The mountain lion
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 1,153
- 412
Habari za usiku wakuu? Ni matumaini yangu sote tu wazima wa afya tele na ambao wana matatizo ya hapa na pale basi Mungu awawekee mkono wa uponyaji.
Wanajamvi kama kichwa cha habari kinavyojipambanua, tangu nikiwa mdogo nimekua nikivutiwa sana na utendaji wa kazi wa idara hii nyeti hapa nchini hivyo ndoto zangu ilikua ni siku moja kuwatumikia watanzania wenzangu kupitia idara hii nyeti.
Tafadhali sana wanajamvi kama kuna mtu anajua hatua na taratibu za kufuata ili kujiunga na idara hii naomba kujuzwa tafadhali. Ni muhimu sana kwangu na ni sehemu ya ndoto yangu ya siku nyingi msaada tafadhali wakuu. Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Tafuta uzi wenye kichwa are spies made or born?utapata Jibu la swali lako.