Uchambuzi wa kina kuhusu kozi za computer - IT, Computer science, Computer Engineering, Software engineering na Cyber security

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,096
Uchambuzi wa kina kuhusu utofauti wa IT, Computer science, Computer Engineering, Software engineering na Cyber security.

Post hii nimewandalia hususan wanafunzi waliomaliza sekondari wakitarajia kwenda vyuoni kusomea kozi za computer ila kwa sababu ya ugeni wa elimu ya chuoni pamoja na muda mfupi wa kufanya maamuzi, wanapata wakati mgumu wa kujua ni kozi ipi ya kuchagua itayowafaa.

Kukosea kuchagua kozi sahihi ni ajali kama ajali zingine. Kukosea kuchagua kozi unaweza kukutana na vitu ndivyo sivyo ulivyodhania, kozi ukikosea kuichagua unaweza kumaliza chuo na hakuna ajira zake hapa bongo.

Kozi ukikosea kuchagua unaweza ukawa umeparamia vitu ambavyo vimekuzidi uwezo na kupelekea usome kwa kutumia nguvu kubwa sana hata kwenye vitu ambavyo ni basic, hii itafanya elimu yako chuoni iwe ya mateso makali kupelekea uwe unafanya mitihani ya marudio (ku supp) na endapo ukishindwa mitihani hii unajiongezea mzigo wa masomo ya ziada kwa kuanza upya kuyasoma darasa moja la wale uliowazidi darasa (ku carry masomo).

Mwisho wa siku unahitimu ukiwa na gpa ya ndogo sana na huwa inawekwa kwenye cheti ama utafukuzwa kabisa chuoni kwa kufeli kupita kiwango unarudi zako mtaani (tunaiita kudisco / kuwa disqualified), n.k. Kwa wale wanaojiandaa kwenda vyuoni ama hapo mbele wana plan za kuja kusomea vyuoni katika kozi za computer, post hii itakuwa ni muhimu kwako kujua ni kozi ipi sahihi itakufaa.

Kwanza kabisa kabla hatujaanza uchambuzi ni muhimu kuelewa tofauti ya Science na Engineering.

🟡 SCIENCE
Scientists study, wanasayansi husoma kitu kwa ndani ili kuelewa ufanyaji wake wa kazi, wanahitaji kuwa na uelewa mkubwa sana kuzijua behind the scenes zinazoendelea pale kitu kinapofanya kazi, kwa kiasi kikubwa sana kozi za science huwa zinafundishwa theoretically zaidi, vitu vingi wanajifunza kwa fundamentals kuvijua kwa undani, hata kama ni formula / theory / principle / law wataichimbua ndani zaidi kujua fundamentals zake, fundamentals hizi ni muhimu pia ili kuja kuwaandaa kuweza kuwa watafiti (researchers) na kuzitumia kufanya experiments, scientific findings zikipatikana zinafowadiwa kwa engineers ili wazitumie kwenye kazi zao.

🟢 ENGINEERING
Engineers create, Engineering hujikita kumuandaa mtu kuwa na skills za kujenga / kutengeneza vitu kwa kutumia misingi ya kisayansi, wanatumia principles, laws, formulas, n.k ambazo zilishafanyiwa utafiti na zikawa proved kufanya kazi, Hawana muda wa majaribio, Ukimpa mhandisi pesa ajenge kitu atatumia maarifa ambayo yameshakuwa proved yanafanya kazi, Kwa hio hata mafunzoni vitu kama formula huwa wanazitumia moja kwa moja kuliko kuanza kuzichumbua kwa ndani wa fundamentals.

Ok, nisiwachoshe sana, tuanze uchambuzi wa hizo kozi sasa, Najua wengi mnaweza kukimbilia chini haraka haraka kwenda kusoma maelezo ya kozi Ya Information Technology (IT), usiwe na haraka tafadhali!! Haraka haraka haina baraka!! tulia usome kwanza uchambuzi wa kozi za computer science na computer engineering ndio utaweza kuelewa vizuri zaidi maelezo niliyotumia kuichambua kozi ya IT.

1️⃣ COMPUTER SCIENCE

Hapa husomei computer, unasomea computing, zile process zinazofanyikaa nyuma ya pazia tunapotumia computer katika upande wa software, haihusu mambo ya hardware kama feni inayozunguka tunavyotumia pc, switch ya kuwasha pc, vioo vya smartphone, n.k. Utajifunza kuna kitu kipi nyuma ya pazia kinaendelea mpaka operating system kama windows / android / ios inafanya kazi, kinachofanyika mpaka game lichezeke kwenye playstation / simu, kinachofanya calculator itoe jibu sahihi, kitu gani kimefanyika mpaka tunaweza kufungua mafaili ya pdf, n.k

Process za computing zinazoendelea nyuma ya pazia ndizo zinawezesha computer iwe kifaa kamili tunachoweza kukitumia, computing huhusisha zaidi muunganiko wa Hesabu na Programming, hivyo computer science ni kama muungano wa programming na hesabu.

Kwenye hesabu zinazofanyika kwenye computer, nadhani neno “compute” si geni kwenye mitihani ya hesabu tuliyowahi kuifanya hata sekondari, kuna yale maswali unaambiwa compute x, basi nikueleze tu ya kwamba hata computer huwa zinachakata hesabu kwa mpangilio maalum kwenye kutafakari, kufanya maamuzi, kutoa majibu, n.k. huku mtajifunza hata hesabu za binary kwa jinsi namba 1 na 0 zinavyotumika kwenye computer, si kwa kuzijibu tu kwenye karatasi kwa usahihi bali kujua ni namna gani zinatumika kwenye computer system, computer science ni kama tawi la hesabu linalodeal na uchakataji wa hesabu kwenye computer, kwa hio hata somo la hesabu ni takribani nusu ya kozi ya computer science na mtazisoma kwa fundamentals kiundani maana hii ni kozi ya science.

Upande wa pili mtajifunza pia programming kwa kiwango cha juu, Programming ni zoezi la kutengeneza programs zinazoweza kutumika kwenye computer ili kufanya kazi flani au kutatua kitu flani, program hizi zinaweza kuwa operating systems kama windows / android / ios , apps za simu, games, Microsoft word, n.k.

kozi hii ipo theoretically sana ili kuzielewa fundamentals, kwenye programming nako ni kuzijua fundamentals kwa theory ila kuna unafuu kidogo wa practicles. vitu mtavyojifunza ni kama computational theories, data processing algorithms, data structures, advanced programming languages, AI, software engineering / development, security, n.k. Kwenye upande wa hesabu kuna Calculus, combinatorics, Discrete math, Numerical analysis, binary numbers, math for algorithms, computational geometry, linear algebra, probability theories. formal methods and models, statistics for scientists, n.k.

Fundamentals zitawezesha pia kujua namna pogramming languages zinavyotengenezwa kiasi kwamba mtaweza kujitengenezea hata programming language zenu.
hakikisha kwenye hesabu upo vizuri unapoingia kozi hii, itakupunguzia mzigo uelekeze nguvu zaidi kwenye masomo mengine na programming.

Kwa watao apply chuo chenye kozi mbili za Bachelor of science in computer scence na Bachelor of science with computer science, hakikisha unachagua yenye “IN”

Programming Level ipo juu zaidi kwenye hii kozi, kama unapenda sana mambo ya programmng basi umegonga ndipo

🔷AJIRA

Mwenye taaluma hii ana sifa ya kufanya kazi nyingi za Information Technology, software engineering na cyber security, ajira zake za ziada ni kama Programmer, Data scientist, Cyber security analyst, Applications developer, Data analyst, Web designer, Web developer, Games developer, Artificial intelligence engineer, UX designer, Researcher (ukiwa na phd)

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za computer science, software engineering, cyber security, information technology.

2️⃣ COMPUTER ENGINEERING

Computer engineer ni ndoa kati ya vipengere vya computer science na electronics engineering vinavyomwezesha mtu kujua ubunifu wa hardware za computer. Ilianzishwa ikiwa kama tawi la electrical engineering (uhandisi wa umeme)

Hardware kivyake haiwezi kufanya kazi bila software, inahitaji program kama drivers ili kufanya kazi kwenye computer, kwa hio kwenye mambo kama haya kuna vitu kama programming vinachomolewa kwenye computer science, mfano mtajifunza kufanya programming ya kutengeneza drivers ili spika itoe sauti ikiunganishwa kwenye computer, kutengeneza bios , firmware za hardware, simple operating sysytems, kuzifanyia programming micro processors, n.k. Programming languages za kufanikisha hivi vitu mnaweza kujifunza nyingi lakini mtajifunza low level programming hususan katika kiwango cha kuzifanya hardware ziweze ku interact na software. Kuna vitu vingine vya ziada pia mtamegua kwenye computer science.

Kwa kuwa computer ni kifaa cha umeme, mtajifunza pia mambo ya electronics engineering, kuijua mifumo ya umeme katika vifaa vya computer, circuits, conducors, resistors, inductors, kuzijua laws za umeme, n.k. Kwa maarifa haya si ajabu mhitimu kuwa fundi umeme, pia anaandaliwa vizuri kuja kuwa fundi wa laptops / simu upande wa hardware na software.

Kwenye hesabu pia huku zipo za kutosha tu, hesabu nyingi za computer science zipo katika hii kozi na pia kuna hesabu za ziada za electronics engineering.

Ni kozi ambayo ni pana sana na ina vitu vingi, utakutana na electronics, hesabu, programming, n.k … Ni vema uwe na uwezo wa kuhandle kusoma vitu vingi kwa mpigo lasivyo kozi itakuwa knock out.

Kozi hii ina added advantage ya kutambulika kuwa engineer, Mfano kama ulikuwa unaitwa Mr au Mrs Fulani utaanza kuwa addressed kwa salutation ya Eng. Fulani.

Programming level sio advanced kama kwenye computer science ila sio basic sana kama kwenye Information Technlogy, Kwenye Programming languages mtajikita kujifunza kuzitumia kwenye kutengeneza interaction kati ya computer system na hardware

Kozi hii inahitaji practicles nyingi sana lakini kibongo bongo vyuoni utakuta hamfaidi vizuri, unakuta sehemu zinazohitaji practicles zinarukwa au zinageuzwa kuwa theory eti msome notes, ikitokea practicle ni mwalimu anaifanya yeye ama kuwaelekeza kwa mchoro au video ya youtube, mkifanya nyinyi basi ni kwa groups tena mara chache, seriously! Vitu hivi inabidi mwanafunzi ndio ajipimie awe anafanya mwenyewe tena kwa kurudia rudia, ajipimie mwenyewe mpaka aive, Kwa ushauri wangu, kwa baadhi ya practicles ikibidi wewe zama tu mfukoni, mfano nunua boards na components zako ufanye mwenyewe practicle za kuunda na kutengeneza motherboards kwa sequence inayofata logic, fanya mazoezi mara kwa mara mpaka uzoee (practice makes perfect).

🔷 AJIRA
Mwenye taaluma hii ana sifa ya kufanya kazi nyingi za Information Technology na computer science, ajira zake za ziada ni kama computer hardware engineer, electronics engineer, Electronics Design Engineer, Robotics Engineer, Micro electronics Engineer, Firmware Engineer, Digital Systems Engineer, fundi wa simu na laptops kote kote kwenye hardware na software.

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za computer engineering, computer science, information technology, electronics engineering.

3️⃣ INFORMATION TECHNOLOGY (IT)

Kozi nyingine mbadala ama zinazofanana ni Information systems na Information and communications technology (ICT)

Neno IT limejizolea umaarufu kimakosa kuwa msamiati mbadala wa ujuzi wa computer, Mitaani ama makazini tukimuona mtu ana ujuzi flani wa computer kwa level hata ya kawaida basi watsaema “yule jamaa ni IT”, hata hizo kozi zingine za Tehama ukiachana na IT watu wamezoea kuziita kimakosa “kozi zingine za IT”, wengine hata hawajuagi kuna kozi zingine kama nilizozichambua wao wanadhani kuna kozi moja tu ya IT, any way wacha niichambue IT ili mjue maana halisi ya IT.

Tofauti na kozi zingine kama computer science inayo deal na software ama computer engineering iliyo deal na hardware, kozi ya IT imejikita kwenye “MATUMIZI” ya hardware na software katika ku assist uendeshaji wa shughuli za serikali, makampuni binafsi, mahospitali, mashirika, biashara, n.k.

IT imelenga kutoa huduma (service) ila kozi zingine zimelenga zaidi kutengeneza bidhaa za software na hardware, IT ni huduma ambayo ni kiunganishi / daraja kati ya pande mbili. Upande wa kwanza ni computer scientists na engineers wanaotengeneza software na hardware, upande wa pili ni mashirika, taasisi, biashara zinazotaka kutumia bidhaa hizo kwenye kufanya shughuli zake kidijitali, IT yeye anakuwa ni middle man kwa kutoa huduma ya kuwezesha walengwa kuweza kutumia mifumo ya computer katika utendaji kazi.

Main focus ni kujifunza namna ya kutumia, kusimamia na ku minain software na hardware katika kuhakikisha mifumo ya tehama katika shirika inafanya kazi kulingana na shughuli zake. Utajifunza namna ya ku install software sahihi kwajili ya kazi flani, ku update software, kuingiza operating systems( almaarufu kupiga window), ku configure/kuseti hardware ifanye kitu flani, kuweka usalama kwa anti virus ama fire walls, kutengeneza data base, kusuka network mfano kuifanya printer moja itumike na computer nyingi, kuchagua software nzuri za kutumia kwenye mifumo ya shirika mfano kuchagua anti virus ipi itumike, kufanya back up ya mafaili, kuvitunza vifaa mfano kufungua hardware kwajili ya kufanya usafi wa ndani, kutengeneza vifaa vinavyosumbua kwa basic level ya ufundi aidha kwa kupiga window, kufungua hardware na kubadili kifaa cha ndani kilichoungua au chakavu, kufanya automatic trouble shooting, n.k.

Kama mnavyoona, vitu hivi hata kwa mtu anayejua matumizi ya kawaida ya kompyuta, vingi anakuwa anavijua tayari, akifika chuoni anakuwa unafanya maendelezo na si kuwa mgeni sana kama kozi nyingine ambazo utakutana na vipya vingi.

vitu mtavyofundishwa ambavyo vitakuwa advanced kiasi na ni muhimu kujifunza ni mambo ya database na networks, vitu hivi huenda bega kwa bega na ni muhimu katika mifumo ya tehama ya shirika kusaidia kupangilia data muhimu za shirika. Ni kama unavyoenda kwenye duka la dawa huwa kuna sehemu ya kuandikisha jina na dawa unayohitaji, sehemu ya kulipia na sehemu ya kuchukulia dawa na kupewa risiti, huu ni mfumo wa network na kuna data zinawekwa kwenye database zinazosaidia kutunza taarifa za mauzo ya kila siku, kujua dawa aina zipi zinauzwa sana, kujua dawa zimebaki kiasi gani kwenye stoo, n.k.

Kuhusu hesabu, Somo hili huchukua nafasi ndogo sana kwenye IT, zipo chache kuzidi kozi za computer science na computer engineering. ondoa hofu! watu wengi wenye ugonjwa wa hesabu za sekondari wakisoma IT huwa wanazipasua fresh maana hesabu ni chache mno kuzidi hata za sekondari. cha muhimu usidharau uchache wake, geuza iwe advantage kwako kwa kuzifanyia mazoezi, kuzi discuss kwenye groups, kufanya mazoezi ya past papers, n.k. ndio maana kozi hii vyuo vingi huwa wanahitaji D nne za masomo yoyote hata kama una F ya hesabu, kwenye kozi zingine huwa wamekazia pass moja angalau iwe ya hesabu. ( Kwepa vyuo vya technical kama kama MUST na Arusha Tech kwenye hii kozi kama una ugonjwa wa namba, hivi vyuo hata kwenye IT wameweka hesabu nyingi sana )

Programming level kwenye kozi hii sana sana ni zile basics / low level programming, itasaidia kwenye vitu kama kutumia compilers ama kutengeneza basic programs, kumbuka unasomea taaluma na huna haja ya kusomea vitu ambavyo vipo nje ya taaluma. pia niweke wazi kwamba programming ni kama mpira ambao inabidi baadhi ya vitu ujifunze mwenyewe, vingine ufundishwe, ufanye mazoezi, ucheze mpira uwanjani, uwe mzoefu, n.k.

Haijalishi hata ukisomea computer science, ukitegemea kufundishwa tu darasani hutaiva kwenye programming utaishia kukariri tu kwajili ya kujibia mtihani, watu wengi sana siku hizi wanajifunza wenyewe programming kama hobby (self taught programmer) na wapo vizuri kuliko hata wale waliosoea computer science / software development ambao kwao programming ilikuwa ni kama somo tu la kusomea darasani na kujibu kwenye mitihani ama kupata marks za project.

Pia kozi hii itakuandaa kuwa customer care / IT support katika shirika kwa kuhudumia wafanya kazi wengine wanapopata tatizo katika matumizi ya computer kwenye kufanikisha shughuli za shirika, Mtu anaweza kushindwa kujua sehemu ipi aminye ili ku print kazi basi atakuita umsaidie, mwengine waya wa mouse umechomoka na hajui wapi pa kupachika itabidi umsaidie, mwengine ku copy mafaili ni shughuli pevu itabidi umsaidie. hivyo inabidi kidogo ujue kutabasamu, kutumia lugha nzuri maana kuna muda unaitwa mara kwa mara kwa muda mrefu kumuelekeza mtu jinsi ya kufanya kitu flani lakini anasahau (hasa wazee), hivyo sura ya kuonesha unakerwa inabidi uifiche, kiburi uweke pemebeni na usichoke kuwasaidia maana ndiyo kazi inayokupa posho na mshahara wa kila mwezi.

Kozi hii ni nzuri sana kama tayari una ujuzi wa matumizi hata ya kawaida ya computer, pia kama hesabu zinakupiga chenga ila unapenda kozi za computer basi kozi hii ndio sehemu sahihi, ni kozi ambayo ina muda wa kupumzika wa kutosha unaoweza kuutumia kujiendeleza kujifunza skills za ziada.

🔷 AJIRA
System administrator, Database administrator, Network administrator, information systems manager, IT support, IT customer care, IT Project Manager, IT consultant, Database Developer, n. k

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za IT / ICT / IS.
Ubaya ni kwamba watu waliosomea kozi zingine kama computer science na computer engineering nao wana sifa za kuweza kuomba kazi nyingi za huku kwahio ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuwa exceptional angalau uwe na gpa nzuri.

4️⃣ SOFTWARE ENGINEERING / DEVELOPMENT
Ni Tawi / Kipengere cha computer science, Ni fani iliyojikita kwa undani na mapana zaidi na kuwekea umakini wote kwenye uwanja wa software development, kujua namna ya kutengeneza software professionally.

Tofauti na computer science ambako kuna mzigo mzito wa theories, huku kwa kuwa ni engineering basi utajikita zaidi kwenye kujifunza kuwa na skills za kukuwezesha kutengeneza software practically.

Kitu kikubwa mtachojifunza ni ku cover kwa undani na mapana software development life cycle, mtajiunza jinsi ya kupata idea ya software, kuichorea design au ramani, jinsi ya kuitengeneza (development), kuifanyia majaribio (testing), kuondoa errors (debugging), kuikagua kama imekidhi vigezo (requirements), kuiweka rasmi sokoni, kuifanyia updates, n.k.

Software zinavyotengenezwa huwa ni kama mradi ambao inabidi ukamilike kwa muda flani na uwe na vigezo flani, Kwahio miradi hii huwa inatekelezwa kwa kugawana majukumu kwenye vikundi / teams maana software kubwa ni ngumu sana kutengenezwa professionaly na mtu mmoja (hata vlc ina wafanyakazi zaidi ya 100), hivyo mtaandaliwa kuweza kutengeneza software kwenye teams ili kuwajengea uzoefu wa kufanya kazi kwa kushirikiana pamoja (co-op work experience).

Hesabu kama kawaida zipo zile za kozi mama ya computer science ambazo zinahusika na hili tawi.

🔷 AJIRA
software engineer, Mobile App Developer, Games developer, Front-End Engineers, Back-End Engineers, Full-Stack Engineer, DevOps Engineer

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za software engineering / development na computer science kwenye masomo yanayo deal na field hii.

Ni kozi nzuri lakini uwanja wake wa ajira hapa bongo ni mdogo, kama umepanga kujiajiri kuwa software developer ni sawa, ila kwa kuajiriwa hapa bongo kwa hii kozi ni changamoto japo kwa marekani na ulaya hii ni taaluma ambayo ina demand kubwa sana na mshahara mnono.

Kwa hapa bongo ni kozi nzuri ya kusomea baada ya kuhitimu degree ya Computer science, Computer Engineering au IT, ukiendelea na masters unaweza ku specialize kwenye mambo haya.

5️⃣ CYBER SECURITY
Ni Tawi lingine la computer science, Ni fani iliyojikita kwa undani na mapana zaidi na kuwekea umakini wote kwenye maswala ya ulinzi wa data, ulinzi wa mitandao, kulinda software, kuviwekea kinga vifaa, n.k. dhidi ya watu wasio na ruhusa kama vie wadukuzi / hackers.

kwa dunia ya sasa watu wengi wamehamia mifumo ya kidijitali katika kutunza picha na video za kumbukumbu, nyaraka muhimu, n.k. hackers wameanza kutengeneza virusi aina ya ransomware ambazo zinafungia mafaili (kidnapping) na wanakwambia kama unataka mafaili yako yafunguliwe inabidi uwalipe hela (ransom) ili uweze kuyakomboa mafaili yako, huwa wanapendelea kulipwa kwa njia ya biitcoins ili wasijulikane kirahisi, wapo watu wengi tu wameshalipia mpaka milioni waliposhambuliwa na hivi vitu ili kukomboa picha zao za familia, kumbukumbu muhimu, n.k. makampuni ndio usiseme yani washalipa mabilioni maana kampuni inakuwa na computer nyingi sana.

Vitu kama hivi ndivyo vinavyoleta umuhim mkubwa wa kuwa na wataalam wa mambo ya cyber security. hata pale panapotokea mashambulizi basi kuwe na mtu wa kututetea, mfano kwenye kwenye baadhi ya ransomware zinazofungia mafaili, watu wa cyber security wameweza kutengeneza mbinu za kufungua mafaili bila kuwalipa wadukuzi.

Mtajifunza vitu kama kutengeneza policies katika taasisi zitazolinda data zisivuje (mfano kubadili passwords pale mtumishi anapofukuzwa), panapotokea shambulizi kufanya uchunguzi wa kujaribu kujua chanzo na kujaribu trace wahusika, kutengeneza fire walls za system, kufanya advanced penetration testing kwa kujaribu kudukua mifumo ya tehama ya shirika ili kujua panapovuja kwa lengo la kuziba, n.k.

kozi hii pia inahusisha kuzijua mbinu za kudukua system za computer, networks, n.k. lengo ni kukufanya ujue kuutumia upanga ule ule unaotumika kufanyia uhalifu kuugeuza utumike kulinda, kuna masomo kama ethical hacking yatawafundisha kufanya mambo haya ila kwa nia njema ya kulinda kwa kuziba matundu.

Hesabu kama kawaida zipo zile za kozi mama ya computer science ambazo zinahusika na hili tawi.

🔷 AJIRA
Information security analyst, Security engineer, Security software developer (mfano anti-virus), Cyber intelligence specialist, IT security architect, Cybersecurity analyst, Cybersecurity engineer, Penetration tester, Security Auditor, Vulnerability Assessor, cryptographer, cyber security consultant, cyber security architect, cyber forensic officer, cyber crime investigator, network security engineer

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za software cyber security na computer science kwenye masomo yanayo deal na field hii.

Ni kozi nzuri lakini uwanja wake wa ajira hapa kwetu ni mdogo, kama umepanga kujiajiri, mfano kuwa independent Cyber intelligence specialist ni sawa, ila kwa kuajiriwa ni changamoto japo kwa marekani na ulaya hii ni taaluma ambayo ina demand kubwa sana na mshahara mnono.
Kwa hapa bongo ni kozi nzuri ya kusomea baada ya kuhitimu degree ya Computer science, Computer Engineering au IT, ukiendelea na masters unaweza ku specialize kwenye mambo haya.

USHAURI WA ZIADA:

🌀 Nakushauri uende chuoni mara tu umalizapo form 4, Nenda form 5 kama kuna changamoto za kiuchumi kulipia ada za chuoni ambazo ni takribani milioni 1 hadi milioni 1.3, umemaliza form 4 lakini bado hujui unataka kusomea taaluma gani, unataka kuja kusomea ualimu wa sekondari advance, bado unajihisi mdogo inabidi uwe chini ya uangalizi, n.k. (kuhusu mikopo ya degree si lazima kusomea form 6, hata wanaomaliza diploma wanapata), Ukimaliza Diploma unaingia degree ambayo utakutana na waliomaliza form 6.

Uzuri wa diploma ni kwamba unavyoingia degree, kwako haitakua mara yako ya kwanza maishani mwako kusomea elimu ya taaluma chuoni na vitu vingi ulivyosoma ukiwa diploma vitakuwa ni marudio kwako. Diploma ni kwamba unapitia NTA level 4, 5 unahitimu na 6. Unavyoingia degree unaendelea na NTA Level 7 unahitimu na 8. Hizo level zisikuchanganye ukafananisha na zile sekondari au shule ya msingi kudani kwamba kila level unaenda kukutana na vitu vipya, hapana!

Huku kwenye elimu za taaluma ni tofauti, vitu vingi utavyovikuta degree huwa tayari mmeshavisoma diploma, hata kwa wale wanaoenda masters huwa wanarudia vitu vingi ambavyo walishasoma degree, ni kama vile diploma ni kupika wali mnaenda degree kuongezea nazi kwenye wali. Si ajabu kumkuta mwalimu anaefundisha diploma kumkuta anafundisha degree kwa mtindo ule ule, kwa notes zile zile na style ile ile ya kutunga mitihani.

Diploma ukiimaliza una sifa ya kitaaluma ya kuajiriwa, kuna vijana wadogo tu wana miaka 20 wapo maofisini huku wakiendelea kujisomesha degree, ikifika jioni wanaenda evening classes kwenye vyuo vyenye kozi za jioni, wengine wanaenda open university wanapewa notes hawaingii darasani wanajisoomea wenyewe, chuoni wanaenda tu kufanya mitihani au kukusanya mazoezi.

🌀 Anza mapema kuizoea taaluma yako iwe kama mchezo ambao inabidi uufanyie mazoezi, ufunzwe, ujifunze, uucheze na uwe na mazoea nao, Hata kwenye kupika huwa inapendeza uwe mzoefu angalau kidogo ili hata ukienda chuoni kujifunza kupika uwe sio mgeni sana na iwe rahisi kwako ku catch up vitu tofauti na yule ambae hajawahi kupika. Kabla hujaenda cuoni unaweza kujifunza languages kama html na css kwenye basic level, hizi ni lugha nyepesi ambazo unaweza jifunza mtandaoni, kama mda upo jiongezee na javscript, c++ na python, n.k. yani ukifika chuoni kuna vitu unakuwa ahead tayari wewe unapukuta tu. inabidi ujiongeze uwe unajifunza vya ziada hata ukianza chuo ujitengee hata dakika 30 tu kila siku, kutegemea kwamba chuo ktakufanya uwe konki utasubiri sana ndio maana wapo wahitimu wana gpa kali (wakiwemo lecturers wanaofunisha vyuoni) lakini vitendo sifuri.

🌀 Kwenye kununua Laptop hakikisha unanua laptop ya “LENOVO THINKPAD” laptop hizi zimetengenezwa kwa sifa ya kuwa imara sana, kama una pesa za kubadilisha laptops vuta tu laptop yoyote utayoipenda ila kinyume na hapo tafuta lenovo thinkpad maana hakunaga kitu kinauzi kama kuanza kwenda kwa mafundi laptop, mara laptop iimechora mistari kwenye kioo, hujakaa sawa motherboard imeungua inabidi ununue mpya laki 3, n.k.. ukianza kufikiria bei ya laptop mpya hadi kichwa kinauma, chukua tahadhari mapema nunua mashine inayodumu.
 
Msidanganye watu kuwa mwanafunzi wa IT anasoma basic Maths na vitu vichache. Hasa kwenye Maths.
Nibishe nini sasa, kwa wengine hata hesabu za kawaida tu za kuzidisha huwa ni shughuli pevu.

Kuna kozi kama za uchungaji, mazingira, ualimu wa kiswahili, n.k. hazinaga hesabu kabisa na kazi zake zipo zenye vipato vizuri tu.
 
Madini mengi sana hii post nimeikuta fb nimeisoma na kuielewa sana, post hii naamini itakuwa msaada mkubwa sana.

Uchambuzi wa kina kuhusu utofauti wa IT, Computer science, Computer Engineering, Software engineering na Cyber security.

Post hii nimewandalia hususan wanafunzi waliomaliza sekondari wakitarajia kwenda vyuoni kusomea kozi za computer ila kwa sababu ya ugeni wa elimu ya chuoni pamoja na muda mfupi wa kufanya maamuzi, wanapata wakati mgumu wa kujua ni kozi ipi ya kuchagua itayowafaa.

Kukosea kuchagua kozi sahihi ni ajali kama ajali zingine … kukosea kuchagua kozi unaweza kukutana na vitu ndivyo sivyo ulivyodhania, kozi ukikosea kuichagua unaweza kumaliza chuo na hakuna ajira zake hapa bongo, kozi ukikosea kuchagua unaweza ukawa umeparamia vitu ambavyo vimekuzidi uwezo na kupelekea usome kwa kutumia nguvu kubwa sana hata kwenye vitu ambavyo ni basic, hii itafanya elimu yako chuoni iwe ya mateso makali kupelekea uwe unafanya mitihani ya marudio (ku supp) na endapo ukishindwa mitihani hii unajiongezea mzigo wa masomo ya ziada kwa kuanza upya kuyasoma darasa moja la wale uliowazidi darasa (ku carry masomo). mwisho wa siku unahitimu ukiwa na gpa ya ndogo sana na huwa inawekwa kwenye cheti ama utafukuzwa kabisa chuoni kwa kufeli kupita kiwango unarudi zako mtaani (tunaiita kudisco / kuwa disqualified), n.k. Kwa wale wanaojiandaa kwenda vyuoni ama hapo mbele wana plan za kuja kusomea vyuoni katika kozi za computer, post hii itakuwa ni muhimu kwako kujua ni kozi ipi sahihi itakufaa.

Kwanza kabisa kabla hatujaanza uchambuzi ni muhimu kuelewa tofauti ya Science na Engineering.

🟡 SCIENCE
Scientists study, wanasayansi husoma kitu kwa ndani ili kuelewa ufanyaji wake wa kazi, wanahitaji kuwa na uelewa mkubwa sana kuzijua behind the scenes zinazoendelea pale kitu kinapofanya kazi, kwa kiasi kikubwa sana kozi za science huwa zinafundishwa theoretically zaidi, vitu vingi wanajifunza kwa fundamentals kuvijua kwa undani, hata kama ni formula / theory / principle / law wataichimbua ndani zaidi kujua fundamentals zake, fundamentals hizi ni muhimu pia ili kuja kuwaandaa kuweza kuwa watafiti (researchers) na kuzitumia kufanya experiments, scientific findings zikipatikana zinafowadiwa kwa engineers ili wazitumie kwenye kazi zao.

🟢 ENGINEERING
Engineers create, Engineering hujikita kumuandaa mtu kuwa na skills za kujenga / kutengeneza vitu kwa kutumia misingi ya kisayansi, wanatumia principles, laws, formulas, n.k ambazo zilishafanyiwa utafiti na zikawa proved kufanya kazi, Hawana muda wa majaribio, Ukimpa mhandisi pesa ajenge kitu atatumia maarifa ambayo yameshakuwa proved yanafanya kazi, Kwa hio hata mafunzoni vitu kama formula huwa wanazitumia moja kwa moja kuliko kuanza kuzichumbua kwa ndani wa fundamentals.

Ok, nisiwachoshe sana, tuanze uchambuzi wa hizo kozi sasa, Najua wengi mnaweza kukimbilia chini haraka haraka kwenda kusoma maelezo ya kozi Ya Information Technology (IT), usiwe na haraka tafadhali!! Haraka haraka haina baraka!! tulia usome kwanza uchambuzi wa kozi za computer science na computer engineering ndio utaweza kuelewa vizuri zaidi maelezo niliyotumia kuichambua kozi ya IT.

1️⃣ COMPUTER SCIENCE
Hapa husomei computer, unasomea computing, zile process zinazofanyikaa nyuma ya pazia tunapotumia computer katika upande wa software, haihusu mambo ya hardware kama feni inayozunguka tunavyotumia pc, switch ya kuwasha pc, vioo vya smartphone, n.k. Utajifunza kuna kitu kipi nyuma ya pazia kinaendelea mpaka operating system kama windows / android / ios inafanya kazi, kinachofanyika mpaka game lichezeke kwenye playstation / simu, kinachofanya calculator itoe jibu sahihi, kitu gani kimefanyika mpaka tunaweza kufungua mafaili ya pdf, n.k

Process za computing zinazoendelea nyuma ya pazia ndizo zinawezesha computer iwe kifaa kamili tunachoweza kukitumia, computing huhusisha zaidi muunganiko wa Hesabu na Programming, hivyo computer science ni kama muungano wa programming na hesabu.

Kwenye hesabu zinazofanyika kwenye computer, nadhani neno “compute” si geni kwenye mitihani ya hesabu tuliyowahi kuifanya hata sekondari, kuna yale maswali unaambiwa compute x, basi nikueleze tu ya kwamba hata computer huwa zinachakata hesabu kwa mpangilio maalum kwenye kutafakari, kufanya maamuzi, kutoa majibu, n.k. huku mtajifunza hata hesabu za binary kwa jinsi namba 1 na 0 zinavyotumika kwenye computer, si kwa kuzijibu tu kwenye karatasi kwa usahihi bali kujua ni namna gani zinatumika kwenye computer system, computer science ni kama tawi la hesabu linalodeal na uchakataji wa hesabu kwenye computer, kwa hio hata somo la hesabu ni takribani nusu ya kozi ya computer science na mtazisoma kwa fundamentals kiundani maana hii ni kozi ya science.

Upande wa pili mtajifunza pia programming kwa kiwango cha juu, Programming ni zoezi la kutengeneza programs zinazoweza kutumika kwenye computer ili kufanya kazi flani au kutatua kitu flani, program hizi zinaweza kuwa operating systems kama windows / android / ios , apps za simu, games, Microsoft word, n.k.

kozi hii ipo theoretically sana ili kuzielewa fundamentals, kwenye programming nako ni kuzijua fundamentals kwa theory ila kuna unafuu kidogo wa practicles. vitu mtavyojifunza ni kama computational theories, data processing algorithms, data structures, advanced programming languages, AI, software engineering / development, security, n.k. Kwenye upande wa hesabu kuna Calculus, combinatorics, Discrete math, Numerical analysis, binary numbers, math for algorithms, computational geometry, linear algebra, probability theories. formal methods and models, statistics for scientists, n.k.

Fundamentals zitawezesha pia kujua namna pogramming languages zinavyotengenezwa kiasi kwamba mtaweza kujitengenezea hata programming language zenu.
hakikisha kwenye hesabu upo vizuri unapoingia kozi hii, itakupunguzia mzigo uelekeze nguvu zaidi kwenye masomo mengine na programming.

Kwa watao apply chuo chenye kozi mbili za Bachelor of science in computer scence na Bachelor of science with computer science, hakikisha unachagua yenye “IN”

🔷AJIRA
Mwenye taaluma hii ana sifa ya kufanya kazi nyingi za Information Technology, software engineering na cyber security, ajira zake za ziada ni kama Programmer, Data scientist, Cyber security analyst, Applications developer, Data analyst, Web designer, Web developer, Games developer, Artificial intelligence engineer, UX designer, Researcher (ukiwa na phd)

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za computer science, software engineering, cyber security, information technology.

2️⃣ COMPUTER ENGINEERING
Computer engineer ni ndoa kati ya vipengere vya computer science na electronics engineering vinavyomwezesha mtu kujua ubunifu wa hardware za computer. Ilianzishwa ikiwa kama tawi la electrical engineering (uhandisi wa umeme)

Hardware kivyake haiwezi kufanya kazi bila software, inahitaji program kama drivers ili kufanya kazi kwenye computer, kwa hio kwenye mambo kama haya kuna vitu kama programming vinachomolewa kwenye computer science, mfano mtajifunza programming languages za kawaida kama C++ kwenye kutengeneza drivers za kufanya spika itoe sauti ikiunganishwa kwenye computer, kutengeneza bios , firmware za hardware, simple operating sysytems, kuzifanyia programming micro processors, n.k. Programming languages za kufanikisha hivi vitu mnaweza kujifunza nyingi lakini mtajifunza low level programming hususan katika kiwango cha kuzifanya hardware ziweze ku interact na software. Kuna vitu vingine vya ziada pia mtamegua kwenye computer science.

Kwa kuwa computer ni kifaa cha umeme, mtajifunza pia mambo ya electronics engineering, kuijua mifumo ya umeme katika vifaa vya computer, circuits, conducors, resistors, inductors, kuzijua laws za umeme, n.k. Kwa maarifa haya si ajabu mhitimu kuwa fundi umeme, pia anaandaliwa vizuri kuja kuwa fundi wa laptops / simu upande wa hardware na software.

Kwenye hesabu pia huku zipo za kutosha tu, hesabu nyingi za computer science zipo katika hii kozi na pia kuna hesabu za ziada za electronics engineering.

Ni kozi ambayo ni pana sana na ina vitu vingi, utakutana na electronics, hesabu, programming, n.k … Ni vema uwe na uwezo wa kuhandle kusoma vitu vingi kwa mpigo lasivyo kozi itakuwa knock out.

Kozi hii ina added advantage ya kutambulika kuwa engineer, Mfano kama ulikuwa unaitwa Mr au Mrs Fulani utaanza kuwa addressed kwa salutation ya Eng. Fulani.

Kozi hii inahitaji practicles nyingi sana lakini kibongo bongo vyuoni utakuta hamfaidi vizuri, unakuta sehemu zinazohitaji practicles zinarukwa au zinageuzwa kuwa theory eti msome notes, ikitokea practicle ni mwalimu anaifanya yeye ama kuwaelekeza kwa mchoro au video ya youtube, mkifanya nyinyi basi ni kwa groups tena mara chache, seriously! Vitu hivi inabidi mwanafunzi ndio ajipimie awe anafanya mwenyewe tena kwa kurudia rudia, ajipimie mwenyewe mpaka aive, Kwa ushauri wangu, kwa baadhi ya practicles ikibidi wewe zama tu mfukoni, mfano nunua boards na components zako ufanye mwenyewe practicle za kuunda na kutengeneza motherboards kwa sequence inayofata logic, fanya mazoezi mara kwa mara mpaka uzoee (practice makes perfect).

🔷 AJIRA
Mwenye taaluma hii ana sifa ya kufanya kazi nyingi za Information Technology na computer science, ajira zake za ziada ni kama computer hardware engineer, electronics engineer, Electronics Design Engineer, Robotics Engineer, Micro electronics Engineer, Firmware Engineer, Digital Systems Engineer, fundi wa simu na laptops kote kote kwenye hardware na software.

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za computer engineering, computer science, information technology, electronics engineering.

3️⃣ INFORMATION TECHNOLOGY (IT)
Kozi nyingine mbadala ama zinazofanana ni Information systems na Information and communications technology (ICT)

Neno IT limejizolea umaarufu kimakosa kuwa msamiati mbadala wa ujuzi wa computer, Mitaani ama makazini tukimuona mtu ana ujuzi fulani wa computer kwa level hata ya kawaida basi watsaema “yule jamaa ni IT”, hata hizo kozi zingine za Tehama ukiachana na IT watu wamezoea kuziita kimakosa “kozi zingine za IT”, wengine hata hawajuagi kuna kozi zingine kama nilizozichambua wao wanadhani kuna kozi moja tu ya IT, any way wacha niichambue IT ili mjue maana halisi ya IT.

Tofauti na kozi zingine kama computer science inayo deal na software ama computer engineering iliyo deal na hardware, kozi ya IT imejikita kwenye “MATUMIZI” ya hardware na software katika ku assist uendeshaji wa shughuli za serikali, makampuni binafsi, mahospitali, mashirika, biashara, n.k.

IT imelenga kutoa huduma (service) ila kozi zingine zimelenga zaidi kutengeneza bidhaa za software na hardware, IT ni huduma ambayo ni kiunganishi / daraja kati ya pande mbili. Upande wa kwanza ni computer scientists na engineers wanaotengeneza software na hardware, upande wa pili ni mashirika, taasisi, biashara zinazotaka kutumia bidhaa hizo kwenye kufanya shughuli zake kidijitali, IT yeye anakuwa ni middle man kwa kutoa huduma ya kuwezesha walengwa kuweza kutumia mifumo ya computer katika utendaji kazi.

Main focus ni kujifunza namna ya kutumia, kusimamia na ku minain software na hardware katika kuhakikisha mifumo ya tehama katika shirika inafanya kazi kulingana na shughuli zake, Utajifunza namna ya ku install software sahihi kwajili ya kazi flani, ku update software, kuingiza operating systems ( almaarufu kupiga window), ku configure / kuseti hardware ifanye kitu flani, kuweka usalama kwa anti virus ama fire walls, kutengeneza data base, kusuka network mfano kuifanya printer moja itumike na computer nyingi, kuchagua software nzuri za kutumia kwenye mifumo ya shirika mfano kuchagua anti virus ipi itumike, kufanya back up ya mafaili, kuvitunza vifaa mfano kufungua hardware kwajili ya kufanya usafi wa ndani, kutengeneza vifaa vinavyosumbua kwa basic level ya ufundi aidha kwa kupiga window, kufungua hardware na kubadili kifaa cha ndani kilichoungua au chakavu, kufanya automatic trouble shooting, n.k.

Kama mnavyoona, vitu hivi hata kwa mtu anayejua matumizi ya kawaida ya kompyuta, vingi anakuwa anavijua tayari, akifika chuoni anakuwa unafanya maendelezo na si kuwa mgeni sana kama kozi nyingine ambazo utakutana na vipya vingi.

vitu mtavyofundishwa ambavyo vitakuwa advanced kiasi na ni muhimu kujifunza ni mambo ya database na networks, vitu hivi huenda bega kwa bega na ni muhimu katika mifumo ya tehama ya shirika kusaidia kupangilia data muhimu za shirika. Ni kama unavyoenda kwenye duka la dawa huwa kuna sehemu ya kuandikisha jina na dawa unayohitaji, sehemu ya kulipia na sehemu ya kuchukulia dawa na kupewa risiti, huu ni mfumo wa network na kuna data zinawekwa kwenye database zinazosaidia kutunza taarifa za mauzo ya kila siku, kujua dawa aina zipi zinauzwa sana, kujua dawa zimebaki kiasi gani kwenye stoo, n.k.

Kuhusu hesabu, zipo chache sana na ni zile basic za kawaida kabisa, ondoa shaka kuhusu ugumu, watu wana F za hesabu sekondari ila hesabu za huku wanapiga fresh tu. Hesabu zenyewe unakuta ni somo moja lenye topics chache tu, mkizisoma kwa muhula moja mnaachana nazo, cha muhimu na wewe utie juhudi kwenye kusoma, ku discuss kwenye groups, kufanya mazoezi ya past papers, n.k. ndio maana kozi hii vyuo vingi huwa wanahitaji D nne za masomo yoyote hata kama una F ya hesabu, kwenye kozi zingine huwa wamekazia pass moja angalau iwe ya hesabu maana hesabu zipo za kutosha.

Pia kozi hii itakuandaa kuwa customer care / IT support katika shirika kwa kuhudumia wafanya kazi wengine wanapopata tatizo katika matumizi ya computer kwenye kufanikisha shughuli za shirika, Mtu anaweza kushindwa kujua sehemu ipi aminye ili ku print kazi basi atakuita umsaidie, mwengine waya wa mouse umechomoka na hajui wapi pa kupachika itabidi umsaidie, mwengine ku copy mafaili ni shughuli pevu itabidi umsaidie. hivyo inabidi kidogo ujue kutabasamu, kutumia lugha nzuri maana kuna muda unaitwa mara kwa mara kwa muda mrefu kumuelekeza mtu jinsi ya kufanya kitu flani lakini anasahau (hasa wazee), hivyo sura ya kuonesha unakerwa inabidi uifiche, kiburi uweke pemebeni na usichoke kuwasaidia maana ndiyo kazi inayokupa posho na mshahara wa kila mwezi.

Kozi hii ni nzuri sana kama tayari una ujuzi wa matumizi hata ya kawaida ya computer, pia kama hesabu zinakupiga chenga ila unapenda kozi za computer basi kozi hii ndio sehemu sahihi, ni kozi ambayo ina muda wa kupumzika wa kutosha unaoweza kuutumia kujiendeleza kujifunza skills za ziada.

🔷 AJIRA
System administrator, Database administrator, Network administrator, information systems manager, IT support, IT customer care, IT Project Manager, IT consultant, Database Developer, n. k

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za IT / ICT / IS.
Ubaya ni kwamba watu waliosomea kozi zingine kama computer science na computer engineering nao wana sifa za kuweza kuomba kazi nyingi za huku kwahio ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuwa exceptional angalau uwe na gpa nzuri.

4️⃣ SOFTWARE ENGINEERING / DEVELOPMENT
Ni Tawi / Kipengere cha computer science, Ni fani iliyojikita kwa undani na mapana zaidi na kuwekea umakini wote kwenye uwanja wa software development, kujua namna ya kutengeneza software professionally.

Tofauti na computer science ambako kuna mzigo mzito wa theories, huku kwa kuwa ni engineering basi utajikita zaidi kwenye kujifunza kuwa na skills za kukuwezesha kutengeneza software practically.

Kitu kikubwa mtachojifunza ni ku cover kwa undani na mapana software development life cycle, mtajiunza jinsi ya kupata idea ya software, kuichorea design au ramani, jinsi ya kuitengeneza (development), kuifanyia majaribio (testing), kuondoa errors (debugging), kuikagua kama imekidhi vigezo (requirements), kuiweka rasmi sokoni, kuifanyia updates, n.k.

Software zinavyotengenezwa huwa ni kama mradi ambao inabidi ukamilike kwa muda flani na uwe na vigezo flani, Kwahio miradi hii huwa inatekelezwa kwa kugawana majukumu kwenye vikundi / teams maana software kubwa ni ngumu sana kutengenezwa professionaly na mtu mmoja (hata vlc ina wafanyakazi zaidi ya 100), hivyo mtaandaliwa kuweza kutengeneza software kwenye teams ili kuwajengea uzoefu wa kufanya kazi kwa kushirikiana pamoja (co-op work experience).

Hesabu kama kawaida zipo zile za kozi mama ya computer science ambazo zinahusika na hili tawi.

🔷 AJIRA
software engineer, Mobile App Developer, Games developer, Front-End Engineers, Back-End Engineers, Full-Stack Engineer, DevOps Engineer

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za software engineering / development na computer science kwenye masomo yanayo deal na field hii.

Ni kozi nzuri lakini uwanja wake wa ajira hapa bongo ni mdogo, kama umepanga kujiajiri kuwa software developer ni sawa, ila kwa kuajiriwa hapa bongo kwa hii kozi ni changamoto japo kwa marekani na ulaya hii ni taaluma ambayo ina demand kubwa sana na mshahara mnono.

Kwa hapa bongo ni kozi nzuri ya kusomea baada ya kuhitimu degree ya Computer science, Computer Engineering au IT, ukiendelea na masters unaweza ku specialize kwenye mambo haya.

5️⃣ CYBER SECURITY
Ni Tawi lingine la computer science, Ni fani iliyojikita kwa undani na mapana zaidi na kuwekea umakini wote kwenye maswala ya ulinzi wa data, ulinzi wa mitandao, kulinda software, kuviwekea kinga vifaa, n.k. dhidi ya watu wasio na ruhusa kama vie wadukuzi / hackers.

kwa dunia ya sasa watu wengi wamehamia mifumo ya kidijitali katika kutunza picha na video za kumbukumbu, nyaraka muhimu, n.k. hackers wameanza kutengeneza virusi aina ya ransomware ambazo zinafungia mafaili (kidnapping) na wanakwambia kama unataka mafaili yako yafunguliwe inabidi uwalipe hela (ransom) ili uweze kuyakomboa mafaili yako, huwa wanapendelea kulipwa kwa njia ya biitcoins ili wasijulikane kirahisi, wapo watu wengi tu wameshalipia mpaka milioni waliposhambuliwa na hivi vitu ili kukomboa picha zao za familia, kumbukumbu muhimu, n.k. makampuni ndio usiseme yani washalipa mabilioni maana kampuni inakuwa na computer nyingi sana. vitu kama hivi ndivyo vinavyoleta umuhim mkubwa wa kuwa na wataalam wa mambo ya cyber security. hata pale panapotokea mashambulizi basi kuwe na mtu wa kututetea, mfano kwenye kwenye baadhi ya ransomware zinazofungia mafaili, watu wa cyber security wameweza kutengeneza mbinu za kufungua mafaili bila kuwalipa wadukuzi.

Mtajifunza vitu kama kutengeneza policies katika taasisi zitazolinda data zisivuje (mfano kubadili passwords pale mtumishi anapofukuzwa), panapotokea shambulizi kufanya uchunguzi wa kujaribu kujua chanzo na kujaribu trace wahusika, kutengeneza fire walls za system, kufanya advanced penetration testing kwa kujaribu kudukua mifumo ya tehama ya shirika ili kujua panapovuja kwa lengo la kuziba, n.k.

kozi hii pia inahusisha kuzijua mbinu za kudukua system za computer, networks, n.k. lengo ni kukufanya ujue kuutumia upanga ule ule unaotumika kufanyia uhalifu kuugeuza utumike kulinda, kuna masomo kama ethical hacking yatawafundisha kufanya mambo haya ila kwa nia njema ya kulinda kwa kuziba matundu.

Hesabu kama kawaida zipo zile za kozi mama ya computer science ambazo zinahusika na hili tawi.

🔷 AJIRA
Information security analyst, Security engineer, Security software developer (mfano anti-virus), Cyber intelligence specialist, IT security architect, Cybersecurity analyst, Cybersecurity engineer, Penetration tester, Security Auditor, Vulnerability Assessor, cryptographer, cyber security consultant, cyber security architect, cyber forensic officer, cyber crime investigator, network security engineer

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za software cyber security na computer science kwenye masomo yanayo deal na field hii.

Ni kozi nzuri lakini uwanja wake wa ajira hapa kwetu ni mdogo, kama umepanga kujiajiri, mfano kuwa independent Cyber intelligence specialist ni sawa, ila kwa kuajiriwa ni changamoto japo kwa marekani na ulaya hii ni taaluma ambayo ina demand kubwa sana na mshahara mnono.
Kwa hapa bongo ni kozi nzuri ya kusomea baada ya kuhitimu degree ya Computer science, Computer Engineering au IT, ukiendelea na masters unaweza ku specialize kwenye mambo haya.

USHAURI WA ZIADA:
🌀 Nakushauri uende chuoni mara tu umalizapo form 4, Nenda form 5 kama kuna changamoto za kiuchumi kulipia ada za chuoni ambazo ni takribani milioni 1 hadi milioni 1.3, umemaliza form 4 lakini bado hujui unataka kusomea taaluma gani, unataka kuja kusomea ualimu wa sekondari advance, bado unajihisi mdogo inabidi uwe chini ya uangalizi, n.k. (kuhusu mikopo ya degree si lazima kusomea form 6, hata wanaomaliza diploma wanapata), Ukimaliza Diploma unaingia degree ambayo utakutana na waliomaliza form 6. Uzuri wa diploma ni kwamba unavyoingia degree, kwako haitakua mara yako ya kwanza maishani mwako kusomea elimu ya taaluma chuoni na vitu vingi ulivyosoma ukiwa diploma vitakuwa ni marudio kwako. Diploma ni kwamba unapitia NTA level 4, 5 unahitimu na 6. Unavyoingia degree unaendelea na NTA Level 7 unahitimu na 8. Hizo level zisikuchanganye ukafananisha na zile sekondari au shule ya msingi kudani kwamba kila level unaenda kukutana na vitu vipya, Hapana!! Huku kwenye elimu za taaluma ni tofauti, vitu vingi utavyovikuta degree huwa tayari mmeshavisoma diploma, hata kwa wale wanaoenda masters huwa wanarudia vitu vingi ambavyo walishasoma degree, ni kama vile diploma ni kupika wali mnaenda degree kuongezea nazi kwenye wali. Si ajabu kumkuta mwalimu anaefundisha diploma kumkuta anafundisha degree kwa mtindo ule ule, kwa notes zile zile na style ile ile ya kutunga mitihani. Diploma ukiimaliza una sifa ya kitaaluma ya kuajiriwa, kuna vijana wadogo tu wana miaka 20 wapo maofisini huku wakiendelea kujisomesha degree, ikifika jioni wanaenda evening classes kwenye vyuo vyenye kozi za jioni, wengine wanaenda open university wanapewa notes hawaingii darasani wanajisoomea wenyewe, chuoni wanaenda tu kufanya mitihani au kukusanya mazoezi.

🌀 Anza mapema kuizoea taaluma yako iwe kama mchezo ambao inabidi uufanyie mazoezi, ufunzwe, ujifunze, uucheze na uwe na mazoea nao, Hata kwenye kupika huwa inapendeza uwe mzoefu angalau kidogo ili hata ukienda chuoni kujifunza kupika uwe sio mgeni sana na iwe rahisi kwako ku catch up vitu tofauti na yule ambae hajawahi kupika. Kabla hujaenda cuoni unaweza kujifunza languages kama html na css kwenye basic level, hizi ni lugha nyepesi ambazo unaweza jifunza mtandaoni, kama mda upo jiongezee na javscript, c++ na python, n.k. yani ukifika chuoni kuna vitu unakuwa ahead tayari wewe unapukuta tu. inabidi ujiongeze uwe unajifunza vya ziada hata ukianza chuo ujitengee hata dakika 30 tu kila siku, kutegemea kwamba chuo ktakufanya uwe konki utasubiri sana ndio maana wapo wahitimu wana gpa kali (wakiwemo lecturers wanaofunisha vyuoni) lakini vitendo sifuri.

🌀 Kwenye kununua Laptop hakikisha unanua laptop ya “LENOVO THINKPAD” laptop hizi zimetengenezwa kwa sifa moja wapo ya kuwa imara sana, utatumia kwa muda mreefu, asiee hakunaga kitu kinauzi kama kuanza kwenda kwa mafundi laptop, pesa inaweza kukutoka acha tu, leo taizo hili, Kesho tatizo flani, siku nyingine tatizo linajirudia, n.k.
BONGE MOJA LA UZI, NIMEOKOTA KITU CHA KUJIFUNZA
 
Nibishe nini sasa, kwa wengine hata hesabu za kawaida tu za kuzidisha huwa ni shughuli pevu.

Kuna kozi kama za uchungaji, mazingira, ualimu wa kiswahili, n.k. hazinaga hesabu kabisa na kazi zake zipo zenye vipato vizuri tu.
Hesabu zote ulizo orodhesha kwa CS pia IT anasoma kama kawaida. Unawaaminisha watu sivyo hasa kwa wale wanafunzi wapya wakienda kusoma watakutana na kitu kizito. Labda ungefanya utafiti kujua kuwa vyuo kadhaa wanasoma basic Maths katika programu ya IT alafu orodhesha hapa.

Nimepinga kwa sababu mimi ni mdau na nimejionea hata hiyo binary number ni basic tu ya kujua namna mifumo ya kompyuta na mtandao inavyofanya kazi ambapo inasomwa level ya certificate kama basic, diploma anaisoma kwa undani kidogo na kwa undani zaidi ukifika bachelor's degree ili kujua kazi zake.

Utasoma na mambo mengine mengi hivyo ulivyovitaja hapo havifiki hata asilimia 5% kwa NTA level 8, na 20% kwa NTA level 6.
 
Nadhani wewe hata hujasoma hio post umekimbilia ku comeent.

Ni chuo kipi hicho ambacho IT wanasomea Hesabu kama za Computer science, get your facts straight mkuu...

Computer science ni lazima ujue vitu kama Calculus, Discrete math, Math for algorithsms, n.k ili ujue compueter inavyozitumia hesabu hizi katika ufanyaji wake wa kazi.

IT hahitaji kujua mambo ya computing na vinavyoendelea nyuma ya pazia, Mambo ya kujua hizo fundamentals za computing yeye hayamuhusu, sasa aanze kujifunza hizo hesabu za computer science kwa lengo lipi ?

IT wengi wanasomea basic math za kawaida kabisa, wala usiwatishe.

Ila hatuwezi jua aisee, huenda kwako hata hesabu za darasa la 7 zinakutoa jasho ndio maana unaona hata basic math ni ngumu.
 
Una tatizo la kuandika bila kufanya utafiti, rejea chapisho lako la awali umekua ukijitahidi kueleza pasipo kuwa na uhakika nilikuelewesha lakini ukapotezea na nimekupa ushahidi lakini unataka kusimama na kile unachoamini pasipo kutaka kukosolewa kwa mifano hai.

Sasa kweli mhitimu wa shahada ya tehama nishindwe na hisabati! Kweli! Mpaka hapo umeonesha una upendeleo. Ila kikubwa nimetaka nikusahihishe kwa kukupa mifano hai ambayo inaweza kukusaidia na kuwasaidia wengine pia sipo kwa ajili ya kubishana.

Ukiwa tayari kuelimika nijuze lakini sipo kwa tayari kwa vijembe visivyokuwa na maana. Na hili ni tatizo kwa wasomi wengi hasa wa kiafrika hatupendi kukosolewa.

Kupitia machapisho yako ulipaswa utoe fursa kwa wengine kuendeleza mawazo kulingana na kile kinachofanyika kwenye tasnia ya tehama na sio kuhitimisha kwa mawazo yako pekee. teknolojia ya kompyuta ni pana kuliko unavyodhani.
 
Post in thread 'Upembuzi yakinifu kuhusu utofauti wa kozi za Computer engineering, computer science na Information Technology / Systems kwa kuzingatia mazingira ya TZ' Upembuzi yakinifu kuhusu utofauti wa kozi za Computer engineering, computer science na Information Technology / Systems kwa kuzingatia mazingira ya TZ

REJEA HAPA
 
BACHELOR OF INFORMATION TECHNOLOGY

BACHELOR OF COMPUTER SCIENCE

HIZO HAPO JUU NI PROGRAMU ZA IT & CS ZINAFUNDISHWA NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

TAFADHALI REJEA MASOMO YAKE ILI UWEZE KUELIMIKA ZAIDI.
 
Uchambuzi wa kina kuhusu utofauti wa IT, Computer science, Computer Engineering, Software engineering na Cyber security.

Post hii nimewandalia hususan wanafunzi waliomaliza sekondari wakitarajia kwenda vyuoni kusomea kozi za computer ila kwa sababu ya ugeni wa elimu ya chuoni pamoja na muda mfupi wa kufanya maamuzi, wanapata wakati mgumu wa kujua ni kozi ipi ya kuchagua itayowafaa.

Kukosea kuchagua kozi sahihi ni ajali kama ajali zingine … kukosea kuchagua kozi unaweza kukutana na vitu ndivyo sivyo ulivyodhania, kozi ukikosea kuichagua unaweza kumaliza chuo na hakuna ajira zake hapa bongo, kozi ukikosea kuchagua unaweza ukawa umeparamia vitu ambavyo vimekuzidi uwezo na kupelekea usome kwa kutumia nguvu kubwa sana hata kwenye vitu ambavyo ni basic, hii itafanya elimu yako chuoni iwe ya mateso makali kupelekea uwe unafanya mitihani ya marudio (ku supp) na endapo ukishindwa mitihani hii unajiongezea mzigo wa masomo ya ziada kwa kuanza upya kuyasoma darasa moja la wale uliowazidi darasa (ku carry masomo). mwisho wa siku unahitimu ukiwa na gpa ya ndogo sana na huwa inawekwa kwenye cheti ama utafukuzwa kabisa chuoni kwa kufeli kupita kiwango unarudi zako mtaani (tunaiita kudisco / kuwa disqualified), n.k. Kwa wale wanaojiandaa kwenda vyuoni ama hapo mbele wana plan za kuja kusomea vyuoni katika kozi za computer, post hii itakuwa ni muhimu kwako kujua ni kozi ipi sahihi itakufaa.

Kwanza kabisa kabla hatujaanza uchambuzi ni muhimu kuelewa tofauti ya Science na Engineering.

🟡 SCIENCE
Scientists study, wanasayansi husoma kitu kwa ndani ili kuelewa ufanyaji wake wa kazi, wanahitaji kuwa na uelewa mkubwa sana kuzijua behind the scenes zinazoendelea pale kitu kinapofanya kazi, kwa kiasi kikubwa sana kozi za science huwa zinafundishwa theoretically zaidi, vitu vingi wanajifunza kwa fundamentals kuvijua kwa undani, hata kama ni formula / theory / principle / law wataichimbua ndani zaidi kujua fundamentals zake, fundamentals hizi ni muhimu pia ili kuja kuwaandaa kuweza kuwa watafiti (researchers) na kuzitumia kufanya experiments, scientific findings zikipatikana zinafowadiwa kwa engineers ili wazitumie kwenye kazi zao.

🟢 ENGINEERING
Engineers create, Engineering hujikita kumuandaa mtu kuwa na skills za kujenga / kutengeneza vitu kwa kutumia misingi ya kisayansi, wanatumia principles, laws, formulas, n.k ambazo zilishafanyiwa utafiti na zikawa proved kufanya kazi, Hawana muda wa majaribio, Ukimpa mhandisi pesa ajenge kitu atatumia maarifa ambayo yameshakuwa proved yanafanya kazi, Kwa hio hata mafunzoni vitu kama formula huwa wanazitumia moja kwa moja kuliko kuanza kuzichumbua kwa ndani wa fundamentals.

Ok, nisiwachoshe sana, tuanze uchambuzi wa hizo kozi sasa, Najua wengi mnaweza kukimbilia chini haraka haraka kwenda kusoma maelezo ya kozi Ya Information Technology (IT), usiwe na haraka tafadhali!! Haraka haraka haina baraka!! tulia usome kwanza uchambuzi wa kozi za computer science na computer engineering ndio utaweza kuelewa vizuri zaidi maelezo niliyotumia kuichambua kozi ya IT.

1️⃣ COMPUTER SCIENCE

Hapa husomei computer, unasomea computing, zile process zinazofanyikaa nyuma ya pazia tunapotumia computer katika upande wa software, haihusu mambo ya hardware kama feni inayozunguka tunavyotumia pc, switch ya kuwasha pc, vioo vya smartphone, n.k. Utajifunza kuna kitu kipi nyuma ya pazia kinaendelea mpaka operating system kama windows / android / ios inafanya kazi, kinachofanyika mpaka game lichezeke kwenye playstation / simu, kinachofanya calculator itoe jibu sahihi, kitu gani kimefanyika mpaka tunaweza kufungua mafaili ya pdf, n.k

Process za computing zinazoendelea nyuma ya pazia ndizo zinawezesha computer iwe kifaa kamili tunachoweza kukitumia, computing huhusisha zaidi muunganiko wa Hesabu na Programming, hivyo computer science ni kama muungano wa programming na hesabu.

Kwenye hesabu zinazofanyika kwenye computer, nadhani neno “compute” si geni kwenye mitihani ya hesabu tuliyowahi kuifanya hata sekondari, kuna yale maswali unaambiwa compute x, basi nikueleze tu ya kwamba hata computer huwa zinachakata hesabu kwa mpangilio maalum kwenye kutafakari, kufanya maamuzi, kutoa majibu, n.k. huku mtajifunza hata hesabu za binary kwa jinsi namba 1 na 0 zinavyotumika kwenye computer, si kwa kuzijibu tu kwenye karatasi kwa usahihi bali kujua ni namna gani zinatumika kwenye computer system, computer science ni kama tawi la hesabu linalodeal na uchakataji wa hesabu kwenye computer, kwa hio hata somo la hesabu ni takribani nusu ya kozi ya computer science na mtazisoma kwa fundamentals kiundani maana hii ni kozi ya science.

Upande wa pili mtajifunza pia programming kwa kiwango cha juu, Programming ni zoezi la kutengeneza programs zinazoweza kutumika kwenye computer ili kufanya kazi flani au kutatua kitu flani, program hizi zinaweza kuwa operating systems kama windows / android / ios , apps za simu, games, Microsoft word, n.k.

kozi hii ipo theoretically sana ili kuzielewa fundamentals, kwenye programming nako ni kuzijua fundamentals kwa theory ila kuna unafuu kidogo wa practicles. vitu mtavyojifunza ni kama computational theories, data processing algorithms, data structures, advanced programming languages, AI, software engineering / development, security, n.k. Kwenye upande wa hesabu kuna Calculus, combinatorics, Discrete math, Numerical analysis, binary numbers, math for algorithms, computational geometry, linear algebra, probability theories. formal methods and models, statistics for scientists, n.k.

Fundamentals zitawezesha pia kujua namna pogramming languages zinavyotengenezwa kiasi kwamba mtaweza kujitengenezea hata programming language zenu.
hakikisha kwenye hesabu upo vizuri unapoingia kozi hii, itakupunguzia mzigo uelekeze nguvu zaidi kwenye masomo mengine na programming.

Kwa watao apply chuo chenye kozi mbili za Bachelor of science in computer scence na Bachelor of science with computer science, hakikisha unachagua yenye “IN”

🔷AJIRA

Mwenye taaluma hii ana sifa ya kufanya kazi nyingi za Information Technology, software engineering na cyber security.

ajira zake za ziada ni kama Programmer, Data scientist, Cyber security analyst, Applications developer, Data analyst, Web designer, Web developer, Games developer, Artificial intelligence engineer, UX designer, Researcher (ukiwa na phd).

Kwa hapa nchini kwetu wengi huishia kufanya kazi za Information Technology maana hizo ajira nyingine ni changamoto kuzikuta hapa nchini.

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za computer science, software engineering, cyber security, information technology.

2️⃣ COMPUTER ENGINEERING

Computer engineer ni ndoa kati ya vipengere vya computer science na electronics engineering vinavyomwezesha mtu kujua ubunifu wa hardware za computer. Ilianzishwa ikiwa kama tawi la electrical engineering (uhandisi wa umeme)

Hardware kivyake haiwezi kufanya kazi bila software, inahitaji program kama drivers ili kufanya kazi kwenye computer, kwa hio kwenye mambo kama haya kuna vitu kama programming vinachomolewa kwenye computer science, mfano mtajifunza programming languages za kawaida kama C++ kwenye kutengeneza drivers za kufanya spika itoe sauti ikiunganishwa kwenye computer, kutengeneza bios , firmware za hardware, simple operating sysytems, kuzifanyia programming micro processors, n.k. Programming languages za kufanikisha hivi vitu mnaweza kujifunza nyingi lakini mtajifunza low level programming hususan katika kiwango cha kuzifanya hardware ziweze ku interact na software. Kuna vitu vingine vya ziada pia mtamegua kwenye computer science.

Kwa kuwa computer ni kifaa cha umeme, mtajifunza pia mambo ya electronics engineering, kuijua mifumo ya umeme katika vifaa vya computer, circuits, conducors, resistors, inductors, kuzijua laws za umeme, n.k. Kwa maarifa haya si ajabu mhitimu kuwa fundi umeme, pia anaandaliwa vizuri kuja kuwa fundi wa laptops / simu upande wa hardware na software.

Kwenye hesabu pia huku zipo za kutosha tu, hesabu nyingi za computer science zipo katika hii kozi na pia kuna hesabu za ziada za electronics engineering.

Ni kozi ambayo ni pana sana na ina vitu vingi, utakutana na electronics, hesabu, programming, n.k … Ni vema uwe na uwezo wa kuhandle kusoma vitu vingi kwa mpigo lasivyo kozi itakuwa knock out.

Kozi hii ina added advantage ya kutambulika kuwa engineer, Mfano kama ulikuwa unaitwa Mr au Mrs Fulani utaanza kuwa addressed kwa salutation ya Eng. Fulani.

Kozi hii inahitaji practicles nyingi sana lakini kibongo bongo vyuoni utakuta hamfaidi vizuri, unakuta sehemu zinazohitaji practicles zinarukwa au zinageuzwa kuwa theory eti msome notes, ikitokea practicle ni mwalimu anaifanya yeye ama kuwaelekeza kwa mchoro au video ya youtube, mkifanya nyinyi basi ni kwa groups tena mara chache, seriously! Vitu hivi inabidi mwanafunzi ndio ajipimie awe anafanya mwenyewe tena kwa kurudia rudia, ajipimie mwenyewe mpaka aive, Kwa ushauri wangu, kwa baadhi ya practicles ikibidi wewe zama tu mfukoni, mfano nunua boards na components zako ufanye mwenyewe practicle za kuunda na kutengeneza motherboards kwa sequence inayofata logic, fanya mazoezi mara kwa mara mpaka uzoee (practice makes perfect).

🔷 AJIRA
Mwenye taaluma hii ana sifa ya kufanya kazi nyingi za Information Technology na computer science.

ajira zake za ziada ni kama computer hardware engineer, electronics engineer, Electronics Design Engineer, Robotics Engineer, Micro electronics Engineer, Firmware Engineer, Digital Systems Engineer, fundi wa simu na laptops kote kote kwenye hardware na software.

Tofauti na computer science ambako ajira nyingi wanafanya za Information Technology kwa hapa Tz, Hawa angalau huwa kuna kazi zao zinazohitaji watu waliosomea computer engineering.

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za computer engineering, computer science, information technology, electronics engineering.

3️⃣ INFORMATION TECHNOLOGY (IT)

Kozi nyingine mbadala ama zinazofanana ni Information systems na Information and communications technology (ICT)

Neno IT limejizolea umaarufu kimakosa kuwa msamiati mbadala wa ujuzi wa computer, Mitaani ama makazini tukimuona mtu ana ujuzi flani wa computer kwa level hata ya kawaida basi watsaema “yule jamaa ni IT”, hata hizo kozi zingine za Tehama ukiachana na IT watu wamezoea kuziita kimakosa “kozi zingine za IT”, wengine hata hawajuagi kuna kozi zingine kama nilizozichambua wao wanadhani kuna kozi moja tu ya IT, any way wacha niichambue IT ili mjue maana halisi ya IT.

Tofauti na kozi zingine kama computer science inayo deal na software ama computer engineering iliyo deal na hardware, kozi ya IT imejikita kwenye “MATUMIZI” ya hardware na software katika ku assist uendeshaji wa shughuli za serikali, makampuni binafsi, mahospitali, mashirika, biashara, n.k.

IT imelenga kutoa huduma (service) ila kozi zingine zimelenga zaidi kutengeneza bidhaa za software na hardware, IT ni huduma ambayo ni kiunganishi / daraja kati ya pande mbili. Upande wa kwanza ni computer scientists na engineers wanaotengeneza software na hardware, upande wa pili ni mashirika, taasisi, biashara zinazotaka kutumia bidhaa hizo kwenye kufanya shughuli zake kidijitali, IT yeye anakuwa ni middle man kwa kutoa huduma ya kuwezesha walengwa kuweza kutumia mifumo ya computer katika utendaji kazi.

Main focus ni kujifunza namna ya kutumia, kusimamia na ku minain software na hardware katika kuhakikisha mifumo ya tehama katika shirika inafanya kazi kulingana na shughuli zake, Utajifunza namna ya ku install software sahihi kwajili ya kazi flani, ku update software, kuingiza operating systems ( almaarufu kupiga window), ku configure / kuseti hardware ifanye kitu flani, kuweka usalama kwa anti virus ama fire walls, kutengeneza data base, kusuka network mfano kuifanya printer moja itumike na computer nyingi, kuchagua software nzuri za kutumia kwenye mifumo ya shirika mfano kuchagua anti virus ipi itumike, kufanya back up ya mafaili, kuvitunza vifaa mfano kufungua hardware kwajili ya kufanya usafi wa ndani, kutengeneza vifaa vinavyosumbua kwa basic level ya ufundi aidha kwa kupiga window, kufungua hardware na kubadili kifaa cha ndani kilichoungua au chakavu, kufanya automatic trouble shooting, n.k.

Kama mnavyoona, vitu hivi hata kwa mtu anayejua matumizi ya kawaida ya kompyuta, vingi anakuwa anavijua tayari, akifika chuoni anakuwa unafanya maendelezo na si kuwa mgeni sana kama kozi nyingine ambazo utakutana na vipya vingi.

vitu mtavyofundishwa ambavyo vitakuwa advanced kiasi na ni muhimu kujifunza ni mambo ya database na networks, vitu hivi huenda bega kwa bega na ni muhimu katika mifumo ya tehama ya shirika kusaidia kupangilia data muhimu za shirika. Ni kama unavyoenda kwenye duka la dawa huwa kuna sehemu ya kuandikisha jina na dawa unayohitaji, sehemu ya kulipia na sehemu ya kuchukulia dawa na kupewa risiti, huu ni mfumo wa network na kuna data zinawekwa kwenye database zinazosaidia kutunza taarifa za mauzo ya kila siku, kujua dawa aina zipi zinauzwa sana, kujua dawa zimebaki kiasi gani kwenye stoo, n.k.

Kuhusu hesabu, zipo chache sana na ni zile basic za kawaida kabisa, ondoa shaka kuhusu ugumu, watu wana F za hesabu sekondari ila hesabu za huku wanapiga fresh tu. Hesabu zenyewe unakuta ni somo moja lenye topics chache tu, mkizisoma kwa muhula moja mnaachana nazo, cha muhimu na wewe utie juhudi kwenye kusoma, ku discuss kwenye groups, kufanya mazoezi ya past papers, n.k. ndio maana kozi hii vyuo vingi huwa wanahitaji D nne za masomo yoyote hata kama una F ya hesabu, kwenye kozi zingine huwa wamekazia pass moja angalau iwe ya hesabu maana hesabu zipo za kutosha.

Pia kozi hii itakuandaa kuwa customer care / IT support katika shirika kwa kuhudumia wafanya kazi wengine wanapopata tatizo katika matumizi ya computer kwenye kufanikisha shughuli za shirika, Mtu anaweza kushindwa kujua sehemu ipi aminye ili ku print kazi basi atakuita umsaidie, mwengine waya wa mouse umechomoka na hajui wapi pa kupachika itabidi umsaidie, mwengine ku copy mafaili ni shughuli pevu itabidi umsaidie. hivyo inabidi kidogo ujue kutabasamu, kutumia lugha nzuri maana kuna muda unaitwa mara kwa mara kwa muda mrefu kumuelekeza mtu jinsi ya kufanya kitu flani lakini anasahau (hasa wazee), hivyo sura ya kuonesha unakerwa inabidi uifiche, kiburi uweke pemebeni na usichoke kuwasaidia maana ndiyo kazi inayokupa posho na mshahara wa kila mwezi.

Kozi hii ni nzuri sana kama tayari una ujuzi wa matumizi hata ya kawaida ya computer, pia kama hesabu zinakupiga chenga ila unapenda kozi za computer basi kozi hii ndio sehemu sahihi, ni kozi ambayo ina muda wa kupumzika wa kutosha unaoweza kuutumia kujiendeleza kujifunza skills za ziada.

🔷 AJIRA
System administrator, Database administrator, Network administrator, information systems manager, IT support, IT customer care, IT Project Manager, IT consultant, Database Developer, n. k

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za IT / ICT / IS.
Kama nilivyoelezea awali, watu waliosomea kozi zingine kama computer science na computer engineering nao wana sifa za kuweza kuomba kazi nyingi za IT hasa computer science ambao kazi zao ni nadra nchini kwetu, Kama una uwezo wa kusomea IT nakushauri ukae huku huku tu, usije kulazimisha kusomea cmputer science kwa kudhani kwamba ndio utakuwa na wigo mpana wa ajira, Kwa hapa bongo ajira nyingi za kozi za computer huwa wanahitaji wenye IT na Computer science, kukuta ajira inahitaji computer science pekee labda zipo ila binafsi sijawahi kuona, Ila kuna ajira ambazo huwa zinahitaji computer engineering. Kwahio nachoweza kusema nenda computer science kama unaiweza na hesabu zinapanda ila usiweke malengo ya kudhani kwamba utakuwa na uwanja mpana wa ajira kama ilivyo huko Marekani, lasivyo utalazimisha kusomea hio computer science na ikakuburuza ukawa na gpa mbovu wakati ni bora tu hata ungesomea IT.

4️⃣ SOFTWARE ENGINEERING / DEVELOPMENT
Ni Tawi / Kipengere cha computer science, Ni fani iliyojikita kwa undani na mapana zaidi na kuwekea umakini wote kwenye uwanja wa software development, kujua namna ya kutengeneza software professionally.

Tofauti na computer science ambako kuna mzigo mzito wa theories, huku kwa kuwa ni engineering basi utajikita zaidi kwenye kujifunza kuwa na skills za kukuwezesha kutengeneza software practically.

Kitu kikubwa mtachojifunza ni ku cover kwa undani na mapana software development life cycle, mtajiunza jinsi ya kupata idea ya software, kuichorea design au ramani, jinsi ya kuitengeneza (development), kuifanyia majaribio (testing), kuondoa errors (debugging), kuikagua kama imekidhi vigezo (requirements), kuiweka rasmi sokoni, kuifanyia updates, n.k.

Software zinavyotengenezwa huwa ni kama mradi ambao inabidi ukamilike kwa muda flani na uwe na vigezo flani, Kwahio miradi hii huwa inatekelezwa kwa kugawana majukumu kwenye vikundi / teams maana software kubwa ni ngumu sana kutengenezwa professionaly na mtu mmoja (hata vlc ina wafanyakazi zaidi ya 100), hivyo mtaandaliwa kuweza kutengeneza software kwenye teams ili kuwajengea uzoefu wa kufanya kazi kwa kushirikiana pamoja (co-op work experience).

Hesabu kama kawaida zipo zile za kozi mama ya computer science ambazo zinahusika na hili tawi.

🔷 AJIRA
software engineer, Mobile App Developer, Games developer, Front-End Engineers, Back-End Engineers, Full-Stack Engineer, DevOps Engineer

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za software engineering / development na computer science kwenye masomo yanayo deal na field hii.

Ni kozi nzuri lakini uwanja wake wa ajira hapa bongo ni mdogo, kama umepanga kujiajiri kuwa software developer ni sawa, ila kwa kuajiriwa hapa bongo kwa hii kozi ni changamoto japo kwa marekani na ulaya hii ni taaluma ambayo ina demand kubwa sana na mshahara mnono.

Kwa hapa bongo ni kozi nzuri ya kusomea baada ya kuhitimu degree ya Computer science, Computer Engineering au IT, ukiendelea na masters unaweza ku specialize kwenye mambo haya.

5️⃣ CYBER SECURITY
Ni Tawi lingine la computer science, Ni fani iliyojikita kwa undani na mapana zaidi na kuwekea umakini wote kwenye maswala ya ulinzi wa data, ulinzi wa mitandao, kulinda software, kuviwekea kinga vifaa, n.k. dhidi ya watu wasio na ruhusa kama vie wadukuzi / hackers.

kwa dunia ya sasa watu wengi wamehamia mifumo ya kidijitali katika kutunza picha na video za kumbukumbu, nyaraka muhimu, n.k. hackers wameanza kutengeneza virusi aina ya ransomware ambazo zinafungia mafaili (kidnapping) na wanakwambia kama unataka mafaili yako yafunguliwe inabidi uwalipe hela (ransom) ili uweze kuyakomboa mafaili yako, huwa wanapendelea kulipwa kwa njia ya biitcoins ili wasijulikane kirahisi, wapo watu wengi tu wameshalipia mpaka milioni waliposhambuliwa na hivi vitu ili kukomboa picha zao za familia, kumbukumbu muhimu, n.k. makampuni ndio usiseme yani washalipa mabilioni maana kampuni inakuwa na computer nyingi sana. vitu kama hivi ndivyo vinavyoleta umuhim mkubwa wa kuwa na wataalam wa mambo ya cyber security. hata pale panapotokea mashambulizi basi kuwe na mtu wa kututetea, mfano kwenye kwenye baadhi ya ransomware zinazofungia mafaili, watu wa cyber security wameweza kutengeneza mbinu za kufungua mafaili bila kuwalipa wadukuzi.

Mtajifunza vitu kama kutengeneza policies katika taasisi zitazolinda data zisivuje (mfano kubadili passwords pale mtumishi anapofukuzwa), panapotokea shambulizi kufanya uchunguzi wa kujaribu kujua chanzo na kujaribu trace wahusika, kutengeneza fire walls za system, kufanya advanced penetration testing kwa kujaribu kudukua mifumo ya tehama ya shirika ili kujua panapovuja kwa lengo la kuziba, n.k.

kozi hii pia inahusisha kuzijua mbinu za kudukua system za computer, networks, n.k. lengo ni kukufanya ujue kuutumia upanga ule ule unaotumika kufanyia uhalifu kuugeuza utumike kulinda, kuna masomo kama ethical hacking yatawafundisha kufanya mambo haya ila kwa nia njema ya kulinda kwa kuziba matundu.

Hesabu kama kawaida zipo zile za kozi mama ya computer science ambazo zinahusika na hili tawi.

🔷 AJIRA
Information security analyst, Security engineer, Security software developer (mfano anti-virus), Cyber intelligence specialist, IT security architect, Cybersecurity analyst, Cybersecurity engineer, Penetration tester, Security Auditor, Vulnerability Assessor, cryptographer, cyber security consultant, cyber security architect, cyber forensic officer, cyber crime investigator, network security engineer

ukiwa na gpa safi unaweza kuwa lecturer wa kozi za software cyber security na computer science kwenye masomo yanayo deal na field hii.

Ni kozi nzuri lakini uwanja wake wa ajira hapa kwetu ni mdogo, kama umepanga kujiajiri, mfano kuwa independent Cyber intelligence specialist ni sawa, ila kwa kuajiriwa ni changamoto japo kwa marekani na ulaya hii ni taaluma ambayo ina demand kubwa sana na mshahara mnono.
Kwa hapa bongo ni kozi nzuri ya kusomea baada ya kuhitimu degree ya Computer science, Computer Engineering au IT, ukiendelea na masters unaweza ku specialize kwenye mambo haya.

USHAURI WA ZIADA:

🌀 Nakushauri uende chuoni mara tu umalizapo form 4, Nenda form 5 kama kuna changamoto za kiuchumi kulipia ada za chuoni ambazo ni takribani milioni 1 hadi milioni 1.3, umemaliza form 4 lakini bado hujui unataka kusomea taaluma gani, unataka kuja kusomea ualimu wa sekondari advance, bado unajihisi mdogo inabidi uwe chini ya uangalizi, n.k. (kuhusu mikopo ya degree si lazima kusomea form 6, hata wanaomaliza diploma wanapata), Ukimaliza Diploma unaingia degree ambayo utakutana na waliomaliza form 6. Uzuri wa diploma ni kwamba unavyoingia degree, kwako haitakua mara yako ya kwanza maishani mwako kusomea elimu ya taaluma chuoni na vitu vingi ulivyosoma ukiwa diploma vitakuwa ni marudio kwako. Diploma ni kwamba unapitia NTA level 4, 5 unahitimu na 6. Unavyoingia degree unaendelea na NTA Level 7 unahitimu na 8. Hizo level zisikuchanganye ukafananisha na zile sekondari au shule ya msingi kudani kwamba kila level unaenda kukutana na vitu vipya, Hapana!! Huku kwenye elimu za taaluma ni tofauti, vitu vingi utavyovikuta degree huwa tayari mmeshavisoma diploma, hata kwa wale wanaoenda masters huwa wanarudia vitu vingi ambavyo walishasoma degree, ni kama vile diploma ni kupika wali mnaenda degree kuongezea nazi kwenye wali. Si ajabu kumkuta mwalimu anaefundisha diploma kumkuta anafundisha degree kwa mtindo ule ule, kwa notes zile zile na style ile ile ya kutunga mitihani. Diploma ukiimaliza una sifa ya kitaaluma ya kuajiriwa, kuna vijana wadogo tu wana miaka 20 wapo maofisini huku wakiendelea kujisomesha degree, ikifika jioni wanaenda evening classes kwenye vyuo vyenye kozi za jioni, wengine wanaenda open university wanapewa notes hawaingii darasani wanajisoomea wenyewe, chuoni wanaenda tu kufanya mitihani au kukusanya mazoezi.

🌀 Anza mapema kuizoea taaluma yako iwe kama mchezo ambao inabidi uufanyie mazoezi, ufunzwe, ujifunze, uucheze na uwe na mazoea nao, Hata kwenye kupika huwa inapendeza uwe mzoefu angalau kidogo ili hata ukienda chuoni kujifunza kupika uwe sio mgeni sana na iwe rahisi kwako ku catch up vitu tofauti na yule ambae hajawahi kupika. Kabla hujaenda cuoni unaweza kujifunza languages kama html na css kwenye basic level, hizi ni lugha nyepesi ambazo unaweza jifunza mtandaoni, kama mda upo jiongezee na javscript, c++ na python, n.k. yani ukifika chuoni kuna vitu unakuwa ahead tayari wewe unapukuta tu. inabidi ujiongeze uwe unajifunza vya ziada hata ukianza chuo ujitengee hata dakika 30 tu kila siku, kutegemea kwamba chuo ktakufanya uwe konki utasubiri sana ndio maana wapo wahitimu wana gpa kali (wakiwemo lecturers wanaofunisha vyuoni) lakini vitendo sifuri.

🌀 Kwenye kununua Laptop hakikisha unanua laptop ya “LENOVO THINKPAD” laptop hizi zimetengenezwa kwa sifa moja wapo ya kuwa imara sana, utatumia kwa muda mreefu, asiee hakunaga kitu kinauzi kama kuanza kwenda kwa mafundi laptop, pesa inaweza kukutoka acha tu, leo taizo hili, Kesho tatizo flani, siku nyingine tatizo linajirudia, n.k.Hu
 
Vyuo vya wenzetu IT ni engineering huyu anasema ni kucopy tu mafile.
Arusha Technical hesabu zote wanazosoma computer science IT anasoma tuletee ushaidi wa ulichokisema.
Kwa vyuo vyetu vya technical hususan Must Na Arusha tech siwezi shangaa kabisa hata wakianzisha kozi za mapishi waweke somo la hesabu, Ni vyuo ambavyo bado havijapevuka kwenye upangaji wa masomo.

Chuo kama MUST diploma wanasoma masomo 14 kwa muhula, What is this ? wao wanasifia kwamba chuo inabidi kiwe kigumu masomo yawe mengi ndio kinamuivisha mtu, Upuuzi mtupu huu.

Hao Arusha Tech nao upangaji wa kozi zao ni shagala bagala, yani hio information technology ni kama vile wame copy na ku paste kutoka modules za computer science, huu kwanini nao nisiuite upuuzi, kuna haja gani kufundisha vitu nje ya taaluma ??
 
Back
Top Bottom