Manabii wa Tanzania hii barua ya Mchungaji wa Kenya inawahusu pia (modern Miracle)

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,515
Mchungaji wa Kenya amewaandikia Barua Manabii kadhaa wa Kenya akitaka ufafanuzi wa kinacho itwa MODERN MIRACLE.

Anasema Yesu wakati anahubiri injili alifanya Miracle kwa watu na kwa eneo fulani.

Mfano; Yesu alimfufua Lazaro kule Bethany na pia kule Jericho akamponya Bartimaeous. Kule Jerusalemi Petro na John walimponya mtu Kilema.

Kenya ina wafu wengi sana, Vilema, Vipofu, Mabubu, Vichaaa na pia wanao sumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Sasa anawataka Manabiii waweke wazi wale watu wanao pokea oponyaji, yaani majina yao yawekwe wazo na ikibidi wanako ishi yaani Vijiji na Mitaaa wanako tokea.

Wakenya wanaona kila siku kwenye Tv za Manabii watu wakitupa magonga kule na kule kwamba wameponywa Ila hakuna Mkenya anaye jua kijiji wanako tokea wale walio pokea uponyaji na kutupa magongo kwamba wanakuwa na sura ngeni sana miongoni mwa Wakenya, na pia kwa nini Media huwa hazireport taarifa za watu kuponywa kama Breaking news? Kwamba kwa yeye swala la mtu kuponywa ukilema au ukiziwa ni jambo kumbwa sana linahitaji Breeking news kabisa.

Je Bongo kuna anaye ishi jirani na mtu alie ombewa akapona au wale wanao toa shuhuda kwenye TV na ni anawajua?

Niliwahi kuwa na wasiwasi wa wale watoa ushuhuda wa kupona.
FB_IMG_1674395285385.jpg
 
Saw atapewa majibu ngoja apigwe upupu ndio ataamini uchawi upo na ulozi na Kisha ndipo atakopojuwa kuwa nguvu zamungu zipo SAS asubiriee shughuli impate
 
Kwani walevi wanavyolewa huko bar na sehemu za starehe kuna mtu huwa anawauliza wanakoishi na mitaa waliyotoka??

Ya Mungu mpeni Mungu na ya Kaisari mpeni kaisari.
 
Mwaka jana nilienda sehemu moja inaitwa Duthumi njia ya kuelekea kisaki, wakati nimeshuka kwenye lile TATA napokelewa na mahubiri ya nguvu, kuna mwamba kakusanya umati unati anatoa neno kwa nguvu kwa ile sauti ya kukoroma , jasho linamtoka, anakemea kiasi unaweza hisi atapasua zile Spika muda wowote, nikapita sikufuatilia sana ukizingatia miaka hii watu wanabet kila mahali maisha yanatuchanganya acha watu watafte nafuu, nikafika kwa mwenyeji wangu.

Sasa shida ikaja baada ya yale Mahubiri si namuona ni Rashid? ( huyu chalii nimekaa nae nyumba Moja Mburahati ) kumbe ndio Baba Mchungaji, dah mimi namjua mwamba ni Mkamaria mmoja matata sana hakuna Dubwi asilolijua dar hii.

Betting zote ni Mdau, Smocker mzoefu, ikabidi kwa Sauti ya Chini na ya ki upole nisichafue hali ya hewa nikamwita jina la DoX oya (anaitwa kISU kitaani ) vipi mwanangu, dah alinikata jicho yule mdwanzi akachukua maji pale dukani akajikataa, nikaona dah kweli pesa inatafutwa, Mwamba kumbe yupo huku? Jamaa akauliza unajuana na Baba Mchungaji? Nikamjibu Yap namfahamu ila naona yeye kanisahau.

Mida kama ya saa nne hivi usiku siku hiyo hiyo yule Mwamba akanipigia Simu, Kaka vipi? Naona ulitaka kunisagia kunguni Muhuni wangu sie wengine hatujui kuiba nimekuja huku kutafta maisha Kaka, kama unavyoona, hapa washanielewa nakula ki ulaini kaka game ime change bro, nikamwambia dua sasa neno umejifunzia wapi? Akasema life nyoso kaka nikishamoka yanakuja yenyewe nakuwa kama Jesus himself! Hahaah mwamba kavurugwa.

Akaja nilipofikia, tukapiga Konyagi pale, majani yakavutwa na mafegi ya kutosha. Kesho yake mi nikaamsha, mwamba nasikia kishapata eneo la kujenga Church.
 
Back
Top Bottom