Blue ticks za whatsapp: Ni kwamba huyo mtu yupo busy sana au ameamua tu kukuonesha dharau za waziwazi?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
11,637
2,000
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Wewe binafsi unalichukuliaje hili suala la blue ticks za whatsapp kukaa muda mrefu (wiki moja)? Ni kwamba, huyo mtu yupo busy sana au ameamua tu kukuonesha dharau?

images.jpg


MFANO MDOGO APRIL 2018
=========
Unakuta una-chat na mtu ambaye ni classmate wako vizuri tu siku ya weekend jumamosi usiku, yeye anakaa Mwanza na wewe upo Dar, labda kuhusiana na masuala ya mpira wa simba na yanga.

Ukimtumia message ndani ya sekunde chache tu zinatokea zile ticks mbili za blue na ndani ya sekunde hizo hizo classmate anajibu na mnaendelea hivyo hivyo hata kwa muda wa dakika 5 huku mkichekeana na emoji mpaka zile za kurusha miguu juu.

Sasa gusia tu suala la kutaka kukopa pesa kisha umrudishie mwakani 2019 ghafla utaona zile blue ticks mbili zimetokea alafu mtu hajibu tena. Hajibu tena na chat chat ndio imeisha hapo hapo. Utangojea weeeeee mpaka basi.

Baada ya week kama tatu hivi classmate huyo huyo ndiye amepata shida ya ghafla na amekutumia message Whatsapp saa 12 asubuhi na wewe umekuja kuiona na kumjibu saa 10 jioni utamsikia "Daaah mwanangu vp, ina maana message ya tangia muda ule ndio unanijibu sasa hivi mkuu?"
=====

Mifano ni mingi kweli kweli na nikisema yote niiweke humu hakika hapatatosha.

USHAURI WANGU: Hao Whatsapp kama wanaweza pale katika emoji zao waweke "quick text" ambayo mtu akibonyeza mara moja itaandika "Nimepokea ujumbe wako ila nitakujibu nikipata nafasi, kwa sasa nipo busy sana"

Wewe binafsi unalichukuliaje hili suala la blueticks za whatsapp kukaa muda mrefu (wiki moja)?

NDUGU YANGU USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya mdau
=====
Kuna za ubize na za dharau pia, ila nyingi ni za dharau.

Mtu uko busy kwanini ufungue msg? Ni bora uache itiki ile ya kuonesha msg imefika vitiki viwili lakini mtu na madharau yake unakuta anafungua na hajisikii kukujibu.
Binafsi uwa najisikia vibaya, na ukiniblue tick kwangu lazima nikulipizie no matter vile utapokea
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,424
2,000
Whatsapp huzuia Msg za Kitaperi za kukopana Msomaji hazimfikii... Wewe huzioni Taasisi za kukopesha hadi uende ukanyonye Jasho la Mtu utokomee zako....
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
11,637
2,000
Kwani ni lazima nikujibu pindi tu ninavyosoma
Usumbufu huu ndio maana nimeamua kutoa option hiyo. Bora mtu asiwe na uhakika kama nimesoma ama bado
USHAURI WANGU: Hao Whatsapp kama wanaweza pale katika emoji zao waweke "quick text" ambayo mtu akibonyeza mara moja itaandika "Kwa sasa nipo busy nitakujibu nikipata nafasi"
 

Depal

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
16,447
2,000
Kuna za ubize na za dharau pia, ila nyingi ni za dharau.

Mtu uko busy kwanini ufungue msg? Ni bora uache itiki ile ya kuonesha msg imefika vitiki viwili lakini mtu na madharau yake unakuta anafungua na hajisikii kukujibu.
Binafsi uwa najisikia vibaya, na ukiniblue tick kwangu lazima nikulipizie no matter vile utapokea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom