Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 1,939
- 4,122
Ikiendelea hivi kama ambavyo wao wanaona ni busara kuwasaka na kuwakamata wanaharakati na wanapigia kelele mkataba!
Ni kukuza joto la upinzani na kuongeza kelele zaidi na hata kuchochea vitu vingine visivyotarajiwa!
Ilikuwa sawa kabisa kwa serikali kupuuza hizi kelele huku wao wakijikita kwenye kuweka sawa mkataba huo
Kitendo cha kuanza kuagiza kukamatwa kwa wanaharakati, ni kuongeza makelele na kuongeza joto la wananchi na hata kusababisha mambo ambayo yanaweza yasidhibitiwe kwa wepesi na badala yake kukawepo matumizi ya nguvu isivyo lazima
Wakati wa utawala wa Magufuli, kulianza kidogokidogo kelele za hapa na pale, mwishoni tuliona mambo magumu kwa serikali kuyadhibiti kiasi kwamba hata Rais alikuwa akiishi kwenye presha ya wananchi wake
Serikali ningeiomba, iendelee kukaa kimya na kuwanyazia hawa watu ingawa ni kweli wana hoja za msingi huku serikali ikifanyia upembuzi yakinifu kuhusu hoja za wananchi
Tumeshuhudia mawaziri wakuu wa zamani, viongozi wa dini mbalimbali, wasomi wa kada mbalimbali na wanazuoni, wanaccm na wasio wanaccm wenye kada mbali mbali wakiungana na watanzan wengine kuhoji mkataba jinsi ulivyo,
Hiyo inamaanusha kwamba, watu wa kada mbali mbali kutoka ndani ya ccm na nje ya ccm, kwa umoja wao wameungana katika hili!
Kwa maana hiyo, sioni kama itakuwa ni busara kuanza kukamatwa kwa wanaohoji mambo hayo
Hii inaweza kuleta shida huko tuendako