Kumbe hii ndiyo Misukule ya Mchungaji Gwajima?

Kumbe hii ndiyo Misukule ya Mchungaji Gwajima?

Status
Not open for further replies.
Mkuu Tunataka Imani iliyokuja kuwakomboa watu Wote duniani!

Sio Kanisa la jina mtu!

Sio Kanisa la Jina la mji Au nchi!

Sio makanisa ya majina ya waasisi wao Wa zamani Au majina ya mataifa yalikotoka hayo makanisa!

Tunataka Imani isiyo na jina la mtu wala nchi ilikotoko Wala Jina la mji!

Sasa ukitazama majina ya makanisa mengi ni ya miji Au waanzirishi Au nchi, kitu ambacho kwenye bibilia Hakuna.

Someni bibilia Au maandiko mpate maarifa.

Mbona kwenye Ufunuo kuna mahali R/Mtakatifu anamwambia Yohana aandike Waraka kwa Makanisa kadhaa, ikiwemo EFESO,SARDI,FILADELFIA n.k je hii sio miji?
 
Yesu nae anasema siku Hiyo wengi watamuijia wakisema tulihubiri Kwa Jina lako na kufanya makubwa Kwa jina lako na Yesu atasema ONDOKENI

Yatupasa kuangalia vizuri ni namna gani Jina la Yesu linatumika!

Na kufanya miujiza kwanza sio kanuni ya injili ya Yesu!

Ebu jiulize, km Yesu angeweka Kwanza mbele Hiyo miujiza ni nani asingeamini Au kukataa?

Miujiza sio kanuni ya Injili ya Yesu!!??
 
Soma biblia wewe,ungewezaje kumtofautisha YESU na manabii wengine kama si kwa ishara na maajabu
aliyotenda?!! maisha yote ya YESU alitenda miujiza kwa kuponya wagonjwa na kufufua wafu na kulisha watu
kwa kumuujiza. Na alisema "Yeye aniaminiye atafanya haya,naam na makubwa kuliko haya". kwa mawazo
yako unamtofautishaje YESU nyakati hizi na mitume wengine,pamoja na neno lazima iambatane na nguvu za
kutenda ishara na maajabu kwa kuponya na kufunguliwa kwa wenye mateso kwa kuliitia jina la YESU'

You are Right!!
 
Mkuu nilichokua nazungumzia ni lile hekalu la Suleiman na Kwa sasa Tunaita makanisa! Sijui mpaka hapo nimeweka sawa?

Hata zamani kipindi cha Mussa lilikuwa linaitwa HEMA.
 
Nani kati yetu wana jf ameshawahi kuona ndugu,mwanafamilia kipofu,kiziwi,kilema kaombewa kapona? marehemu kafufuliwa?

Mfu sijaona ingawa najua wapo ila hao wengine nimewaona wengi sana including waliokuwa wamethibitishwa kuwa wana ukimwi muhimbili, mama Ngoma hosp na Kairuki anbao baada ya maombi walipona kabisa na hadi leo ni mwendo mdundo.
 
Mbona kwenye Ufunuo kuna mahali R/Mtakatifu anamwambia Yohana aandike Waraka kwa Makanisa kadhaa, ikiwemo EFESO,SARDI,FILADELFIA n.k je hii sio miji?

Ulishawahi kujiuliza juu ya Hilo andiko?
 
Mkuu nilisema Kua hii mada ni ndefu kidogo Kwasababu inaanzia mbali ingawa ilikua ikimlenga Yesu!

Labda niseme kidogo! Neno Kanisa Lina maana nyingi sana Lakini maana iliyo kubwa ni Mimi na wewe yani sisi tu hekalu la bwana! Na ukitaka kujua haya inakupasa uanzie kwenye Hema ya Patakatifu pa hapa duniani pa kwanza nyakati za Akina Aron na Musa!

Bwana Yesu anaposema kanisa lake anamaanisha wale wote wanaomwamini na ambao wanaelekea mbinguni. Kwahiyo Petro alikuwa amekabidhiwa watu hao, yaani, wafuasi wa Yesu awachunge na kuwalisha. Huu sasa ndiyo mwili wa Kristo. Kanisa maana nyingine ni jengo ambapo kunakuwa na kusanyiko la watu wanaomwabudu Mungu. Hili ni kanisa la mahali pamoja ambalo linaweza pia kujulikana kama hekalu. Vilevile hekalu linaweza likawa ni mwili wa mwamini mmoja mmoja ambapo unakuwa ni hekalu la Mungu kwa maana kwamba Mungu huishi ndani mwake na kumwongoza katika kutenda mema. Kumbuka Mungu hakai kwenye dhambi.
 
Watu ni wengi sana!Pembeni lilipaki Hummer kubwa jekundu. Majukwaa makubwa kabisa na maspika yasiyopungua 50 yanaashiria uwepo wa Mch mahiri na kijana kabis Gwajima hapa Morogoro! Waimbaji wakubwa nchini Flora Mbasha,John Lissu na wengine wanasifu kwa bidii sana! Baada ya sifa Mch anaalikwa na anaanza kuhubiri sana kuhusu uchawi. Ameelezea aina za misukule na kwa nini hakumrudisha Amina Chifupa. Amepiga mkwara sana na kusema leo wanarudishiwa uhai.
Kweliii...
Baada ya mahubiri anaomba kwa bidii na kuita njoooo... Watu kadhaa wanaanguka chini, wengine wanatembea kama wanyama, wengi wanakimbia kwenda mbele, baadhi ya watu wanakimbia kuogopa mikiki mikiki! Wanaoitwa misukule baaadhi wanatoa shuhuda walikokuwa wamefichwa!
Lakini nikajiuliza maswali kadhaa:
1. Mchungaji mbona anautajiri mkubwa sana?
2. Hawa misukule ni halisi na je, ndugu zao watawapokea ikiwa watajua kweli ni wao (maana kuna mmoja kadai alichukuliwa na mpangaji wao miaka 5 ilopita)
3. Hii injili inaelekea wapi? Sio kwamba hapa tunapigwa changa la macho?
4. Kwa uchunguzi mdogo, wengi wanaoenda wanapelekwa na kushangaa misukule, je jamaa anatumia nguvu za Kristu kweli aliye hai?
Please, mwenye historia kidogo ya huyu mchungaji atujuze.
Asanteni.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Asante Kwa Post Yako

Tulipokuwa Na Mkutano Tanga tulialika kila Mtu Kupitia humu Jf Na pengine aje ashuhudie kile Mungu anachotenda Leo. Nitoe tena Wito, Mkutano Wa Hapa Morogoro Kwenye uwanja Mkubwa wa Shule ya sekondari ya Morogoro unaishia Jumapili hii ya tarehe 22 Dec. tafadhali WAHi Ujionee Mwenyewe kile kinachotokea Na si kusikiliza propaganda Za mitandaoni wakati una akili zako Na utashi wako.

Mungu wetu anatenda zaidi ya Tuwazavyo.. Hakuna anayeweza kuzidhibiti nguvu zake.. NJOO JIONEE

Also visit post Na Majibu ya Saa ya Ufufuo Na Uzima via

https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/538286-ufufuaji-wa-misukule-ina-tofauti-gani-na-maigizo-14.html#post7818886
 
Bwana Yesu anaposema kanisa lake anamaanisha wale wote wanaomwamini na ambao wanaelekea mbinguni. Kwahiyo Petro alikuwa amekabidhiwa watu hao, yaani, wafuasi wa Yesu awachunge na kuwalisha. Huu sasa ndiyo mwili wa Kristo. Kanisa maana nyingine ni jengo ambapo kunakuwa na kusanyiko la watu wanaomwabudu Mungu. Hili ni kanisa la mahali pamoja ambalo linaweza pia kujulikana kama hekalu. Vilevile hekalu linaweza likawa ni mwili wa mwamini mmoja mmoja ambapo unakuwa ni hekalu la Mungu kwa maana kwamba Mungu huishi ndani mwake na kumwongoza katika kutenda mema. Kumbuka Mungu hakai kwenye dhambi.

Mkuu umesema vema ila hapo Kwa swala Petro umenipoteza kidogo!
 
Je kulikuwa na kanisa wakati wa Musa jangwani?
Lilikuwa na sifa gani (ukizingatia kanisa linakuhitaji uamini kwanza, wakati uyahudi, ukiri na kufuata taratibu za kabila)?
Kanisa lipi ni la kweli, kulingana na maono yako kwa nini?

Ndio, lilikuwepo. MATENDO 7:38 ' Yeye ndiye aliyekuwa ktk kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye ktk mlima Sinai, tena pamoja na baba zetu, ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.
 
Naamini ktk kujifunza kwanza mambo ya Mungu then hayo mengine yatafata!

Yah, nakubali. Neno ni la muhimu sana ila kama Mungu akikuongoza kufanya chochote kati ya hayo waweza kufanya kwasababu sio sheria kwamba ni lazima Neno kisha ndo Ishara au Ishara kwanza kisha Neno. Inategemea na R/Mtakatifu atavyoamua muda huo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom