Kumbe hatuna wataalamu wa hili pia?

Ushauri wangu: In the short run, Marmo apangiwe kazi ya kufundisha wataalamu wa arbitration ili kulinusuru taifa katika gharama za kupeleka wataalamu wetu nje.In the long run, tufikirie kupeleka wanafunzi katika vyuo vya nje.

Hivi ni nini hasa unachosomea ukisomea usuluhishi?
 
Ndugu yangu Nyani, we acha tu. Kwanza siamini kwamba hatuna wataalamu wa usuluhishi. Ninavyofahamu miye, arbitration ni uwanja wa wanasheria. sasa wanaposema hatuna wataalamu wa arbitration ni kuwakashifu wanasheria wote tulio nao tanzania.

Back to your question. Sijui ni mambo yepi yanayofundishwa katika fani ya abitration. Japo kuwa miye naona hili ni swala la kutumia common sense.

Angalia posti yangu iliyopita. Nimedokeza kuwa hii ni justification ya kusaini mikataba mibovu, which is bullshit!
 
Hata miye naliona kuwa ni suala la common sense na busara. Sasa hayo mambo mawili sijui nayo unasomea au vipi lakini nakubaliana nawe kuwa huu ni uwanja wa wanasheria more than anything. Wenye kujua zaidi tuelimisheni.
 
Kwa nini serikali kwa kushirikiana na chuo kikuu cha dar or mzumbe, isifanye utaratibu wa kumtumia mheshimiwa marmo kama muhadhiri wa arbitration katika hivyo vyuo???

Hili limenifurahisha sana mzee. Mwanasiasa hawezi kufundisha vyuo vyetu, wanafikiria wako standard ya juu sana.
 
nimeongea na mtaalam mmoja, rafiki yangu ambaye yuko UDSM kwa further studies (LLD), na ni lecturer MU, nikamuuliza jambo hilo. Ila hata yeye ameshangaa na kuona ujumbe huu wa waziri ni uongo mtupu, sababu yeye anasema kachukua hiyohiyo na anatumika kila kukicha. akaongeza kuwa yeye anaamini kunaowengi wenye hizo sifa.

yakwake kachukulia london, ila nipeni muda nitaleta chuo chake alichochukulia baada muda kudogo.

yeye anasema kuwa ndiyo kasumba ya serikali kutowathamini wazalendo.
 
Imeripotiwa Bungeni kuwa hatuna wataalam wa abirtration serikalini ndio maana serikali inabidi kukodi wataalamu binafsi kutuwakilisha katika kesi nyingi za abirtration na kuwalipa watu mamilioni. Katika Bunge zima ati ni Mhe. Phillip Marmo pekee ndiyo ana cheti kinachomtambua kimataifa..!

Sasa kwanini tusiamue kuomba wataalamu toka Ulaya tu?

Mkuu, heshima mbele, kama unakumbuka Muungwana alishaomba ulaya huko watupatie wataalamu kwa 'kuandaa mikataba', na nadhani kwa kweli tunastahili hasa ukikumbuka huu wa Buzwagi, so sishangai kama hao wa arbitration hatuna kabisa!
 
Ina maana yawezekana wanasheria wetu wanaogopa kuwa certified au hawana uwezo wa kuwa certified na vyombo vinavyohusika na wao wakishapata Bar basi ndio imekuwa mwisho?
 
nimeongea na mtaalam mmoja, rafiki yangu ambaye yuko UDSM kwa further studies (LLD), na ni lecturer MU, nikamuuliza jambo hilo. Ila hata yeye ameshangaa na kuona ujumbe huu wa waziri ni uongo mtupu, sababu yeye anasema kachukua hiyohiyo na anatumika kila kukicha. akaongeza kuwa yeye anaamini kunaowengi wenye hizo sifa.

yakwake kachukulia london, ila nipeni muda nitaleta chuo chake alichochukulia baada muda kudogo.

yeye anasema kuwa ndiyo kasumba ya serikali kutowathamini wazalendo.
nakubaliana na mtaalam huyo !!
An arbitrator is an impartial person chosen by the parties to solve a dispute between them, who is vested with the power to make a final determination concerning the issues in controversy.
.source:answers.com
Na ndio baada ya kusoma hiyo nikajiuliza kama kweli Watanzania hatuwezi kuwa wasuluhishi...? Usuluhishi? Ni kakumbana na hii nayo...Arbitration:The submission of a dispute to an unbiased third person designated by the parties to the controversy, who agree in advance to comply with the award — a decision to be issued after a hearing at which both parties have an opportunity to be heard.
Ingawaje hii inatumika marekani, je tunahitaji sayansi ya roketi?
Nafikiri kuna watu wengi wana qualify!
 
Sasa kwenye usuluhishi unasomea nini...? Watu wengine bwana..wanapenda kukompliketi mambo utadhani nini sijui...mi nataka kujua ni nini hasa mtu anachosomea ktk hiyo arbitration...Kuna mtu anajua humu?
 
Bwana Nyani Ngabu...mimi nafikiri Mushobozi atuletee huyo mtaalam na rafiki yake humu JF atueleze bayana!
 
nilipotea gafla na data ila sasa nimerudi; ninatanguliza heshima mbele,
mtaalamu huyo ni yahya Hamad, ana masters mbili, na sasa hivi anachukua PHD pale udsm. masters ya kwanza ni hiyo ya arbitration ambayo kachukulia cambridge, na masters ya pili ni ya jurisprudence.

yeye ni mzanzibar, ila ni par time lecturer wa Mzumbe university-mbeya campus kwa sasa hivi.

pia yeye sasa hivi anachukua PHD ya jurisprudence.
 
Naomba nizungumzie suala hili kidogo. Tofauti na wengi wanavyoelewa, arbitrators si lazima kuwa wanasheria. Arbitration ni njia mbadala iliyowekwa kwa pande zinazohusika katika mkataba kutumia kabla ya kwenda mahakami. Mara nyingi, arbitrators ni watu waliobobea katika fani inayohusika na mkataba nawamesoma masomo ya ziada ya arbitrators. Kwa mfano katika miradi ya majengo hawa wanaweza wakawa wahandisi, wasanifu majengo (architects) au wakadiriaji majengo. Orodha yao inatunzwa na National Construction Council (NCC). Hawa wanatumika kwa vile wanauelewa zaidi wa complexities zinazoweza kutokea wakati wa kutekeleza mkataba. Utaalamu huu unatokana na experience ambayo mwanasheria hawezi kuwa nayo. Katika miradi ya ujenzi dispute inapotokeza, wahusika wanapelekewa majina ya arbitrators na wao wanachagua wale wanaoona wanawafaa mpaka hapo watakapokubaliana. Gharama zinawekwa wazi na zinagawiwa sawa sawa kwa wahusika. Wahusika wanatakiwa kuweka deposit kabla suala halijaanza kushughulikiwa. Kama tulikuwa tunapeleka wanasheria pekee yao kwenye masuala ya arbitration tulikuwa tunafanya makosa. Kule ni utaalamu kuhusu ishu ndiyo muhimu. Sijui kwenye fani nyingine, lakini hawa ndugu kwenye masuala ya majengo wapo wengi tu.
 
It is all about Certification.
A lawyer and a certified lawyer are two different people.

Madilu umesema kile ambacho nilitaka kusema.Huwezi kusema chochote katika hili jambo bila kujua Marmo ana certification gani inayokubalika kimataifa na kaipataje, na kama kuna wengine waliyo nayo nchini, kama inaweza kupatikana nchini au ni lazima ikatafutwe nje.
 
Nyani

maelezo sahihi kuhusu arbitrators ni kama alivyoyaweka ndg yetu Fundi hapa chini...watch out the highlighted....

Naomba nizungumzie suala hili kidogo. Tofauti na wengi wanavyoelewa, arbitrators si lazima kuwa wanasheria. Arbitration ni njia mbadala iliyowekwa kwa pande zinazohusika katika mkataba kutumia kabla ya kwenda mahakami. Mara nyingi, arbitrators ni watu waliobobea katika fani inayohusika na mkataba nawamesoma masomo ya ziada ya arbitrators. Kwa mfano katika miradi ya majengo hawa wanaweza wakawa wahandisi, wasanifu majengo (architects) au wakadiriaji majengo. Orodha yao inatunzwa na National Construction Council (NCC). Hawa wanatumika kwa vile wanauelewa zaidi wa complexities zinazoweza kutokea wakati wa kutekeleza mkataba. Utaalamu huu unatokana na experience ambayo mwanasheria hawezi kuwa nayo. Katika miradi ya ujenzi dispute inapotokeza, wahusika wanapelekewa majina ya arbitrators na wao wanachagua wale wanaoona wanawafaa mpaka hapo watakapokubaliana. Gharama zinawekwa wazi na zinagawiwa sawa sawa kwa wahusika. Wahusika wanatakiwa kuweka deposit kabla suala halijaanza kushughulikiwa. Kama tulikuwa tunapeleka wanasheria pekee yao kwenye masuala ya arbitration tulikuwa tunafanya makosa. Kule ni utaalamu kuhusu ishu ndiyo muhimu. Sijui kwenye fani nyingine, lakini hawa ndugu kwenye masuala ya majengo wapo wengi tu.

kwa hiyo Arbitrators...............husomea disputes resolution kwa fani husika as outlined in their Contracts and as per Conditions of Contracts
 
Cha kufanya hapa ni kuhakikisha serikali inasomesha wasuluhishi wa kutosha kwenye fani nyeti (madini na biashara za kimataifa) kwa kutumia vyombo vinavyoheshimika kimataifa na kushurutisha katika mikataba hiyo kwamba wasuluhishi wawe na certification hizi ambazo watanzania watakuwa nazo.Kutoka hapo kutakuwa hamna haja ya kuwatoa wasuluhishi hawa nje.

Maadamu ubaki (neutrality) wa msuluhishi haupotezwi mimi sioni tatizo wasuluhishi kutoka ndani wakifanya hizi kazi kwani inawezekana kabisa wao ndiyo wakawa na taarifa na elimu nzuri zaidi kuhusu migogoro hii kuliko hata watu wa kutoka nje.
 
Unfortunately, Pundit, arbitrators ni lazima wakubalike na pande zote zinazohusika kwenye mgogoro. Na watatoka wapi, hii huwekwa kwenye Conditions of Contract. Katika mikataba ya mataifa mara nyingi arbitration inafanywa chini ya usimamizi wa the International Chamber of Commerce http://www.iccwbo.org/court/

Ni vigumu katika mikataba ya aina hii kudai kuwa arbitrators watoke katika institute ya nchi yeyote husika maana neutrality ya arbitrators ni paramount. Kwenye mikataba ya ujenzi nyumbani mara nyingi NCC ndiyo wanakuwa wasimamizi. Cha msingi ni kuwa na wataalamu wa kwetu wanaojua taratibu za ICC na kuwatumia ipasavyo. Cha muhimu kukumbuka ni kuwa katika arbitration si sheria peke yake ndiyo inayotawala, expertise nayo ni muhimu. Matatizo yetu ni kuwa tunapo'sign' mikataba tunakuwa wagumu sana kukubali kuwa kuna uwezekano wa disputes kwa hiyo suala la dispute resolution hatulipi kipaumbele. Hulka yetu ni kufikiri kuwa tukukazania suala hili itaonekana kama hatumwamini mwenzetu. Mara nyingi, si suala la ufisadi bali hulka yetu ya kiswahili. Inabidi tubadilike na kuangalia mkataba kama mkataba na si vinginevyo. Inabidi vilevile wataalamu wetu wachangamkie nyanja hii. Si wajibu wa serikali kusomesha watu hawa. Ni sisi wenyewe ku'take advantage' ya void iliyokuwepo. Serikali haiwezi kupendekeza waajiri wake wawe ma arbitrators lakini kama kuna independent experts kutoka Tanzania waliokuwa cerified kwa mfano na ICC, inaweza kuwapendekeza wawe kwenye panel. Tukumbuke lakini si lazima upande wa pili iwakubali hata kama tumewapendekeza!!!
 
Fundi,

Kama serikali ni sehemu ya mkataba, na Tanzania kuna watu waliokuwa certified na vyombo vinavyoheshimika kimataifa, sioni kwa nini serikali isihakikishe kuwa katika vifungu vinavyohusu mizozo na upatanishi wasiweke wazi kuwa kukitokea mzozo basi msuluhishi lazima awe certified na chombo chenye heshima ya kimataifa.Uzuri ni kuwa kama tuna Watanzania wenye hizo certifications wata-qualify.Juhudi ziwekwe ku-define wasuluhishi kwa taaluma zao (e.g certification) na siyo kwa utaifa.

Tukifanya hivi, na kama mikataba inaandikwa vizuri, wawekezaji hawatakuwa na msingi wa kisheria kutoka kwenye mkataba kukataa msuluhishi kutoka Tanzania.Mara nyingi kutambua certification maana yake ni kumtambua mbeba certification, hiyo pia inakuja na kutambua neutrality yake.Unless ame-Kivuitu something in which case he should be immediately de-certified kama UDSM wanavyotaka kumvua degree Kivuitu.
 
Back
Top Bottom