Kuliko kuajiri mfanyakazi wa ndani tuwe na utaratibu wa kuchukua watoto wa ndugu kwa nia ya kuwaendeleza

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Unakaa na mtoto kwa mkataba wa kumsomesha au kumuendeleza. Mnapanga muda wake wa kwenda shuleni au mafunzoni na muda wake wa kazi. Anaishi kama mtoto wa nyumbani, unamnunulia mahitaji yake madogo madogo. Sehemu kubwa ya mshahara unakwenda kulipia ada na Bima ya afya.

Akihitimu mafunzo unamuwezesha kujitegemea na unatafuta mwingine. Kama ndugu zako wote mambo safi unaweza kuchukua vijana wa kijijini kwenu. Hii ni njia ya kurudisha katika jamii na kukwamuana kimaisha.
 
Hongera Sana mdada. Mwenyewe nimechukua mtu wa hivyo Mana pia unaendeleza watu wa karibu yako.atasoma mazingira mazuri ya kujisomea ni Tofauti akiwa huko makwetu.

Sema naona hanipi morale Mana hakeshi Kama nilivyokuwa nakesha.anawaza kunyoosha nguo ya shule ili apendeze.mie namwambia ukifaulu ukipata hesabu A utakuwa unaonekana tu msafi na una nidhamu hata shati hujafua mwezi.

Mana binadamu bana hajui anachotaka ama akipendacho
 
So akisifiwa kuwa ni mzuri ndo anazidi kuwa msafi ili awavutie wale.
Yaani ego inazidi kujaa kichwani kwake.ni Kama wame induce so inafanya kazi saivi.isnt it?
Wa kwangu nikiondoka tu anaingiza vidume ndani. Hakuna kusafisha nyumba wala kuosha vyombo. Akila shuleni mchana ndo basi, jioni hapiki hadi nirudi. Mwanangu mdogo anateseka na njaa.

Fadhila afadiliwe mbuzi iko siku atanywewa mchuzi.
 
Ni jambo zuri sana ikiwa utapata watu wanaojitambua na kuelewa wajibu wao.

Kwa uzoefu wangu, ndugu au jamaa wanaweza kukupa kero na namna ya kushughulika na kesi zao inajumuisha watu wengi ambao inawezahatarisha mahusiano kwenye familia.

Ukipata anaejitambua, ni raha sana, lakini wengi wao wanakuja na mtazamo kwamba hapo wapo kwa ndugu yao na wao sio wafanyakazi, wanaweza kumvimbia wife ikawa tafrani.

Nawasaidia lakini mmalawi lazima awepo kufanya wajibu ambao mahusiano yetu ni kazi na ujira.
 
Uzoefu wangu: watoto wa ndugu (baadhi) ni shida sana. Akitumwa kazi hakawii kupiga simu kwao kusai anateswa sana

Bora umsaidie kivingine tu ila linapokuja suala la kazi/usaidizi kuwe na options nyingine
Asili ya binadamu ni majungu na wengine wanasahau hali zao. Na yeye anataka aishi kama Junior, ale chocopops kwa breakfast. Mkishindwana unamridisha kwao salama.
 
Tatizo wanawake wengi wanapenda kuwapelekesha au kuwafanyisha kazi nyingi hao wadada wa kazi. Kwa hiyo kwa mtoto wa ndugu hutaweza kumfanyia hivyo kwa sababu ndugu lawama ataona unamnyanyasa atataka kurudi kwao.

Pili kwa upande wa wanaume wengine wanapenda "kujisevia" kwa wadada wa kazi. Kwa hiyo housegirl akiwa ni ndugu atawezaje kumfanya?
 
Ni jambo zuri sana ikiwa utapata watu wanaojitambua na kuelewa wajibu wao.
Kwa uzoefu wangu, ndugu au jamaa wanaweza kukupa kero na namna ya kushughulika na kesi zao inajumuisha watu wengi amvao inawezahatarisha mahusiano kwenye familia.

Ukipata anaejitambua, ni raha sana, lakini wengi wao wanakuja na mtazamo kwamba hapo wapo kwa ndugu yao na wao sio wafanyakazi, wanaweza kumvimbia wife ikawa tafran.

Nawasaidia lakini mmalawi lazima awepo kufanya wajibu ambao mahusiano yetu ni kazi na ujira.
Malawi Ishakuwa official,sio Iringa tena?
 
Unakaa na mtoto kwa mkataba wa kumsomesha au kumuendeleza. Mnapanga muda wake wa kwenda shuleni au mafunzoni na muda wake wa kazi. Anaishi kama mtoto wa nyumbani, unamnunulia mahitaji yake madogo madogo. Sehemu kubwa ya mshahara unakwenda kulipia ada na Bima ya afya.

Akihitimu mafunzo unamuwezesha kujitegemea na unatafuta mwingine. Kama ndugu zako wote mambo safi unaweza kuchukua vijana wa kijijini kwenu. Hii ni njia ya kurudisha katika jamii na kukwamuana kimaisha.
Wazo zuri hili ila sio kila mtu anaweza kuishi na mtoto wa mwenzie kwa usawa bila ubaguzi. Kuna wamama wengine mna ubaguzi wa dhahiri kabisa inapelekea kumtia mtu uchungu na kujuta hata kuwafahamu.

Nia ni njema ila inapofikia watoto wako wanakuwa of more concern kuliko yeye inafikia stage unamfanya kama kijakazi huo unakuwa sio msaada tena bali ni kumfanya mtumwa! Kumgeuza mtoto wa kaka yako mtumwa its the worst form of relationship you can ever thought of creating.

Wengine tumekulia mazingira hayo watoto wa nyumba hio wao wanakula cakes na mayai asubuhi nyie mnakula magimbi. Wanalia sahani nyie mnapigwa kwenye sinia chini! Nyama za baba tu japo baba kanunulia familia nzima ile ila anapikiwa yeye na wanae nyie mwendo wa kabichi na maharage tu. Siku za shopping ya vyakula watoto wake wananunuliwa chocolates na pringles wanalia chumbani na kupangusa midomo mtakutana na maganda tu. Alfajiri uamke ufagie kiwanja na banda la mbuzi kisha unaenda shule hata chai hujanywa hupewi hata sh.100 utembee wao wanapandishwa school bus na buku ya kuspend on break time hapo washakula cakes, mayai na chai asubuhi! I don’t wanna remember that life aisee...Siwezi ruhusu mtoto wa mtu apitie ile hali akiwa kwangu! I rather not take him/her.
 
Tatizo wanawake wengi wanapenda kuwapelekesha au kuwafanyisha kazi nyingi hao wadada wa kazi. Kwa hiyo kwa mtoto wa ndugu hutaweza kumfanyia hivyo kwa sababu ndugu lawama ataona unamnyanyasa atataka kurudi kwao. Pili kwa upande wa wanaume wengine wanapenda "kujisevia" kwa wadada wa kazi. Kwa hiyo housegirl akiwa ni ndugu atawezaje kumfanya?
Hii mkuu ni ukweli 200%,,
Wanawake wanajua kuwatumikisha hawa mabint,
Unakuta ana mpa kazi ad wewe unaona aibu,
Na ukimtetea t atakuambia utakua unatembea nae huyu sio bure kwann umtete..
Ukisema ujaribu t kujiweka nae karbu a feel comfortable ndo unazidi kuchochea moto 😁
 
Wa kwangu nikiondoka tu anaingiza vidume ndani. Hakuna kusafisha nyumba wala kuosha vyombo. Akila shuleni mchana ndo basi, jioni hapiki hadi nirudi. Mwanangu mdogo anateseka na njaa.

Fadhila afadiliwe mbuzi iko siku atanywewa mchuzi.
Waeleze theorists
 
Hongera Sana mdada.mwenyewe nimechukua mtu wa hivyo Mana pia unaendeleza watu wa karibu yako.atasoma mazingira mazuri ya kujisomea ni Tofauti akiwa huko makwetu.
Sema naona hanipi morale Mana hakeshi Kama nilivyokuwa nakesha.anawaza kunyoosha nguo ya shule ili apendeze.mie namwambia ukifaulu ukipata hesabu A utakuwa unaonekana tu msafi na una nidhamu hata shati hujafua mwezi.
Mana binadamu bana hajui anachotaka ama akipendacho
Achana na habari za kum control! Ukimsaidia mtu mwache free afanye anachopenda you guys mnafeli hapa...Unapomsaidia mtu usimuhenyeshe maana ile mantiki ya msaada inakuwa haipo kabisa na wala hizo thawabu unazozitaka hutazipata! Assist someone with a clean heart. Sio ndio umfanyishe makazi kama punda na kumkosesha amani!

Kuna watu wanakaa na watoto wa wenzao yani mtoto hawezi juta kuishi hapo sababu wote wanapata fair treatment! Sio mtoto wako shopping Mlimani wa mwenzio unampa hela aende Ilala Boma akanunue mtumba! Haya ndio mambo ya hovyo
 
Back
Top Bottom