Kumbe hii ndiyo Misukule ya Mchungaji Gwajima?

Status
Not open for further replies.
Mkuu Tiba umeupinga uchunguzi wangu Kwa hoja ya mdomoni tu!

Nikuombe kitu kimoja fungua Biblia kuanzia kitabu Cha Mwanzo mpaka Ufunuo Kama utaona makanisa unayoyatetea yapo!?

Narudia tena ktk bibilia Mimi Sijaona hayo makanisa!

Na Kanisa halali Au Imani ya kweli ipo kabisa! Soma maandiko vizuri utaona Imani ya kweli ni ipi!

wewe ni msabato????
 
Mbona watu tumekuwa tukimpa shetani utukufu, kuliko tunavyompa Mungu utukufu, mtumishi wa Mungu yeyote anapohibiri na miujiza ikatendeka, watu humshambulia kuwa anatumia nguvu za giza, hii inamaanisha Mungu hawezi tenda hayo mambo makuu ila shetani.

Sijawahi kuona mtu hapa JF anasifia na kukubali kazi ya mtumishi wa Mungu yeyote hapa Tanzania!! Kweli sasa naamini lile andiko mungu wa dunia hii (shetani) amepofusha fikra zao isiwazukie nuru ya wokovu!!

Binafsi sijawahi hudhuria kusanyiko la huyo mch Gwajima, lakini si anahubiri kwa jina la Yesu?? Aniaminiye mimi (Yesu) kazi nifanyazo atazifanya, naamu hata kubwa kuzidi hizo

Yesu nae anasema siku Hiyo wengi watamuijia wakisema tulihubiri Kwa Jina lako na kufanya makubwa Kwa jina lako na Yesu atasema ONDOKENI

Yatupasa kuangalia vizuri ni namna gani Jina la Yesu linatumika!

Na kufanya miujiza kwanza sio kanuni ya injili ya Yesu!

Ebu jiulize, km Yesu angeweka Kwanza mbele Hiyo miujiza ni nani asingeamini Au kukataa?
 
Ila kweli duniani wapagani, watu wasiomjua Mungu ingawa wana dini ndio wengi!. Poleni wafuga majini na misukule!.
 
Nani kati yetu wana jf ameshawahi kuona ndugu,mwanafamilia kipofu,kiziwi,kilema kaombewa kapona? marehemu kafufuliwa?

Mimi ndugu zangu wengi wamepona magonjwa mengi kwa kuombewa,mpaka mwenye ukimwi aliombewa
na akapona' Mimi mwenyewe ni shuhuda niko hivi nilivyo kwa sababu ya maombi'
 
Mkuu nashurukuru Kwa hoja zako Nzuri!

Ningependa turudi kwenye wakati Wa Yesu! Yesu alipokua hapa Dunia alifanya shughuli zake za injili bila kujihusisha na taasisi zilizokuwepo na km unakumbuka kulikua na Kanisa la Mfalme Suleiman na viongozi Wa Kanisa walikuwepo lkn Yesu alikwenda kubatizwa na Yohana Kule kwenye mto Yordan. Na sio viongozi Wa Kanisa Wa wakati ule Ndo waliombatiza!
Hii inaonesha Kua Kanisa Kwa wakati ule lilikua limeacha njia sahihi na kufata mafundisho ya Dunia na ndio maana Yesu alirudi na kuanza kuwafundisha wale viongozi Wa Kanisa! Na Hao Hao viongozi ndio walifanya mpango Wa kumuua Yesu! Kwa Hiyo utaona Yesu hakua na mpango Wa kujenga taasisi na makanisa ki vile!

Nikirudi kwenye hoja yako Kua ni Kanisa gani ndani ya bibilia lisilo jina la mtu Au nchi Au mji!

Nikuombe kwanza wewe ufanye utafiti kuanzia mwanzo mpaka ufunuo uone Kama hayo makanisa yamo!

wakuu, naomba msaada kidogo juu ya uhusiano wa kanisa na dini ya kikristo.
Kwa uelewa wangu mdogo nimekua nikichukulia kanisa ni nyumba ya ibada ya wakristo.
Kwakuwa ukristo ulikuwa dini rasmi baada ya kupaa kwa kristo: matumizi ya kanisa kabla ya tukio hilo huwa yananipa tabu kidogo.
Naomba uelekezo.
 
Mkuu nashurukuru Kwa hoja zako Nzuri!

Ningependa turudi kwenye wakati Wa Yesu! Yesu alipokua hapa Dunia alifanya shughuli zake za injili bila kujihusisha na taasisi zilizokuwepo na km unakumbuka kulikua na Kanisa la Mfalme Suleiman na viongozi Wa Kanisa walikuwepo lkn Yesu alikwenda kubatizwa na Yohana Kule kwenye mto Yordan. Na sio viongozi Wa Kanisa Wa wakati ule Ndo waliombatiza!
Hii inaonesha Kua Kanisa Kwa wakati ule lilikua limeacha njia sahihi na kufata mafundisho ya Dunia na ndio maana Yesu alirudi na kuanza kuwafundisha wale viongozi Wa Kanisa! Na Hao Hao viongozi ndio walifanya mpango Wa kumuua Yesu! Kwa Hiyo utaona Yesu hakua na mpango Wa kujenga taasisi na makanisa ki vile!

Nikirudi kwenye hoja yako Kua ni Kanisa gani ndani ya bibilia lisilo jina la mtu Au nchi Au mji!

Nikuombe kwanza wewe ufanye utafiti kuanzia mwanzo mpaka ufunuo uone Kama hayo makanisa yamo!

You are wrong,kabla na na wakati wa YESU hakukuwa na makanisa,kanisa limeanza kutokana na YESU,
na wewe soma biblia vizuri'
 
Nakubali uponyaji NAOMBA USHUHUDA wako hapa ili wengine wafaidike.
1. ulikoombewa
2. Nini kilitokea
3. Maisha yako/ uhusiano wako na mungu baada ya kuombewa
4. Je una ushindi dhidi ya dhambi ??
Mimi ndugu zangu wengi wamepona magonjwa mengi kwa kuombewa,mpaka mwenye ukimwi aliombewa
na akapona' Mimi mwenyewe ni shuhuda niko hivi nilivyo kwa sababu ya maombi'
 
Ndugu yangu, kama una jibu nipe, mimi huo muda wa kufanya "utafiti" kwa kweli sina.

Tiba

Mkuu Tiba, ni vema ukatenga japo nusu saa kila siku kujifunza neno la Mungu!

Jibu lipo ndani ya Biblia! Bibilia ndio kila kitu Ina majibu yote ! Ni wewe kuiuliza tu Unataka kujifunza juu ya nini na yenyewe itakujibu!
 
Yesu nae anasema siku Hiyo wengi watamuijia wakisema tulihubiri Kwa Jina lako na kufanya makubwa Kwa jina lako na Yesu atasema ONDOKENI

Yatupasa kuangalia vizuri ni namna gani Jina la Yesu linatumika!

Na kufanya miujiza kwanza sio kanuni ya injili ya Yesu!

Ebu jiulize, km Yesu angeweka Kwanza mbele Hiyo miujiza ni nani asingeamini Au kukataa?

Soma biblia wewe,ungewezaje kumtofautisha YESU na manabii wengine kama si kwa ishara na maajabu
aliyotenda?!! maisha yote ya YESU alitenda miujiza kwa kuponya wagonjwa na kufufua wafu na kulisha watu
kwa kumuujiza. Na alisema "Yeye aniaminiye atafanya haya,naam na makubwa kuliko haya". kwa mawazo
yako unamtofautishaje YESU nyakati hizi na mitume wengine,pamoja na neno lazima iambatane na nguvu za
kutenda ishara na maajabu kwa kuponya na kufunguliwa kwa wenye mateso kwa kuliitia jina la YESU'
 
Nakubali uponyaji NAOMBA USHUHUDA wako hapa ili wengine wafaidike.
1. ulikoombewa
2. Nini kilitokea
3. Maisha yako/ uhusiano wako na mungu baada ya kuombewa
4. Je una ushindi dhidi ya dhambi ??

Muujiza mkubwa kuliko yote Mungu alifanya kwangu ni kuniokoa na kunipa uwezo wa kushinda dhambi'
 
You are wrong,kabla na na wakati wa YESU hakukuwa na makanisa,kanisa limeanza kutokana na YESU,
na wewe soma biblia vizuri'

Mkuu nilichokua nazungumzia ni lile hekalu la Suleiman na Kwa sasa Tunaita makanisa! Sijui mpaka hapo nimeweka sawa?
 
Huyu si ndio yule aliyepakiza watu kwny mafuso akawakusanya pale kawe (tanganyika packers) akidai kwa anamfufua Amina Chifupa...? Cjui baada hapo alitoa sababu gn?
 
Soma biblia wewe,ungewezaje kumtofautisha YESU na manabii wengine kama si kwa ishara na maajabu
aliyotenda?!! maisha yote ya YESU alitenda miujiza kwa kuponya wagonjwa na kufufua wafu na kulisha watu
kwa kumuujiza. Na alisema "Yeye aniaminiye atafanya haya,naam na makubwa kuliko haya". kwa mawazo
yako unamtofautishaje YESU nyakati hizi na mitume wengine,pamoja na neno lazima iambatane na nguvu za
kutenda ishara na maajabu kwa kuponya na kufunguliwa kwa wenye mateso kwa kuliitia jina la YESU'

Mkuu hoja hapa si kuweka miujiza mbele! Ata Yesu hakufanya hivyo! Yesu alifundisha kwanza!
 
