Kumbe hii ndiyo Misukule ya Mchungaji Gwajima?

Status
Not open for further replies.

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
6,167
2,000
Watu ni wengi sana!Pembeni lilipaki Hummer kubwa jekundu. Majukwaa makubwa kabisa na maspika yasiyopungua 50 yanaashiria uwepo wa Mch mahiri na kijana kabis Gwajima hapa Morogoro!

Waimbaji wakubwa nchini Flora Mbasha,John Lissu na wengine wanasifu kwa bidii sana! Baada ya sifa Mch anaalikwa na anaanza kuhubiri sana kuhusu uchawi. Ameelezea aina za misukule na kwa nini hakumrudisha Amina Chifupa. Amepiga mkwara sana na kusema leo wanarudishiwa uhai.

Kweliii

Baada ya mahubiri anaomba kwa bidii na kuita njoooo. Watu kadhaa wanaanguka chini, wengine wanatembea kama wanyama, wengi wanakimbia kwenda mbele, baadhi ya watu wanakimbia kuogopa mikiki mikiki! Wanaoitwa misukule baaadhi wanatoa shuhuda walikokuwa wamefichwa!

Lakini nikajiuliza maswali kadhaa:
1. Mchungaji mbona anautajiri mkubwa sana?

2. Hawa misukule ni halisi na je, ndugu zao watawapokea ikiwa watajua kweli ni wao (maana kuna mmoja kadai alichukuliwa na mpangaji wao miaka 5 ilopita)

3. Hii injili inaelekea wapi? Sio kwamba hapa tunapigwa changa la macho?

4. Kwa uchunguzi mdogo, wengi wanaoenda wanapelekwa na kushangaa misukule, je jamaa anatumia nguvu za Kristu kweli aliye hai?

Please, mwenye historia kidogo ya huyu mchungaji atujuze.

Asanteni.


Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Tony Gwanco

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
5,915
0
kristu au kristo.hapo kwenye jogoo sijaelewa yaani badala ya kuita yesu yeye anaita jogoo
 
  • Thanks
Reactions: ilu

Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,419
2,000
Mathayo 24:24 Inasema;

For false christs and false prophets will arise and show great signs and wonders, so as to deceive, if possible, even the elect.


Jamani Yesu aliyaona haya nu Ukisoma Hiyo Mathayo yote 24 utaona Yesu akiweka wazi juu ya haya mambo!
 

Kingsimba

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
383
225
kuna bango moja pale mwenge linasema hivi kama sikosei njoo upewe kweli mzee kakobe yule me namkubali pomoja me ni muslim yule tyt yulemchungaji wa kweli hawa wengine duu namisukule yao tofauti kabisa bora babu marehemu kulola
 

kapuyanga mkware

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
589
0
kuna bango moja pale mwenge linasema hivi kama sikosei njoo upewe kweli mzee kakobe yule me namkubali pomoja me ni muslim yule tyt yulemchungaji wa kweli hawa wengine duu namisukule yao tofauti kabisa bora babu marehemu kulola

Tanzania hakuna uhaba wa wajinga.
 

Lusam

Senior Member
Apr 4, 2013
195
0
Mimi huwa najiuliza watu wanaenda kufanya nini kwenye hiyo mikutano ya matapeli. Mimi kamwe siwezi kanyaga.
 

Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,419
2,000
kuna bango moja pale mwenge linasema hivi kama sikosei njoo upewe kweli mzee kakobe yule me namkubali pomoja me ni muslim yule tyt yulemchungaji wa kweli hawa wengine duu namisukule yao tofauti kabisa bora babu marehemu kulola

Mkuu Tunataka Imani iliyokuja kuwakomboa watu Wote duniani!

Sio Kanisa la jina mtu!

Sio Kanisa la Jina la mji Au nchi!

Sio makanisa ya majina ya waasisi wao Wa zamani Au majina ya mataifa yalikotoka hayo makanisa!

Tunataka Imani isiyo na jina la mtu wala nchi ilikotoko Wala Jina la mji!

Sasa ukitazama majina ya makanisa mengi ni ya miji Au waanzirishi Au nchi, kitu ambacho kwenye bibilia Hakuna.

Someni bibilia Au maandiko mpate maarifa.
 

Free ideas

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
3,171
2,000
fanyeni kaz zenu achaneni na huyu tapel,ni mwiz wa kawaida sana na hana kipya zaidi ya marudio.nilishasema humu jinsi wanavo waandaa watu hawa na kuwapa maneno ya kusema na kisha kuwapa pesa kam elfu 50,kila mmoja.jamni mtaelewa lini???,
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom