Kujengea makaburi ya Waliotutangulia - Kuna umuhimu wowote?

Kujengea makaburi ya Waliotutangulia - Kuna umuhimu wowote?

Makaburi hupotea lakini ukiyajenga huweka kumbukumbu japo Ardhi hii tuliopo ina makaburi ya wafu wengi waliotutangulia enzi za Gharika, njoo uandaliwe michoro ya kaburi hapa kama uonavyo design hii na nyinginezo
 
Attachments

  • 1411292548203.jpg
    1411292548203.jpg
    78.9 KB · Views: 459
Ni siku ya huzuni,yatupasa siku hiyo kumwombea dua,ili mwenyezi mungu ampe punziko lililo jema..
 
Hahaha kwa kweli umenipa raha! Uswahili mzigo, bongo tambarare fursa kila kona. Heri yako Una macho. Hebu niambie cost ya kujenga kaburi kama hilo Na kuweka marble Ni bei gani?
Makaburi hupotea lakini ukiyajenga huweka kumbukumbu japo Ardhi hii tuliopo ina makaburi ya wafu wengi waliotutangulia enzi za Gharika, njoo uandaliwe michoro ya kaburi hapa kama uonavyo design hii na nyinginezo
 
Makaburi hupotea lakini ukiyajenga huweka kumbukumbu japo Ardhi hii tuliopo ina makaburi ya wafu wengi waliotutangulia enzi za Gharika, njoo uandaliwe michoro ya kaburi hapa kama uonavyo design hii na nyinginezo

Ningekuwa nimezaliwa ulaya nisingejua mambo ninayoyajua namshukuru mungu kwa kuzaliwa Afrika huku kila kitu dili

They call it Africa we call it home (hili ni tangazo)
 
Naomba mnitoe porini wana Jf, eti kujenga makaburi au kumbukumbu ya kifo ni Siku ya SHEREHE au HUZUNI?

Kwakuwwa sote huamini kuwa kifo cha mpendwa wetu ni MAPENZI YA MUNGU siku ya ujenzi wa kaburi huwa ni maadhimisho ya kifo cha ...... Ni siku ambayo huwa ni ya furaha katika kumtukkuza Mungu.
 
Makaburi hupotea lakini ukiyajenga huweka kumbukumbu japo Ardhi hii tuliopo ina makaburi ya wafu wengi waliotutangulia enzi za Gharika, njoo uandaliwe michoro ya kaburi hapa kama uonavyo design hii na nyinginezo
naona unajipiga promo
 
Habari za asubuhi ya leo wapendwa wana Jamvi....

Kwanza niombe radhi kwa nitakaowakwaza kwa namna moja ama nyingine.

Kuna suala hili huwa linanitatiza naomba kuelewesha.

Kumezuka tabia ya kujengea makaburi kwa marumaru ya samani za aina tofauti tofauti tena zenye gharama kubwa, Utakuta mtu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu lakini watu hawakujitokeza kumhudumia lakini baada ya mtu huyo kufariki dunia wanajitokeza ndugu, jamaa na marafiki wanapanga mipango ya kujengea kaburi lake na kuweka nakshi ya kila aina.

Je watu hawa walikuwa wapi wakati wa ugonjwa??

Je kujengea kaburi hilo kutamsaidia nini yule marehemu??

Kuna watu wanafariki ghafla aidha kwa ajali ama kifo cha aina yoyote ila kwa ghafla... Kuna ulazima gani wa kulinakshi kaburi???

Tena kuna wengine wamekwenda mbali wakaanza kutafuta makaburi haya ya mababu zao na kuanza kuyajengea na kuyaweka katika hali ya unadhifu kana kwamba kilichomo ndani yake kina thamani... Tena na kufanya sherehe sijui ya kujengea makaburi... Ni nini maana yake???

Kwa mtazamo wangu ujenzi huu wa kuweka nakshi ni kugharamika kusiko na faida...

N.B. Ni mtazamo tu naomba nisipondwe mawe....

Wasabato na sera za makaburi, mbona Kristo alizikwa humo na kaburi lile lilinunuliwa kwa shekeli nyingi tu, mkifa mnawekwa wapi!?!? Unamaanisha taratibu za kuhifadhi mwili mfano, uundaji wa jeneza lake kuwa bei ghali ni kosa!?!? Sijaona hoja hapa
 
upuuz tu kujengea makaburi na inatokana na mila za kipagani wale wanaoamini ukimuomba marehem basi atakusaidia WENYEWE WANA SALA HATA ZA MAREHEMU kinachoharibu ni kuwa wengine wamerithi hizi tabia bila kufahamu kama vile walivyomzalisha Yesu trh 25/12 HAKIKA ni vijidalili vya dunia kupinduka ndio maana tumesahaulishwa kumuuguza mgonjwa hila kufanya laana ya kifedha kwenye msiba DUNIA TAMU SANA HII.
 
Mnajifanya mnajua kukosoa kila kitu,mwisho wa Siku mtahoji kwa mini maiti zizikwe badala ya kutupwa jalalani kama zinavyotupwa takataka zingine.
 
Back
Top Bottom