Kujengea makaburi ya Waliotutangulia - Kuna umuhimu wowote?

Kujengea makaburi ya Waliotutangulia - Kuna umuhimu wowote?

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,999
Habari za asubuhi ya leo wapendwa wana Jamvi....

Kwanza niombe radhi kwa nitakaowakwaza kwa namna moja ama nyingine.

Kuna suala hili huwa linanitatiza naomba kuelewesha.

Kumezuka tabia ya kujengea makaburi kwa marumaru ya samani za aina tofauti tofauti tena zenye gharama kubwa, Utakuta mtu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu lakini watu hawakujitokeza kumhudumia lakini baada ya mtu huyo kufariki dunia wanajitokeza ndugu, jamaa na marafiki wanapanga mipango ya kujengea kaburi lake na kuweka nakshi ya kila aina.

Je watu hawa walikuwa wapi wakati wa ugonjwa??

Je kujengea kaburi hilo kutamsaidia nini yule marehemu??

Kuna watu wanafariki ghafla aidha kwa ajali ama kifo cha aina yoyote ila kwa ghafla... Kuna ulazima gani wa kulinakshi kaburi???

Tena kuna wengine wamekwenda mbali wakaanza kutafuta makaburi haya ya mababu zao na kuanza kuyajengea na kuyaweka katika hali ya unadhifu kana kwamba kilichomo ndani yake kina thamani... Tena na kufanya sherehe sijui ya kujengea makaburi... Ni nini maana yake???

Kwa mtazamo wangu ujenzi huu wa kuweka nakshi ni kugharamika kusiko na faida...

N.B. Ni mtazamo tu naomba nisipondwe mawe....
 
Ww usijenge sist tutawaenzi marehemu mpk kufa.baba yangu kafariki nikiwa mdogo. Sasa nimekua nna uwezo nisimjengee kaburi lake?angekua hai ningemnunulia suti. Kafariki hela ya suti itamjengea kaburi. We yako kanywee bia bahili wahed
 
Ni mtazamo wangu mkuu, naona una maneno makali sana.... Kama angekwua mzima ungemnunulia suti ili kujihifadhi, sasa kumjengea kaburi kutamsaidia nini ilhali ashakuwa marehemu? Hata umejengee kwa dhahabu na lulu haitomsaidia chochote.......
 
Tunajengea ili lisipotee kama kumbukumbu kwa wapendwa wetu, njoo uone makaburini ya Kinondoni ambayo hayajengewa yanavyo potea.

Mkuu unajua kujengea hakuna shida ila kuweka nakshi, mara marumaru, mara kuweka kivuli ndio shida! kwani ukijenga kawaida kumbukumbu haibaki???
 
Mkuu unajua kujengea hakuna shida ila kuweka nakshi, mara marumaru, mara kuweka kivuli ndio shida! kwani ukijenga kawaida kumbukumbu haibaki???
Kuna aliyekulazimisha ukamjengee ndugu yako yeyote? Achana na wenye uwezo wa kufanya hivyo wafanye. Maadam hawajakuomba mchango wa kufanikisha hilo zoezi.
 
kinachomuenzi na kuwafanya watu kukumbuka marehemu ni matendo yake wakati wa uhai wake, mengine ni mbwembwe tu! Kujengea kaburi ni woga wa kifo wa wanaojenga- yaani hofu ya kutojua ni kipi kitatupata baada ya kufa hutufanya tupambe mabaki ya miili ya wenzetu ambayo ndani ya nusu saa tu 'recycle process' imeishaanza kuchukua nafasi yake, kila element inarudi kwenye mzunguko wake!

Hebu tutoke nje ya maboksi, tukishaondoka kwenye miili mwili hauna kazi tena.
Oh! Nimekumbuka baba yangu aliacha sifa ya ugomvi kijijini hata nisipojengea kaburi lake a.k.a yake ya 'EVANDA' itabaki milele!
 
Uko sahihi dada yangu hakuna ulazima wa kujengea makaburi...unachoweza kufanya ni kuweka kisaruji upande wa kichwani na ukaandika jina lake, siku alozaliwa na kuzikwa...Kinachomfaa maiti baada ya kufa ni mambo ma3 tu:

1. Sadaka yenye kuendelea kama aliacha kitu cha kuwasaidia watu....Kisima, Hospitali, Public toilet au hata miti kama aliipanda. Watu,wanyama,ndege au hata wadudu wakiwa wanaendelea kunufaika.
2. Elimu yenye kuwafaa watu...Alimfundisha mtu kuchonga vitanda,uhasibu, au taaluma yoyote ile ya halali...yeye ataendelea kupata malipo ya elimu ile kwa kila ataenufaika na elimu ile...hata wakisomeshwa watu wengine...madhali yeye ndo chanzo basi yeye atapata malipo.
3.Mtoto mwema/au Jamaa wema ambao wanaendelea kumuombe dua.

Kwa hio kujengea makaburi ni kupoteza muda na kujidanganya kwa roho zetu...wadudu chini hawana habari na Tazi zetu.

Tujiandae na safari sisi...ni msosi wa wadudu tu!
 
Habari za asubuhi ya leo wapendwa wana Jamvi....

Kwanza niombe radhi kwa nitakaowakwaza kwa namna moja ama nyingine.

Kuna suala hili huwa linanitatiza naomba kuelewesha.

Kumezuka tabia ya kujengea makaburi kwa marumaru ya samani za aina tofauti tofauti tena zenye gharama kubwa, Utakuta mtu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu lakini watu hawakujitokeza kumhudumia lakini baada ya mtu huyo kufariki dunia wanajitokeza ndugu, jamaa na marafiki wanapanga mipango ya kujengea kaburi lake na kuweka nakshi ya kila aina.

Je watu hawa walikuwa wapi wakati wa ugonjwa??

Je kujengea kaburi hilo kutamsaidia nini yule marehemu??

Kuna watu wanafariki ghafla aidha kwa ajali ama kifo cha aina yoyote ila kwa ghafla... Kuna ulazima gani wa kulinakshi kaburi???

Tena kuna wengine wamekwenda mbali wakaanza kutafuta makaburi haya ya mababu zao na kuanza kuyajengea na kuyaweka katika hali ya unadhifu kana kwamba kilichomo ndani yake kina thamani... Tena na kufanya sherehe sijui ya kujengea makaburi... Ni nini maana yake???

Kwa mtazamo wangu ujenzi huu wa kuweka nakshi ni kugharamika kusiko na faida...

N.B. Ni mtazamo tu naomba nisipondwe mawe....

Hii ni point ya msingi sana ambayo hata mm huwa najiuliza kila siku,ukijenga kawaida tu ni dhahiri kuwa linaweza kuonekana na lisipotee tena,hii ya kuweka nakshi za gharama kwangu siipendelei afterall pale mbagala mission huwa wanachimbua na kuiba vilivyomo katika makaburi hayo kila siku
 
Kujenga kaburi ili lisipoteze ndugu wa marehemu,nakshi ziwekwzo sio muhimu sana....
 
kujengea kaburi si tatizo maana kunalifanya lidumu usipojenga linapotea na kufutika kabisaa..tatizo kuweka nakshi za thamani sioni maana yeyote
 
kwahiyo hata akiwa hai hakuna haja ya kumnunulia suti
Ni mtazamo wangu mkuu,
naona una maneno makali sana.... Kama angekwua mzima ungemnunulia suti
ili kujihifadhi, sasa kumjengea kaburi kutamsaidia nini ilhali ashakuwa
marehemu? Hata umejengee kwa dhahabu na lulu haitomsaidia
chochote.......
 
charminglady Je siku ukifa watoto zako wasijengee kaburi lako?
Si litapotea kabisa, kule moshi utasikia hapo kwenye sale alizikwa
mzee fulani siku hizi wanajengea, huku mjini wasipojengea ndo
kabisa utakuta siku moja mtu mwingine amezikwa juu yako.

Hizo nakshi ni matanuzi tu, kama pesa ipo nao wanataka wajitanue hivyo.

Kuhusu kumjali mgonjwa hilo nalo ni neno kwa kuwa huwa tunajisahau sana
wakati mwingine.
 
ww kama huna hela za kujengea kaa kimya. mama yangu amefariki tumetumia uwezo wetu wote lkn Mungu hakupends apone. Kaburi tumejengea na kulinaksh kwa tulikopa kwako au kwa mtu yeyote? kaa kimya bwana
 
Mdada charminglady katika siku ambazo umepost utumbo, basi leo ndo nimeshuhudia utumbo wako,.....
Hili swali alitakiwa akuulize mwanao,au mtoto wa darasa la tatu(hasa kwa ujanja wa watoto wa siku hiz]
KI MSINGI
Makaburi yanajengewa ili yasipotee.na yanajengewa kwa vitu ambavyo ni imara,ambavyo sio rahisi kupotea tofaut na vumbi/mchanga ni pamoja na mawe,kokoto uki mix na cement,na baadhi miti n.k
Sasa mtu anapo amua kujengea kaburi kimsingi anakuwa anfanya, kwa mantiki hiyo hapo juu,jiulize wanaoenda ku hiji makka hilo kaburi la mtume wangelijuaje kama lisingejengewa!wanaoenda kwaajili ya makumbusho kujua kaburi la Mitume,Wafalme na Hata Yesu unadhani ingekuwa rahisi kuyaona hayo makaburi endapo wangefukiwa chini na watu kutawanyika?
Wengine wazazi,ndugu au jamaa zao walifariki ilihali wao wakiwa wadogo,na wamekuwa wakakuta alama ya Misaraba,Viapnde vilivyoandikwa majina ya ndg zao au mawe na hata miti wakaambiwa Hapo ndipo walipozikwa ndg/jamaa zao ,sasa kwanini wao washindwe kuwajengea ili iwekumbukumbu kwa kizazi chao?
Tafakari Chukua hatua
huko misri kuna mapango ya wafalme ambao wamezikwa humo na mpaka leo historia umeikuta na ukitaka kujionea unakwea pipa moja kwa moja mpaka Misri na utayakuta mapango hayo yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu na wafalme wakazikwa humo.
Sometimes unafanya anasa mbalimbali,bar unazungusha raund ngapi na maswaiba zako,unanunua body spray ya gharama ilihali wajua mwili wako ni wa kuoza tu,na tena kunuka jasho muda woote ukiwa hai,umemiliki smart phone ngapi na ushindwe kumjengea kaburi ndg,jamaa,rfk au hata mwanao ili wadogo zake waje wafahamu ndg yao alizikwa mahala flani kwa alama flan?
Tafakari Chukua Hatua!
 
Last edited by a moderator:
Wadau mbona mna maneno makali sana... Nazungumzia nakshi jamani yaan inafika mahali watu wanapamba makaburi as if aliyekufa anashuhudia au kutoa shukrani kwa kilichofanyika!

Kuweka kumbukumbu sio issue issue ni kunakshi mpaka inakuwa kufuru. Kwanini ile pesa isitumike kuyaenzi mazuri aliyoyaacha au kusaidia watoto au jamaa zake????
 
Back
Top Bottom