivyo lakini hakustuka maana alishajua wanapendana kupita kiasi kumbe mwenzie anakula kona.