Kukopa mtu pesa kunadhalilisha sana

Kukopa mtu pesa kunadhalilisha sana

Pole sana Mkuu.

Kumkopa mtu pesa kunadhalilisha sana mbaya zaidi umuelezee mtu tatizo lako akukopeshe pesa halafu asikukopeshe aseme hana, inafedhehesha sana.

Au uwe na rafiki unamkopa pesa na huwa unamlipa kwa wakati lakini yeye hajawahi kukukopa nayo inafedhehesha sana siku mkigombana atatumia nafasi hiyo kukunyanyasa.

Kuna baadhi ya watu ukiwa text wanadhani unataka uwakope pesa.

Kuna wengine wakikukopesha wanaenda kukutangaza.
 
ishi kulingana na kipato chako..acha ku over budget thats why unajikuta unapanga budget kwa zilizopo mifukoni mwa wenzako.
 
Kuna wengine ukiwapigia Simu,,au ukiwa nae kumueleza tatizo,, vile ukianza kujieleza shida yako tu!!,hata kabla hujamaliza kujieleza anakukatisha,,,
Utasikia duu!! Kama ni suala la pesa mambo yangu pia magumu sn..
Inafedhehesha sn..
Mbaya zaidi unafika dukani kwa Mangi,,watu wamejaa unasubiri wapunguwe umsomeshe ukope unga na sukari,,,, na yeye anakulazimisha useme unachotaka mbele za watu,, na baada ya kujieleza kwake hata kabla hujamaliza kujieleza anakukatisha,,
Duu,,Leo bwashee niache kidogo..
Kwa kweli inafedhehesha sn....
Na inaumiza sn kumwambiya mtu shida zako na asikusaidie..
 
Kwa upande wangu bora nkupe Tu kama ninayo kukopesha najua kutaua kama sio kuweka mashakani uhusiano wowote uliopo baina yetu.
 
Leo nimesikia kisa kwamba mtu kakopa laki mbili na anatakiwa kurejesha laki nane huko babati, Mkopaji amelipa laki nne zimebaki laki nne akaona inakua ngumu kulipa ikabidi awatafute takukuru waingilie kati.
 
Back
Top Bottom