Kukopa mtu pesa kunadhalilisha sana

Kukopa mtu pesa kunadhalilisha sana

Mkuu Usiogope ,anakopa pesa Bakhresa tajiri wa kwanza Tanzania ndio itakuwa wewe?
Tatizo ni kuwa unakopa kwa nani!! Kukopa kwa Shabani au kukopa salary advance kipi kina unafuu hapo?
 
Tatizo ni kuwa unakopa kwa nani!! Kukopa kwa Shabani au kukopa salary advance kipi kina unafuu hapo?
Kama una access na salary advance why not usikope? Kama una mtu wa karibu na ana mpunga ambao unaweza kumkopa why not usimkope? Akienda kutangaza kwani kuna shida gani? Mimi nikikopa nasema kabisa flani ananidai kihasi flani maana mwanamme asiyekuwa na madeni bas ajitakafari huyo....Mtu asiyekuwa na madeni basi hakuna anachofanya zaidi ya kutafuta hela ya kula na kununua nguo tu kwa kifupi hana majukumu.
 
Hii ni kutokana na mazingira ambayo wewe umeyatengeneza kwao. Usipende kujionesha kuwa unashida sana ya pesa. Kuna wakati huwa ninakuwaga na shida saaana ya kifedha. Unakuta sina hata 5,000/= kwenye wallet ila ninakuwa normal sana na sioneshi kupapatikia wala kujipendekeza kwa watu.

JIFUNZE KUTOKA KWANGU!
hujui shida wewe. Unadaiwa ada halafu ubaki nomrmal.
Luku imeisha na familia yote inakuangalia wewe halafu unabaki normal
Hakuna cha kujifunza kutoka kwako mkuu
 
Una weza mkuta tajiri kakaa sehemu ukafika pale kwa nia nzuri tu kuwasalimia utakapoanza kitoa salamu yeye atawazia unashida napesa
 
Mbona wanawake hawana aibu ya kukukopa (bby nikope laki )bby naomba vocha
 
Kumkopa mtu pesa kunadhalilisha sana mbaya zaidi umuelezee mtu tatizo lako akukopeshe pesa halafu asikukopeshe aseme hana,inafedhehesha sana.

Au uwe na rafiki unamkopa pesa na huwa unamlipa kwa wakati lakini yeye hajawahi kukukopa nayo inafedhehesha sana siku mkigombana atatumia nafasi hiyo kukunyanyasa.

Kuna baadhi ya watu ukiwa text wanadhani unataka uwakope pesa.

Kuna wengine wakikukopesha wanaenda kukutangaza.
Tafta hella dogo acha kulialia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanaume/ mtu asiye na madeni ajitafakari kivipi tena? Kama ana kipato kinachomtosha matumizi yake + saving why akope? Usijaribu kutuaminisha kwamba ukopaji ni kitu essential kwa maisha ya watu.
Hakuna mtanzania anayejiyosheleza kihasi asikope kamwe ila kama tajiri sana atapungua mikopo binafsi na kufanya ile ya taasisi kama bank.
 
Unapokopa unatakiwa umtamanishe mkopeshaji kama kweli unajiamini Unakopa na utarudisha, nenda mfate mkopaji mwambie "nikope 50,000 nitakurudishia 70,000 naweka hii CM yangu bondi" mkopaji kama kweli hela anayo lazima akupe tu>

maana akili yake itawaza ile riba lkn pia itawaza ile cm yako endapo itatokea ukashndwa rudsha, kwahyo akiona vtu vyote hivyo uhakika wa wewe kupata mkopo ni 81%.

Ila haya maswala ya kwenda kukopa kwa maneno makavu eti "nikopeshe 100,000 nitakurudishia next week" asee kumpata ataekukopesha n nadra sana na hapo ndio ile ya mkopeshaji anaanza kukuuliza "ooh unataka yanini" ukafanye nini,nk nk maswali ya kipambe pambe tu.

MWISHO : acha kutilia huruma unapoenda kukopa,act as if hata akikunyima "ni sawa tu" Jiamini,yani kopa kama vile akikupa hiyo hela unaenda nywea K vant na Balimi,usimuonyeshe dalili za huzuni/uhitaji ulioptliza.

Usiseme sababu yako ya kwann unakopa,MWIKO kama ni wakukupa atakupa kama hakupi hakupi tu.
siwezi kukopa zaidi ya elfu 10 huwezo wa kulipa sina ,nakopaga elfu 2 -10 sana sana elfu 5 ndo ipo ndani ya uwezo wangu.
 
Una weza mkuta tajiri kakaa sehemu ukafika pale kwa nia nzuri tu kuwasalimia utakapoanza kitoa salamu yeye atawazia unashida napesa

Tatizo;

<Tajiri yuko DESPERATE
<Wengi Wanaomzunguka Wako DESPERATE
<Amepata Utajiri Through DESPERATION

Ndivyo Ilivyo Kwa Walio Wengi...

Utajiri ni MOYO...

Jah Bless
 
Faida ya kukopa ni kwamba aliyekukopesha anakua anakuombea maisha marefu na afya njema ili uweze kumlipa deni lake.
haaa..haaaa.........haa.hh..... nilijua kutatoka kauli moja nzuri sana ambayo itajenga ukuta wa nguvu kuliko ule wa Tanzanite kwa kuwa wengi tuna kopa nimeipenda hii nimejikuta naiona ijumaa ghafla kwa furaha.
 
Once binadamu wote tumeumbwa na chembe za Ego na Privacy ila umasikini unapoingilia kati inauwa chembe zote mbili.

Period, kila mtu anapenda kuwa na Privacy na sdida zake asijue mtu ila shida inakuwa no way out ya kuSolve shida ndio unauwa Privacy yako.

"Hakuna masikini mwenye Privacy duniani" privacy ni kwa aliye vizuri tu.

_Utapofanya upembuzi hata jukwaani JF utaona wasio kuwa Financial Stable malanyingi ndio wanaandika nyuzi za maisha yao binafsi kama kuomba kazi, mtaji, msaada nk.

Bottomlime
tupambane tuweze kulinda privacy zetu na Ego.
Umeiweka kitaalamu na kiuhalisia sana, bravo.
 
siwezi kukopa zaidi ya elfu 10 huwezo wa kulipa sina ,nakopaga elfu 2 -10 sana sana elfu 5 ndo ipo ndani ya uwezo wangu.
Acha uwoga dogo mimi juakali tu ila nikipata Access ya kukopa 3M nabeba mzigo.
 
Ukweli mchungu ambao inabidi ujue ili kutengeneza maisha yale ambayo hutakuwa na shida za kukopakopa hovyo moja ya njia ya kufika huko ni kukopakopa.

Bottomline
_Usijione upo salama sana eti kwasababu wewe ukopikopi unajidanganya shida za kipuuzi zinakulia rada tu.
 
Kumkopa mtu pesa kunadhalilisha sana mbaya zaidi umuelezee mtu tatizo lako akukopeshe pesa halafu asikukopeshe aseme hana,inafedhehesha sana.

Au uwe na rafiki unamkopa pesa na huwa unamlipa kwa wakati lakini yeye hajawahi kukukopa nayo inafedhehesha sana siku mkigombana atatumia nafasi hiyo kukunyanyasa.

Kuna baadhi ya watu ukiwa text wanadhani unataka uwakope pesa.

Kuna wengine wakikukopesha wanaenda kukutangaza.
usiogope hakuna binadamu au mtu anayeweza kujitosheleza, wote tunategemeana tu. kama hakopi kwako iko sehemu anakopa na wewe kipo anachokitegemea kwako huenda inaweza kuwa goodwill yako na mawazo unayompa yanampa faraja ambayo ni zaidi ya pesa. hivyo haoni sababu ya kutokukupesha au huenda wewe bado unahangaikia basic needs yeye anahitaji mahitaji mengine ya uwekezaji je waweza kumkopesha? unakopa kwake hela ya kula je aje kwako akope hela kutengenezea gari utamwelewa?
unahitaji kuwa mwaminifu katika kurejesha vinginginevyo maneno yasikutie hofu kwanza watu husahau.
lakini ni vizuri kuwa na bajeti kwa kuwa itatusaidia kuwa na mipango mizuri ya matumizi yetu na kupunguza mikopo isiyohitajika. kwa kuwa tunaweza kujua matumizi yetu na vyanzo vyetu kwa uhakika na kutafuta jinsi ya kukabiriana navyo.
 
Niliona jamaa anakopa laki 4 ,anaweka bondi pikipiki na kudai atarudisha laki 7 baada ya wiki 2! nikajiuliza huyu jamaa yupo sawa kweli
Na akaenda mbali akaahidi zikipita hizo wiki 2 adaiwe milioni moja.
Wiki 2 zilipita hakuonekana. Mpaka leo naona mkopeshaji anatumia hiyo boda

Mmhh hiyo kali
 
Back
Top Bottom