Uzalendo ni chanzo cha Usalama wa Taifa?

Richard mtao

JF-Expert Member
May 13, 2018
209
236
Habari wana JF.
Naomba kuanza kwa kuzungumza machache sana ili tuelewane kutokana na mada hii.
Kumekuwa na mada mbalimbali zinazozungumzia maswala ya uzalendo, usalama wa taifa,maafisa usalama wa taiafa, majeshi na vyombo mbalimbali na kila mmoja amezungumzia kwa namna ya peke yake.

Leo mimi nazungumzia je ni kweli kwamba uzalendo unaweza kuwa chanzo cha usalama wa taifa? Sina maana ya kupotosha ama kutengeneza taharuki kwa namna yoyote ile, ninahitaji tujifunze na kuona mambo haya yanaoana kwa kiasi gani na yanaweza vipi kuchangia katika usalama wa taifa lolote duniani.

Nianze kwa kuelezea uzalendo/usalama wa taifa ni nini?
Uzalendo ni imani, hisia ya mtu kufanya jambo lolote ama kujitoa kwaajili ya taifa lake. Unaweza kujumuisha mambo mbalimbali yanayoashiria upendo na kuwakilisha nchi husika katika maeneo mbalimbali imiwemo lugha, alama,michezo na n.k.

Usalama wa Taifa ni ile hali ya nchi au taifa kuwa salama na ulinzi wa kutosha dhidi ya wanainchi, uchumi na taasisi zake zote. Vilevile usalama wa taifa unahusishwa na kutokuwepo kwa matukio ya kigaidi, uhaini, uhujumu, uhasi au mapinduzi yanayosababishwa na mambo mbalimbali.

Uzalendo unanafasi kubwa sana ya kuhakikisha nchi inakuwa salama sana, lakini hiyo itawezekana endapo serikali itashirikiana vyakutosha na jamii katika kuandaa kizazi ambacho kinamapenzi ya dhati na nchi yao, tukiachana na mifumo ya sasa iliyopo(elimu, afya, utawala na uongozi) ambayo kimsingi inasaidia katika kuandaa kizazi bora bado naona kuna haja ya serikali kufanya zaidi ili kuboresha mazingira hayo hasa ukizingatia nchi yetu inakua kila siku na kujifungulia fursa mpya za kiuchumi, kijamii na teknolojia. Na kama mnavyojua hakuna vitu ngumu kwasasa kama vita vya kiuchumi, afya, teknolojia. Hivyo ipo wazi pale taifa lolote linapopiga hatua kubwa basi maadui wanakuwa ni wengi sana kwa lengo la kuishusha au kuififisha kabisa kwenye ramani ya dunia.

Sasa kama huku ndiko tunakoenda( tunakua kiuchumi na kiteknolojia) je mifumo hii iliyopo sasa ambayo kimsingi imetusaidia sana je inaendana na kasi hii? Je wanainchi wangapi wenye uwezo wako tayari kufanya chochote kwajili ya nchi yao?

Nnachomaanisha ni kwamba kuna haja kubwa ya serikali kupitia wizara ama mamlaka husika kuwekeza na kuandaa mpango madhubuti wa muda mrefu utaowezesha jamii zetu kuandaa vizazi vinavyoelewa vinawajibu gani kuanzia katika ngazi za jamii hadi taifa, yaani kwa mfano watu kutotanguliza rasimali mbele kuliko kitu anachopaswa kufanya au mtu yoyote kutomuumiza mwenzie kwasababu zozote zile ambazo ziko nje ya sheria za nchi, ili tuweze kupata watu/viongozi/watumishi ambao sio wezi, sio wenye tamaa, sio wabadhirifu, sio viongozi wenye uchu wa madaraka.

Endapo serikali ikilifanikisha hili kutakuwa na faida nyingi sana zinazoweka uhakika wa usalama wa taifa,baadhi ya faida hizo ni pamoja na Kupungua au kuondokana kabisa kwa matukio ya kihalifu, ubadhirifu,uhujumu, ugaidi,uhaini,mapinduzi, uhasi,upinzani,machafuko,utoroshwaji wa rasilimali za nchi, vita, utakatishaji fedha, umaskini, magonjwa, njaa, ukame nakadharika.

Hivyo nahitimisha kwa kusema Uzalendo ndio msingi Mkuu wa usalama wa taifa. Kwakua unatoa fursa nyingi zinazoweza kulisaidia Taifa wakati wowote. Mfano endapo nchi itakuwa na wazalendo angalau kwa asilimia 90 maan yake nchi ina asilimia 90 za watu wanaoweza kufanya jambo lolote kwajili ya nchi na kama serikali ikihitaji wafanyakazi katika vyombo vya ulinzi na usalama au sekta nyingine yoyote maana yake ina uhakika wa kupaata idadi kubwa sana ya watumishi walio na uzalendo wa hali ya juu sana.

Uzi huu ni kwa maana ya kutaka kuamsha fikra mpya. Karibuni tujengane zaidi.
 
Mada nzuri hii. Na sijui kwanini dhana ya uzalendo ni lazima uwe kada mtiifu wa chama fulani.
Wanaodhani ivyo wanakosea sana, kuna watu wa kawaida kabsa wasio na chama chcht ila ni watiifu sana kwa mamlaka mpka unasema tungepata watu 10000 huyu dah
 
Siku hizi uzalendo ni pesa. Zamani watu walikua wazalendo toka moyoni ila kadri siku zinavyozidi kwenda neno uzalendo linafifia kwa umaskini uliotukumba kila kona.
Hili ni pigo kubwa kwa vizazi vijavyo. Unahis tufanye nini angalau kupunguza hii dhana mpya na kuufanya uzalendo kuwa hoja ya kila mtanzania bila kujali, dini, chama, kabila au aina fulan fulani iv
 
Habari wana JF.
Naomba kuanza kwa kuzungumza machache sana ili tuelewane kutokana na mada hii.
Kumekuwa na mada mbalimbali zinazozungumzia maswala ya uzalendo, usalama wa taifa,maafisa usalama wa taiafa, majeshi na vyombo mbalimbali na kila mmoja amezungumzia kwa namna ya peke yake.

Leo mimi nazungumzia je ni kweli kwamba uzalendo unaweza kuwa chanzo cha usalama wa taifa? Sina maana ya kupotosha ama kutengeneza taharuki kwa namna yoyote ile, ninahitaji tujifunze na kuona mambo haya yanaoana kwa kiasi gani na yanaweza vipi kuchangia katika usalama wa taifa lolote duniani.

Nianze kwa kuelezea uzalendo/usalama wa taifa ni nini?
Uzalendo ni imani, hisia ya mtu kufanya jambo lolote ama kujitoa kwaajili ya taifa lake. Unaweza kujumuisha mambo mbalimbali yanayoashiria upendo na kuwakilisha nchi husika katika maeneo mbalimbali imiwemo lugha, alama,michezo na n.k.

Usalama wa Taifa ni ile hali ya nchi au taifa kuwa salama na ulinzi wa kutosha dhidi ya wanainchi, uchumi na taasisi zake zote. Vilevile usalama wa taifa unahusishwa na kutokuwepo kwa matukio ya kigaidi, uhaini, uhujumu, uhasi au mapinduzi yanayosababishwa na mambo mbalimbali.

Uzalendo unanafasi kubwa sana ya kuhakikisha nchi inakuwa salama sana, lakini hiyo itawezekana endapo serikali itashirikiana vyakutosha na jamii katika kuandaa kizazi ambacho kinamapenzi ya dhati na nchi yao, tukiachana na mifumo ya sasa iliyopo(elimu, afya, utawala na uongozi) ambayo kimsingi inasaidia katika kuandaa kizazi bora bado naona kuna haja ya serikali kufanya zaidi ili kuboresha mazingira hayo hasa ukizingatia nchi yetu inakua kila siku na kujifungulia fursa mpya za kiuchumi, kijamii na teknolojia. Na kama mnavyojua hakuna vitu ngumu kwasasa kama vita vya kiuchumi, afya, teknolojia. Hivyo ipo wazi pale taifa lolote linapopiga hatua kubwa basi maadui wanakuwa ni wengi sana kwa lengo la kuishusha au kuififisha kabisa kwenye ramani ya dunia.

Sasa kama huku ndiko tunakoenda( tunakua kiuchumi na kiteknolojia) je mifumo hii iliyopo sasa ambayo kimsingi imetusaidia sana je inaendana na kasi hii? Je wanainchi wangapi wenye uwezo wako tayari kufanya chochote kwajili ya nchi yao?

Nnachomaanisha ni kwamba kuna haja kubwa ya serikali kupitia wizara ama mamlaka husika kuwekeza na kuandaa mpango madhubuti wa muda mrefu utaowezesha jamii zetu kuandaa vizazi vinavyoelewa vinawajibu gani kuanzia katika ngazi za jamii hadi taifa, yaani kwa mfano watu kutotanguliza rasimali mbele kuliko kitu anachopaswa kufanya au mtu yoyote kutomuumiza mwenzie kwasababu zozote zile ambazo ziko nje ya sheria za nchi, ili tuweze kupata watu/viongozi/watumishi ambao sio wezi, sio wenye tamaa, sio wabadhirifu, sio viongozi wenye uchu wa madaraka.

Endapo serikali ikilifanikisha hili kutakuwa na faida nyingi sana zinazoweka uhakika wa usalama wa taifa,baadhi ya faida hizo ni pamoja na Kupungua au kuondokana kabisa kwa matukio ya kihalifu, ubadhirifu,uhujumu, ugaidi,uhaini,mapinduzi, uhasi,upinzani,machafuko,utoroshwaji wa rasilimali za nchi, vita, utakatishaji fedha, umaskini, magonjwa, njaa, ukame nakadharika.

Hivyo nahitimisha kwa kusema Uzalendo ndio msingi Mkuu wa usalama wa taifa. Kwakua unatoa fursa nyingi zinazoweza kulisaidia Taifa wakati wowote. Mfano endapo nchi itakuwa na wazalendo angalau kwa asilimia 90 maan yake nchi ina asilimia 90 za watu wanaoweza kufanya jambo lolote kwajili ya nchi na kama serikali ikihitaji wafanyakazi katika vyombo vya ulinzi na usalama au sekta nyingine yoyote maana yake ina uhakika wa kupaata idadi kubwa sana ya watumishi walio na uzalendo wa hali ya juu sana.

Uzi huu ni kwa maana ya kutaka kuamsha fikra mpya. Karibuni tujengane zaidi.
Mkuu umegusia kitu ambacho kwa uzoefu wangu nimekiona.

Ni kweli kabisa ukiwa mzalendo wa kweli/ halisi kabisa kwa taifa na sio huu wa vyama na uchawa... unakua katika nafasi nzuri zaidi ya kutoa mchango wako katika taifa hasa ukiaminiwa.

Mfano na 1;
Kwa uzoefu wangu... Ukiwa mzalendo mawazo fikra na mipango yako yakimaisha/kiuchumi unaielekezea kwenye taifa automatically pasipo wewe kujua. (yaani mawazo yako asilimia kubwa yanakua kwenye level ya kitaifa) mipango yako na familia yako unaisahau/hujizingatii wewe/unakua Huna ubinafsi(umimi).

Kuna muda unajistukia unaona Sasa huu ni ubwege
Hivi hizi fikra na mawazo nayoyawaza juu ya taifa kwanini nisijiwazie mimi nipange mipango na mbinu kujikomboa mimi na familia yangu kiuchumi.