Muujiza mkubwa kuliko yote Mungu alifanya kwangu ni kuniokoa na kunipa uwezo wa kushinda dhambi'

Mkuu hapa sijaelewa kidogo! Unaweza ukafafanua kidogo?
 
Watu ni wengi sana!Pembeni lilipaki Hummer kubwa jekundu. Majukwaa makubwa kabisa na maspika yasiyopungua 50 yanaashiria uwepo wa Mch mahiri na kijana kabis Gwajima hapa Morogoro! Waimbaji wakubwa nchini Flora Mbasha,John Lissu na wengine wanasifu kwa bidii sana! Baada ya sifa Mch anaalikwa na anaanza kuhubiri sana kuhusu uchawi. Ameelezea aina za misukule na kwa nini hakumrudisha Amina Chifupa. Amepiga mkwara sana na kusema leo wanarudishiwa uhai.
Kweliii...
Baada ya mahubiri anaomba kwa bidii na kuita njoooo... Watu kadhaa wanaanguka chini, wengine wanatembea kama wanyama, wengi wanakimbia kwenda mbele, baadhi ya watu wanakimbia kuogopa mikiki mikiki! Wanaoitwa misukule baaadhi wanatoa shuhuda walikokuwa wamefichwa!
Lakini nikajiuliza maswali kadhaa:
1. Mchungaji mbona anautajiri mkubwa sana?
2. Hawa misukule ni halisi na je, ndugu zao watawapokea ikiwa watajua kweli ni wao (maana kuna mmoja kadai alichukuliwa na mpangaji wao miaka 5 ilopita)
3. Hii injili inaelekea wapi? Sio kwamba hapa tunapigwa changa la macho?
4. Kwa uchunguzi mdogo, wengi wanaoenda wanapelekwa na kushangaa misukule, je jamaa anatumia nguvu za Kristu kweli aliye hai?
Please, mwenye historia kidogo ya huyu mchungaji atujuze.
Asanteni.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
ujalazimishwa kuamini na silazima uamini wewe moyoni mwako kuna hisia gani?
 
Hebu linganisha hili fungu na hayo unayosema;
Isaiah 4:1
And in that day seven women shall take hold of one man, saying, We will eat our own food and wear our own apparel;
Only let us be called by your name, to take away our reproach!

Soma biblia wewe,ungewezaje kumtofautisha YESU na manabii wengine kama si kwa ishara na maajabu
aliyotenda?!! maisha yote ya YESU alitenda miujiza kwa kuponya wagonjwa na kufufua wafu na kulisha watu
kwa kumuujiza. Na alisema "Yeye aniaminiye atafanya haya,naam na makubwa kuliko haya". kwa mawazo
yako unamtofautishaje YESU nyakati hizi na mitume wengine,pamoja na neno lazima iambatane na nguvu za
kutenda ishara na maajabu kwa kuponya na kufunguliwa kwa wenye mateso kwa kuliitia jina la YESU'
 
Watu ni wengi sana!Pembeni lilipaki Hummer kubwa jekundu. Majukwaa makubwa kabisa na maspika yasiyopungua 50 yanaashiria uwepo wa Mch mahiri na kijana kabis Gwajima hapa Morogoro! Waimbaji wakubwa nchini Flora Mbasha,John Lissu na wengine wanasifu kwa bidii sana! Baada ya sifa Mch anaalikwa na anaanza kuhubiri sana kuhusu uchawi. Ameelezea aina za misukule na kwa nini hakumrudisha Amina Chifupa. Amepiga mkwara sana na kusema leo wanarudishiwa uhai.
Kweliii...
Baada ya mahubiri anaomba kwa bidii na kuita njoooo... Watu kadhaa wanaanguka chini, wengine wanatembea kama wanyama, wengi wanakimbia kwenda mbele, baadhi ya watu wanakimbia kuogopa mikiki mikiki! Wanaoitwa misukule baaadhi wanatoa shuhuda walikokuwa wamefichwa!
Lakini nikajiuliza maswali kadhaa:
1. Mchungaji mbona anautajiri mkubwa sana?
2. Hawa misukule ni halisi na je, ndugu zao watawapokea ikiwa watajua kweli ni wao (maana kuna mmoja kadai alichukuliwa na mpangaji wao miaka 5 ilopita)
3. Hii injili inaelekea wapi? Sio kwamba hapa tunapigwa changa la macho?
4. Kwa uchunguzi mdogo, wengi wanaoenda wanapelekwa na kushangaa misukule, je jamaa anatumia nguvu za Kristu kweli aliye hai?
Please, mwenye historia kidogo ya huyu mchungaji atujuze.
Asanteni.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Asante lkn tumsubiri Gwajima mwenyewe au kampani yake ya karibu watujuze km wapo jf.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom