talentbrain
JF-Expert Member
- Oct 5, 2009
- 1,187
- 760
Dah!!! Kuna wakati nilivutika saana na kanisa hili mpaka nikajiunga na kuanza kwenda kufanya ibada katika makanaisa yao. Ila baada ya kubaini mambo kadhaa na uigizaji wa kanisa hili niliamua akuacha kwenda huko na kuendelea na maisha yangu kama kawaida.
1. Maombi kuchukua muda mrefu sana huku tumefumba macho na kuinua mikono yetu juu. Kisayansi ni rahisi saaana mtu anayesimama muda mrefu huku ameinua mikono kuanguka. Nimejaribu kufanya hivyo hata nyumbani na matokeo ni yale yale.
2. Kuanguka na kupandwa na mashetani kwa watu wale wale kila siku ya ibada. Nilishangazwa saana kuona mashetani yanaendelea kuwarudia watu walewale kila siku. Hii ilininyima imani kabisa kiasi cha kuona ni usanii, Iweje Yesu aondoe mashetani na yarudie tena na tena??
3. Watu ambao huwa tunawaona mitaani na tunakula nao na hata wengine ni waume au wake wa watu kuombewa na kuanguka baadae kusema walikuwa wamechukuliwa na jirani, baba, mama au huyu na yule kishirikina. Hawa ndio watu wanaoitwa misukule katika kanisa hili. Kila nilipokwenda kanisani nilishuhudia mtu akisema amerudi kutoka alikokuwa amefungwa n.k Huu niliuona kuwa udhaifu mkubwa mno na kutudanganya. Kilichoniacha hoi ni msukule uliorudishwa jana yake kesho yake kuangushwa chini eti ana mapepo!!!!
Mnisamehe jamani ila mie siwezi rudi tena huko aseee!!!