Kujengea makaburi ya Waliotutangulia - Kuna umuhimu wowote?

Kujengea makaburi ya Waliotutangulia - Kuna umuhimu wowote?

Kuzaliwa tu ukiwa hai ni alama tosha kwamba kwenye universe ulikuwa na nafasi yako! Binafsi sioni ubaya wowote wa kutunza kumbu kumbu za wapendwa wetu waliotutangulia mbele ya haki kwa kutunza maeneo yalipohifadhiwa masalia ya miili yao kwa kunakshi kwa namna ambayo wahifadhi wataona inafaa! Nafikiri ifike mahali hata Architects wadesign makaburi kiusanifu ili kuwa sehemu ya landscape badala ya kuruhusu tu kuinuka kwa landmark ambazo zinachukua sehemu kubwa na kuwa uchafu kwa kukosa matunzo
attachment.php
 
Attachments

  • Arch.jpg
    Arch.jpg
    54.1 KB · Views: 261
Charminglady kujengea ni kuweka kumbukumbu kupitia uimara. Makaburi yasipotunzwa vizuri hupotea kabisa. Sisi tunaoishi mbali na miji yetu ya asili na kuwa na makaburi ya wazee ni rahisi sana kupotea maana watunzaji si rahisi kama tunavyofikiria. Hivyo ukilijengea litadumu na vizazi vitajifunzia historia pale. Tena weka na maneno ya jina, mwaka wa kuzaliwa, kufa, kuzikwa etc. Archeologists wanajua maana ya ancestral record keeping.

Issue siyo kujengea mkuu.

Suala ni kutumia gharama kubwa (kwa kuomba omba ndugu na jamaa au hata majirani/marafiki) ili kujengea hayo makaburi.

Kujenga kwangu ni sawa ila kutumia gharama kubwa (bila uwezo huo) si sawa kabisa!
 
Mimi nilikuwaga na mawazo kama yako nilikuwa sioni umuhimu wa kujengea makaburi, lakini baada ya baba yangu kufariki na ndugu zake kututelekeza nililijengea mwenyewe ili kutunza kumbukumbu yake. Tena sikumshirikisha mtu zaidi ya mama na kaka zangu.
Now am happy ninaweza kwenda kumsalimia na kumbukumbu yake ipo. Mambo mengine huwezi kuona umuhimu wake hadi yakukute.
 
Hauna haja ya kusema samahani, ni kweli nilimpoteza mzazi mmoja tayari na kaka yangu mkubwa.

But I have nothing to do with their graves.. Hainisaidii na wala haitonisaidia chochote katika.maisha yangu. Walisharudi mavumbini kama lilivyo agizo la Mwenyezi Mungu....

Wewe umekumbana na utaendela kukumbana na kizingiti kimoja kwenye hii thread yako! Unataka KUONGOZA WATU KIMAISHA kwa kutumia imani yako ya dini! Hutafanikiwa kamwe! Kwanza anza kugeuza watu waingie kwenye imani yako halafu hapo ndio uendelee na USHAURI WAKO. Kwa mfano una mtu atakuambia yeye analinakshi kaburu la babu yake kwasababu anamini kuwa mzimu wa marehemu utamwongezea baraka.
 
Suala la kujengea makaburi wala halina shida maana hata jamii za hapo awali walikuwa wanaweka walau mawe kama alama ya kaburi.

Mambo ya kuweka nakshi za gharama kubwa Ni kutokana na uwezo WA mtu ama familia husika nalo pia halina tatizo Sana.

Tatizo lililopo siku hizi Ni ULIMBUKENI tena wa hali ya juu maana hata kina Pangu Pakavu nao wanataka ufahari kwenye kuzika wapendwa wao,matokeo yake ni kuchangishana michamgo isiyo ya lazima.

Imefika mahali ambapo mgonjwa akizidiwa Sana,watu wanaanza kuhaha kutafuta pesa SI za matibabu bali gharama za ujenzi wa kaburi.Shame!!!
 
Issue siyo kujengea mkuu.

Suala ni kutumia gharama kubwa (kwa kuomba omba ndugu na jamaa au hata majirani/marafiki) ili kujengea hayo makaburi.

Kujenga kwangu ni sawa ila kutumia gharama kubwa (bila uwezo huo) si sawa kabisa!

Nakubaliana na wewe... uko sahihi.... ila sio kujenga makaburi tu... kwenye maisha binadamu anapogharamia jambo lolote kuzidi uwezo wake (ambalo si la lazima) anafanya ndivyo sivyo! eg simu ya gharama, harusi, mavazi, gari, etc
 
charminglady my dia waache wafu wawazike wafu wao. Binadamu anakabiliwa na wimbi kubwa la ignorance na hata ukitaka kutazama jambo hili kwa undani utakuta ya kwamba hizi rabsha zote ni kujiridhisha nafsi zao tu wala aihusiani na marehemu. Binadamu tuna ubinafsi wa ajabu
 
Last edited by a moderator:

Ni juzi tu nimegoma kuchangia 200,000/- eti kwa ajili ya ujenzi wa uzio/ukuta wa kuzungushia makaburi ya ukoo.

'Hivi kumekuwepo na kesi ngapi za marehemu kutoroka hapo makaburini?',ndo swali nililouliza.

Ulimbukeni Ni tatizo kubwa mno kwenye jamii zetu.
 
Nakubaliana na wewe... uko sahihi.... ila sio kujenga makaburi tu... kwenye maisha binadamu anapogharamia jambo lolote kuzidi uwezo wake (ambalo si la lazima) anafanya ndivyo sivyo! eg simu ya gharama, harusi, mavazi, gari, etc

Kwa upande wangu, hilo ndiyo tatizo kubwa ambalo linatukumba kama jamii ya watanzania. Tunalimbuka hadi kupitiliza...

Kama watu wangekubali kufanya yale wanayoyaweza, watu tusingesumbuana na michango isiyo ya lazima.

Kwa sasa mtu anajikutua akitoa karibia 500K hadi milioni kwenye misimba, harusi, kipaimara na sherehe nyingine!

Hivi angetumia hizo pesa kuwekeza tungefika wapi?
 
Ni juzi tu nimegoma kuchangia 200,000/- eti kwa ajili ya ujenzi wa uzio/ukuta wa kuzungushia makaburi ya ukoo.

'Hivi kumekuwepo na kesi ngapi za marehemu kutoroka hapo makaburini?',ndo swali nililouliza.

Ulimbukeni Ni tatizo kubwa mno kwenye jamii zetu.

Ni mambo ya kushangaza sana hayo mkuu....

Pesa zote hizi kujenga ukuzio tu??

Tunahitaji kujiangalia upya kwenye mambo ya matumizi ya pesa na kuweka akiba...

Kuna kipingi cha Sixtus Mtsimbe jamaa aliongelea mambo ya saving...tunahitaji sana hiyo shule!
 
Ni kweli kabisa Mkuu,
Jamii imeyapa vipaumbele mambo yasiyo ya msingi na kuacha mambo muhimu.

Ni nadra Sana kusikia michango ya kupeleka wanafunzi shule/chuo,watu wamejikita kwenye harusi,uzio wa makaburi etc

"Ni vigumu mno kumshawishi nyani mzee kwamba asali ni tamu kuliko ndizi mbivu" Ni kwenda nao hivyohivyo tu.
 
Last edited by a moderator:
Sikumbuki ni mstari gani kwenye biblia yesu anasema "waacheni wafu wazikane wenyewe". Swali kama yesu mwenyewe hakumthamini aliyekufa wewe mwanadamu ndo ujifanye unampenda kiasi kwamba unapoteza ghalam na muda kwa ajili yake? kujengea makaburi hakuna maana hangaika na walio hai kuwaonesha njia na matendo mema, marehem yeyw hesabu yake imefungwa.
 
Issue siyo kujengea mkuu.

Suala ni kutumia gharama kubwa (kwa kuomba omba ndugu na jamaa au hata majirani/marafiki) ili kujengea hayo makaburi.

Kujenga kwangu ni sawa ila kutumia gharama kubwa (bila uwezo huo) si sawa kabisa!

Mkuu Dark City unataka kuniambia kuna watu wanatembeza bakuli kuomba mchango wa kujengea makaburi? Nijuavyo mimi wanandugu yaani watoto wa marehemu ndiyo wanapaswa kujenga. Kwani wanajenga hekalu au kitu gani? Yaani mchanga, kokoto, cement na marumaru kwa kaburi la 2.5 m inagharimu mamilion mangapi?
 
Mie hata wakinitupa bila kuzika it up to wao.. Wakati huo sitakuwa charminglady bali marehemu. Uzuri hakuna jalala la binadamu najua tu watanichimbia shimo waniweke....

Tena nitapenda hata mwili wangu ufanyiwe "practical" Ngoja nitafute ni jinsi gani naweza fanya hivi. Sitaki kumbukumbu yangu iwekwe katika kaburi langu!!! Nawish nipoteelee mavumbini tu!!

Sijui avatar yako ni wewe. Tukianza kuchunguza vitu hata lotion kusingekuwa na haja ya kujipaka. kwani hakubadilishi kuwa binadamu. Sina hakika kama hao wasionakshi makaburi savings wanapeleka kwa watoto yatima. Mi nadhani ni tofauti tu kama mavazi kila mtu huchaguan rangi , aina na wakatimwingine hutofautiana kulingana na hali lakini pia na matakwa. Kama mimi kwa kweli ni mshamba wa kuvaa suti!
 
Ni kweli kabisa Mkuu,
Jamii imeyapa vipaumbele mambo yasiyo ya msingi na kuacha mambo muhimu.

Ni nadra Sana kusikia michango ya kupeleka wanafunzi shule/chuo,watu wamejikita kwenye harusi,uzio wa makaburi etc

"Ni vigumu mno kumshawishi nyani mzee kwamba asali ni tamu kuliko ndizi mbivu" Ni kwenda nao hivyohivyo tu.

ndo mana hata yule mwanamke aliyeenda kumuosha Yesu miguu na nywele zake na mafuta ghali mmoja wa wanafunzi akauulza kwanini anatumia mafuta ghali kwanini yasiuzwe wapewe maskini Yesu akamwambia umaskini mtakuwa nao siku zote hyo ya michango ni case nyingne niache kufanya vitu vya muhmu michango ndo mana huwa hatuendelei tunategemea misaada na michango fanyeni kazi kwa bidii mtu hata akifanya harusi au kujengea kaburi ni maamuzi yake
 
Ni upumbavu na ujinga, Mzoga mzoga tu mnataka kuniambia paka, mbwa, chura nk hawana roho? mbona hao uchimbiwa shimo na maisha yanendele kwa wengine, acheni kukalili.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Watu wanajisahau tu...ukisoma Bible kwa makini utagundua wala haikatazi kama wengi wanavyotaka kutuaminisha.

Ila ukijenga kwa lengo la kupaweka pawe SHRINE...hapo ndo utakuwa unatenda kinyume na maandiko!

Turejee wakati wana wa Israel walipokuwa wanatoka Misri...walibeba mpaka mifupa ya mababu zao ili waipeleke Kaanani. This means kuwa waliyatunza makaburi ya hao wapendwa wao ndo maana muda wa kuondoka ulipofika yalikuwa traceable... kwa mtindo wa dunia ya leo ndo sawa na kuyajengea.

Binafsi sioni tatizo...la mamangu nililijengea na la baba nipo mbioni kulijengea pia. If you have a motive behind huko kujengea...hilo ni TATIZO!

umenena point muhimu sana ukiyajengea kama sehemu ya matambiko ndo inakuwa si vzuri lakini watu wanajengea ukumbusho wa wapendwa wao
 
Ni upumbavu na ujinga, Mzoga mzoga tu mnataka kuniambia paka, mbwa, chura nk hawana roho? mbona hao uchimbiwa shimo na maisha yanendele kwa wengine, acheni kukalili.

umri tu, subiri kidogo ufiwe na mama yako kisha uone mzoga wake, nina imani maiti yake utaifanya kama kama inavyofanyiwa mizoga ya mbwa.
 
Back
Top Bottom