Mfano na 2;
Kama ikatokea we ni mzalendo halisi na unakipawa cha kua na maono maono yako hayawi ya kikwakokwako kua umeona mbaya wako au umeona tukio baya linataka kukutokea mbeleni na kweli dalili zote za tukio hilo utaziona.

Sasa basi kwamzalendo halisi ambae mawazo na fikra zake mara nyiki ni Kuhusu taifa, yeye maono yake yanakua kitaifa zaidi ikitokea taifa linaelekea kwenye changamoto flani huyo mtu ataitambua hiyo changamoto kabla haijalikabili taifa. Hii ni moja ya potential iliyojificha nyuma ya uzalendo.

Kwa lugha nyingine sio rahisi kupata mawazo bora zaidi juu ya kitu husika kama Huna passion/hobby nacho, hivyo basi ukiwa mzalendo au tukawa na idadi kubwa ya wazalendo hasahasa viongozi tutakua na nchi yenye uongozi sahihi wenye maono sahihi maradufu zaidi ukilinganisha na wakawaida hawa (wabinafsi/wachumia tumbo)
 
Kaka umeandika hoja nzito sana aisee. Endapo waty sahihi wakiona huu ujumbe kuna kazi ya kufanya kaakwel
 
Kuna haja yakuhamasisha uzalendo nadhani itakuwa njia sahihi yakuijenga jamii yetu katika nyanja tofauti tofauti.

Inafikia hatua watu wanakosa uzalendo kiasi kwamba tunakosa kuaminiana kama nchi(yaani suala liko out of control kiasi kwamba hata uongozi wa nchi anaona liko nje ya uwezo wao wanaona bora watu kutoka nje(wawekezaji)wasaidie kupunguza wizi bandalini. Najua hii point iliibuka katika lile sakata la bandari na lengo lilikua zuri tu kutetea uwekezaji katika bandari, ila tafsiri yake ndio hio kua uraisi na mamlaka yake pamoja na viongozi wote wameshidwa kuongoza nchi (kuwadhibiti wahuni bandarini.)))
Kuna wale wa bonde la Usangu(12familia)

Sababu kubwa ni kwamba watu wamekosa uzalendo kwa taifa wanahujumu taifa.

Itafutwe namna ya kuukuza na kuuendeleza huu uzalendo katika maeneo yanayofaa kama vile;
=>JKT(Makambini)
=>Mashuleni
=>Nyumba za ibada.
=>Katika michezo mbalimbali (soccer), (jogging clubs)
=>makazini hususani kwenye mashilika ya umma.

Kama ulivyo elezea kukiwa na muamko mkubwa wa uzalendo mambo mengi ya yasiyofaa/yasiyokubalika na jamii yatapungua, mambo hayo ni kama;

=>Vijana wa kitanzani kulaghaiwa kuingia na kujihusisha na vitendo vya kigaidi/uzandiki/uhaini na yafananayo nahayo, uzalendo ukitamalaki katika jamii haitakua rahisi Mtanzania kujiunga na makundi ya kigaidi. (Hata ukiwa mjinga uliekosa elimu ila kwakua tu mzalendo wajanja hawataweza kukutumia kuihujumu nchi yako).

=>Uzalendo unaweza ukapunguza tatizo la brain drain vijana wenye vipawa na uwezo mkubwa kitaaluma kutumikia mataifa mengine ilhali huku nyumbani tunauhitaji nao(ingawaje huku kwetu sera na miundombinu bado ni changamoto haimshawishi kijana kurudi kutumikia taifa, na wanaongea wazi wazi kabisa kua akipata fursa akaenda ng'ambo bongo harudi)...

Sasa uzalendo unauwezo wa ku-mretain mtu mwenye fikra hizi, kikubwa tu awe mzalendo halisi, Sasa anakuwaje mzalendo?

Ongezea mambo mengine kama yafuatayo yanomfanya mtu kuwa mzalendo.

1. Kujitoa na kuwa tayari kufa kwa ajili ya taifa lako.
2. Kutunza siri za nchi na kuzilinda kwa gharama yoyote ile.
3. Kujiona na kujisikia weye ni sehemu ya taifa.
4. Kujivunia utaifa na kuwa tayari kupigia kifua utaifa huo.
5.Kujisifia utaifa wako na kuwa tayari kuutangaza utaifa huo popote pale.
6 Kuweka kumbukumbu na historia ya taifa hilo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
7.Kulinda Mali na Rasilimali za nchi na mipaka yake yote.

Namba 1, 2 na 7 ni Usalama wa Taifa vikiwemo vyombo vyake vyote.

Namba 3-7 ni wananchi .
 
UZALENDO NA AMANI

Naunga mkono hoja kwa kadri ulivyoijadili ingawa nitaongeza mtizamo wangu kwa kadri ya uelewa.

Kwanza ni kutambua kwamba hili ni suala muhimu sana na la msingi sana kwenye jamii iliyostaarabika na kuendelea.

Tunapozaliwa mara nyingi vichwa vyetu huwa wazi(vacuum) bila maarifa yoyote, hii ni kwa mujibu wa wanasaikolojia ya makuzi). Baada ya hapo mtoto huanza kujazwa maarifa kulingana na wale au yale yaliyomzunguka naye huwa mwanafunzi mwaminifu na baadaye kuja kuwa mwalimu.

Hivyo, msingi wa kwanza wa yote ni maarifa tunayopata wakati tukiwa wadogo na yale tunayoyaona. Maarifa haya ndo huja kuza msingi wa utambuzi wetu wote. Kujua thamani jema na baya na kiasi chake.
Samaki mkunje angali mbichi.

Kwa sababu hiyo, chachu muhimu ya uzalendo inaanza kwenye familia au jamaa waishio pamoja ikijumuisha makuzi yao kwa kila mmoja(mwanajumuiya).

Kujitambua:
Kutambua ubinadamu wako na mahitaji yako(wewe ni nani na unahitaji nini na vitatoka wapi)ni suala muhimu pia. Kama tunavyofahamu ukamilifu wa ubinadamu hautokani maarifa au mali, bali mahusiano na wengine wanaomzunguka. Hivyo, kujifunza thamani ya mahusiano mema ni kitu cha msingi ndani ya jamii yako ya awali. Tambua thamani ya unachopata toka kwenye mazingira na watu wanaokuzunguka. Huwezi kutoa chochote kwa mwenzako au kuwa tayari kutoa chochote bila kujua umuhimu wake kwa kuanzia kwako mwenyewe.

Kumtambua wenzako:
Kuwatambua binadamu mwezako na mahitaji yao. Baada ya safari ya kujitambua, safari inayofuata ni namna gani utamtambua binadamu mwenzako bila mipaka yoyote mfano: mrefu, mfupi, mweupe, aliye au asiye na mali nk. Pia kutambua mahitaji yake ya msingi na kujua kuwa mahitaji mengine yanatoka kwenye himaya yako. Utakapotambua kuwa hitaji la binadamu mwenzako ndilo lako basi kinachofuata ni kujengewa imani/ moyo wa kuthamini binadamu mwenzio. Hapo, utampa thamani linganifu na wewe kulingana na nafasi uliyopata kwenye makuzi yako.
Binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja.

Kujiweka tayari unapohitajika.
Baada ya safari mbili hapo juu, safari inayofuata ni kuuweka tayari moyo wako na akili kujitoa kwa hali na mali wakati wa hitaji na pasipokuwa na hutaji. Kwani mzalendo hasubiri kuhimizwa. Hata pale adui atakapofanikiwa kujipenyeza sehemu yoyote basi atakutana na nguvu ya uzalendo na kujitoa ambayo itampa wakati mgumu kutimiza azma yake.

Tukumbuke hata wakoloni walipokuja na siraha zao za kisasa, sehemu walizokuta umoja na uzalendo basi walipata shida kubwa kutawala. Hivyo, kuwa na idadi kubwa ya watu wenye mioyo ya uzalendo ni nafasi kubwa ya maendeleo na amani kwa taifa. Kama wakiws wachache kulingana na jamii au kizazi mara myingi watashindwa au kuangamizwa.
Umoja ni nguvu

Safari hizo hapo juu zaweza kwenda kwa pamoja ndani ya makuzi mtu. Zimewekwa kwa mafungu ili kuweza kuzieleza vyema.

Kwa msingi huo kaya zetu, jamii zetu, taasisi zetu zitakuwa zimejengwa na misingi ya uzalendo madhubuti. Uzalendo utasukuma kutokuwa tayari kuona haki ya binadamu mmoja inapotea au haki ya jamii au taifa.

Kwa msingi huo pia mnyororo huu uliofungwa ndani ya jamii zetu(uzalendo) utakuwa ndio ngome imara itakayomshinda adui kuibomoa na kupenyeza yasiyofaa.
Amani ni tunda la haki na penye haki pana uzalendo.

Ukitaka kumfumza mtu mkubwa uzalendo, kuna mambo mengi ya kuzinhatia:

1: Umuondoe mhusika kwenye yale aliyokwisha yabeba kichwani mwake(pre-empty), ndo uendelee na mafunzo yako.

2: Wewe unaemfunza basi uwe unauishi uzalendo wa kweli na kimatendo kwani unaemfunza pia ana akili ya kupima hali halisi.

3: Kama hauta ondoa maarifa aliyonayo basi uhakikishe mafunzo ya uzalendo yanabeba uzito wa juu saya kuyazidi aliyokuwa nayo.

4: Utahitaji mazingira mazuri, muda mzuri na wa kutosha ili kufanikisha haya na si crash programme.

Tunachokiona kwa sasa kwenye jamii na taasisi zetu ni mbwa mwitu waliovaa ngozi ya kondoo. Kwa maana ya kwamba mioyo ya watu haiendani na matendo yao. Watu hawajaiva kwenye uzalendo ila wanajua ukionyesha picha ya mzalendo watanufaika sana kwenye maisha yao binafsi. Kwa msingi huo watu wanaigiza uzalendo na wale wanaouishi uzalendo wa kweli wanapata shida hata kutoka kwa wasiojua uzalendo na wanaoigiza uzalendo.

Kiongizi mzalendo, awe ni wa mtaa, kikoba au kikundi cha ngoma hayuko tayari kuishi kwa kuwabebesha mzigo wanakikundi wake. Hatakuwa tayari kuzurula na usafiri wa ghali au misafara ya ghali wakati michango ya walionunua hayo magari au usafiri wako ni hohehahe. Huwezi kila siku unatembea umekalia gari ambalo ni sawa na utatuzi wa shida ya elimu au afya sehemu unayoihudumia. Huwezi kutembea na msafara ambao kwa siku unaweza kumaliza utatuti wa elimu au afya kwenye wilaya na una furaha. Moyo wako utakusuta. Hata kama ni sera utaiondoa ili kuwapa nafuu wanakikundi au umoja.

Hivyo, kabla ya kuulilia uzalendo ni vyema kujiuliza na kutafakari kwa muktadha huu:

1: Je ndani ya familia zetu kuna uzalendo?

2: Je tunajifunza uzalendo ndani ya familia?

3: Je tunaweza kutoa mafunzo ya uzalendo kwa watu wasiojua wala kuelewa umuhimu wa uzalendo tangu walipozaliwa?

4: Je tunaweza kuwafundisha watu uzalendo na wakauvaa bila kuona matunda ya uzalendo au uzalendo ndani yetu?

5: Je ndani ya nchi yetu kuna uzalendo wa kweli?

6: Je viongozi wetu wanaongoza kwa uzalendo wa kweli?
 
Kivipi Mkuu??
Maisha yakiwa magumu, tunaanza kuona mara wewe Mkenya, au ni Mtusi sijui ni Mnyasa
Na ndio imekuwa wakati huu, kwa jinsi kundi ya kubwa la wajinga linavyoongezeka mpaka uafrika unafatiliwa hata kama ni mzaliwa wa vizazi na vizazi, Mjaluo wa Musoma au Muha wa Kigoma tunamuona mgeni wa nchi
Zamani walikuwepo wanoko wanawaita Waarabu wa Mwamashilingi na Wahindi wa Kahama ni magabacholi
 
Kuna haja yakuhamasisha uzalendo nadhani itakuwa njia sahihi yakuijenga jamii yetu katika nyanja tofauti tofauti.

Inafikia hatua watu wanakosa uzalendo kiasi kwamba tunakosa kuaminiana kama nchi(yaani suala liko out of control kiasi kwamba hata uongozi wa nchi anaona liko nje ya uwezo wao wanaona bora watu kutoka nje(wawekezaji)wasaidie kupunguza wizi bandalini. Najua hii point iliibuka katika lile sakata la bandari na lengo lilikua zuri tu kutetea uwekezaji katika bandari, ila tafsiri yake ndio hio kua uraisi na mamlaka yake pamoja na viongozi wote wameshidwa kuongoza nchi (kuwadhibiti wahuni bandarini.)))
Kuna wale wa bonde la Usangu(12familia)

Sababu kubwa ni kwamba watu wamekosa uzalendo kwa taifa wanahujumu taifa.

Itafutwe namna ya kuukuza na kuuendeleza huu uzalendo katika maeneo yanayofaa kama vile;
=>JKT(Makambini)
=>Mashuleni
=>Nyumba za ibada.
=>Katika michezo mbalimbali (soccer), (jogging clubs)
=>makazini hususani kwenye mashilika ya umma.

Kama ulivyo elezea kukiwa na muamko mkubwa wa uzalendo mambo mengi ya yasiyofaa/yasiyokubalika na jamii yatapungua, mambo hayo ni kama;

=>Vijana wa kitanzani kulaghaiwa kuingia na kujihusisha na vitendo vya kigaidi/uzandiki/uhaini na yafananayo nahayo, uzalendo ukitamalaki katika jamii haitakua rahisi Mtanzania kujiunga na makundi ya kigaidi. (Hata ukiwa mjinga uliekosa elimu ila kwakua tu mzalendo wajanja hawataweza kukutumia kuihujumu nchi yako).

=>Uzalendo unaweza ukapunguza tatizo la brain drain vijana wenye vipawa na uwezo mkubwa kitaaluma kutumikia mataifa mengine ilhali huku nyumbani tunauhitaji nao(ingawaje huku kwetu sera na miundombinu bado ni changamoto haimshawishi kijana kurudi kutumikia taifa, na wanaongea wazi wazi kabisa kua akipata fursa akaenda ng'ambo bongo harudi)...

Sasa uzalendo unauwezo wa ku-mretain mtu mwenye fikra hizi, kikubwa tu awe mzalendo halisi, Sasa anakuwaje mzalendo?
Aisee kaka umeandika hoja nzito nzito sana.
Me nadhan kuna haja serikali ifanye jambo maana sis wanainchi mmoja mmoja tunaweza kukwama.
Unaonaje ikaanzishwa shirika lisilo la kiserikali ambalo halifungamani na itikadi yyt ya chama likajikita katk kueneza uzalendo wa kweli..hasa katik jamii moja kwa moja.
Kupitia mikutano ya hadhara, majarida, machapidho, vyomb vya hbr na mambo kama hayo??
 
Back
Top Bottom