Stori ya mkazi wa Hanang aliyepoteza mke na watoto 4 imenibadilisha sana

Kamkunji

Member
Sep 14, 2023
92
273
Nimeona BBC kupitia mitandao ya kijamii, Jamaa anaitwa Fanuel John, amepoteza familia yake na mali zake zote familia yake ni mke wake, mtoto wa miaka 13, 10, 8 na miaka 4 kwa mfuatano kama kijana mwenye familia nimehuzunika sana, nimewaza sana kuhusu maisha, watoto wangu, mke wangu, kazi yangu, wazazi wangu, ndugu zangu, Nchi yangu na kila yeyote anayenizunguka.

Nimekumbuka kaka yangu mmoja ambaye hua kila akiambiwa aoe anajivuta vuta sahv ana miaka 43, na anasema yeye ataishi na kurudi mbinguni (kufa) kama alivyokuja duniani(peke yake), nimejisemea inamaana Fanuel anaenda kufanana na kaka ambaye yeye hajawahi kuoa wala kua na mtoto, inshort anajiwazia yeye tu?

Fanuel anaenda kuanza upya kabisa kujitafuta, kutoka kuitwa baba kila siku mpaka kuzika familia nzima, na kati ya hao watoto kuna mmoja hajapatika sasa hapo ndiyo mtihani, atakutwa hai ama amekufa, maana yake tayari kazikiwa watoto watatu na mke mmoja maana yeye yuko hospitali.

Kweli hii dunia haina huruma, nimeumia sana. Kwa nionavyo mitandaoni kwingine maisha yanaendelea vizuri kama kawa, sehemu za starehe zinafurika, kina Vunjabei wanafungua maduka yao mapya weekend wakiwa na kina Harmonize, ziara zinaendelea kama kawaida na hakuna kilichosimama.

Nimekumbuka ujumbe mmoja niliuona kwa yule kijana wa Singida anaitwa Joram nkumbi anasema maisha ni yako na kifo ni chako pia, usilalamikie mtu, wewe wakati utakufa hakuna kitakachobadilika, ratiba zote za nchi na dunia zitaendelea kama zilivyopangwa, ratiba pekee inaweza kubadilika kidogo ni ratiba ya familia yako nayo ni kwa siku chache then itaendelea kama kawaida, hivyo sisi wote ni wa kawaida sana japo ni wa thamani,

Madhira aliyopata Fanuel anahitaji psychotherapist haraka sana na wengine wengi wenye tatizo kama lake huko Hanang, la sivyo mtu anaweza kuamua kuifuata familia yake, moyo wa mtu kichaka usimuone anasimulia tu huwezi jua.

Nimejifunza mengi kutoka katika tukio hilo la mafuriko, nimegundua maisha haya si chochote wala lolote yanaweza kuyeyuka wakati wowote kama mshumaa tusali sana ndugu zangu kila mmoja kwa imani yake, wa kanisani asali huko, wa msikitini vile vile, waamini mizimu pia, suala ni kujiombea mwisho mwema haijalishi unaomba kwa njia gani, wapi na kwa nani, huyo unaemwamini atakusaidia.

Maisha ni nini, binadamu anawaka na kuzimika muda wowote, unapoteza familia yako nzima ndani ya masaa machache unakua mtu mwingine kabisa, kwann usichanganyikiwe, yote kwa yote ni kushukuru kwa kila jambo lakini hiyo shukran sidhani kama akielezwa Fanuel sasa hv ataelewa.

Sijafuatilia namna ya kuwapa msaada watu wa Hanang, hasa wa kifedha maana niko mbali na nchi yangu, lakini naweza kutuma kwa mitandao kadhaa, naomba nielekezwe ama nipewe link nikatoe chochote kitu wakati nikiendelea kutafakari maisha vizuri, maana nahisi bado sijayajua vizuri, nahitaji kutuliza akili sana na kutafakari upya na upya tena.

Niwatakie nyote ijumaa njema, Mwenyezi Mungu aendelee kutusimamia maana hatujui siku wala saa
 
Nchi hata maomboleze ya siku 2 hakuna...basi hata ya siku 1 hakuna
Media zote wao ni singeli misondo amapiano udaku tu unaendelea
Anyway hili taifa ndiyo lishafikia hivyo

Ova
Nimejaribu kufuatilia vyombo vya habari nilivyo na access navyo, imegeuzwa kama story ya kuchekesha, hakuna utu, kila mtu ameshikilia cha kwake kama ulivyosema, ile Tanzania ya ujamaa siioni, imekuwa ya kibepari, kila mtu anakufa na msalaba wake.
 
nimejaribu kufuatilia vyombo vya habari nilivyo na access navyo, imegeuzwa kama story ya kuchekesha, hakuna utu, kila mtu ameshikilia cha kwake kama ulivyosema, ile Tanzania ya ujamaa siioni, imekua ya kibepari, kila mtu anakufa na msalaba wake,
Kuna mtu jana kaleta uzi hakuna video za kutosha za hilo janga la Hanang, na ukifikiria ni kweli matukio mengine kama ziara yanakua na full coverage, hili halina.

Viongozi wamegeuza tukio kua PR yao, wanajisafishia majina, hakuna impact yeyote
 
Nimeona BBC kupitia mitandao ya kijamii, Jamaa anaitwa Fanuel John, amepoteza familia yake na mali zake zote
familia yake ni mke wake, mtoto wa miaka 13, 10, 8 na miaka 4 kwa mfuatano
kama kijana mwenye familia nimehuzunika sana, nimewaza sana kuhusu maisha, watoto wangu, mke wangu, kazi yangu, wazazi wangu, ndugu zangu, Nchi yangu na kila yeyote anayenizunguka. Nimekumbuka kaka yangu mmoja ambaye hua kila akiambiwa aoe anajivuta vuta sahv ana miaka 43, na anasema yeye ataishi na kurudi mbinguni(kufa) kama alivyokuja duniani(peke yake), nimejisemea inamaana Fanuel anaenda kufanana na kaka ambaye yeye hajawahi kuoa wala kua na mtoto, inshort anajiwazia yeye tu.?, Fanuel anaenda kuanza upya kabisa kujitafuta, kutoka kuitwa baba kila siku mpaka kuzika familia nzima, na kati ya hao watoto kuna mmoja hajapatika sasa hapo ndiyo mtihani, atakutwa hai ama amekufa, maana yake tayari kazikiwa watoto watatu na mke mmoja maana yeye yuko hospitali
kweli hii dunia haina huruma, nimeumia sana
kwa nionavyo mitandaoni kwingine maisha yanaendelea vizuri kama kawa, sehemu za starehe zinafurika, kina Vunjabei wanafungua maduka yao mapya weekend wakiwa na kina Harmonize, ziara zinaendelea kama kawaida na hakuna kilichosimama,
Nimekumbuka ujumbe mmoja niliuona kwa yule kijana wa Singida anaitwa Joram nkumbi anasema maisha ni yako na kifo ni chako pia, usilalamikie mtu, wewe wakati utakufa hakuna kitakachobadilika, ratiba zote za nchi na dunia zitaendelea kama zilivyopangwa, ratiba pekee inaweza kubadilika kidogo ni ratiba ya familia yako nayo ni kwa siku chache then itaendelea kama kawaida, hivyo sisi wote ni wa kawaida sana japo ni wa thamani,

Madhira aliyopata Fanuel anahitaji psychotherapist haraka sana na wengine wengi wenye tatizo kama lake huko Hanang, la sivyo mtu anaweza kuamua kuifuata familia yake, moyo wa mtu kichaka usimuone anasimulia tu huwezi jua,
Nimejifunza mengi kutoka katika tukio hilo la mafuriko, nimegundua maisha haya si chochote wala lolote yanaweza kuyeyuka wakati wowote kama mshumaa
tusali sana ndugu zangu kila mmoja kwa imani yake, wa kanisani asali huko, wa msikitini vile vile, waamini mizimu pia, suala ni kujiombea mwisho mwema haijalishi unaomba kwa njia gani, wapi na kwa nani, huyo unaemwamini atakusaidia
Maisha ni nini, binadamu anawaka na kuzimika muda wowote, unapoteza familia yako nzima ndani ya masaa machache unakua mtu mwingine kabisa, kwann usichanganyikiwe, yote kwa yote ni kushukuru kwa kila jambo lakini hiyo shukran sidhani kama akielezwa Fanuel sasa hv ataelewa,
sijafuatilia namna ya kuwapa msaada watu wa Hanang, hasa wa kifedha maana niko mbali na nchi yangu, lakini naweza kutuma kwa mitanda kadhaa, naomba nielekezwe ama nipewe link nikatoe chochote kitu wakati nikiendelea kutafakari maisha vizuri, maana nahisi bado sijayajua vizuri, nahitaji kutuliza akili sana na kutafakari upya na upya tena,

Niwatakie nyote ijumaa njema, Mwenyezi Mungu aendelee kutusimamia maana hatujui siku wala saa
Hopefully msaada wako utapokelewa kwani kuna viongozi waandamizi wa CDM walienda na misaada kwaajili ya wahanga na wakazuiwa na jeshi la Polisi kuingia Hanang then wakaamriwa warudi walipotoka.
 
Hili janga la Hanang ni kubwa mno kuliko mtu ambae halijamkuta kuweza kutafakari.

Inawezekana kuweka maombelezo hata ya siku 3 kusingebadilisha athari iliyotekea lakini nahisi ingeweka muamko juu ya athari hasa iliyotokea.

Ufikishaji wa taarifa ya hili janga na vyombo vya habari unafanywa kwa wepesi mno kama vile ni kitu kidogo kimetokea. Nahisi hata hao BBC wamefanya jitihada zaidi ya kuhoji na kufuatilia kuliko hawa wa kwetu huku.
Kikubwa kinachoripotiwa na selfies zinazoenda kupigwa na wanasiasa.

Mungu ampe subira na ustahmilivu Bw. Fanuel na awape nguvu wengine wote walioathirika na kubwa na muhimu zaidi atuepishe wengine na majanga yote. Amiin.
 
Back
Top Bottom