Kumbe hii ndiyo Misukule ya Mchungaji Gwajima?

Kumbe hii ndiyo Misukule ya Mchungaji Gwajima?

Status
Not open for further replies.
fanyeni kaz zenu achaneni na huyu tapel,ni mwiz wa kawaida sana na hana kipya zaidi ya marudio.nilishasema humu jinsi wanavo waandaa watu hawa na kuwapa maneno ya kusema na kisha kuwapa pesa kam elfu 50,kila mmoja.jamni mtaelewa lini???,

tungepata shuhuda anayelipwa nitakuamini. inamaana hata mmoja hakuna wakusema kuwa wachungaji ni matapeli zaidi ya maneno kama yako?
 
who are u to judge him?
yangu macho na masikio.
 
kama ulitoa sadaka nakupa pole. huyo ni msanii kama masanja ila yeye anatishia watu kwa majini. misukule n.k. ni wapi kwenye biblia misukule imetajwa. hana lolote mwizi tu huyu.

John: 10:11-12 Inasema,

I am good shepherd. The good shepherd gives his life for sheep.

But he who is hireling and not the shepherd, one who does not own the sheep, sees the wolf coming and leaves the sheep and flees; and the wolf catches the sheep and scatters them.

Jamani Mchungaji mzuri huutoa uhai wake Kwa kondoo Lakini Yule Wa mshahara tena ata Hao kondoo si Mali yake hukimbia na kuwaacha mbwa mwitu kuwatafuna tu Hao kondoo!

Tuyachunguze mafundisho Yao kwakupitia maandiko!
 
Nani kati yetu wana jf ameshawahi kuona ndugu,mwanafamilia kipofu,kiziwi,kilema kaombewa kapona? marehemu kafufuliwa?

mimi nimewahi kuona kichaa kabisaaa na kilema wanapona baada ya maombezi...though sio maombezi ya siku moja.walifanyiwa maombezi ya kila siku kwa kama wiki mbili na wakapona kabisaaaaa
 
Watu ni wengi sana!Pembeni lilipaki Hummer kubwa jekundu. Majukwaa makubwa kabisa na maspika yasiyopungua 50 yanaashiria uwepo wa Mch mahiri na kijana kabis Gwajima hapa Morogoro! Waimbaji wakubwa nchini Flora Mbasha,John Lissu na wengine wanasifu kwa bidii sana! Baada ya sifa Mch anaalikwa na anaanza kuhubiri sana kuhusu uchawi. Ameelezea aina za misukule na kwa nini hakumrudisha Amina Chifupa. Amepiga mkwara sana na kusema leo wanarudishiwa uhai.
Kweliii...
Baada ya mahubiri anaomba kwa bidii na kuita njoooo... Watu kadhaa wanaanguka chini, wengine wanatembea kama wanyama, wengi wanakimbia kwenda mbele, baadhi ya watu wanakimbia kuogopa mikiki mikiki! Wanaoitwa misukule baaadhi wanatoa shuhuda walikokuwa wamefichwa!
Lakini nikajiuliza maswali kadhaa:
1. Mchungaji mbona anautajiri mkubwa sana?
2. Hawa misukule ni halisi na je, ndugu zao watawapokea ikiwa watajua kweli ni wao (maana kuna mmoja kadai alichukuliwa na mpangaji wao miaka 5 ilopita)
3. Hii injili inaelekea wapi? Sio kwamba hapa tunapigwa changa la macho?
4. Kwa uchunguzi mdogo, wengi wanaoenda wanapelekwa na kushangaa misukule, je jamaa anatumia nguvu za Kristu kweli aliye hai?
Please, mwenye historia kidogo ya huyu mchungaji atujuze.
Asanteni.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Kwa hiyo ndugu uliiona hiyo misukule ikitoa ushuhuda palepale uwanjani...?!...
Najiuliza, katika hali ya umsukule mtu anaweza kutambua ni nani alimchukua na kwa kipindi gani!!!? Nimeona hapo umeandika kuna mmoja kashuhudia alichukuliwa na mpangaji wao kwa mida wa miaka mitano. Bado hainiingii akilini vizuri mtu ambae ni msukule bado awe na kumbukumbu ya aliyemuua na hata miaka aliyokaa huko... 😕😕😕
 
mimi nimewahi kuona kichaa kabisaaa na kilema wanapona baada ya maombezi...though sio maombezi ya siku moja.walifanyiwa maombezi ya kila siku kwa kama wiki mbili na wakapona kabisaaaaa
wapi huko, ila sio kwamba nabisha
 
kama ulitoa sadaka nakupa pole. huyo ni msanii kama masanja ila yeye anatishia watu kwa majini. misukule n.k. ni wapi kwenye biblia misukule imetajwa. hana lolote mwizi tu huyu.
Sijawahi kuona post yako inayoashiria heli,au wewe ni msukule wenyewe nini?
 
Kwa hiyo ndugu uliiona hiyo misukule ikitoa ushuhuda palepale uwanjani...?!...
Najiuliza, katika hali ya umsukule mtu anaweza kutambua ni nani alimchukua na kwa kipindi gani!!!? Nimeona hapo umeandika kuna mmoja kashuhudia alichukuliwa na mpangaji wao kwa mida wa miaka mitano. Bado hainiingii akilini vizuri mtu ambae ni msukule bado awe na kumbukumbu ya aliyemuua na hata miaka aliyokaa huko... 😕😕😕

Nimefanikiwa kuiona hiyo misukule, sasa hiyo ya kukumbuka aliyemchukua mmh! Hapo panahitaji hekima!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kweli wajinga ndio waliwao, jamani watu ni weeeeengi ajabu, wengi sana. Huenda wengi wanakuja kuona hii movie ya misukule. Naamini sana ktk ukristu ila hii injili ya Gwajima mmmh! Manake kijana anatajirika sana. Kweli injili inalipa, uwe tu mbunifu, maana wengine wana ubunifu wa upako, mara kuhubiri nje bila viza, mara kuwatafutia watu kazi nje, huyu kaja na kurudisha misukule, mmmh!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ntapata tu data za kutosha wiki hii. Khs Ngwajima! Naendelea kusisitiza, tusiziamini kila roho...

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hayo ni mazingaombwe. Ukristo kamili ni kuhubiri kwamba sasa ni siku za mwisho na kuwa Yesu aja upesi yu aja na tuchague utakatifu na tuweze kwenda Mbinguni. Chochote juu ya miili na anasa za dunia hii huo ni ubatili na uongo. Itakusaidia nini kwenda motoni na viungo vyako vyote? Ni afadhali kwenda Mbinguni bila jicho au kiungo kimojawapo. Tafakari. Chukua hatua sahihi. Acheni dhambi na anzisheni ushirikiano na Kristo. Hapo utatambua mhubiri/nabii wa uongo
 
Huyo mwizi tu anacheza na ujinga wa binadamu. tungekua na dola makini watu kama hao wangekua jela badala ya kuendesha magari ya gharama kama hammer.
 
gia yake ni kufufua misukulue
alisema atawatoa Sokione na Amina Chifupa live na kila tv duniani itaonyesha na dunia itazizima
hadi leo hatujaona lolote.....wajinga ndio waliwaoo
 
mimi nimewahi kuona kichaa kabisaaa na kilema wanapona baada ya maombezi...though sio maombezi ya siku moja.walifanyiwa maombezi ya kila siku kwa kama wiki mbili na wakapona kabisaaaaa
Wacha uongo wewee!....Nyie mashahidi wa uongo ndio mnaoendeleza imani za kichawi...Hakuna maombi yanaponya kilema, ila ukienda hospitali kama ccbrt baadhi ya ulemavu unaweza kupona. Gwajima kama ana imani ya mungu basi inafaa aanze kuchomwa moto hapa duniani. Tapeli A1
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom