#COVID19 Hoja za Askofu Gwajima kuhusu chanjo ya Corona hazina mashiko, isipokuwa zina agenda nyingine nyuma yake

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
✳️HOJA ZA ASKOFU GWAJIMA KUHUSU CHANJO YA CORONA HAZINA MASHIKO(ZINA MAPUNGUFU MENGI), ISIPOKUWA ZINA AGENDA NYINGINE NYUMA YAKE

🔵Na:Shujaa©️®️Ⓜ️

Leo nimeona mjadala mkubwa unao-trend kwenye mitandao yote ya kijamii kuhusu hoja za Askofu Gwajima kuhusu CHANJO YA CORONA ambayo akishauri watanzania wote watumie hiyari Yao kukataa CHANJO hiyo ya Corona kwasababu mbalimbali alizozitoa ambazo ndizo nimeziona zina mapungufu makubwa na hazina tija, na pia nimeona maoni watanzania wengi wakimpongeza kwa ujasiri wake wa kuwa kinyume na msimamo wa serikali yake na Chama chake

Ukimsiliza vizuri na kwa makini Askofu Gwajima utaziona hoja zake Zote zimebase Katika maeneo 4

1️⃣ Anadai HAKUNA research(study) za kutosha zinazoonyesha kuwa Chanjo hii ya Corona inaweza kuwa salama kabisa kwa miaka 3 au 4 au 10 ijayo baadae hasa inapoingia Katika DNA na RNA za binadamu Yaani Anadai HAKUNA reaserch Kama Chanjo Ina madhara au la!

Anadai hao watu watakaochanjwa watakuwa Nini baaadae na kwa vizazi vyao, kwamba huenda ikasababisha miaka ya baaadae au vizazi vijavyo ikatuletea madhara ya makubwa ya watu kukosa akili,Kuwa mazezeta au Misukule(Mazombie)

Hatimaye Anadai kwa kukubali Chanjo hizo hasa kwa makundi matano ambayo yamewekwa Kama makundi ya ulazima kuchanjwa yaani makundi ya ulinzi na usalama,Madaktari,Viongozi wa dini n.k kuwa TUNAWEZA kuwapoteza hao wetu wa muhimu Katika taifa na kuliacha Taifa kutokuwa salama Katika Ulinzi,Afya na Usalama kwa ujumla was maliasili zetu

2️⃣ Anadai kwa uwazi kabisa kuwa wanasayansi wetu wote wamekula hela Yaani wamepewa rushwa ya hela ili watoe ripoti za uongo kwa watanzania Ili wakubali kuchanjwa Hiyo Chanjo ya Corona!!

Maanake hata kamati iliyoundwa na serikali kuchunguza juu ya ubora na uhalali wa Chanjo hii ya Corona inayoitwa Jonhson Jonhson(JJ) kuwa hao wote wamepewa rushwa ili tu kupitisha chanjo hii

3️⃣ Ni Kama anaishutumu Serikali ya CCM ya Mama Samia Suluhu iliyopo madarakani kwamba imeshinikizwa na mataifa ya dunia au na wazungu ili kukubali Chanjo isiyo salama iingie nchini akidai kuwa ndio wazungu Wana Nia yao chafu ndio maana wanatupatia Chanjo hizi Bure na kwa kutupa misaada ya Bure kwasababu Anadai kuwa serikali imeshinikizwa kuwafanyia majaribio watanzania zaidi ya milion 60

Anadai Africa NI bara linalotamaniwa Sana na wazungu kwasababu ya rasilimali zetu, Ndio maana wanaruhusu tuletewe Chanjo ya JJ ambayo siyo Kama waliyochanjwa wamarekani au Kama waliyochanjwa Waingereza akidai ile chemical content inayotumika huko sio hii inayotumika kwetu!Hivyo ndio maana ana mashaka na Chanjo hii

4️⃣ NI Kama Pia anaishutumu Serikali yake ya CCM inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan !Kwani anahoji Kwanini baada tu ya Magufuli kufa ndio swala la Corona limeanza kupewa Nguvu na uzito mkubwa?Wakati kabla ya Kufa kwa magufuli Tulifanya kampeni salama,hatukuvaa barakoa,Tulimuaga magufuli kwenye msiba wake tukiwa kwa maelfu? Hivyo anahoji mbona magufuli alipinga hii Chanjo Ila mbona sasa hili swala limepewa uzito?

Hizo ndizo hoja za Askofu Gwajima ambazo wengi kwa kutotumia akili kufikiri wameingia Katika mkumbo wa kupongeza tu.Ila nami naomba nimuhoji Mambo machache au tutafakari nami Mambo machache ambayo yatatufanya kuona kuwa hoja hizi za Gwajima hazina maana Wala Msingi na Pili zina agenda NYINGINE NYUMA YAKE

🔜 KWANZA, NI muhimu kujua Utafiti unapingwa na Utafiti kinzani, Hoja inapingwa na hoja!Hivyo unavyoleta hoja ya kudai hakuna utafiti wa kutosha kuwa Chanjo iliyoletwa sio salama kwetu, ulipaswa wewe utupe ni utafiti gani uliokuthibitishia wewe au ulioufanya au uliofanywa kuwa kilicholetwa sio salama na kwamba kinaweza kuleta madhara ya watu kuwa vichaa,mazezeta au kushindwa kuzaa Viumbe wenye akili?

PILI Kwanini uwaze Negative tu Yaani madhara mabaya tutakayoweza kuyapata kwa kukubali kuchanjwa Chanjo hii ya Corona ikiwa Kama Ina madhara? Kwanini usiwaze au kufikiri what if ikiwa Haina madhara na wengi wao wamekataa,NI Nini kitakachowapata au kitakachozaliwa kwa kukataa Hiyo chanjo,maana amesema Hana uhakika(Possibility)?

Hivyo kwa namna ile ile ambavyo Hauna uhakika wa scientific research juu ya madhara ya chanjo Hiyo kwa mtu kwamba inaharibu Gene(tabia )zake ndivyo Hivyo Hivyo watu wanaweza wakapatwa madhara zaidi ikiwa kweli Hiyo Chanjo itafanya kazi vizuri,waliokataa ndio watadhurika zaidi!

🔜TATU NI akili ndogo na za kijinga Sana na za kimaskini kufikiri kwamba eti wazungu wametutengenezeshea Chanjo waafrica ili kutuua, kudumaza akili zetu,Kutufanya mazezeta au vichaa,Kuharibu vizazi vyetu vya baadae, kutaka kutuibia rasilimali zetu kupitia hii Chanjo ya Corona

Hata Kama una akili ndogo tu Kama Mimi ebu tutafakari tu jambo Moja!Hapo kwetu Africa au Hapa Tanzania ni vitu vingapi, au bidhaa ngapi au madawa gani ambayo tunayatengeneza sisi wenyewe wazawa wa nchi? Utapata Jibu kuwa karibia 80% ya bidhaa au vitu tunavyotumia Zote zimetoka kwa hao wazungu,vyote vimetengenezwa na hao hao wazungu ambao leo ndio unawaza kuwa wanataka kukufanya zezeta eti kwasababu ya Corona?

Madawa karibu yote tunayotumia yametoka kwa wazungu, Kama kuchanjwa tumechanjwa Chanjo nyingi Sana tangu utotoni (Chanjo ya polia,Surua,ndui) ambazo zimetoka kwa hao hao wazungu ambao leo tunawahofia

Kama NI hofu ya kudukuliwa,Sisi Tanzania tunatumia Google au Email au Network ambazo server zake zipo huko huko kwa wazungu!Hivi Kama wangetaka kutuibia na kutufilisi wangeshindwa kufanya Hivyo?Au kwamba Corona ndio imefanya washtuke kwamba waafrika wapo wengi Hivyo wanahitaji kutupunguza kwa Kutumia Chanjo?Kuwa Hivyo au kufikiri Hivyo inaonyesha una mawazo ya kimaskini na NI mawazo ya kitoto

Wakuue wewe leo kwasababu ya nini?Kwanini wasingekuua Jana? Shirika la Afya la WHO na mengine mengi ndio limekuwa likitumika kuidhinisha Chanjo hizo na ndio yameendelea kufanya study nyingi mbalimbali duniani kulitia wanasayansi mbalimbali kuhalikisha janga hili linapungua Kama si kutokomezwa!!

Hivyo kuwa na mashaka na wanasayansi wako ambao siku Zote ndio wamekuwa wakikuhudumia na kukupatia Dawa NI sawa kujitekenya mwenyewe alafu ukacheka mwenyewe

NNE Kwa Askofu mkubwa Kama Gwajima kusimama hadharani na kuishutumu serikali yake na ya chama chake CCM kuwa eti imeunda kamati ya wana sayansi ya kutafiti Hiyo Chanjo ya Corona ya JJ ambayo Anadai wanasayansi wote hao wamepewa hela Yaani Rushwa ili kuleta ripoti ya uongo kwa watanzania!!!Kuleta taharuki na shutuma nzito Kama hizo dhidi ya serikali NI Kosa kubwa Sana ambalo inapaswa hata afikishwe mahakani na ahojiwe ili athibitishe hao wanasayansi NI Nani na wapi na shilingapi wamepewa ili walete tafiti za uongo zitakazotupa kuhatarisha usalama wa watanzania wote mil 60.

NI makosa makubwa Sana kwa Askofu Gwajima kumshutumu Rais wa Nchi Samia Suluhu Hassan kuwa anayoyafanya anayafanya kwasababu ya presha ya mataifa makubwa ya dunia.Yaani anaona sio akili zake!Mbaya zaidi anampambanua Raisi Samia na Hayati Magufuli na kumuona Rais Samia amekosea Sana kulieleza taifa juu ya wimbi hatari la tatu la Corona kwa kuwaonya watu kuchukua tahadhari Zote ikiwa pamoja na Kutumia Chanjo ya Corona.

Anachofanya Askofu Gwajima mbele ya watanzania NI kujaribu kuwachonganisha watanzania na Raisi wao Samia Suluhu Hassan ambao wengi wao waliona njia alizokuwa anatumia Hayati Raisi Magufuli kuwa ndio sahihi.Hivyo anataka kuwaaminisha watanzania wamuone Raisi Samia kuwa ni mbaya na ndiye anatumiwa na mabeberu Kama alivyokuwa anaeleza mtangulizi wake na anachofanya NI kuleta uchonganishi wa wazi.

Lazima tufahamu Raisi Magufuli sio Mungu na sio kipimo Cha usahihi wetu, Na sio lazima kilichokuwa sahihi Jana basi hata leo kinaweza kuwa sahihi!Yapo makosa mengi sana ambayo Rais Magufuli aliyafanya yaliyolisababishia Taifa kuwa kwenye Hali nzito, pamoja na kwamba pia Kuna mazuri mengine aliyafanya katika maamuzi yake ya namna ya kushughulika na Corona kwa Wakati wake ambayo kwa Wakati huu hatupaswi Kutumia approach zile zile

Niseme wazi ndugu zangu watanzania, mtu asiwadanganye CORONA IPO na watu wanakufa Kama Kuku wenye mdondo! Usiwe shabiki tu wa mtandaoni na kuwasikiliza Hawa Wana siasa akina Gwajima anawatia Moyo Kuona Corona Haina Nguvu na haipo.Toka huku mitandaoni ebu zunguka kwenye hospitali kadhaa za rufaa unazozijua Kama upo kwenye majiji makubwa alafu ufanye utafiti wako!Utakuta hospitali zimeshona na wagonjwa was Corona wanaongezeka kila kicha na wanakufa kwa namna isiyo ya kawaida-...

Nimeona nieleze hayo kwa ufupi, ili usichukuliwe tu na maneno ya kisiasa yanayoletwa kutokea madhabahuni kwa Jina la Yesu Lakini hayana Mungu ndani yake.Katika makala nyingine nitaeleza sababu za kiroho kinyume na anazoeleza Askofu Gwajima,Sababu za Kiimani na yapi tunayopaswa kuyafanya Kama Kweli sisi ni watu wa Mungu?Je kutojilinda na kuvaa barakoa NI kukosa imani?Usikose....Asante kwa kufuatilia

🔵Na:Shujaa Charles Richard Mwaisemba(©️®️Ⓜ️)

stmwaisembac@gmail.com

0712054498/0759420202
 
Hebu naomba mnikumbushe wana JF, hivi HIV AIDS iliingia ulimwenguni/duniani mwaka gani? HIV AIDS, kwa wale wenye takwimu, IMEUA WATU WANGAPI HADI LEO aidha hapa Tanzania au duniani, WHO najua wanazo hizi data, hebu zichimbeni huko WIKIPEDIA!? Kwa wenye kumbukumbu sahihi, HIV AIDS ilishawahi kutafutiwa au kupatiwa CHANJO?

Jibu la hili swali hata mimi nalijua ni HAPANA! Yaani ninachojua ni kwamba haina dawa ya kuutibu ila ina dawa za kufubisha makali ya wale wadudu kwa muda wa SAA 24! Baada ya hapo, "kazi inaendelea"! Sasa kwa miaka hiyo ya dunia kuishi na HIV AIDS wataalam mmeshindwa kupata angalau tiba yake?!

LAKINI in less than two years, wataalam mmeshapata CHANJO YA UVIKO - 19?! Ninyi mna UTANI KWELI KWELI kama siyo kutaka kupiga pesa za maskini wa dunia hii au KUTAKA KUTIMIZA AGENDA ZENU ZA SIRI.

Tuacheni kila mtu APAMBANE NA HALI YAKE na GOD FOR US ALL. Hivyo nashauri tusikilize hoja zote na kisha kila mmoja afanye uamuzi wake mwenyewe lakini mwisho wa yote NCHI IMURUDIE MUNGU, Mungu Mwenyezi, Mweza wa yote.
 
Ndio maana mimi hapa huwa nasisitiza umuhimu wa mtu siyo awe msomi tu bali awe na elimu. Mtu aliyeelimika atajua tu kwamba si kila kitu alichokizungumza Gwajima kipuuzwe. Uwezo wa kupambanua mbivu na mbichi kati ya yote aliyoyamwaga Gwajima ndio unahitajika hapa.

Yote kati ya yote si wamesema kinga ni hiyari? Basi waachwe wale wanaotaka wachanjwe wasiotaka wabaki walivyo. Ila ukweli utabaki kwamba ugonjwa wa corona na kinga zake umeshaingiliwa na wajanja wa mjini watakaoutumia kupenyeza ajenda zao, kuwablackmail viongozi wa nchi za kwetu, na kufanya wanayoyataka.
 
This is stupidly:

KWANZA, NI muhimu kujua Utafiti unapingwa na Utafiti kinzani, Hoja inapingwa na hoja!nHivyo unavyoleta hoja ya kudai hakuna utafiti wa kutosha kuwa Chanjo iliyoletwa sio salama kwetu, ulipaswa wewe utupe ni utafiti gani uliokuthibitishia wewe au ulioufanya au uliofanywa kuwa kilicholetwa sio salama na kwamba kinaweza kuleta madhara ya watu kuwa vichaa,mazezeta au kushindwa kuzaa Viumbe wenye akili?
 
Acha kuleta siasa kwenye afya za watu. Hizi siasa peleka huko kwenye miamala ya simu na siyo kwenye suala linalogusa miili ya watu. Kabla ya Gwajima kuleta tafiti zake, serikali ndiyo ilipaswa kuja na scientific research evidence kwamba hizo chanjo ni salama.
 
Acha kuleta siasa kwenye afya za watu. Hizi siasa peleka huko kwenye miamala ya simu na siyo kwenye suala linalogusa miili ya watu. Kabla ya Gwajima kuleta tafiti zake, serikali ndiyo ilipaswa kuja na scientific research evidence kwamba hizo chanjo ni salama.
Kwani serikali SI ilishaunda kamati ya kuangalia ubora was hizi Chanjo?Kwanini leo Tena mnakataa?
 
This is stupidly:

KWANZA, NI muhimu kujua Utafiti unapingwa na Utafiti kinzani, Hoja inapingwa na hoja!nHivyo unavyoleta hoja ya kudai hakuna utafiti wa kutosha kuwa Chanjo iliyoletwa sio salama kwetu, ulipaswa wewe utupe ni utafiti gani uliokuthibitishia wewe au ulioufanya au uliofanywa kuwa kilicholetwa sio salama na kwamba kinaweza kuleta madhara ya watu kuwa vichaa,mazezeta au kushindwa kuzaa Viumbe wenye akili?
Sawa!
 
Nasubiria majibu ya Gwajima maana alisema atamjibu mara 2 mjinga yeyote(hata rais) atakayefunua mdomo kumjibu
 
Nasubiria majibu ya Gwajima maana alisema atamjibu mara 2 mjinga yeyote(hata rais) atakayefunua mdomo kumjibu
WALIMNYIMA UJUMBE WA NEC, SASA ATATUMIA CHANJO, UKABILA NA UJINGA WA WATANZANIA KUWAMALIZA.

CCM WALIINGIA CHOO CHA KIKE KUMKARIBISHA GWAJIMA NA KUMPA UBUNGE. SASA ANAKWENDA KUWAMALIZA.

HUKO FACEBOOK NA INSTAGRAM KASHAWASHIKA WATU KARIBIA WOOOTE!.
 
Kama ukichanjwa bado unapata Covid sasa chanjo ya nini? Au ndio twende na Dunia? Ona huko duniani sasa ....
marcusrogerschildoftheking_1627385186409.jpg
marcusrogerschildoftheking_1627385186554.jpg
marcusrogerschildoftheking_1627385186523.jpg
marcusrogerschildoftheking_1627385186494.jpg
 
Back
Top Bottom