Kula ndotoni...

kula nini lakini, mi sijaelewa, unaweza kuota unakula (kutenda tendo la ndoa na mtu)...na ukaamka umelowa...wakati mwingine nindoto tu ila wakati mwingine majini au vizee vichawi vimekutembelea....kuna mbibi mmoja alishawahi kukamatwa kazi yake ili kulisha uchawi ufanya kazi vizuri alitakiwa usiku kuwatembelea vijana wa kiume na kuwachezesha chumvini kwake weeee, ndo kafara yake ya uchawi...w.adada wengi tu wanaota usiku wanaliwa na wanaume asubuhi waamka wamelowa...ndo maana nikauliza kula nini? be straight tafadhali....mtatembea/chezewa na majini ya kike na kiume kina maimuna hadi mkome nyie msokuwa na Mungu.
 
Swali linanitatiza, jawabu natafutia,
Nimebaki ninawaza, nani atanipatia,
Sina wa kunijuza, bora kuwaulizia,
Mtu akila ndotoni, huamka ameshiba?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)
Anayekula ndotoni,hashibi asilani
Asubuhi na tongo jichoni,hodi nyingi kwa jirani
Nimekuja sabahini,mwala nini jamani?
 
Swali linanitatiza, jawabu natafutia,
Nimebaki ninawaza, nani atanipatia,
Sina wa kunijuza, bora kuwaulizia,
Mtu akila ndotoni, huamka ameshiba?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)
Mhhhhhhhh! Kwa jinsi ulivyo mtu wa hoja kali, napata shida kidogo kujibu swali hili. Sijajua kama huku kula ni kula kwa kawaida au kuna zaidi ya ujumbe ambao ungependa sisi tukujuze. Nachelea kufananisha na ule wimbo wa taarabu wa mdudu kaingiaje ndani ya kokwa la embe. Ngoja nifikiri kidogo, maana waswahili husema, anapoongea profesa, ni vyema waungwana mfikirie maana hatutegemei profesa aongee kitu kwa upeo wa kawaida.

Ntarudi baadae mwanakijiji, bado natafakari hilo neno 'kula ndotoni'.
 
Mara nyingi nikiota ndoto inayohusu chakula, sifanikiwi kula. Yaani ile nikitaka kuanza kula tu, nashtuka! Pia niliwahi kusikia kula ndotoni sio vizuri, sijui kama kuna ukweli wowote.
 
Swali linanitatiza, jawabu natafutia,
Nimebaki ninawaza, nani atanipatia,
Sina wa kunijuza, bora kuwaulizia,
Mtu akila ndotoni, huamka ameshiba?

kwa nini asishibe alichokuwa amekula.....................ingawaje kula siyo lazima ushibe inategemea umekula kwa kipimo au vipi.............
 
Swali linanitatiza, jawabu natafutia,
Nimebaki ninawaza, nani atanipatia,
Sina wa kunijuza, bora kuwaulizia,
Mtu akila ndotoni, huamka ameshiba?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)

Ni bure watatizika, kwa swali ulouliza
chakula huwa chalika, tena wengine husaza
Kipikwe kikapikika, mlaji kukimaliza
yategemea mlaji, kula ndotoni washiba.

Kwa alaye bakulini, au alaye kwenye mwiko
kushiba ni majinuni, atashiba mwenye mwiko
Hupunjwa wa bakulini, kushiba kwake ni mwiko
Atashiba mwenye mwiko, na sahani kuchafua.

Mwanakijiji hujambo? umelishwa ndotoni nini baba?
 
Ni bure watatizika, kwa swali ulouliza
chakula huwa chalika, tena wengine husaza
Kipikwe kikapikika, mlaji kukimaliza
yategemea mlaji, kula ndotoni washiba.

Kwa alaye bakulini, au alaye kwenye mwiko
kushiba ni majinuni, atashiba mwenye mwiko
Hupunjwa wa bakulini, kushiba kwake ni mwiko
Atashiba mwenye mwiko, na sahani kuchafua.

Mwanakijiji hujambo? umelishwa ndotoni nini baba?

Mj1 mwenye bakuli ndo hufaidi, huchagua kivuli apate kufaidi,tena kelele apiga pilipili ikinoga,mwenye bakuli afaidi mchuzi pia na ujira..mwenye upawa huonja mchuzi mwenye bakuli kushiba ndo jadi...m'kijiji ashibaye ndotoni ndiye mlaji wa ukweli...tena atakula..
 
Mj1 mwenye bakuli ndo hufaidi, huchagua kivuli apate kufaidi,tena kelele apiga pilipili ikinoga,mwenye bakuli afaidi mchuzi pia na ujira..mwenye upawa huonja mchuzi mwenye bakuli kushiba ndo jadi...m'kijiji ashibaye ndotoni ndiye mlaji wa ukweli...tena atakula..

Ndotoni MORIA??

Wa bakuli yake mboga, akaitia kwa ndani
Wa mwiko ni kukoroga, Hiyo mboga bakulini
Akashiba na kumkoga, mwenye yake bakulini
Ashibaye mwenye mwiko, akachafua sahani

Ashiba aliye na mwiko, wa bakuli akadoda
ushahidi wake mwiko, ni sahani yenye mashada
Kujua kashiba mwiko, kusafisha ndio kada
Ndoto atashiba mwiko, asubuhi asafishe.

Anayeshiba ni mwenye mwiko na ushahidi ni makombo ya chakula alokula ndotoni. Mwenye bakula japo atakula lakini hatoshiba!

Labda Mwanakijiji aseme kushiba ni tofauti na kucheua/beua!!
 
Haa haaa mj1,moria na mwanakijiji bigup sanaaaaa duu mko vizuri ila mfundisheni moria kupanga mashairi yake bana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom