Dear CL, kuna issues 3 hapa zihusuzo kujengea makaburi!.
- Kuweka Alama- Hii ndio sababu kuu ya kujengea makaburi, ili tuu kuweka mark, nani alizikwa hapa, kaburi lisipotee. Ujenzi wa kuweka alama ni simple na wala hautumii gharama kubwa!.
- Kumplease Marehemu!. Watu wanajengea makaburi kwa gharama kubwa ili kujifariji nafsi zao kuwa ndio namna bora ya kumuenzi marehemu!, kwa kadri familia ilivyo na uwezo, ndivyo kaburi la thamani linavyojengwa hadi mengine kuwa kama minara, hivyo kuonyesha jeuri ya pesa.
- Kujengea makaburi kama sehemu ya kuabudia!. Hizi ni ibada za wafu!. Kuna makaburi yanajengwa kama shrines kwa watu wa ukoo ule kwenda hapo, kufanya misa, ibada, kumbukumbu hata kutoa makafara ya kiukoo!, hawa ndio wale utasikia hata akifia wapi, lazima akazikwe kwao ili wakafanye mambo yao!.
My take:
Mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, mwili na roho!. Mwili unakufa na kugeuka mavumbi, roho haifi, inadumu milele!. Mwili ukiishakufu, its nothing!, hata wafanyao ibada za wafu kwa kuombea dua miili, kupeleka nyumba za ibada, kusali misa za kumbukumbu za marehemu, kwenda kusali makaburini, kujengea makaburi, au anything to do with a dead body ni ubatili tuu, kwa watu kujifariji na kujifurahisha nafsi zao, a dead body is a dead body!.
Wako wengi wanaofanya ibada za wafu!, hawajijui kuwa hizo ni ibada za mashetani !. Bwana Wetu Yesu Kristu, alituasa
"Waacheni wafu wawazike wafu wao!".
Watu enlightened, wanakuwa wamefunuliwa kuijua kweli, ndio maana wengi wakifa, wanachomwa au kufanyiwa creamation kwa sababu the deadbody or lifeless body is nothing at all!.
Kwenda kusali makaburini ni ibada za kishetani kwa kujua au kutojua!.
Mtu anayetoa mwili wake kufanywa cadaver is better of kuliko ule mwili, uliovishwa vito vya dhahabu na almasi, ukazikwa kwenye jeneza la kioo, alminium au la mbao lilitengenezwa vizuri na kupabwa sana hadi maua!, kisha kaburi likajengwa na marumaru, granite, tiles, etc ili lipendeze machoni, what befals that body huko ulimo, its the same!.
Pasco