naona unajichanganya kidogo mkuu wangu! kinacho"mata" hapa ni DHAMIRA YA NAFSI, unapoamua kujengea kaburi la mpendwa wako aliyetangulia ni kwa msukumo upi? je unataka kwa ajili ya ufahari tu kujionesha kwa watu au kuna kitu kinakugusa moyoni? kuna mila za wengine haziruhusu hata kuweka jiwe la kumbukumbu juu ya kaburi, hakuna msalaba, hakuna kupanda hata mauwa; ndugu zangu wajaluo wakizika wanafukia kisha wanacheza disko juu ya kaburi mpaka linapotea, wanafanya hivi ili kujaribu kufuta kumbukumbu ziletazo sononeko la moyo, ni mila zao na wako sahihi kabisa, wengine mtu akifa wanachoma moto na mabaki wanayasaga yanakuwa unga na wanaenda kumwaga baharini, na wao pia wako sahihi. sisi wabantu tunaweka alama kama kumbukumbu, zamani kabla hatujabadilika na kunakili mila za wenzetu tulikuwa tunaweka jiwe, hata hilo jiwe ilikuwa linatafutwa jiwe lililo zuri lenye utofauti na mawe mengine, ukiona tu unajua kuna kaburi hapa hata kama ni porini, tukabadili mila na kuanza kuweka misalaba ya miti, ya chuma, na ya mawe yaliyochongwa vizuri, baadaye tukawa tunajengea, yote sioni ubaya, kikubwani dhamira ya nafsi. Binafsi nina madeni kadhaa kwa wapendwa wangu waliotutoka, nitajitahidi kadri niwezavyo kama nipo hai nitembelee kaburi moja baada ya lingine na kuwakumbuka kwa kuyaboresha, nitatembelea kaburi la rafiki yangu mpendwa wa shule, nitakaa juu ya kaburi, nitalia nitaomboleza mpaka chozi langu likauke, sitataka mtu anishike wala kunipooza kwani ni mimi tu nijuaye machungu ya moyo, nitamtengenezea kumbukumbu, najua haitapoza machungu yangu lakini nafsi yangu ndivyo inavyonituma. :rip: